Mgombea ubunge katika jimbo la Igunga kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Kashindye (wa pili kushoto), akijumuika na wanakijiji cha Lugubu, kucheza, mara baada mkutano wa kampeni za chama hicho katika kijiji hicho leo


 Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe akihutubia katika mkutano wa kampeni Igunga
 Viongozi wa CHADEMA wakiwasili na mgombea wa chama hicho wa jimbo la Igunga
 Vijana wa Igunga wakiwa wenye furaha wakati wa maandamano ya Chadema kuelekea kwenye mkutano  wa kampeni 
Mbunge wa Mbeya Mjini, Mh. Joseph Mbilinyi, ‘Mr Sugu, akiwasili kuhutubia wananchi wa Igunga katika mkutano wa ufunguzi wa kammpeni juzi. 
Picha zote na mdau Joseph Senga wa Tanzania Daima

Baadhi ya Viongozi wa Kitaifa wa CHADEMA wakiongozwa na Katibu Mkuu wa chama hicho,Dr Willbroad Slaa wakiwaaga wananchi wa kijiji cha Lukubu Kata ya Itumba,Wilayani Igunga jioni ya leo wakati wa mwendelezo wa kampeni ya kumnadi mgombea Ubunge wa Chama hicho,Bwa.Kashindye Joseph ambaye anagombea nafasi hiyo ndani ya jimbo hilo lenye jumla ya kata 26.Kata hiyo ipo takribani kilometa 35 kutoka Igunga mjini.CHADEMA wamezindua rasmi kampeni zao jana.
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Lukubu kata ya Itumba,wakifuatilia mbio za mkutano wa kampeni wa chama cha CHADEMA uliokuwa ukifanyika leo katika uwanja wa Mnadani na kuhudhuriwa na mamia ya Watu.
Baadhi ya Wanakijiji cha Lukubo wakifuatilia mkutano wa kampeni ya chama hicho,ambacho kilikuwa kikimnadi mgombea wake wa Ubunge kwa jimbo la Igunga,Bwa.Kashindye Joseph.
Wakiendelea kumsikiliza Katibu mkuu wa Chama cha CHADEMA,Dr Willbroad Slaa alipokuwa akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Igunga jioni ya leo.
Mbunge wa jimbo la Maswa Mashariki,kupitia chama cha CHADEMA,Mh.Silyvester Kasumbulai,ambaye pia ni Waziri kivuli wa Mifugo na Uvuvi kupitia chama hicho,akizungumza na wakazi wa kijiji cha Lukubu,Kata ya Itumba jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea wa chama hicho.

Mgombea Ubunge wa jimbo la Igunga kupitia chama cha CHADEMA akijinadi mbele ya mamia ya wakazi wa kijiji cha Lukubu,kata ya Itumba jioni ya leo kwenye uwanja wa Mnadani.

Mmoja wa wanakijiji cha Lukubu akifautia kwa makini mkutano wa kampeni wa chama cha CHADEMA jioni ya leo.
Baadhi ya Wananchi waliofika kwenye mkutano wa kampeni za chama hicho wakishangilia jambo.

Wakazi wa kijiji cha Lukubu wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni za chama cha CHADEMA,jioni ya leo kwenye uwanja wa Mnadani.
Mbunge wa Viti maalumu (CHADEMA) na Mwenyekiti wa Chama hicho mkoa wa Morogoro,Mh.Susan Kiwanga akizungumza mbele ya mamia ya wakazi wa kijiji cha Lukubu,kata ya Itumba jioni ya leo wakati wa mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Igunga kupitia cha hicho jioni ya leo kwenye uwanja wa Mnadani.
Katibu Mkuu wa chama cha CHADEMA,Dr Willbroad Slaa akiwasalimia wakazi wa kijiji cha Lukubu,waliokusanyika jioni ya leo kabla ya mkutano wa kampeni wa chama hicho kuanza.Dr Slaa alikuwa akiwasili kwenye uwanja huo kwa ajili ya kumnadi mgombea wa jimbo la Igunga kupitia chama hicho.
Wakazi wa kijiji hicho wakukosa kubeba mambo yenye jumbe kama uonavyo pichani.
Mgombea Ubunge wa jimbo la Igunga,Mh.Kashindye Joseph (wanne kulia) akisindikizwa na baadhi ya wafuasi wa chama hicho kwenye uwanja wa kufanyia mkutano wao wa kampeni jioni ya leo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Duh wanasiasa wana mkwara, utadhani wataondoa matatizo kwa usiku mmoja! Waone watoto na wazazi wao walivyokaa; Shida yenu wanasiasa mkishatoka hapo mnawasahau wananchi hadi nyakati za kampeni tena.

    ReplyDelete
  2. Tutawashangaza kwelikweli huko Igunga na kila mtu atajua kuwa kudeka kwa CHADEMA hakusaidii kitu.
    CCM OYEE!

    ReplyDelete
  3. Wonder where the guy got the konyagi package from?

    ReplyDelete
  4. na bia kwenye chupa ya maji mkutanoni , sijui alichokihutubia kama hakitokana na hiyo pombe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...