Gwaride la Askari wa JWTZ Base ya Anga ya Ngerengere, wakifanya onesho la namna mazishi ya Askari mwenzao aliyefariki dunia yanavyokuwa upaande wa Kijeshi na kiraia , wakati wa maadhimisho ya siku ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) ya kutimiza miaka 47 tangu kuanzishwa kwake Septemba mosi, 1964.
Gwaride la Askari wa JWTZ Base ya Anga ya Ngerengere, la mazishi wakipinga risasi baridi hewani , kuonesha mfano wa namna ya mazishi ya Askari mwenzao aliyefariki dunia yanavyokuwa upaande wa Kijeshi na kiraia , wakati wa maadhimisho ya siku ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) ya kutimiza miaka 47 tangu kuanzishwa kwake Septemba mosi, 1964.
Mkuu wa Komandi ya Vikosi vya Anga Base ya Ngerengere,Brigedia Jenerali Joseph Kapwani ( kushoto) akigonganisha glasi na Mkuu wa Wataalamu wa Kijeshi kutoka Jeshi la Anga la Watu wa Jamhuri ya China, hapa nchini, Kanali Mwandamizi , Zhu You Yu ( kati kati) na (kulia ) ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) ya kutimiza miaka 47 tangu kuanzishwa kwake Septemba mosi, 1964.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu( wapili kutoka kushoto) akiwa na mweyeji wake Mkuu wa Kamandi ya Base ya Anga Ngerengere, Brigedia Jenerali, Joseph Kapwani ( watatu kutoka kushoto) pamoja na maafisa waandamizi wengine wa base hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu ( wenye suti) akisalimiana na Askari wanafunzi wa chuo cha Kijeshi cha Anga, Base ya Ngerengere.
Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii, Morogoro
Daa WAKUU wetu wa Wilaya na Mikoa mmmmhhhhhhh karne ya kale!!!!! Kama CCM na Kikwete wangependa Mapinduzi ya HARAKA waingize vijana wenye Exposure ya kutosha kushauri mikakati ya mapinduzi ktk nyanja za usalama na maendeleo kwa ujumla.
ReplyDeleteKarim
Wajeda acheni ushamba jama, mwaka 2011 huu... Si uchuro huo, eti akifa anazikwa/anaagwa hivi! Pigeni sarakasi na hizo Chengdu zenu na MiGs walau mshtue kidogo. Hamjui parade za uhuru ni za kupiga bakora? Unadhani wenzetu wanavyopitisha miBulava na miICBM yao ni wajinga?
ReplyDeleteMambo ya kizamaaani ndo maana mnafanyia humohumo ndani kwenu, aagh! Make it a public parade/celebration. Earn some respect, threat some enemies... ndo maana ya hizo shughuli, eti jinsi ya kumzika mwenzetu, du hii kali!