Gari aina ya Mitubishi Pajero likiwa eneo la tukio mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo mbaya siku ya Alhamisi majira ya saa 11:30 jioni barabara kuu ya Singida Nzega kilomita 15 kutoka mjini singida na kusababisha vifo vya watu watano na kujeruhi watatu akiwemo mtoto mdogo wa miaka miwili.Mtoto Yohanes Josephat (2) akiwa wodi namba mbili  na msamaria mwema akiuguza jicho baada ya kutokea kwa ajli hiyo ambayo wazazi wote wawili walifariki dunia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. This is very sad. I'm so hurt to come across this news. Jamani, huyu mtoto (pengine na ndugu zake) ndio hawana baba na mama tena. Madereva, tuwe makini jamani kuzuia ajali unless haziepukiki kabisa.

    ReplyDelete
  2. Imenitilisha huruma na huzuni nyingi...Mungu akutunze mtoto Yohanes. Nakuombea na wote walioumizwa na hii ajali. Mungu akuponyesheni na huzuni na majeraha.

    ReplyDelete
  3. Asante sana mama msamalia mwema kwa kumuuguza mtoto Yonanes, na Mwenyezi Mungu akubariki.

    ReplyDelete
  4. Mwenyezi Mungu aziweke mahali pema peponi roho za marehemu wote. Na tunazidi kumwombea mtoto Yohanes apate nafuu,Inshaallah aepukane na maradhi ili aweze kuwa na afya njema. Ni pigo kubwa sana kwa mtoto Yohanes kuondokewa na wazazi wake. Poleni sana wafiwa wote.

    ReplyDelete
  5. Kutokana na jinsi gari ilivyopondeka, bila shaka dereva alikuwa anaenda mwendo wa kazi mno. Mungu alaze roho za marehemu mahala pema mbinguni. Poleni sana wafiwa.

    Mtoto Yohanes ni yatima sasa. Nalia, huyo mtoto hawezi kuelewa wazazi wake wamekwenda wapi. Mungu ambariki huyo msamaria mwema.

    ReplyDelete
  6. eeeh Mungu ulisema hutatupa waja wako, naomba uumtunze huyu mtoto salama na ulale roho za marehemu mahala pema peponi, this is terribly sad jamani!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...