Vodacom Tanzania inapenda kuwashukuru sana watanzania wote na hasa wateja wetu kwa kuendelea kushirikiana nasi hadi hivi sasa tumefikisha wateja milioni 10.


Tuna kila sababu ya kuendelea kuwashukuru wateja wetu na watanzania wote kwa ujumla kwa uaminifu na mchango wao mkubwa wanaoendelea kuuonyesha kwetu kwa kipindi chote cha miaka 11 sasa.

Mafanikio mbalimbali tuliyoyapata hadi hivi sasa ni matokeo ya kuelewa mahitaji muhimu ya wateja wetu na kuhakikisha kuwa tunayatimiza na kuwafanya wateja wetu waendelee kufurahia huduma zetu.

Kama tulivyowaahidi wakati wa mabadiliko ya muonekano wetu, tunapenda kuwasisitizia kuwa tutaendelea kuyatimiza yale yote tuliyowaahidi na kuyaboresha zaidi.

Vilevile, tunawahakikishieni kuwa tutaendelea kuwa mtandao ulio bora na unaotoa huduma na bidhaa za bei nafuu zaidi hapa nchini.

Ripoti ya idadi ya wateja kama ilivyotolewa na TCRA

Mtandao
Vodacom
Airtel
Tigo
Zantel
TTCL
Sasatel
Benson
Wateja
10,000,000
5,927,417
4,671,263
1,354,098
226,153
8,498
2,074

Ahsante Tanzania.
Vodacom, kazi ni kwako

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

 1. Hongereni,lakini mjitahidi kuwaelimisha wafanyakazi wenu namna ya kutatua matatizo ya wateja maana wakati mwingine tatizo moja linatolewa maelezo tofauti na wafanyakazi tofauti.Uelewa wao unatofautiana.Mfano mtu anapoteza line,akienda kurenew anaambiwa akalete loss report toka polisi,anaifuatilia loss report siku nzima,jioni akiipeleka ofisini anakutana na mhudumu mwingine na anaambiwa haihitajiki,atoe tu copy ya kitambulisho na ajaze form.Inauma sana kupoteza muda ambao ungenisaidia kufanya kazi zangu za kunipa kipato kwa ajili ya kitu halafu baadae kinabaki kuwa mzigo tu.IMENITOKEA,SIO KWAMBA NI UZUSHI,NIMEPOTEZA SIKU NZIMA NA HATA HIYO LINE IMEKUJA KUFANYA KAZI BAADA YA SIKU NZIMA.NIMEKASIRIKA KATIKA HILI. Maliki Mahmoud Mang'indo

  ReplyDelete
 2. Jamani makampuni ya simu pelekeni huduma za simu za mikononi hadi huko vijijini badala ya kung'ang'ana mijini tu wakati huko vijijini kuna watu wengi sana wanahutaji kupata mawasiliano ya simu,mfano kwenye vijiji vya wilaya ya Mbinga mawasiliano ni ya shida sana kajengeni minala ya simu huko.

  ReplyDelete
 3. Hongera sana Voda Com kwa mafanikio hayo na naomba MSIBWETEKE bali mkaze Buti.Pili napenda kujua ni lini wananchi wa MWANDOYA Wilayani Meatu tutapata huduma hii.Naomba wahusika wanifahamishe kwa Namba yangu 768 761038 ama kwa Barua Pepe newubora@yahoo.com
  Tatu na mwisho ni hii huduma ya M-PESA hasa inapotokea umekosea destination.Ile namba ya customer service haitoi maelezo ya jinsi ya kurudishiwa pesa badala yake inaelekeza huduma mbalimbali za M-PESA na mahali zinakopatikana.Naomba mjitahidi kurekebisha hali hiyo

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...