Mwenyekiti wa CHADEMA,
Mh. Freeman Mbowe
NA MERY AYO, Arusha.

Mwenyekiti CHADEMA Mh Freeman Mbowe leo amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa makosa mawili ambayo aliyafanya mjini hapa na kukiuka sheria za nchi

Mwendesha mashtaka wa serikali Bw Haruna Matagani mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Bi Devotha Kamuzora, amesema mtuhumiwa mbowe alidaiwa kufanya makosa hayo wakati wa mkutano wa hadhara.

Aliendelea kudai  kuwa katika kosa la kwanza mtuhumiwa alikuwa ni miongoni mwa watu ambao waliongoza mkutano baada ya muda wa mkutano kuisha, jambo ambalo ni kinyume cha sheria na taratibu za jeshi la polisi.

Kosa la pili, alisema,  ni kukataa kutii amri halali ya polisi iliyowataka  kutawanyika kwa ajili ya sababu za kiusalama, jambo ambalo mtuhumiwa huyo alikataa.

‘Jeshi la polisi liliwataka wafuasi watawanyike baada ya kumazika kwa mkutano ambao ulikuwa na kibali halali lakini haikuwa hivyo. Badala yake waliendeleza mkutano pamoja na jeshi hilo kuwasihi juu ya kutawanyika hivyo sheria na amri za polisi zilikiukwa” iliongezwa mahakamani hapo.

Mh Mbowe  alikana mashitaka yote na kesi hiyo imeahirishwa mpaka November 22 mwaka huu ambapo itasomwa tena mahakamani hapo. Vile vile  mahakama iliridhia kumuachilia huru mara baada ya kukidhi masharti ya dhamana.

Leo jiji la Arusha limekuwa shwari  bila shaka ni baada ya kusitishwa kwa maandamano ambayo yalikuwa yamepangwa kufanyika siku hii.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. mbona hamjaweka jinsi ya kushiriki au tayari mnaowashiriki wenu

    ReplyDelete
  2. HAUJATAJA MASHARTI HAYO YA DHAMANA NI YEPI DADA YANGU KWANI NI MUHIMU HASA KUTOKANA NA KESI YA LEMA KUKATAA DHAMANA LAZIMA TUFANYE OBJECTIVE JOURNALISM

    ReplyDelete
  3. HUYU Mwenyekiti wa siasa za usanii ilibidi akamatwe tokea siku ya kwanza ya maandamano KABLA HAJATOROKA NA KUJISALIMISHA MWENYEWE POLISI...Tanzania itaingia mahali pagumu kama tutaongozwa na viongozi WASALITI KAMA HUYU NA WASIO NA MSIMAMO...GEREZA NI HAKI YA GODBLESS LEMA PEKE YAKE NA WENZAKE 9 WALIOKOSA SIFA ZA WADHAMINI KUWASHIKIA DHAMANA?

    ReplyDelete
  4. Najua hii ni blog ya sirikali kama siyo ya wana CCM lakini ukweli ni kwamba wananchi wa Arusha wanabakwa na CCM kama siyo serikali kisiasa.Na kinachofanywa na wana CDM ni harakati za kuwakomboa wana A Town na udhalimu huu.

    ReplyDelete
  5. Kuna watu wachache wasioitakia Tanzania mema ambao hata ukiwauliza tunasherehekea miaka 50 kwa lipi hawana la kusema....baadhi wa wanaCCM waelewa wameikubali CHADEMA na katika mikutano yao hili liko wazi. Tatizo wamebaki wale wanaCCM wasielewa hata kama uchumi wa nchi umeharibiwa na CCM. Hawa ni wale wanaokwenda kwa nguvu za khanga, vitenge, tshirts na kofia, na chumvi na sukari...bila kujua kuwa wanapoteza haki zao za msingi pamoja na kusababisha kudorora kwa uchumi wa nchi na bila kujali ama kufikiria kuwa watoto wanaowazaa watakuja kuishi kwenye mazingira gani. Mchango wa CHADEMA katika siasa za Tanzania uko wazi na kila mtu hata watoto wanautambua. Hata CCM yenyewe imeanza kujisafisha baada ya CHADEMA kuanza kuanika uovu na uchafu wao. Watanzani tuwe waelewa katika masuala makubwa ya nchi yetu. Tufanye maamuzi magumu jamani...hata Mhe. Lowassa amesema ambaye ni mwanaCCM! Big Up Mhe. Mbowe, tuko nyuma yako.....peoples power..no one can stop it...

    ReplyDelete
  6. Kelkaf bwana mdogo, nimesikia malalamiko yako,,,,sawa purukushani ni ya kuwasaka hao CDM (walio wakorofi)kwa kuwa mahali anapo sakwa nyati(jeuri) ila kwa nia njema ili apigwe risasi nyasi ndio ziumiazo....wananchi itawagharimu hakuna jinsi!

    ReplyDelete
  7. Kwa kuwa CDM inaleta siasa za umwamba,kutofuata taratibu,kiburi, mabavu na ujambazi....hakuna njia nyingine zaidi ya kutumia msuli!.

    ReplyDelete
  8. Wewe dogo,,,ala, hakuna nini wala nini atakaebakwa Arusha labda mwenyewe kwa hiari yake atakuwa amezikubali sera za Donald Cameron!.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...