Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo akingumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya aina yake ya kuwatafuta na kuwawezesha wajasiriamali wadogowadogo katika shindano la wezeshwa na Safari Lager jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Meneja Masoko wa Tbl,Mamongae Manlare na Kulia ni Meneja wa Matukio wa Tbl, Zozimick Kimati.
Kikundi cha burudani kinachoitwa Bombeso Artist Group cha Dar Es Salaam kilitoa burudani yake wakati wa uzinduzi huo.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo Imezindua rasmi kampeni ya aina yake ya kuwatafuta na kuwawezesha wajasiriamali wadogowadogo katika shindano la wezeshwa na Safari Lager ambalo linaweza kumpatia mtu yeyote ruzuku ya kusaidia kuona njia ya mafanikio katika maisha yake.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo alisema Bia ya Safari Lager imezindua program hiyo ya wezeshwa ili kuwasaidia wamiliki wa biashara ndogondogo na za kati kukuza biashara zao,kuweza kuajiri zaidi ,kupata faida zaidi na pia kusaidia jamii yao.

Alisema program ya Wezeshwa na Safari lager itatoa ruzuku yenye thamani ya jumla ya Tsh Milioni 200 kwa kuwawezesha wafanyabiashara watakaoingia na kufuzu vigezo vya program hii.Uwezeshwaji utakuwa kwa kupewa vitendea kazi muhimu vinavyohitajika ili kukuza biashara zao.

Alisema zoezi hili litawahusu wafanyabiashara wenye ueledi wa uchapa kazi,wanaomiliki biashara binafsi na atakaeweza kusaidia jamii inayomzunguka.

Kwa taarifa zaidi kuhusu program hii ya wezeshwa na Safari Lager unaweza kutembelea kiwanda chochote cha Tanzania Breweries Ltd ,Bohari kuu au wauzaji wa jumla na kuchukua fomu ya usajili au unaweza kutembelea tovuti ya www.wezeshwa.co.tz kisha jaza fomu hiyo na ipeleke katika kiwanda cha TBL hapa nchini au tuma barua pepe kwenda info@wezeshwa.co.tz au unaweza kupiga simu nambari 0763 600041 (Dar es Salaam) 0763600042 (Arusha) 0763 600044 Mwanza) na 0763 600045 (Mbeya) na mwisho wa kurudisha fomu ni 02Machi 2011

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...