Wakaazi wa Dar es salaam wakitembea baada ya barabara ya Morogoro road sehemu za Jangwani kufungwa kwa muda kutokana na mafuriko yaliyoikumba jiji hilo kwa siku mbili mfululizo na hadi sasa imefahamika kuwa watu 13 wamepoteza maisha yao. Picha zote na Francis Dande wa Globu ya Jamii



Boti kutoka feri likitelemshwa kusaidia zoezi la uokoaji


Askari wakiwa tayari kulinda usalama wa mali na watu









Mto Msimbazi ukifurika kuingia bahari ya Hindi
Daraja la Jangwani halipitiki


Askari wa JWTZ katika kuokoa wananchi



Boti za Fibre toka JWTZ zawasili kusaidia uokoaji

Picture
Gari la Serikali namba STK 3316 likiwa limetumbukia kwenye daraja lililobomoka kutokana na mvua iliyonyesha leo eneo la Makondeni kwa Mahita, Mbezi, Dar es Salaam. Dereva na abiria waliokuwemo walinusurika kwenye ajali hiyo. 
Picture
Gari la Zimamoto mali ya Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam likiwa limetumbukia kwenye daraja lililoharabiwa na mvua 
Picture
Picture
Picture
Picture


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. Mimi nilijua mafuriko ya kawaida lakini hizi picha zimenistua sana tu, Mwenyezi Mungu azipumzishe roho zao mahali pema waliofikwa na umauti

    ReplyDelete
  2. sasa afande chacha kicho kirungu cha nini kwenye uokoaji tena unaonekana ukiwapigia watu mkwala.anyway poleni sana ndugu zangu wa dar.

    ReplyDelete
  3. hii ni hatari kubwa.. poleni waathirika wote

    ReplyDelete
  4. Hali inatisha inasikitisha mungu saidia watanzania

    ReplyDelete
  5. jamani mungu waokoe wenzetu.

    ReplyDelete
  6. Hata mimi nilikuwa nadhani kama miaka yote, kumbe hali siyo ya kawaida haijawahi kutoke hii, naona zimesombwa hata nyumba zilizo mbali na bonde la mzimbati, poleni sana, mambo kama haya mamlaka ya hali ya hewa, wenzao huku juu, wana shika vipaaza sauti kutangaza watu waondoke waondoke sasa haraka haraka na magari wakizunguka kabla ya mvua yenyewe kunyesha, sasa hawa jamaa wana subiri mpaka watu waathilike ndo waseme eti mvua hii haijaisha, mbona hata mimi naweza kutabiri hivi.

    ReplyDelete
  7. Mwenyezi Mungu awalinde waja wake. Hii hali inastua sana

    ReplyDelete
  8. Poleni waathirka wa mafuriko, na pia hameni mabondeni!

    ReplyDelete
  9. poleni sana ndugu zangu mana kweli hizi picha zinashtua inaonekana sio mafuriko ya kawaida, tutaomba watu wote tushirikiane kwenye kusaidiana katika janga hili tusisubiri tu serikali mana kutokea imeshatokea...

    ReplyDelete
  10. Eee Mwenyezi Mungu tusaidie waja wako! Hizi picha zinatisha kwa kweli. Wakati mie nalalamika kuwa umeme umekatika kumbe sijui kuna binadamu sehemu nyingine wanateseka hivi! Mungu nisamehe!

    ReplyDelete
  11. Mwenyezi Mungu atawasahilishia ndugu zetu na mitihani yake Allah. Na Mwenyezi Mungu atakupeni vilivyobora kuliko mlivyovikosa Insha'Allah. Kuweni waja wenye subra ndugu zangu.

    ReplyDelete
  12. Mungu wanusuru ndg zetu na hili janga..dah poleni sana waTz

    ReplyDelete
  13. polen ndugu zangu wa dar jamani mungu awalinde ee mungu waone waja wako katika hiki kipindi kigumu

    ReplyDelete
  14. Mamlaka ya hali ya hewa ilishatangaza siku nyingi ila wananchini wabishi.
    Kwa hapo hata siwezi walaumu serikali, walishaambiwa wahame kwenye mabonde miaka mingi sana, hawataki. Wanataka walipwe fidia na kupewa viwanja maeneo mengine kwani serikali ndio iliwapimia hapo mabondeni.
    Waulize kama hata wana hati za hivyo viwanja adi kusema walipwe fidia..

    ReplyDelete
  15. Kutoka maisha ya nyumbani hadi makazi ya muda Darasani ktk Shule kwa wahanga wa mafuriko,,,kuyamudu mabadiliko kugumu, bahati watoto shule zimefungwa wapo likizo,,,ile kwaaa unatoka na taulo kiunoni kwenda kuoga watoto wapo ktk darasa wanasoma!

    ReplyDelete
  16. MADHARA YA BAADAE NI KIPINDUPINDU MAJI SIO SALAMA SERIKALI KAZI HIO.

    ReplyDelete
  17. hivi sasa jamani walio bomokewa na nyumba zao,ndio tena watabaki mitaani au serikali hua inamipango ya kuwasaidia makazi mapya?maana kwa mtanzania wa kawaida aliye weza kujibana akajenga banda lake miaka hiyo,sidhani kama ni rahisi kurudia tena ujenzi miaka hii,maisha yenyewe miaka 50 ya uhuru mpaka chakula imekua ngumu kununua kwa bei zilivyo panda!! Poleni sana waathirika wa mafuriko,Mungu yu pamoja nanyi,kweli miaka 50 ya uhuru imekuja na mengi.

    ReplyDelete
  18. Mdau wa 14 hapo juu, Duhh inakuwa ni kumbukumbu mfano mtu Mhanga wa mafuriko unapangiwa makazi ya muda ktk Darasa la Shule halisi uliyosoma miaka takribani 30 na ushee iliyopita huko nyuma????,,,tofauti inakuwa ni kuwa mwanafunzi wa umri mkubwa safari hii unakuwa na familia yako ahh ndio maisha,,, maiti haichagui KABURI!

    ReplyDelete
  19. HAPO HAPOOOO,,,,,,MBINU YA KUHAMISHA MAKAZI HARAMU MABONDENI, JANGWANI KIGOGO MTO MSIMBAZI NA KWINGINEKO!.

    Muda huu hao wakazi haramu wakiwa ktk makazi ya muda ya Msaada wa Serikali ktk madarasa ya Shule, KABLA MAJI HAYAJATOKA HUKO MAKWAO, WASIJE WAKARUDI MAKWAO TENA,,,ILI WAPATE AKILI YA MAKAZI MAPYA YANAYOKUBALIKA,,,GREDA IPITISHWE HARAKA KUBOMOA!

    ReplyDelete
  20. TANZANIA NCHI YANGU NAKUPENDA KWA MOYO WOTE.....

    TANZANIA BADO TUPO NYUMA SANA TUACHANE KABISA NA KUJISIFU ETI TUNA MAENDELEO

    POLISI WANAFIKA ENEO LA TUKIO HUKU WAMESHIKA MABUNDUKI NA MABOMU YA MACHOZI ETI WANALINDA RAIA NA MALI ZAO

    HAO PILISI WAMEFIKA SEHEMU KAMA HIYO INATAKIWA WAONYESHE UTU WAO NA SIO KUSHIKA MIBUNDUKI KAMA KUNA VITA

    WANATAKIWA WASHIKE VIFAA VYA KUOKOLEA NA KAMA NI ULINZI BASI WAUFANYE KIUSTAARABU NA SIO KUJIONYESHA KAMA WANA UGOMVI NA RAIA

    NJIA ZA MAJI TAKA NI NDOGO MNO KIASI KWAMBA LIKITOKEA LA KUTOKEA TUTAKUJA KUPOTEZA HIYO NCHI

    NA WATU NI WENGI SANA HUKO MJINI KIASI KWAMBA INATISHIA HIVI KWELI WATU WANAOFIKA MJINI KILA SIKU NA KURUDI MAKWAO KILA JIONI NI KIASI KANA KWAMBA WANASHANGAZA

    YOTE NI SERIKALI MBOVU AMBAYO IMEJENGA KILA HUDUMA YA KIJAMII KUPATIKANA MJINI WAMESHINDWA KUPANUA MJI KWA KUJENGA VITUO VYA HUDUMA YA JAMII KWENYE KILA KITONGOJI

    NI WAKATI WA SERIKALI KUBADILIKA NA KUANZA UJENZI WA KISASA ILI KUPUNGUZA MSONGAMANO WA HUKO MJINI

    MAGARI UTATESA HAYAENDI YAMEUNGANA UTASEMA NYORORO KUTOKANA NA MSONGAMANO WA MJINI

    CHONDE CHONDE SERIKALI TUJENGEENI VITUO VYA HUDUMA KWA JAMII KWENYE VITONGOJI VYETU ILI TUWEZE KUPATA HUDUMA BILA KUFIKA MJINI.

    POLENI SANA WAFIWA NA WALE WALIOPATWA NA SHIDA ZOTE ZA MAFULIKO HAYO.

    MUNGU IBARIKI TANZNAIA DUMISHA AMANI NA UMOJA.

    ReplyDelete
  21. Mungu Baba, tunakuomba uinusuru nchi yetu Tanzania kwenye balaa hili la mafuriko hasa ukizingatia kwamba hatuna uzoefu wa maafa kama haya. Baba tunaziweka mikononi mwako roho za wahanga waliopoteza maisha yao kutokana na mafuriko haya na pia uwape hekima viongozi wetu kama ulivyompa Mfalme Solomon ili waweze kuwa na busara ya kulitatua tatizo hili kwa ufanisi na kuwajali kwa hali na mali wote waliopatwa na maafa haya, tukizidi kukuomba na kukushukuru kwa jina la mwanao Yesu Kristo. Amen.

    ReplyDelete
  22. Naona Ras Makunja juu ya farasi? kweli mambo yao sio mabaya

    ReplyDelete
  23. akina ras makunja wapo kazini sasa mbona magitaa kiunoni kulikoni?

    ReplyDelete
  24. Mkiona watu wanakaa Mbagala mnawaona washamba na wakulima... haya sasa Msaada wa Serikali wa makazi ya muda kukaa maisha ya Shule ktk Madarasa uzeeni ndio ujanja?

    ReplyDelete
  25. Huyo farasi mpeni lishe

    ReplyDelete
  26. Askari mpaka mabomu ya machozi ya nini?. Je farasi analishwa kweli amekonda!

    ReplyDelete
  27. typical ya askari wetu wa Tanzania hata kwenye maafa haweajui kuongea kidiplomasia. Wao ni virungu na bunduki tu mkononi.

    Watu wamefikwa na maafa, wamepoteza mali zao na hata ndugu zao, wanachihitaji ni msaada, uongozi na moyo wa huruma kutoka katika vyombo vya serikali. Hivi kweli kulikuwa na haja ya askari kuchukua bunduki na virungu? Ona picha hiyo boti inashushwa ni askari mmoja tu anaesaidia wengine wako wapi?

    Na sio kama kumezuka wimbi la wizi, hasha!!!!!

    ReplyDelete
  28. Huyu afande na bunduki tena kulikoni jamani si mafuriko tuu?? I hate seeing these guns on people's hands! Watanzania hatujazoea vitu hivi sana sana mabomu ya machozi kaaaaaaaaaaaaa.

    ReplyDelete
  29. Ni kweli walibaki mabondeni lakini adha ilipotokea tulikuwa tayari au tulibahatisha tu kama kawaida yetu? Tunahitaji kuwa na taratibu za kukabili majanga kwa haraka na kwa kutumia utaalamu unaojulikana unafanya kazi. Kila janga kwetu ni matatizo makubwa sana. Pia janga ndio linalotuonyesha wote sie ni binadamu ila kwa walionacho au wenye majina suluhu ni haraka na rahisi zaidi. NCHI YANGU TANZANIA je lipi lingine lifanyike?

    ReplyDelete
  30. hii picha ya mwisho mi naogopa hii boti/mtumbwi ilivojaza watu. sasa hapo mtumbwi ungepinduka kati kati ya maji mengi si ndo ingekuwa shughuli nyingine!

    ReplyDelete
  31. POLENI NDUGU ZANGU WAFIWA NA WAANHGA KTK JANGA ILI,ILA NAPENDA KUITUPIA LAWAMA KIDOGO OFIC ZETU ZA IDARA YA HALI YA HEWA,HAWASEMI MAPEMA WANASUBIRI HARI ITOKEE NDIO WAPATE SABABU YA KUJIFANYA WAO NDIO WATAALAM WA KUTABIRI,HII SIO SAWA KWA KWELI.ALAFU NAITUPIA KIDOGO MAMLAKA HUSIKA YA UOKOAJI KWA KUCHELEWA KUFIKA ENEO LA TUKIO HADI KUSABABISHA ONGEZEKO LA VIFO.NDUGU ZANGU NI JAMBO LA KITAIFA HILI TUNAOMBA TUWE PAMOJA KWA KUWACHANGIA NDUGU ZETU WAISHI KAMA SISI KWA SASA KTK KIPINDI HIKI KIGUMU.
    Ni mimi Cloud John wa Ubungo DSM.
    Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...