Mshambuliaji wa Kilimanjaro Stars, Mrisho Ngasa akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Uganda, Godfrey Walusimbi katika mchezo wa Nusu Fainali ya michuano ya Kombe la Chalenji uliofanyika jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaama.Katika mchezo huo timu ya Uganda imetoka kifua mbele kwa kuinyuka timu ya Tanzania goli 3-1,kufuatia matokeo hayo timu ya Uganda inatinga fainali na itapapambana na timu ya Rwanda,utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa,siku ya jumamosi. (Picha na Francis Dande).
Baadhi ya Mashabiki  mbalimbali waliofika kushuhudia nusu fainali ya michuano ya CECAFA Tusker Challenge cup 2011,iliofanyika jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa,jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

 1. Advocate JashaDecember 08, 2011

  KATIKA UONGOZI HUU CHINI YA CHAMA TAWALA CCM KUPATA MAFANIKIO KATIKA SEKTA YOYOTE IKIWEMO MICHEZO NI NDOTO YA MWENDAWAZIMU.WALIKUA WANADAI WASHANGIRIWE WASHANGIRIWE KWA LIPI.TUJITOE KATIKA MASHINDANO YOTE YA NJE TUSUBIRI UTAWALA MPYA MUNGU IBARIKI TANZANIA

  ReplyDelete
 2. Makelele ya Julio yako wapi? Sasa asubiri kipigo kingine toka kwa Sudan. Takwimu zinajisemea zenyewe mmenyukwa na Rwanda, Uganda na Zimbabwe. Mkawafunga Djibouti wanaofungwa na kila timu. Mkabahatisha kwa Rwanda. Na sasa mnakwenda kudinywa na Sudan. Kazi ya ukocha ni profession siyo ya kubahatisha. Micho hakukaa na Rwanda kwa muda mrefu lakini kashinda mechi zote. Williamson kila mwaka anafika fainali. Poulsen alikaa na stars muda mfupi akachukua kombe. Massimo alikuwa hafungwi kama hivi. Tumechoka na visingizio vingi kutoka kwa makocha wazawa kazi hii bado hawana utaalamu wa kutosha. Tuiombe serikali ianze kusomesha makocha katika vyuo vikuu. Hii sio kazi ya kubahatisha!

  ReplyDelete
 3. As long as mna wachezaji dizaini ya Ngassa TZ kamwe hamtoshinda mashindano ya kimataifa. Kumbukeni, mpira ni kipaji na si uchawi. Wachezaji wa TZ wameweka uchawi mbele badala ya kujituma, yaani kama vile Simba na Yanga. Michuzi kumbuka, kubania ukweli ni kuficha magonjwa na kama utaficha maoni haya basi na wewe ni wale wale mnaobeza ujinga wa wachezaji wa TZ na kuwafanya wasikue kimpira. Wachezaji wa Bongo ni wachawi na ndiyo maana hawana mbinu za uchezaji kwani hawafundishiki hata.

  ReplyDelete
 4. Hakuna mchezaji hapo wapeni kanga wachezee taaraabu, mbona wa bongo mwaji─▒tia ugonjwa wa moyo?,Rwanda?,Burundi?,Zimbabwe? Wa2 na shida zao wanatutesa kama cc ,tungekua kama wao na shida c ndo tungeolewa kabisa?,m tz unaweza nn?,hata kesho Rwanda,Burundi,Zimbwabwe akiamua kucheza taarabu watatushinda, kubalini ushoga kwani hakuna mume tz wote ni kama madenu taka uctake? kazi kuiga wenzenu bila manufaa pumbavu

  ReplyDelete
 5. Michuzi naomba utoe kombe kwa huyu mdau wa Thu Dec 08, 08:34:00 PM 2011 kwani aliyoyasema ni ukweli mtupu. Uchawi na kipaji haviingiliani kamwe!

  ReplyDelete
 6. Hii mechi Kilimanjaro Stars na The Uganda Cranes,,,kimtazamo wa ki Uchawi (MARA NYINGI MTAZAMO WA KI UCHAWI UNAKUWA NI WA KINYUME CHAKE)

  KILIMANJARO STARS-3 (Winners)
  UGANDA CRANES-1 (Lossers)

  kama ilivyo imani ya wachezaji wetu,,,tumefika fainali na matokeo tumewafunga Uganda Cranes mabao ma 3 wao wametufunga 1,,,hivyo tumeshinda na tumechukua KOMBE LA TUSKER!

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...