Kiongozi wa timu ya mpira wa miguu ya mlale JKT ya ruvuma,Luten Kulwa Msimbe (kushoto) akipokea moja ya mipira 11 kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu ofisini kwa mkuu wa mkoa huyo
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu (wa pili kushoto) akieleza mambo ya kuzingatia katika michezo kwa kiongozi wa timu ya Mlale JKT,Luten Kulwa Msimbe (kushoto) kabla ya kumkabidhi mipira 11 ili iweze kuwasaidia katika michezo ya ya ligi daraja la kwanza taifa inayotarajia kuanza mwezi ujao
Kiongozi wa timu ya Mlale JKT ya Ruvuma Luten Kulwa Msimbe (kushoto) akitoa shukurani kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu baada ya kupokea msaada wa mipira 11 iliyotolewa na mkuu wa mkoa huyo.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said mwambungu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya mlale jkt baada ya kukabidhi mipira 11 kwa timu hiyo.Picha na Muhidin Amri wa Globu ya Jamii,Ruvuma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. ila jamaa mwenye simu hayuko kiofisi kabisa yaani uko ofisini kwa muheshimiwa halafu wewe uko na simu huna hata habari na kinachoendelea

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...