Na Woinde Shizza,Arusha

Msaniii wa muziki wa kizazi kipya (bongo Flava) Abeli Motika alimaarufu kwa jina la Mr .Ebbo mwenye umri wa miaka 37 amefariki dunia mkoani hapa.

Msanii huyo amefariki dunia juzi saa nne usiku katika hospitali ya dream seminari inayomilikiw ana kanisa katoliki lililopo Usa river Wilalyani Arumeru mkoani hapa.

Baba wa marehemu wa msanii huyo Olais Loshila Motika alisema kuwa marehemu Mr.Ebbo alifariki dunia jana usiku kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya damu.

Alisema kuwa marehemu alisumbuliwa na ugonjwa huo kwa zaidi ya miezi tisa ambapo kabla ya kuumwa alikuwa anaishi mkoani Tanga na alipozidiwa aliletwa mkoani hapa kwa ajili ya matibabu na aliwahi kutibiwa katika hospitali nyingi ikiwemo Mounti meru ,KCMC pamoja na hospitali ya kanisa ya seliani.

Aidha alibainisha kuwa marehemu Mr.Ebbo ameacha mjane na watoto watatu na anatarajiwa kuzikwa December tano katika makaburi ya nyumbani kwao Masai Camp Olorieni ndani ya manispaa ya mkoa wa Arusha.

Loshika alisema kuwa wamepokea msimba huu kwa masikitiko makubwa sana kwani marehemu alikuwa anategemewa na familia hiyo pamoja alijuwa ni kioo cha jamii hivyo familia hiyo imepokea msiba huo kwa masikitiko makubwa na mwenyezi mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.


HISTORIA FUPI YA MR. EBBO

Jina kamili ni Abel Loshilaa Motika a.k.a Mr Ebbo, azaliwa tarehe 26 may 1974 jijini Arusha. Elimu ya msingi aliianza mwaka 1982 katika shule ya msingi kijenge baadae mwaka 1984 aliamia tanga na kuendelea na masomo katika shule ya msingi nguvumali. Nakumaliza elimu ya msingi mwaka 1988.

Alijiunga na elimu ya sekondari katika shule iitwayo jumuiya sec school. iliyopo jijini Tanga. Alimaliza elimu ya sekondari mwaka 1992. Na kwa kipindi hicho chote wakati yuko shuleni alikuwa akiimba kwaya kanisani. Kwenye kanisa la kisosora (lutheran church) ambapo ilimsaidia sana kujifunza muziki.

Alirudi Arusha mwaka 1993  na kubahatika kupata kazi kwenye night club ambapo alitumia mishahara yake kurekodi nyimbo ambazo hazikumpa mafanikio yeyote isipokuwa zilimuweka katika ramani ya muziki. Baada ya hapo alifanya kazi ya kuandaa matangazo ya biashara na vipindi vya redio kwenye studio iliyojulikana kama Supreme recording studios iliyopo mjini Arusha. kipindi hicho kilijulikana kama “Mambo gani haya” Alirekodi nyimbo kadhaa ambazo hazikumpa mafanikio yoyote kwa mara nyingine na hali hiyo ikamkatisha tamaa kabisa.

Baadae mwaka 1995 Alipata kazi ya kuuza nguo kwenye duka la JJ BLACK lililopo jijini Arusha. Mwaka 1999 Aliamua kurudi jijini Tanga na akafanikiwa kufunga ndoa na kubahatika kupata watoto wawili Ashley na baadaye Alicia. Alianza kazi ya uwakala wa kuuza magazeti mwaka 2000.

Kazi ambayo pia haikumletea mafanikio yeyote makubwa kama alivyokuwa anatarajia, baadaye mwaka 2001 akaanzisha biashara ya kuuza mchele kwa jumla ambayo pia haikuwa na mafanikio aliyoyatarajia. kipindi hicho chote alipokuwa Tanga alifahamiana na Wasanii wa Muziki wa Bongo Fleva,Professor J na Wagosi wa kaya, na wao pia walijua kuwa Mr. Ebbo ni Msanii asilia. Baadae alijiunga na chuo cha kozi za computer jijini tanga.

Wagosi waliporekodi wimbo wao wa Tanga kunani ,Mr Ebbo alihamasika kurudi tena kwenye Muziki na ndipo alipoandika wimbo wa kwanza wa "Mimi Mmasai mwaka 2002". Wimbo huo ukatambulisha Album yake ya kwanza kisha wimbo wa “ Fahari yako “ Baadaye mwaka 2003 akafungua studio ( MOTIKA RECORDS) Ambayo ilifanikiwa kuwatambulisha wasanii kama, Danny Msimamo, Dr Leader, Mo-Kweli, na wengineo wengi , wote hawa aliwaproduce yeye mwenyewe. kama producer wa MOTIKA RECORDS.

Mwaka 2003 akarekodi Album yake ya pili iliyojulikana kwa jina la Bado Ijasungumiswa. Mwaka 2004 akarekodi Album yake ya tatu iliyoitwa Kazi gani. Mwaka 2005 akarekodi Album ya nne iliyoitwa Alibamu. Mwaka 2006 akarekodi Album ya tano inayoitwa Kamongo.

ambayo ndio albamu ya mwisho kwa uhai wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 40 mpaka sasa

  1. May you Rest In Peace Mr. Ebbo. bll

    ReplyDelete
  2. Richard jackson M.December 02, 2011

    R.I.P Mr. ebbo the unique icon of african music. As one of your die hard fan we will cherish your music forever..... condolences to your wife and children ...

    ReplyDelete
  3. Dah! Inatia uchungu sana lkn ndo mwenyezi mungu kasha amua iwe hivo. Poleni sana wafiwa

    ReplyDelete
  4. Maskini jamani. RIP. tutamiss nyimbo zake.

    ReplyDelete
  5. Michuzi hebu kuwa makini na machapisho yako usije ukachafua hali ya hewa kama ulivyo tahadharisha hapo juu. Mr. Ebo amefia hapa hapa Arusha nyumbani kwao sekei na sii tanga kama ulivyoandika hapo. Mipango ya mazishi inafanyika hapa hapa sekei kwao ila bado kuna utata azikwe arusha ama tanga. Chunguza kwanza utabaini usikurupukee

    ReplyDelete
  6. masikini! Mungu aiweke roho yake mahala pema peponi amina.

    ReplyDelete
  7. Pole nyingi kwa familia yake,wasanii na watanzania wote kwa ujumla.Hakikika mmoja kati ya watu waliokuwa wanaelimisha jamii kwa njia ya nyimbo ameondoka.

    ReplyDelete
  8. its a sad sad for all Tanzanians and the music industry Mr.Ebbo was a legend and his music transformed the bongo music which enspires us all.

    ReplyDelete
  9. RIP Mr Ebbo!

    ReplyDelete
  10. RIP MR EBBO!!!!

    ReplyDelete
  11. Ankal tuelewe lipi Ebo kafia nyumbani kwao Arusha na vyombo vingine vya habari vimesema kaugua kwa muda mrefu na kafia Arusha wewe unasema kaugua muda mfupi kafia tanga tuelewe lipi nyie kama watoa taarifa kwa uma hata ukibania utaisoma kimya kimya na utaifanyia kazi

    ReplyDelete
  12. RIP Mr. Ebo

    ReplyDelete
  13. Tunamuona Mwenyezi Mungu mwenye huruma amuweke mahali pema peponi, kwa hakina kila nafsi itaonja mauti, mwenzetu ametangulia tu, tulitokana na udondo tutarudi kwenye udongo.

    ReplyDelete
  14. Mimi na familia yangu tunatoa pole kwa msiba wa huyu mtunzi mahiri na muimbaji ambae tulimshabikia sana alikuwa anaelimisha sana na pia kuturubudisha(kutuburudisha. Sina hakika kama jamii ilimuelewa ujumbe aliokuwa akiwatolea, kuna mengi sana mazuri wanamuziki wa kibongo wanatakiwa wajifunze kwake na si kuimba mapenzi,ngono na upuuzi tu daima..RIP Mr, Ebbo.

    ReplyDelete
  15. Sad news. RIP Mr Ebbo. Anony

    ReplyDelete
  16. Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu Mr Ebbo,,, Amina

    ReplyDelete
  17. POLENI KWA MSIBA KWA NDUGU NA MARAFIKI WA MAREHEMU,MWENYEZI MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI/

    MDAU VUMBI DEKULA SWEDEN

    ReplyDelete
  18. Haki ya nane. kweli chema Hakidumu.Umeondoka Upesi" gone so soon" Mungu aiweke pema Roho Yake Mr. Ebbo

    ReplyDelete
  19. Inna lillahi ....

    ReplyDelete
  20. Mwenyezi Mungu ilaze roho ya marehemu pema peponi. Amen.

    ReplyDelete
  21. Mwenyezi Mungu ailaze ROHO yake mahali pema peponi....Amin

    ReplyDelete
  22. RIP Mr. Ebbo. You were a fighter and struggled to make things happen but you left us too soon.May you rest in eternal peace.

    ReplyDelete
  23. R I P Mr Ebbo, tumepoteza nguzo ktk muziki wetu wa kizazi kipya, tutakukumbuka daima milele, mungu ailaze roho yako mahali pema peponi, Amen. Mdau Uk.

    ReplyDelete
  24. Duh, nimepokea taarifa hii kwa mshtuko na huzuni sana. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu peponi. Amina.

    ReplyDelete
  25. RIP Mr. EBBO..

    ReplyDelete
  26. Duuuuuh tutam-miss kinoma!!

    ReplyDelete
  27. RIP jamaa aliwawakilisha wamaasai vizuri sana

    ReplyDelete
  28. SOOO SAD, inasikitisha sana kusikia habari hii.
    Kweli maisha ni mafupi sana kuliko tunavyodhania wakati mwingine.
    Mungu aiweke roho yake pema peponi, Amen.

    ReplyDelete
  29. Ooh mr Ebo may God Rest your soul in peace. Nimehuzunishwa sana na kifo chake. Historia yake inaonyesha alikuwa mtafutaji sana. Poleni wote mliopatwa na huzuni hii kubwa

    ReplyDelete
  30. HAKUNA HATA ALOITIKIA AEEN,AAMEEEN IJAPOKUA ALIKUA ANAMTANIA MUNGU KWENYE NYIMBO ZAKE,MUNGU AMLAZE PEMA HAKIKA SISI NI WA MUNGU NA KWAKE TUTAREJEA.E MUNGU TUPE MWISHO MWEMA,AMEEN

    ReplyDelete
  31. Hili ni pigo kubwa kwa sote watanzania,hivyo tusiweke utani au mzaha wowote ule.Michuzi ni binadamu,kukosea ni jambo la kibinadamu

    Mungu ailaze roho ya Mr.Ebo mahala pema..Amen

    ReplyDelete
  32. Aliwakilisha vazi la kimasai vilivyo na sasa limerudi kua fashion.R.I.P MR EBBO

    ReplyDelete
  33. RIP Mr. Ebbo ama kwa hakika wanamuziki wote nchini wameondokewa na mtu muhimi sana. Jamii nzima tumeondokewa na mwalimu aliyetufundisha kwa nyimbo zake nzuri za kuchekesha, kufurahisha na tulizipenda sana. Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana Libarikiwe! Amen

    ReplyDelete
  34. REST IN PEACE TO THE ETERNAL PLACE>>>>>>ABEL LOSHILAA MOTIKA (MR.Ebbo)!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    Forever!

    ReplyDelete
  35. Mimi Maasai bana, mimi masaai, nadumisa mila ile wengine walisasindwa!

    Mimi Maasai bana, mimi maasai,
    Maisa ya mujini sasa kilabu soda magadi mingi hakuna sukari!

    R.I.P Mmaasai!

    ReplyDelete
  36. Tulikupenda Maasai wetu,na ucheshi wako ukatupunguzia mawazo.Njia uliyoipita nasi twaelekea huko huko,ulichofanya ni kututangulia tu.Watumbuize na wao utakaowapata huko.Mungu awe nawe Maasai wa Tanga.Amin.

    ReplyDelete
  37. From Beijing - China.
    Kwa kweli nimeshtushwa na kifo cha Mr. Ebbo. Nawaombea faraja familia, ndugu, marafiki na washabiki wa Mr. Ebbo katika kipindi hiki cha majonzi. Pumziko la milele umpe ee Bwana na mwanga wa milele umwangazie. RIP MR. EBBO.

    ReplyDelete
  38. Alikuwa kijana wa mfano, alijichanganya na watu, kuna vitu vya kuigwa kwa huyu jamaa, nakumbukuka hakuwa anakosa ibada ya kwanza pale kisosora. Kifo ni njia ya kila mmoja wetu, swali ni Je tuko tayari kukutana na aliyetuumba?

    ReplyDelete
  39. Poleni sana wafiwa.Hii taarifa inahuzunisha.Katika dunia ya sasa ambapo mataifa yanapoteza uasilia,msanii kama Mr Ebbo ni chombo muhimu kwa jamii.Napenda kutoa mchango wa rambirambi. Email ngu ni bigyosam@yahoo.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...