Pichani kulia ni Meneja wa kinywaji cha Malta Guinness Bw. Maurice Njowoka akizungumza na Wanahabari (hawapo pichani),mapema leo asubuhi kuhusiana Kampuni ya bia Serengeti (SBL) kupitia kinywaji chake kisicho na kilevi cha Malta Guinness kudhamini siku moja ya mazoezi ya viungo itakayoitwa ‘MALTA GUINNESS GOODNESS DAY’ itakayofanyika katika viwanja vya posta kijitonyama jijini Dar es Salaam siku ya jumamosi kuanzia saa 12:30 asubuhi hadi saa 4 asubuhi.


Mratibu wa tamasha hilo la ‘MALTA GUINNESS GOODNESS DAY’,Bw.Sas pichani shoto akionyesha kinywaji cha ‘MALTA GUINNESS  ambacho kimedhamini tamasha hilo la siku moja.

Bw,Njowoka amesema kuwa kampuni hiyo imedhamini siku hiyo maalum kama sehemu mojawapo ya kuihamasisha jamii kujijengea tabia ya kufanya mazoezi ili kuboresha na kuimarisha afya zao,amesema na kuongeza kuwa kampuni imekuwa na desturi ya kutoa huduma mbalimbali kwa jamii ya Tanzania kama sehemu ya mchango wake katika kuisaidia serikali katika kupambana na umasikini na maradhi na kujiletea maendeleo bora kwa watanzania wenye afya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...