By US Blogger

Ankal Michuzi, naomba unipe nafasi kuandika kidogo juu ya mambo niliyokumbana nayo ili wa-Tanzania hasa waishio nje ya nchi waelewe hali halisi jinsi inavyosikitisha na kukatisha tama.

Viongozi wamekuwa na safari za kila siku na wamekuwa wakihalalisha gharama za safari zao ya kwamba wanahimiza uwekezaji na sisi wana diaspora tumekuwa tukiambiwa tujenge nchi kwani hakuna tuliyemuwachia nchi atujengee. Kwa heshima na taadhima baadhi yetu tukaitikia wito. Mimi nikajikusanya na wenzangu ili tuanzishe mradi ambao ulikwa na malengo ya sisi wanasiriamali tupate faida kwa ajili ya juhudi zatu na pia wenzetu wa nyumbani wapate ajira. Tulifanya utafiti wa kisayansi na mtu yoyote amabaye angeona business plan yetu na ni mtalamu wa biashara angeamini kabisa tumejitahidi. Biashara yetu ilikuwa ijishughulishe na ununuzi wa bidhaa kutoka mbalimbali na kupeleka nyumbani.

Wakati tunasafarisha mzigo tulishafanya utafiti wa viwango vya kodi, TRA wenyewe walishatupa makadirio ya kodi kutikana na invoices zetu. Baada ya mzigo kufika Dar es Salaam biashara yote iligeuka na kuwa janga, kwanza TRA  walitupatia viwango vya kodi kama jinsi tulivyotarajia, baada ya siku 2-3 clearing agent wetu anatuambia ya kwamba wame ‘uplift’ thamani na hivyo kodi inaongezeka kwa asilimia 100, tukahoji kwa nini iwe hivyo tukaambiwa ya kwamba tathmini ya kwanza hailingani na ‘minimum values’ za TRA wakati ni haohao TRA ndio waliotoa makadirio ya kodi ya awali (preliminary). Agent wetu anasema hakuna namna kwani hata mtu uki appeal inachukua muda mrefu, nilivyojaribu kuangalia online namna yak u appeal harakaharaka hakuna maelezo yoyote, nikajaribu kuwasiliana na watumishi wa TRA ninaowafahamu nao pia wakasema kama kuna mtu ame uplift hakuna namna. Sasa kama bidhaa inatarajiwa kupatya faida ya kama 20% utawezaje kupata faida endapo kodi inapandishwa kimchezomchezo.

Tukasema haya maji tumeyavulia nguo sasa tunaoge, tukakubali kulipa hiyo kodi. Kam hiyo haitoshi wakati wa kukagua hakuna lolote jipya lakini mkaguzi naye akasema anaongeza kodi. Pia tulikuwa na bidhaa chache amabazo thamani yake haizidi hata $150, bidhaa hizo zilikuwa kama sample kwa wateja wetu kwa hiyo hatukuziweka kwenye invoice, jamaa wa TRA wakadai hilo ni kosa na adhabu yake ni dola $10,000. Hawa jamaa hawana hata ubinaadamu, wao lengo lao ni kukomoa tu na kujifanya Miungu watu. Wana ubinafsi wa hali ya juu na wala hawajali ya kwamba wakimfilishi mjasiriamali atawacha kufanya biashara na wao mapato yatapungua, wanaangalia wakomoe leo bila ya kujali mapato ya kesho. Yote haya wanayafanya kwa lengo la kushawishi rushwa na online hakuna namna ya kuwasiliana harakaharaka na wakubwa ili waingilie kati. Matokeo yake ni kwamba tumejikuta tumelipa asilimia 500 ya makodi kulinganisha na mahesabu yetu wakati timu yetu ya biashara ina mpaka wahasibu wanaofanya kazi marekani katika taasisi muhimu. Yaani elimu ya mtu haina thamani yoyote katika kufanya biashara Tanzania, ili ufanikiwe inabidi uwe mtoa rushwa vinginevyo ni kupoteza muda. Nimewasiliana na baadhi wa wafanyabiashara waliofanikiwa na kuwasimulia na wanasema hayo ndio mambo ya kawaida na kwamba ‘huku hakuna formula’. Sasa nchi ambayo mambo yanakwenda kijanjajanja sisi diaspora tutawezaje kuchangia maendeleo kama TRA kazi yao ni kukomoa tu watu. Nimejikuta nalipa kodi zaidi ya hata gharama za kununulia bidhaa.

Mimi nashauri viongozi waache mara moja kushawishi wajasiriamali kuwekeza nchini na kupoteza hela za safari za nchi mpaka hapo vyombo husika vitakapokuwa tayari kufanya kazi na diaspora.

Katika nchi za ulaya na marekani ukinunua chochote hata kama ni gari ama nyumba unapata makadirio ya kodi na wakati wa kulipa unalipa mpaka cents kama jinsi ilivyo makadirio, kufanya hivyo hakuhitaji fedha kwa hiyo umasikini sio sababu, tatizo letu ni kwamba hakuna utamaduni wa uadilifu na watumishi wa Serikali wameweka ubinafsi mbele na uwajibikaji pia hakuna.

Leo tumesoma ya kwamba Serikali inataka kukopa fedha kwa ajili ya kuendesha shughuli zake, kama TRA kazi yao ni kuuwa biashara kwa nini Serikali isifilisike?

Ujanja unaofanywa na TRA sio kubadilisha  rate ya kodi kwani rate inapangwa na sheria, wanapowakaba watu ni kwenye thamani ya mali, nunua mali ya $1 lakini ikifika kwenye kupiga hesabu za kodi wao wanakwambia tunaanzia na $5 na unajikuta unalipa mara tano ya ulichotegemea ama unalazimika kuacha mzigo wago uwe mali ya TRA ili wapige mnada na hapo wanashirikiana na marafiki zao kupata makontena ya watu kwa bei ya kuokota wakati mwenye mali ameshakula hasara

Ushauri wangu wa bure kwa wajasiriamali wanaoishi nje ya nchi hasa wale ambao wana matatizo ya moyo ama blood pressure ni kwamba kama kama rushwa kwako ni mwiko na ni dhambi usipoteze muda wako na biashara za Tanzania zinazohusu kuingiza bidhaa, TRA watakuliza na wanaweza kukuua kwa heart attack.

Usblogger11@gmail.com

 





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 74 mpaka sasa

  1. Hiyo ndio hali halisi ya uingizaji bidhaa, jamaa wa TRA wanafaidika kwa kukomoa wafanyabiashara na hawana hata chembe ya ubinadamu wao wanatizama mifuko yao wala hiyo uplifted usifikiri inakwenda serikali bali hiyo ni kwa ajili yao. makaratasi wanayaandika upya na wanalipa serikali ile bei ya mwanzo waliokuambia kilichozidi ni makato yao. Tena usiombe ukakutana na wale wamama ndio ujue utajuta kuingiza mzigo. mie kidogo niache RaV 4 yangu pale lakini ndio hivyo. Jamaa wametengeneza mazingira ya rushwa na kudhulumu watu. wafanyabiashara wadogo wala usiingize mzigo pale utaweza kujinyonga. watu wengi washajuta..hii serikali haina macho wala masikio kwasababu tushalalamika sana lakini hakuna mabadiliko..au labda na sisi tuanze kuchukua sheria mikononi...

    ReplyDelete
  2. Hii nchi huwezi kuisaidia kwani wenye dhamana ya uongozi hawana dhamira halisi ya kuisaidia nchi.
    Sisi wafanyabishara tunalazimika kudangaya sana kwa sababu kutokana na uelewa mdogo wa TRA staffs, tunakadiriwa "annual turnover" kama gross sale badala ya kukadiriwa fidia. So hata mtaji wetu unakatwa kodi ya mapato. Hii ndo sababu kubwa kila mtu anakwepa kodi kwani kulipa kodi sahihi wanavyotaka inabidi ukubali kufilisika.

    ReplyDelete
  3. Nimegundukua kitu kimoja hapa TZ. Mtu akisema ukweli kuhusu nchi yetu ilivyooza watu (baadhi) wanakuwa na hasira na kuanza kuongea maneno ya ajabu. Juzi hapa kuna jamaa mmoja alitoa maoni yake juu ya customer service TZ watu wakabisha tena kwa hasira wakati aliyoyazungumza yule jamaa ni ya ukweli kabisa na yapo hapa TZ tunayaona kila siku. Sitashangaa na tuhuma hizi alizotoa USblogge kupingwa na baadhi ya watu wasiopenda kuambiwa ukweli. TZ has to change for real, Kikwete inabidi awe dikteta kubadilisha hii nchi, tunakwisha jamani na hizi dhuluma za kila kukicha. Kikwete uko wapi babaaaa?

    ReplyDelete
  4. Ndiyo maana bongo haiendelei!

    ReplyDelete
  5. Mdau, nakubaliana na wewe 500%.

    1. Mimi baada ya kutua tu ng'ambo nikafanya shopping ya zawadi kadhaa na kuwatumia watu wa nyumbani. Cha ajabu, nililipa kodi mara nne ya gharama nilizotumia kununua zawadi zenyewe. Toka wakati huo nimeacha kabisa kutuma zawadi nyumbani. Cha ajabu, waafrika wengine wanashangaa inakuwaje nalipa zaidi kiasi hicho wakati wao wakituma zawadi makwao ni kupeta tu.

    2. Baada ya kuji-establish huku na kujenga mtandao na watu wenye akili na uwezo, nikawashawishi tukawekeze Tanzania. Jamaa wakakubali na tulitimiza taratibu zote. Kasheshe likaja kwa TRA, wazungu walikiri hawajawahi kufikiria kunaweza kuwa na ushenzi wa namna hiyo duniani katika uwigo wa uwekezaji. Mimi mwenyewe, japo nilihisi kungekuwa na mambo hayo, sikudhani yangekuwa kiasi hiko. Tuligairi kuwekeza bongo, na sasa biashara zetu zinashamiri vilivyo nchini Botswana na Kenya, mwakani tunafungua matawi Uganda na Zambia. Ila Tanzania marufuku, kamwe!!! Na nimekuwa balozi mzuri sana kuwashauri watu huku wajiulize mara kumi kumi kabla ya kuamua kwenda na kuwekeza Tanzania. Kwa ufupi, Tanzania stori nyingiiii, ila vitendo ni vya kikatili kupitiliza, hata mkoloni asingetubana namna hii.

    3. Mwaka jana mmoja wa wakurugenzi wenzangu alifunga safari kwenda kutalii Tanzania. Yaliyomkuta hataki hata kutuambia kiundani, anachosisitiza ni kuwa mgeni yeyote anayerudia kwenda Tanzania kwa mara ya pili hawezi kuwa na akili sawa. Anailalamikia sana sekta ya huduma katika utalii.

    ...Tanzania yetu ndio nchi ya salamaaaa....!

    ReplyDelete
  6. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  7. MDAU SIO WEWE TU WATU WOTE WA NJE HILO TATIZO LINATUHUSU.YAANI YOTE HIO NI KWAMBA UNALAZIMISHWA UTOE RUSHWA.MIMI NIMEKWAMA NA MZIGO WANGU DAHACO, JAMAA ANANAMBIA KAMA NIMETOKA ULAYA HIII NI BONGO! WATAKULA POLISI AU KWA KIKWETE?

    YAANI SIO SIRI INAKATISHA TAMAA HATA RAIS ANAPOKUJA KUTUPA DOMO ETI MSISAHAU BONGO MATOKEO YAKE NDIO HAYO, nIMEPELEKA USED REFRIGERATORS 40ft CONTAINER AMBAZO NI 100 units, NIMEFANYA MAONGEZI KABLA NA TRA WAKANIHAKIKISHIA NI 5 MILLIONS SHS, SAWA NIMEJIFUNGA MWANAUME MZIGO KWANZA PAPER WORKS ZAKE, NI TAYARI MILLION 2. WAKAJA SASA WAZEE WA KALAMU IKAFIKA MILLION 11,500,000/= SAWA KUTOA MZIGO MPAKA UNAFIKA NYUMBANI ZINGINE MILLION 3, HIO NI PAMOJA NA RUSHWA ASKARI BARABARANI, DORIA NA MENGINE MENGI TU HATA KAMA UNAKARATASI ZOTE NI LEGAL. FAIDA NILIOKUWA NIKITEGEMEA NI HIO MILLION 7 AMBAYO IMEKWISHA NA MINUS JUU. KWA KWELI INAKATISHA TAMAA WALA WABONGO MSIMSIKILIZE HUYO RAIS WETU NA POROJO ZAKE ZA KUTUVIKA VITAMBAA HAKUNA LOLOTE LA MAANA HUKO

    ReplyDelete
  8. Ndugu yangu US blogger, mimi mambo ya Tanzania nchi yetu tuipendayo nilishayasema mno humu mpaka mwisho nimechoka. Ni kama kumpigia mbuzi gitaa. Sisi tumelogwa, na aliyetuloga alishakufa. Ndiyo maana watu tuliopata nafasi ya kuishi ughaibuni na kuzoea systems za huku tunasita kurudi nyumbani au ku-invest huko (Tanzania). Nchi inanuka rushwa, wizi nje nje, hakuna principles wala kanuni rasmi za biashara, alimradi shida tu. Mimi nimeshaamua, bongo ni kuja likizo kumsalimia mama tu. Kama ni biashara, kazi, au proper safari holiday ya kuangalia wanyama nitaenda Masaai Mara (Kenya) au visiwa vya Bermudas ambako wanajua maana ya Customer Service ni nini.

    Buckinghamshire

    ReplyDelete
  9. HAO NDIO TRA (TANZANIA ROBBERY AUTHORITY) pole bwana, tushazowea hayo mambo kwa sisi tunaoka nje

    ReplyDelete
  10. kwanza pole sana ndugu yangu hiyo ndio hali halisi kabisa ya hapa nyumbani

    ReplyDelete
  11. Kuna wakati niliwahi kuandika makala humu yenye title 'Nchi Yetu Ni Kichwa Cha Mwendawazimu' lakini ikapuuzwa. Hata hivyo leo nasisitiza tena, japokuwa Tanzania ninaipenda lakini ukweli ni kuwa nchi yetu ni kichwa cha mwendawazimu.

    Hatuhitaji ujuzi wa sayansi ya roketi kudhibiti uchafu na ubadhirifu unaofanyika pale longroom (TRA). Lakini why toka nikingali mtoto nikiishi TZ mpaka leo hii niko overseas bado tabia yao ni ile ile? Hiyo ina maana AMA viongozi wa nchi hawajui kazi yao, au wao nao pia wanakula nao hao wabadhirifu wa TRA!

    Cha kusikitisha ni kwamba hata kila baada ya uchaguzi hakuna bunge hata moja linaloraise hiyo issue... Wabunge wetu nao (wote wa upinzani na wa chama tawala nao pia wanatafuta kula tu) alimradi total chaos. Anyway mimi kama nilivyosema, nilishasema sana mpaka nimechoka, bongo mimi basi, hata mama watoto nitatafuta huku huku :)

    Pole sana US blogger, baadae nitakuemail.

    Buckinghamshire

    ReplyDelete
  12. You are off the hook if you do your things right and play no poker games with TRA.
    When you think you are smart and want to conceal some financial deal with TRA- thats when problem begins.

    ReplyDelete
  13. US Blogger, a house divided can not stand. It is the government versus the government. And it is the government by the people for the people. So why blame the government if "by the people" is incompetent. No president in the world can supervise everything. I think TRA jobs in Tanzania have sworn to corruption and destruction of the country. It is a people's choice. Let go!

    ReplyDelete
  14. Yaani huu mswada ni wa maana sana na unaumiza wadau wengi wenye nia nzuri ya kuanzisha maisha yao. TRA kweli kuna WEZI wa kutupa. Uaminifu hakuna na kila mtu anataka kujinufaisha yeye mwenyewe kupitia JASHO la wavuja jasho.

    Ustaarabu kwao ni Msamiati ambao hauleweki na hata kwenye kamusi zao haupatikani. Hawa wafanyakazi mafedhuli wa TRA wanashindwa kuelewa kuwa hawa watu wa kawaida(na Wajasilimali) wanajitahidi kuanzisha/kuendeleza maisha yao, na kulisha/kuelimisha na kuvisha familia zao.

    KWANINI ubeberu wa namna hii? Mnaonesha nini na mnashawishi vipi watu wasitoe Rushwa ama kutumia njia za mkato????? Tanzania itakuwa lini????

    Huu ni uozo unaonuka kabisa!!

    Mdau na Mkereketwa!!

    ReplyDelete
  15. Bongo mwisho. Lakini kwanini mpate taabu wakati huko mliko mnaweza fanya biashara. Kuna vijana hapa UK wamefungua Pub wanaalika kina Kopa, Diamond, na wengine kupiga muziki. Kuna Serengeti anasafirisha mizigo, kuna Wakenya wanalinda. Biashara za nyumbani ni kuliana pesa tu. Kama unataka kuliwa pesa zako basi fanya biashara TZ wakati wewe unaishi ughaibuni!!

    ReplyDelete
  16. baba karibu mjini.. ila nakushauri usiskilize maneno ya maagenti kwani wao lao ni moja na watu wa TRA wakikwambia kodi wame 'uplift' waambie sawa mi na appeal as long as you have your supporting documents usiskilize hizo stori za kuchukua muda mrefu ni sound tu za kutaka uwape hela wenzio tunakomaa nao mpaka sa ivi wameshatuzoea michezo ka hiyo hawatufanyii..

    ReplyDelete
  17. Ndugu yangu uliyoyaandika kwakweli yote nisawa yamewatokea wengi na watu wameandika kila sehemu na wamelalamika kila kona mimi mwenyewe niliingiza gari nikawapa kila kitu na wakaenda mpaka company nilionunua gari wakaapewa kopi za risit kwamba bei nisawa lakini wakanipangia bei yao wanayotaka wenyewe nikalipa %110 kwakweli inasikitisha!
    Nakuhusu webside unazosema ziko mapambo tu wala hazifanyi kazi na simu zao sizo!
    mimi nilitaka kutapeliwa kiwanja changu nikaingia webside ya wizara ya Ardhi nikaandika email na nika wapigia hakuna anaepokea na email mpaka leo sijajibiwa!
    chakuchekesha nikwamba viongozi wako wapi?Hawasomi magazeti watu wanavyofanyiwa?wananchi wananyanyasika sana viongozi hakuna Tanzania wenzetu kenya kwakweli wanaendelea vizuri ukilinganisha na sisi!Na nikweli sisi tunapenda nchi yetu lakini viongozi hawako pamoja na sisi na pia watanzania wenzetu waliokuwa tanzania wanakuwa kama na wivu hawatusaidii chochote kushirikiana kujenga nchi yetu kwa pamoja!
    sisi tunajitahiid lakini sidhani kama watoto wetu watakuwa na mioyo kama yetu!Tunahitaji viongozi Tanzania kwa kila sekta kwakweli kuanzia raisi mpaka mesenja!

    ReplyDelete
  18. Nakubaliana kabisa na mdau hapo, nilipeleka vitu Tanzania inaishia kuletewa kodi ambazo bei ya vitu haiwiani, 5 times most likely. TRA Tanzania watakuua

    ReplyDelete
  19. tra ni washenzi na wauaji hasa kuna mzee mmoja anaitwa mwaseba yeye ndio anajifanya tra ni ya kwake.

    hawa ma clearing nao huwa ni waizi wakubwa mno shenzi zao.

    ReplyDelete
  20. Ni kweli kabisa ndugu zangu, mimi nimejionea mwenyewe, & we have to do something !. Ngoja tuanze sasa na hii dawa ya kuwataja hapa hadharani kwa majina sasa maana tumechoka sasa !!!, kuna mzee mmoja yupo TRA ya pale manzese anaitwa Mr. Bungenyi !!!, huyu mzee na najua pia wapo wengi sana wa namna hiyo !!, ni rushwa tu !, wanawajengea wananchi makusudi mazingira ya rushwa !!,jamani TAKUKURU mpo wapi ???!!!!!.We are tired kwa kweli !!! wizara zote za serikali zinanuka rushwa !!!, God will punish u one day !!!, leaders ( Viongozi ) !!!!!

    ReplyDelete
  21. Poleni ndugu zangu kwa yaliyowakuta. Viongozi wanalijua hili lakini 10%je?wanatumwa hao kutekeleza kazi yao,mwisho wa siku wanagawana, kwanza hakuna kiongozi anayelipa hayo makodi sijui mavalue, nyie wadanganyika ndio mnaolipishwa, Gari au mzigo ukifika bandarini na ni wa mkubwa, inapigwa simu tu hapo gari inatoka. Cha muhimu ni kwamba sasa hivi mfumo wa sheria Tanzanania umekuwa mzuri, jamani si tutumie recoding device kuwarecord tu, peleka kwenye dola tuone kama haki haitatendeka. Tuna simu hizi siku hizi unaweza kurecord video, peleka kwa pilato tuone kama haki haitendeki!!!kabla ya kuipeleka huko tuwekee kwenye blog hapa tuone wanavyoomba na kupekea rushwa, alafu huyo hakimu tuone asitende haki.
    Hiyo ndio miaka 50 ya uhuru wa kuiba bila woga.
    Mungu tubariki watanzania, maana tukisema ibariki nchi, nchi nadhani imeshaoza na tumelogwa, achilia mbali ni nchi ya kina nanii tu.

    ReplyDelete
  22. pole sana mdau..
    aisee Bongo kama unataka mambo yako yaende vizuri we jifanye fala flani ndo hutasumbuliwa sana.ukijifanya we ni mtu honest wallah itakula kwako.
    TRA ni mbwa maaana nikiwa likizo dukani kwa mzee jamaa sometimes huwa wanaingia hadi kwenye droo kuhesabu pesa ili kuona kama ziko sawa na hizo ulizoandika kwenye risiti.Sasa sheria gan inasema hivyo kama sio wizi tu?
    We dawa kula na wakubwa tu....

    Hata kontena kipindi wanakagua huwa wanachukua baadhi ya vitu alafu wanasema eti ni sample.sasa cjui wanajua mwenye mzigo anaviokota?TZ bila rushwa haiwezekaniiiiiii..............................
    Davy-muni
    Manichester

    ReplyDelete
  23. Wenzao huwa wanafukuza wote kisha wanaajiri wengine wapya, nao wakianza kujua mbinu za rushwa tu unatimua wote na kuajiri wapya, yaani unawaweka wafanyakazi mguu ndani mguu nje. Lakini twende mbele na turudi nyuma mnategemea nini ikiwa TRA yote imejaa kabila la wezi watupu? Wizi ni jadi yao na ili uwe mwizi lazima uwe na roho mbaya, roho ya kishetani. Tazama maghorofa yaliyoporomoshwa na wafanyakazi wa TRA? Tazama mahekalu waliyojenga huko kwao? Hiyo lifestyle yao unafikiri wanapata wapi hizo pesa?

    Na ni nani anaruhusu hilo suala la kuuplift kodi iliyokwishakadiriwa kama sio kutengeneza mazingira ya rushwa? Na wao wanajua uovu wote wanaoufanya watalaumiwa viongozi, ifike mahala tuwalaumu wahusika moja kwa moja, na ikiwezekana watajwe kwa majina, kuwa fulani kaniomba rushwa nimemnyima, tuone kama hii tabia ya kuombana ombana rushwa haitaisha. Mtu akikuomba rushwa hakuna cha kwenda TAKUKURU wala nini unatoa tu tangazo lako kwenye vyombo vya habari basi, lazima tutengeneze HALL OF SHAME ndio tutaweza kurekebishana otherwise mmhh kumeoza hakufai hata kidogo. Mimi nafikiria mwakani kuhama nchi nikawalee watoto wangu mahali ambako kuna ustaarabu, heshima, utu na kufuata sheria maana wasijeambukizwa uozo bure!!

    ReplyDelete
  24. Dah, inasikitisha mno. Kuna jamaa aliandika kitu kama hiki kwamba hatuna customer service na ubabaishaji hapa TZ kumbe ni kweli? Sasa rais wetu kipenzi anafanya nini maana hili suala la TRA ni la muda mrefu sana. Hapa Dar kuna secretary tu wa TRA kajenga bonge la ghorofa kule (jina kapuni), sasa jiulizeni mdada tena secretary ana jumba kama lile analipwa mshahara gani mpaka awe na lijumba kama lile? TRA inabidi ishughulikiwe haraka. Haiwezekani mtu ananunua kitu bei ndogo toka ughaibuni kuleta bongo analipa zaidi ya thamani aliyonunulia. Na ndiyo maana watu wanashindwa kugomboa mali zao pale bandarini mwishowe zinaliwa na jamaa wa TRA. TZ tuamke jamani. Hii serikali ya Kikwete hii?

    ReplyDelete
  25. Ngojeni nakuja kuchukua hiyo nchi nitairekebisa, nitaweka ma watchdogo wangu mtu akienda tu kimzunguko out next day maana tunao wasomi wengi kwanini tumtunze huyu mla rushwa, nitawatupa gabage wasahaulike, maana watu tunaleta utani, siyo TRA tu na kwingineko nasikia hata bank kuu, nao wakipelekewa hayo makusanyo ya TRA wanaweka kwenye akauti zao badala ya akaunti ya serikali, nita kula nao sahani moja mpaka watafute kuniua na wala hawata weza nitawafagia wote sitaki uchafu mimi, nataka nchi hiyo niifanye kama Marekani sasa hivi, Ok.

    ReplyDelete
  26. nchi imeoza mimi naishi na watu wa nchi za afrika nyingine wao wanatuma mizigo kwao na hata magari wanalipia hela ndogo sana kiasi kwamba utawaonea wivu maana wanatuma kila siku ukiwaambia kodi ya nchi yetu kutuma gari au mizigo wanashangaa

    nchi mbovu sana eti wanataka kuiombea ikiwa nchi imejaa rushwa maombi yatafika wapi

    ReplyDelete
  27. Nilikua na mpango mkubwa sana wakupeleka watu TZ ku invest ila nikawa na doubts baada ya kuongea na watu wachache, na sasa najiuliza mara kumi kumi... Nimechanganyikiwa, hawa fellows wanataka kwenda lakini mimi naogopa lawama kwa yatakayowapata! Stressed right out!!! Botswana ni second choice na so far nimesikia mazuri tu, la sivyo kwa Kagame!

    ReplyDelete
  28. Kila nchi ina matatizo yake, tofauti yetu ni kwamba hatutoi enough information, huu ni uozo na lazima uanikwe. Maoni yangu
    tuanze kufichua mambo haya with more details ili hata kama kuna mambo
    ya kulindana iwe ngumu; kwa mfano sakata la mdau na TRA; toa majina, idara, na
    tarehe (hata time ikiwezekana) - hii ifanyike idara zote za serikali, Pia kama ulipewa quotation kimaandishi;
    then unaweza claim "refund"..offcourse itachukua muda kidogo! Kila mtu akifanya hivi, watendaji wetu watafanya kazi zao ipasavyo.
    Pia, ningewashauri wadau ambao wamegive-up na nchi yao kwamba "Tanzania is a land of opporturnity"
    ;offcourse kila mahali kunakuwa na chalenges zake;kama Wachina wameweza ku-survive Kariakoo, mbongo huwezi shindwa,
    ukizijua vyema sheria za nchi hakuna mtu atayekubabaisha
    -Jukumu la kuijenga nchi yetu ni letu sote. Asanteni!

    ReplyDelete
  29. Hao Jamaa ni wabaya sana. yaani kama una mzigo basi hadi mlinzi anataka kula rushwa. ovyo sana hiyo nchi. TRA inanuka uozo na uvundo. Wadau hawa jamaa tusiwape nafasi wakapumua safari hii tule nao sahani moja katika mablog humu hadi kitaeleweka, ikiwezekana kila mtu akiletewa kizungumkuti kutoka mizigo yake aweke report halafu tuishambulie kwa nguvu zote, kitaeleweka tu siku moja. Si wanajifanya hawasomi hizi, lakini najua hata kama hawasomi basi watasomewa na watoto au wajukuu zao kuambiwa kwamba Mzee jamaa wanalipua TRA. pumbavu sana. Nchi gani isiyokuwa na viwango maalum, watu tunapata hasara kila mzigo bwana kwa ujinga wa TRA. yaani kama ulianza na Dola laki moja basi mzigo unaofuata utajikuta unanunua mzigo wa dola 75,000,ukienda ukirudi mara nyingine 50,000 mara ya mwisho unaweza ukarudi huna kitu kabisaaa usiposhtuka na kujitoa. Bongo hovyooo sana.

    ReplyDelete
  30. Kwani unadhani huo utajiri walio nao maafisa wa TRA wanautoa wapi kama siyo kwa waingiza mizigo na walipa kodi kama wewe. Kungekuwa na accoutability, kila afisa wa serikali ambaye utajiri wake hauendmani na kipato chake halali kinachojulikana angetakiwa afungwe kifungo cha miaka 20 hivi. Lakini wa TZ, mtu anaweza kuandikisha mali kwa jina la ndugu wa mbali ambaye hana uwezo na mali hizo na bado mambo yakapeta tu. Rwanda inaendelea kwa kasi pamoja na kutokuwa na raslimali kutokana na discipline katika utendaji wa serikali.

    ReplyDelete
  31. Pole sana blogger na wengineo wote .

    binafsi story yako imepinda sana. Kama unajua thamani ya mzigo wako kwanini ukubali kulipa 500% times more. Hii inamaana ulishadanganya ya kutosha mpaka ukubali kutoa 500% zaidi.

    Pili huyo agent unayemtumia inawezekana hajui kazi kwani maana ya kuwa agent anatakiwa awe kama mwana sheria wako kukutetea . Halafu kama ulikuwa na uthibitisho wa risiti, kwanini ulikubali kulipa zaidi ya kiwango ulichopanga?

    Kama vitu vinacost $150, kwanini unegotiate in the tone of $10,000 bribe? Ulikuwa umeweka nini mpaka issue ikawa hivyo?

    Next time mrekodi huyu ofisa wa TRA wakati mnaongea then mgeuzie kibano kuwa asipo lower duties unampripoti. Akigoma basi wewe mpe michuzi aipost au irushe youtobe free, Mabosi wake watajua sauti ya mtu wao anayewaharabia sifa za TRA.

    Dawa ya moto ni maji.

    Kama mnatoa rushwa kupitisha mambo yenu then malizaneni huko huko bandarini au Longroom. Acheni umbea na kuwaaribia watu majina. Unless you start the change, don't expect kupost hap a utapata changes unazotaka.

    Next time tumia agent mwenye sifa za kazi nzuri, magenta wenye ofisi za briefcase ni wasanii wa mjini.... umechakachuliwa ... Pole in advance

    ReplyDelete
  32. we michuzi kenge maji naweka comment kuhusu mwaseba unaficha??? kazi yako kunya mavi ya mbuzi.

    ReplyDelete
  33. Uzalendo unatakiwa, dawa si kuzira na kuacha kuwekeza nchini unless ndugu zetu hawajabaki tz. Tupambane na rushwa hadi mwisho. Poleni.

    ReplyDelete
  34. i like T. robbers Agent -(TRA) man that hurt because you have already committed your money. this is HONGO HONGO BONGO. dont you wonder how these chinese items are all over the place available cheaply? where is that uplifting thing?

    ReplyDelete
  35. Inasababishwa na system nzima kuwa mbovu wandugu!

    Wanatakiwa waseme may be gari aina fulani la mwaka fulani linapoingia unalipa kiasi fulan.

    badala yake ukishaingiza ndo wanaanza biashara ya ' usheikh Yahaya'!

    Mie ningekuwa mwarabu kuna siku ningejifunga BOMU niende Long Room 'niondoke nao'Pambaf

    ReplyDelete
  36. TRA-INANUKA RUSHWA:

    TUMEIORODHESHA JANA KTK KUMUUNGA MKONO MADAI YA MDAU WA NEW YORK, NA LEO IMEWEKWA HEWANI !!!

    HII TRA IMETUMIA GAHRAMA KUBWA YA PESA YA WALIPA KODI KWA TEKNOLOJIA KUBWA KTK KUENDESHA KAZI ZAKE KWA MASHINE ZAKE ZA KODI (EFD)Electronic Fiscal Devices AMBAZO HUUZWA KWA WALIPA KODI BADALA YA KUZITOA ILI WALIPE KWA MAREJESHO:

    HUU NI WAKATI SASA PCB (MAMLAKA YA KUDHIBITI RUSHWA )NAYO KUTUMIA FEDHA ZA KODI KWA KUFUNGA MITAMBO YAKE YA TEKNOLOJIA YA KISASA KUDHIBITI RUSHWA KTK OFISI ZOTEEE ZA MAMLAKA YA TRA !!!

    (KWA VILE MWOSHA NAYE HUOSHWA!)

    ReplyDelete
  37. UOZO WA RUSHWA KTK TRA!

    Imejengeka dhana potofu kuwa kila mfanyakazi wa Mamlaka ya TRA anakuwa ni mtu wa maisha ya kuwa na fedha nyingi MAJUMBA na MAGARI MAGARI NA ANASA!

    ReplyDelete
  38. Yaani umesema kweli ukirudi hata na bag lako moja pale airport wale wanaofungua masanduku wanakuuliza umenunua zawadi za shilingi ngapi ukisema $ 500 wanaanza kujenga mazingira ya rushwa unajua vitu vyote lazima vilipiwe kodi anaanza kupiga hesabu za kukuchanganya ina maana ukienda nje ya nchi kwenye semina huruhusiwi kuletea watoto wako hata nguo za ndani allowance unayopewa ni yanini sasa. Wanakera na naomba viongozi wa TRA tupieni jicho wale wanokagua airport wanahakikisha karibu kila msafiri anayepita unaacha hata elf hamsini ndio kiwango cha chini.

    ReplyDelete
  39. Pole sana mdau.Hii ni kawaida bongo (yamewakuta wengi si wewe tu)kwani serikali haina hela kwa hiyo wanatumia pia njia hii ili kuongeza mapato na kunusuru nchi

    ReplyDelete
  40. HIVI HAWA VIONGOZI WAMELALA AU MIMI SIELEWI HILI LI NCHI VIPI LIMEOZA LINANUKA, RUSHWA TUU NDIO MNAJUA NA UFISADI,KHAAAAAA KWELI TRA WAMEZIDIIIIIIIII PUMBAVU ZAO MIMI MWENYEWE NILITUMIWA MZIGO TOKA USA UNAFIKA HAPA ETI WANANIAMBIA NILIPE KODI NAWAKATI KULE ULIPOTOKA UMELIPIWA KILA KITU MPAKA INSURANCE SASA HAPA WANANCHOHITAJI NI NINI??? HII NCHI BASI TU, HAIFAI

    ReplyDelete
  41. KUKABILIANA NA UBABAISHAJI WA KIUTENDAJI KWA MISINGI YA WATUMISHI WA TRA KUOMBA RUSHWA!

    Kama SERIKALI imetoa GHARAMA KUBWA TU KWA KUFUNGA MITAMBO YA KODI YA KISASA (EFD) KWA AJILI YA VAT (KUKUSANYA KODI YA SERIKALI),

    1.ITAFAA KODI ZILIPWE KWA NJIA YA MTANDAO BILA YA KUKABILIANA NA WATU USO KWA USO KITU KINACHOWEKA MAZINGIRA NA MIANYA YA KUOMBWA RUSHWA.

    2.KWA NINI ISIFUNGE KAMERA NA MITAMBO YA KISASA NA KUIWEKA PCB (MAMLAKA YA UDHIBITI RUSHWA NA POLISI) ????

    HALI HII INAONDOA MATUMAINI NA KUKATISHA TAMAA WATU KABISA!!!

    ReplyDelete
  42. Stori stori.........mbona biashara za endelea kama kawaida? Tatizo la TRA ni nyinyi wenyewe wafanya biashara kwa kuwa wajanja wajanja,otherwise hakuna namna yoyote hayo mazimwi ya TRA yangeweza kuwadhulumu. "Eti mzigo mwingine hukuuweka kwa invoice kwakuwa ni sample na bei yake ni$150" unashangaza wewe!

    ReplyDelete
  43. Kwanza nampa pole ndugu yangu uliyepata usumbufu huu. Nafikiri si vizuri kwa wabongo kukata tamaa kufanya biashara katika nchi yetu. Nchi hii ina opportunities nyingi sana ila pia kuna vikwazo vyake. Mimi si mfanyakazi wa TRA ni mwanasheria niliyesomea masuala ya kodi.
    Pamoja na yote hayo nafikiri ukipewa assesment ya kodi ambayo unaona ni kubwa unaweza kutoa notice ya objection kwa kamisha general ww TRA kupitia sheria inayoitwa Ta Revenue Appeals Act, Cap 408 (R.E. 2006, katika mchakato huo unaweza kulipa kodi ambayo haibishaniwi au 1/3 ya kodi ambayo inabishaniwa, au kati ya hizo mbili, ambayo ni kubwa (whichever is greater). Mchakato unaanzia hapo kwenda hadi Baraza la Kodi, kuhusu muda si mrefu sana kwa sababu mahakama pamoja na mabaraza yana muda wa kumaliza kesi, mfano, katika mahakama zote kulingana na Mkataba wa Huduma Kwa Mteja wa Idara ya Mahakama muda wa kuandika hukumu ni miezi mitatu baada ya kesi kumalizwika kusikilizwa, kwa hiyo suala ni kupata mwanasheria atakayekuongoza vizuri. Nafikiri haina haja ya kuogopa, kama kuna preliminary assesment na baadaye wakajichanganya ni vizuri kuwapeleka katika chombo hiki cha haki, ni chombo kina watumishi waadilifu na wanajali muda.

    katerero73@gmail.com

    ReplyDelete
  44. Kwanza nampa pole ndugu yangu uliyepata usumbufu huu. Nafikiri si vizuri kwa wabongo kukata tamaa kufanya biashara katika nchi yetu. Nchi hii ina opportunities nyingi sana ila pia kuna vikwazo vyake. Mimi si mfanyakazi wa TRA ni mwanasheria niliyesomea masuala ya kodi.
    Pamoja na yote hayo nafikiri ukipewa assesment ya kodi ambayo unaona ni kubwa unaweza kutoa notice ya objection kwa kamisha general ww TRA kupitia sheria inayoitwa Ta Revenue Appeals Act, Cap 408 (R.E. 2006, katika mchakato huo unaweza kulipa kodi ambayo haibishaniwi au 1/3 ya kodi ambayo inabishaniwa, au kati ya hizo mbili, ambayo ni kubwa (whichever is greater). Mchakato unaanzia hapo kwenda hadi Baraza la Kodi, kuhusu muda si mrefu sana kwa sababu mahakama pamoja na mabaraza yana muda wa kumaliza kesi, mfano, katika mahakama zote kulingana na Mkataba wa Huduma Kwa Mteja wa Idara ya Mahakama muda wa kuandika hukumu ni miezi mitatu baada ya kesi kumalizwika kusikilizwa, kwa hiyo suala ni kupata mwanasheria atakayekuongoza vizuri. Nafikiri haina haja ya kuogopa, kama kuna preliminary assesment na baadaye wakajichanganya ni vizuri kuwapeleka katika chombo hiki cha haki, ni chombo kina watumishi waadilifu na wanajali muda.

    katerero73@gmail.com

    ReplyDelete
  45. Kwanza nampa pole ndugu yangu uliyepata usumbufu huu. Nafikiri si vizuri kwa wabongo kukata tamaa kufanya biashara katika nchi yetu. Nchi hii ina opportunities nyingi sana ila pia kuna vikwazo vyake. Mimi si mfanyakazi wa TRA ni mwanasheria niliyesomea masuala ya kodi.
    Pamoja na yote hayo nafikiri ukipewa assesment ya kodi ambayo unaona ni kubwa unaweza kutoa notice ya objection kwa kamisha general ww TRA kupitia sheria inayoitwa Ta Revenue Appeals Act, Cap 408 (R.E. 2006, katika mchakato huo unaweza kulipa kodi ambayo haibishaniwi au 1/3 ya kodi ambayo inabishaniwa, au kati ya hizo mbili, ambayo ni kubwa (whichever is greater). Mchakato unaanzia hapo kwenda hadi Baraza la Kodi, kuhusu muda si mrefu sana kwa sababu mahakama pamoja na mabaraza yana muda wa kumaliza kesi, mfano, katika mahakama zote kulingana na Mkataba wa Huduma Kwa Mteja wa Idara ya Mahakama muda wa kuandika hukumu ni miezi mitatu baada ya kesi kumalizwika kusikilizwa, kwa hiyo suala ni kupata mwanasheria atakayekuongoza vizuri. Nafikiri haina haja ya kuogopa, kama kuna preliminary assesment na baadaye wakajichanganya ni vizuri kuwapeleka katika chombo hiki cha haki, ni chombo kina watumishi waadilifu na wanajali muda.

    katerero73@gmail.com

    ReplyDelete
  46. Kwanza nampa pole ndugu yangu uliyepata usumbufu huu. Nafikiri si vizuri kwa wabongo kukata tamaa kufanya biashara katika nchi yetu. Nchi hii ina opportunities nyingi sana ila pia kuna vikwazo vyake. Mimi si mfanyakazi wa TRA ni mwanasheria niliyesomea masuala ya kodi.
    Pamoja na yote hayo nafikiri ukipewa assesment ya kodi ambayo unaona ni kubwa unaweza kutoa notice ya objection kwa kamisha general ww TRA kupitia sheria inayoitwa Ta Revenue Appeals Act, Cap 408 (R.E. 2006, katika mchakato huo unaweza kulipa kodi ambayo haibishaniwi au 1/3 ya kodi ambayo inabishaniwa, au kati ya hizo mbili, ambayo ni kubwa (whichever is greater). Mchakato unaanzia hapo kwenda hadi Baraza la Kodi, kuhusu muda si mrefu sana kwa sababu mahakama pamoja na mabaraza yana muda wa kumaliza kesi, mfano, katika mahakama zote kulingana na Mkataba wa Huduma Kwa Mteja wa Idara ya Mahakama muda wa kuandika hukumu ni miezi mitatu baada ya kesi kumalizwika kusikilizwa, kwa hiyo suala ni kupata mwanasheria atakayekuongoza vizuri. Nafikiri haina haja ya kuogopa, kama kuna preliminary assesment na baadaye wakajichanganya ni vizuri kuwapeleka katika chombo hiki cha haki, ni chombo kina watumishi waadilifu na wanajali muda.

    katerero73@gmail.com

    ReplyDelete
  47. Kwanza nampa pole ndugu yangu uliyepata usumbufu huu. Nafikiri si vizuri kwa wabongo kukata tamaa kufanya biashara katika nchi yetu. Nchi hii ina opportunities nyingi sana ila pia kuna vikwazo vyake. Mimi si mfanyakazi wa TRA ni mwanasheria niliyesomea masuala ya kodi.
    Pamoja na yote hayo nafikiri ukipewa assesment ya kodi ambayo unaona ni kubwa unaweza kutoa notice ya objection kwa kamisha general ww TRA kupitia sheria inayoitwa Ta Revenue Appeals Act, Cap 408 (R.E. 2006, katika mchakato huo unaweza kulipa kodi ambayo haibishaniwi au 1/3 ya kodi ambayo inabishaniwa, au kati ya hizo mbili, ambayo ni kubwa (whichever is greater). Mchakato unaanzia hapo kwenda hadi Baraza la Kodi, kuhusu muda si mrefu sana kwa sababu mahakama pamoja na mabaraza yana muda wa kumaliza kesi, mfano, katika mahakama zote kulingana na Mkataba wa Huduma Kwa Mteja wa Idara ya Mahakama muda wa kuandika hukumu ni miezi mitatu baada ya kesi kumalizwika kusikilizwa, kwa hiyo suala ni kupata mwanasheria atakayekuongoza vizuri. Nafikiri haina haja ya kuogopa, kama kuna preliminary assesment na baadaye wakajichanganya ni vizuri kuwapeleka katika chombo hiki cha haki, ni chombo kina watumishi waadilifu na wanajali muda.

    katerero73@gmail.com

    ReplyDelete
  48. Mdau pole sana,Sijasoma maneno mengi ya kwako ila kichwa tu kwa kuwa ni TRA kimenishawishi kuacha kusoma kwa kuwa hawa jamaa ni kama miungu watu.Tatizo ni moja TRA ni kama kila mtumishi ana maamuzi ya kupanga ushuru,mimi binafsi nilipeawa assessment ya kulipia ushuru gari yangu nikalipa na mwisho wa siku nikaambiwa ushuru niliolipia ni mdogo haulingani na thamani ya gari.Sasa je huo wa kwanza alinipangia nani?Tin number hutolewa bure cha kushangaza ni lazima utoe chochote ili uipate kwa haraka,Release order ni haki ya mtu akishalipia ushuru mzigo wake nayo ni lazima utoe japo 50,000 ili ipatikane haraka ukwepe storage charge.Jamani eeeh nadhani imetosha sasa mbadirike na kila mtu atimize wajibu wake pale alipo.

    ReplyDelete
  49. Mimi nimefukuzwa kazi TRA Mwezi wa oktoba. Dili letu pale lilikuwa ni kucheza na wachina na wahindi. Katika miaka yangu 5 niloyofanya kazi TRA sikumbuki kuona kontena la mchina lilopita pale bila ya sisi kupata chetu. Bidhaa nyingi sana zinapita pale za wachina ambao wanatueleza wao thaman yake bila ya sisi kuscrutinize chochote. Katika kila kontena tunatengeneza kwenye milioni 30 ili tugawane. Naweza kusema Mara nyingi sana mzigo unapita pale pasi na sisi Kufanya inspection yoyote ya Maana. Nyumbani kwangu karibia vifaa vyote vya ndani ni zawadi kutoka kwa jamaa wa kichina. Tunawapigia simu mchina anakwambia njoo uchukue friji hapa warehouse pugu road, free of charge.

    ReplyDelete
  50. USHAURI KWA ANKAL MICHUZI.

    Anzisha Coloumn ya kila wiki kwenye gazeti/magazeti uwe unatoa issues hizi kama zilivyo. Unatoa mada kama ilivyowakilishwa na mwandishi alafu unatoa comments. Kwa njia hii Ankal utakuwa umesaidia sana nchi yako kwani watu wataogopa uozo wao kutoka kila jumapili au siku yoyote ya wiki.

    MUNGU IBARIKI TANZANIA

    David,Dar Es Salaam.

    ReplyDelete
  51. UKIWA NA MZIGO WAKO UPITISHIE KENYA. TANZANIA IMEJAA MASHETANI, AU HATA SHETANI ANA NAFUU.

    ReplyDelete
  52. kwa kweli TRA wanaharibia watu maisha,mimi nilipata mgeni mcanada alitaka kuwekeza tukapanga mengi kiasi cha kumfanya arelocate kutoka canada aje aishi Tanzania,akapakia contena 2 moja ya vitu vya nadni yaani used house wear na ya 2 ilikuwa na magari na baadhi ya vitu vya ndani,tukafatilia garama ya kuvitoa my dia trust me ni zaidi ya garama ya vitu vilivyomo ndani ya contena moja kwa maana ni bora angenunua hivyo vitu hapa dar, hivi navyoandika hapa jamaa alibadilisha mawazo na yuko nairobi amewekeza na mizigo yake alitolea bandari ya mombasa,

    kodi ya biashara TRA ni 30% kwanini mtu asiwekeze malaysia au kenya au nchi nyingine ambapo standard ya kodi ni 15 up to 20%?

    tanzania inapendwa sana ila TRA mnaiua kwa tamaa za mali ambazo mkifa mtaziacha hamtazikwa hata gari wala nyumba mtaenda empty na kuwaacha wengine wakiijoi mali mlizowatapeli watanzania wanyonge,

    inauma sana

    ReplyDelete
  53. Nchi imeoza hii jamani. Watu wachache wanaiharibu hii nchi. Kikwete, please fukuza kazi wafanyakazi wote wa TRA na uajiri wapya kwa mikataba ya miaka miwili tu renewable kutokana na utendaji. Labda hiyo itasaidia

    ReplyDelete
  54. YOTE YANAYOSEMWA NI KWELI,MIMI NAISHI FINLAND KWA SASA,MWAKA 2000-2002 NILIKUWA USA.NILIJARIBU KUSHAWISH RAFIKI YANGU MZUMGU AMABAYE ANAFANYA KAZI YA UWINDAJI WA MSIMU.ALIKATAA KABISA KUJA TANZANIA.MAELEZO YAKE YALIKUWA HIVI-TANZANIA KODI NYINGI NA HAZINA UTARATIBU MAALUMU,KILA MAHALI UNAPOENDA UNAAMBIWA ULIPE KWA NINI WASIWEKE SEHEMU MOJA MTU UKALIPIA HALAFU WAO WAKABAKI WANAGAWA MAPATI WANAVYOTAKA?SASA ANAENDA SOUTH AFRICA,ZAMBIA KENYA NA BOTSWANA

    ReplyDelete
  55. TRA ni bullshit!! kwanza wamejaa wachaga,wote wezi watupu!!! kazi wanapeana wenyewe wachaga ili kuwe na connection nzuri ya kuiba. Kama alivyosema mdau hapo juu,ni kweli wafanyakazi wa TRA wote wanamaghorofa kama mahekalu, kwa mshahara upi haswaa? magorofa yanjengwa ndani ya miezi sita hadi mwaka yameisha kila kitu mtu anahamia.

    Serikali inajua a-z ila inakaa kimya kwa kuwa nao wanahusika katika hili. Nchi hii uozo mtupu!!! nimeshaishi nje,nilivyorudi bongo nilihisi kudata kwa poor services,in almost all sectors.

    Mdau aliyelalamika juzi kuhusu customer care yote ni kweli kabisa,airport kuambiwa ufungue mabegi wacheck vilivyomo ndani ni kitu cha kawaida kabisa,nashangaa watu wanavyobisha. Nadhani sasa hivi ni kwamba mtu akikuzingua unamuwasha hapo hapo,mbona tutachapana muda si mrefu!!

    ReplyDelete
  56. Poleni sana,

    Mimi naomba MUWATAJE hao watu! kukaa kimya hakutasaidia chochote! WATAJENI na sheria itachukuwa mkondo ! na hapo ndio watakapojirekebisha kwa kuogofya kutajwa! tusaidiane katika kujenga nchi! Rais anajitahidi lakini hajui kuna wacache wanarudisha taifa nyuma! WATAJENI tutawachukulia HATUA KALI!

    ReplyDelete
  57. Nashauri waliopatwa na maswahiba hayo wawasiliane na wabunge wetu ili hiyo issue iweze kuzungumziwa kwenye kikao kijacho cha Bunge la February, inawezekana kabisa ya kwamba hawa viongozi wetu hawajui haya mambo kwakua wao wana ma EXEMPTION wanapo import vitu. Ingia kwenye tovuti ya Tanzania Parliament na utapata contacts zao.
    These issues are are a seriuos threat to the development of our country.
    Happy 2012 to all.

    ReplyDelete
  58. MDAU POLE NI KWELI TRA IMEOZAAAAA LAKINI HILO LAKO LA KUWEKA MZIGO BILA KUUTAJA KWENYE INVOICE ULICHEMSHAAAAAAAA HAPO LAZIMA UBANWE

    ReplyDelete
  59. Wabunge wako wapi hawasomi hii issue lazima ichukuliwe bungeni kuikandamiza serikali kwakweli nchi haina viongozi!Huyu alieandika hii mada ninampa pongzi kubwa sana na aichukuwe aiweke kwenye facebook watu wasaport na tuandamane na viongozi wa Diaspora mko wapi mnaliangaliaje swala hili nyinyi ndio mnawza kuongea na hao wanaokuja kutafuta wawekezaji!wanawezwa na wachina tu kwakupelekewe vitu feki!

    ReplyDelete
  60. Kudadadeki, Michuzi copy hii kitu kwa JK aone jinsi nchi yake ilivyooza. Kwa mwendo huu kwanini tusitembeze bakuli kwa wahisani kila mwaka wakati nchi kama Kenya zilishaacha zamani kufanya hivyo?

    ReplyDelete
  61. Wasalaam,
    Watajeni kwani maneno yenu hayasaidii kwa sababu hata mtoa malalamiko hakutaja idara gani na wapi alipata shida na maofisa wote wa TRA wanavaa vitambulisho wakiwa kazini huyu jamaa alikua hajui taratibu zake na wala haki yake.
    Kwa mfano huyu jamaa kaleta bithaa eti hakuzitaja katika invoice sasa alikua anataka asilipie ushuru, hilo ni kosa dunia nzima huwezi import vitu na ukataja nusu na vingine unasema ni sample, kama ni sample unaisema, kwa hiyo alishulikiwa kwa mujibu wa sheria na sio afisa aliyekagua mzigo, afisa hana mamlaka ya kujiamulia tu anavyotaka.
    TRA inaongozwa kwa sheria na Takukuru ipo kwa ajili ya kazi kama hizi.
    TATIZO WATANZANIA TUNAPENDA LAWAMA BADALA YA KUTOA TARIFA KWA VYOMBO HUSIKA NA TATIZO LITATULIWE, TUNABAKI KULAUMU TU.

    ReplyDelete
  62. Wasalaam,
    Watajeni kwani maneno yenu hayasaidii kwa sababu hata mtoa malalamiko hakutaja idara gani na wapi alipata shida na maofisa wote wa TRA wanavaa vitambulisho wakiwa kazini huyu jamaa alikua hajui taratibu zake na wala haki yake.
    Kwa mfano huyu jamaa kaleta bithaa eti hakuzitaja katika invoice sasa alikua anataka asilipie ushuru, hilo ni kosa dunia nzima huwezi import vitu na ukataja nusu na vingine unasema ni sample, kama ni sample unaisema, kwa hiyo alishulikiwa kwa mujibu wa sheria na sio afisa aliyekagua mzigo, afisa hana mamlaka ya kujiamulia tu anavyotaka.
    TRA inaongozwa kwa sheria na Takukuru ipo kwa ajili ya kazi kama hizi.
    TATIZO WATANZANIA TUNAPENDA LAWAMA BADALA YA KUTOA TARIFA KWA VYOMBO HUSIKA NA TATIZO LITATULIWE, TUNABAKI KULAUMU TU.

    ReplyDelete
  63. Wasalaam,
    Watajeni kwani maneno yenu hayasaidii kwa sababu hata mtoa malalamiko hakutaja idara gani na wapi alipata shida na maofisa wote wa TRA wanavaa vitambulisho wakiwa kazini huyu jamaa alikua hajui taratibu zake na wala haki yake.
    Kwa mfano huyu jamaa kaleta bithaa eti hakuzitaja katika invoice sasa alikua anataka asilipie ushuru, hilo ni kosa dunia nzima huwezi import vitu na ukataja nusu na vingine unasema ni sample, kama ni sample unaisema, kwa hiyo alishulikiwa kwa mujibu wa sheria na sio afisa aliyekagua mzigo, afisa hana mamlaka ya kujiamulia tu anavyotaka.
    TRA inaongozwa kwa sheria na Takukuru ipo kwa ajili ya kazi kama hizi.
    TATIZO WATANZANIA TUNAPENDA LAWAMA BADALA YA KUTOA TARIFA KWA VYOMBO HUSIKA NA TATIZO LITATULIWE, TUNABAKI KULAUMU TU.

    ReplyDelete
  64. Mimi nafanya kazi ya hali ya chini sana TRA lakini namiliki ukwasi wa kutosha. mwenyhezi mungu Subhwana akipenda mwaka huu 2012 nitamalizia kajumba kangu pale Likoni mombasa kaliko-nigharimu kiasi 3.6Bn. hapa nyumbani vile vile nimfanikiwa nyumba zangu 6. ndio maana simsemi mtu, sikasiriki na matusi yenu, sina taabu na nyie, fanyani kazi zenu tuacheni sisi tuishi maisha yetu! mipango ya mungu!! binadamu mungu alikupa akili uziumie kufikiri!! kwani nikikosa mimi ndio wewe utapata??
    kaa huko uliko ukiotea baridi yako.

    ReplyDelete
  65. Cha ajabu ni kuwa jamaa wa TRA wanasoma hizi tuhuma, na wala hawajibu au kutoa maelezo au hata msemaji wa TRA kutoa tamko!! inakera sana...

    ReplyDelete
  66. mbongowakweliDecember 30, 2011

    Sio siri ndio wanajenga yale majumba ya kifahari kule Tegeta, Mbezi Beach, Mbezi Kimara, Kunduchi,Boko n.k. Na tena sio moja, wanaendesha magari ya kifahari kwa kula kodi ya serikali na rushwa, cha kushangaza, mtu kaajiriwa mika 2 tu, unashangaa ana majumba na magari, shopping Dubai, Far East na Europe!
    Kwanini hawachunguzwi?! Hawa ni wahujumu uchumi, nchi yetu itaendelea kivipi kama hawa wahujumu uchumi wataendelea kutafuna hizi hela za nchi?
    Tunasema basi, umefika wakati mkuu wa kaya na wahusika kuwashughulikia wote wanaosadidika wanahusika na huu wizi.
    Tunawajua, wanajulikana, wanaonekana, sasa tatizo liko wapi?
    Funga wote wanaohusika, hapo ndipo tutakapokomesha huu unyama!

    ReplyDelete
  67. piga chini TRA kuanzia top hadi mfagizi waanze kuajiri wengine.ndio maana serikali haina pesa kisa ni TRA.

    ReplyDelete
  68. NADHANI ITAKUWA VIZURI KUWATAJA KWA MAJINA HAO WATU WOTE WANAOHUSIKA NA RUSHWA.HILI LIWE NI ZOEZI LA KUDUMU NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO IKIWEMO KUFUKUZWA KAZI NA KUFUNGWA.KINGINE NI KUWAREKODI IWE KWA CMU AU KIFAA CHOCHOTE KAMA USHAHIDI MAANA TULIPOFIKIA SASA NI PABAYA.WANATUPA WAKATI MGUMU SANA SISI TUNAOISHI UGHAIBUNI KWANI NI NGUMU MNO KUFIKIRIA KUWEKEZA NYUMBANI.
    Piscilla,Denmark

    ReplyDelete
  69. Uchaga si hoja

    ReplyDelete
  70. HAO WANADECLARED VITU NUSU NUSU NI WAKWEPA KODI,KWANZA ALITAKIWA ASHITAKIWE NA TRA KWA KUTAKA KUKWEPA KODI, DUNIANI KOTE INAJULIKANA MFANYABIASHARA YOYOTE NIA YAKE NI KUWEPA KODI ILI ATAPE FAIDA KUBWA KWENYE BIASHARA ZAKE, WATU WANAFANYA KAZI KUTOKANA NA SHERIA NA UTARATIBU ULIOPANGWA NA NCHI, HAWA WAKWEPA KODI NDIO WANAIRUDISHA NCHI YETU NYUMA

    ReplyDelete
  71. Kwanza natoa pole kwa nyie mlioadhirika. Kwa kweli ni jambo la kusikitisha na ni kilio kikubwa kwetu sote kama Watanzania au Waafrika. Ukifikiri kuwa kuna waliotutangulia amabo walimwaga damu ili tujitawale na matokeo yake ni kwamba tumejenga taifa ambalo halina tofauti na Waliotutia utumwani na kwenye ukoloni. Lakini kwa hao amabo alikuwa na nia njema ya kutukomboa, tuna budi kuendeleza mapambano ya kuondoa hawa mafisadi amabo wangawa nchi na mali bure na kujenga vyombo vya umma ambavyo vina wafanyakazi wasiokuwa na ethics wala morals. Mwalimu Nyerer alikuwa na nia njema na baadhi ya viongozi. Hatuna tena uongozi kwa hiyo kila mtu anajifanyia mambo kiholela. Mimi naamini kuwa tunahitaji kujipiga msasa na kubanga mwenendo kamambe amabo utaokoa nchi. Hatuwezi kuachia hao vibaraka na madume zao kufilisi nchi na kutuvunja moyo

    ReplyDelete
  72. MIMI NAFIKIRI HAWA VIONGOZI WETU WAACHE LONGOLONGO LA KUWASHAWISHI WADANGANYIKA WAISHIO NJE KUJA KUWEKEZA TANZANIA, KIKWAZO KIKUU NI TANZANIA ROBBERY AUTHORITY (TRA), WEWE HUSHANGAI MTU ANAANZA KAZI MWEZI MMOJA MWEZI WA PILI ANAMILIKI GARI LA THAMANI, BAADA YA MWAKA KAJENGA BUNGALOW AU GHOROFA,
    HEBU NAMBIE NI MFANYAKAZI GANI ALIYE KWENYE KUKUSANYA AU KUKADIA KODI HANA GAI LA THAMANI? IWEJE MTU MSHAHARA NA MARUPURUPU YAKE YANAJULIKANA LAKINI KATIKA KIPINDI KIFUPI YULE MTU ANAMILIKI RANGE ROVER VOGUE NA ANA NYUMBA YA THAMANI, BAA NDIO HAKAUKI. MIMI NILIIPAYTA FRESHI KWANI NILITUMA FLAT SCREEN TV, NILINUNUA $250.00 LAKINI NILIPOKWENDA NAYO BONGO PAMOJA NA KUONYESHA PASSPORT YANGU KUWA NILIKUWA NJE KWA MUDA WA MIAKA MITANO, NILILIPISHWA USHURU WA $750.00 ETI KWA SABABU NI FLAT SCREEN, NILIPOLALAMIKA NIKAAMBIWA YULE MAMA ANAITAKA YEYE UKIIACHA KACHUKUA, ILIBIDI NILIPE NA RISITI NINAZO MPAKA LEO. CHA AJABU TV KAMA ILE ILIKUWA INAUZWA TANZANIA $300 TU. JE HEBU HUONI TRA SI AJABU KUITWA - TANZANIA ROBBERY AUTHORITY?

    ReplyDelete
  73. Jamani tatizo pia hakuna wabunge nchi kwetu angalieni wenzetu wabunge wanafanya kazi zao sisi tanzania wako na shida gani posho na mishahara inaongezeka outomatik!!Pumbavu wote lakini iko siku watatafutana!

    ReplyDelete
  74. Wasaalam
    ndugu wadau poleni sana kwa yale yaliyotokea kutokana na usumbufu wa TRA, mimi nadhani hawa TRA sio rahisi wabadilike cha kwanza hakuna maadili yoyote ya kazi wanajisahau kwamba wako pale kwaajili ya sisi tunaoingiza bidha na mishahara yao inatokana na malipo tunayotoa,pili ni jambo la kushangaza kumbana mtanzania kwenye inchi yake amejiajiri anatakiwa apewa kipao mbele ili atoke kwenye umaskini aweze kundeleo, lakini kwetu tanzania kama watu waliokwenye madaraka wa laana vile hawajali kama wako pale ni wanainchi ndio wamewaweka pale,
    kingine kama kweli serikali haisiki malamiko ya watu basi nimakosa yatu pia kwanini watu wasifanye juhudi ikifika siku ya uchaguzi basi wapige kura kwa chama kingine, hii ndio fimbo pekee yake kwa tanzania kuheshimiwa na serikali yao, Nchi yoyote duniani change inatoka kwa wanainchi,tatu kuna watanzania zaidi ya Million mbili Diaspora kama kweli tunataka kuwa na change Inawezekana kwa mfano kekwete kachaguliwa na kura million tano ni karibia ya nusu ya watanzania wanaoshi nje ya nchi, kama tunafanya kampeni kila mtanzania anayoishi nje ya nchi aongea na ndugu zake jamaa za na marafiki zake apate kura tano tu, angalia kura ngapi hizo zitakuwa kama million Kumi hapo nakwambia serikali ya wala rushwa imekwanda na maji, thinks twise change comes from you!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...