Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Kanali Mstaafu Ameen Kashmiri wakati wa sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam wiki iliyopita, ambapo alimmwagia sifa mwanajeshi huyu mstaafu kwa kuwa mmoja wa mashujaa wachache wa Uhuru walio hai hadi sasa. Kanali Kashmiri ndiye aliyebeba bendera ya Tanganyika huru siku ile hapo hapo uwanja wa Uhuru wakati Tanganyika inapata Uhuru na bendera yake kupandishwa.
Mwalimu Nyerere akijiandaa kuishusha bendera ya mkoloni na kupokea ya Tanganyika huru iliyobebwa na Kanali Ameen Kashmiri (kushoto) usiku huo wa uhuru miaka 50 iliyopita
Watoto wa Marehemu Brigedia Alex Gwebe Nyirenda,Tima pamoja na kaka yake Alex wakiwa wameshika koti ambalo baba yao alilivaa wakati alipopanda Mlima Kilimanjaro na kuweka Mwenge wa uhuru pamoja na bendera ya Taifa kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro  Nchi yetu ilipopata Uhuru mwaka 1961. 


Alex ameshika Mwenge ambao nao pia watauwasha na kuuweka kileleni  huko siku ya  Desemba 9, 2011 ikiwa kama heshima na kumbukumbu ya kazi aliyoifanya marehemu baba yao miaka 50 iliyopita.


Kwa mujibu wa Suzyo Gwebe-Nyirenda, binti wa Brigedia Nyirenda,  tukio hilo, linaloenda kwa jina la GWEBE-NYIRENDA MEMORIAL KILIMANJARO EXPEDITION, litafanyika kila mwaka na kwamba mwakani hata wajukuu watashiriki pamoja na wadau wataopenda kujiunga katika msafara huo.  Suzyo Gwebe-Nyirenda hakuweza kushiriki kutokana na kupata ajali ya gari, na hali yake inaendelea vyema. Kitindamimba wao, Tiwonge Gwebe-Nyirenda hakuweza kuja kutoka Lusaka, Zambia, aliko kikazi  kwa sababu zisizozuilika.
Kwa habari zilizopita za Meja Alex Gwebe Nyirenfa BOFYA HAPA
Watoto wa  Nyirenda akiwa anajiandaaa kupanda Mlima Kilimanjaro huku kaka yake akimsubiria.
Watoto wa Marehemu Mzee Alex Nyirenda,Alex Foti Gwebe Nyirenda akiwa na mdogo wake Tima Gwebe Nyirenda wakiwa wameshasaini kwenye geti la kuingilia na kupata kibali wakati wa kupanda Mlima Kilimanjaro.
Juu na chini  ni watoto na marafiki wa Mzee Nyirenda wakipata semina ya namna ya kukwea mlima Kilimanjaro kabla ya safari kuanza
Watoto wa Marehemu Mzee Nyirenda,Alex pamoja na nduguye Tima wakiwa pamoja na watu walioongozana nao wakiwa wanamsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa hoteli ya Marangu,Desmond Brice -Bennnett wakati alipokuwa akiwapa maelekezo kuhusu sheria za mlima kilimanjaro pamoja na njia ambazo watapita
Picha ya pamoja kabla ya kuanza kupanda mlima Kilimanjaro. Wapandaji hao ni  pamoja na Kanali mstaafu Ameen Kashmiri (wa nne toka kushoto) ambaye ndiye aliyekuwa mmoja wa maafisa wa jeshi katika kikosi cha bendera usiku wa manane wakati Tanganyika inapata Uhuru wake.

Wengine ni Mobeen Kashmiri, Paul Mason, Aunali Rajabali, Lorley  Lavilla, Mohamed Khimji, Tima Gwebe-Nyirenda Kuwani na Alex Foti Gwebe-Nyirenda. Meja Kashmiri, ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa marehemu Meja Nyirenda, ndiye baba mlezi wa familia hiyo ya rafikiye kipenzi
 Meja Alex Gwebe Nyirenda akiweka Mwenge wa Uhuru pamoja na bendera katika kilele cha mlima Kilimanjro usiku wa manane wa Desemba 9, 1961
 Meja Alex Gwebe Nyirenda akiwa na Mwenge wa Uhuru alioupandisha kileleni Kilimanjaro
Mwalimu N yerere akifurahi na Meja  Alex Gwebe Nyirenda katika mnuso wa kusherehekea Uhuru wa Tanganyika alioandaa Ikulu, Dar es salaam.



By Madaraka Nyerere
At the eve of Tanzania's independence, Brig. Nyirenda hoisted Tanzania's flag (then Tanganyika) and placed the Uhuru Torch on the summit of Mt. Kilimanjaro as the Union Jack was lowered at the National Stadium in Dar es Salaam at the same time.


Two years earlier, former President Julius K. Nyerere, in a speech to the Tanganyika Legislative Assembly, said the following:
"We the people of Tanganyika, would like to light a candle and put it on top of Mount Kilimanjaro which would shine beyond our borders giving hope where there was despair, love where there was hate, and dignity where there was before only humiliation...."


That candle (which came to be known to Tanzanians as the Uhuru torch) was placed on Mt. Kilimanjaro by Lt. Nyirenda, and signalled Tanzania's long and unwavering commitment to the liberation struggle of those African countries that remained in the early sixties under colonialism and white minority rule.


Brig. Nyirenda was the first Tanganyikan in 1958 to graduate from Sandhurst Military Academy in England. He also became, prior to independence, the first African to become an officer in the King's African Rifles.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Michuzi, cheo halisi cha Nyirenda kilikuwa kipi? Kwenye maelezo yote uliyotoa anatajwa kwa vyeo vingi. Brigadier Nyirenda, Major Nyirenda, Lietenant Nyirenda, hata niliwahi kumwona Channel 10 akitambulishwa kama Lt-Col. (yaani Luteni Kanali) sasa cheo chake ni kipi alichostaafu nacho?
    Asante.
    Muga, DSM

    ReplyDelete
  2. Kanali Ameen Kashmiri alikuwa Kapten wakati wa uhuru - hiyo caption ya picha ya pili ina makosa kwani alikuwa kapten enzi zile na sio kanali.

    ReplyDelete
  3. MIAKA 50 YA UHURU:::::::::::::::;;;

    Nimesoma kwa makini historia ya suala hili sambamba na Kuupandisha Mwenge na Bendera usiku wa manane wa Uhuru tarehe 9 Disemba,1961 juu ktk kilele cha Mlima Kilimanjaro, ni simulizi ya kusisimua.

    Kitu kama hiki, hasa wana familia wa Nyirenda wamefanya jambo la busara kiwe ni cha muendelezo na itasaidia kujenga Ari na Mwamko wa Utaifa hata kwa vizazi vijavyo!.

    TUACHE KUBEZA USHEREHEKEAJI WA UHURU WA TANZANIA ILIYOKUWA INAITWA TANGANYIKA KABLA!.

    Si kweli kwamba hatujapiga hatua kabisa, mfano mtu unafanya biashara unatumia gharama ya Shs. 50 Milioni ukitarajia kuuza 75 Milioni faida 25 Milioni,,,ikatokea ukapata 55 Milioni (faida ya 5 Milioni) itakuwa hujapata hapo?

    ReplyDelete
  4. Nimefurahi sana kumuona Col (mstaafu) Kashmir. Japo nimetoka jeshini nawakumbuka yeye, Mayunga, Walden wakati wa vita vya Kagera 1978-79 wakati nikiwa NCO mwenye umri wa miaka 18 tu.

    ReplyDelete
  5. Aliyepanda kileleni na kuinasa hii taswira ya kihistoria alikuwa nani? Naye tunapaswa kumuenzi, alifanya kazi kubwa ambayo vizazi na vizazi vitaiona na kuihusisha na historia yenyewe.

    ReplyDelete
  6. Yaani nimeguswa sana na hii hadithi! Huyu Mzee Kashmiri hata hatujawahi kumsikia kabla lakini nawapongeza sana kwa kujitokeza na kutujulisha yaliyojiri siku ile.

    Kwa kweli hatupaswi kuwasahau watu hawa na kuweka focus kwa Nyerere tu kwani hili taifa lilipiganiwa na wengi lakini michango yao haikutambuliwa.

    Tuendelee kujifunza na kuwatambua wote bila ya upendeleo.

    ReplyDelete
  7. Nawaombea kila lakheri watoto wa marehemu waende wafike mpaka kileleni kama alivyofika baba yao sio waaishie njiani. all the best kids. bll

    ReplyDelete
  8. kwa upeo wangu na nijuavyo mimi ni kwamba ankali michuzi unabana sana comment za watu pasipo na sababu muhimu ndio maana watu wamepunguza kutuma comment zao maana mtu anatumia muda wake kutuma maoni yake alafu anakuja kuona maoni yake hayajatolewa sasa inatia uvivu kwa kweli na haswa kwenye blog hii ambayo unaitangaza kuwa ni glob ya jamii inakuaje jamii wanashindwa kufikisha walau maoni yao
    fatilia kwa makini utagundua
    fanya mabadiliko

    ReplyDelete
  9. Hata mimi imenichanganya kidogo kwenye hivyo vyeo. Meja, Luteni, Brigedia. Inawezekana kabisa alikuwa na vyeo vyote hivyo kwa nyakati tofauti kulingana na wakati ambao kila picha ilipigwa. Lakini maandiko ya Madaraka Nyerere nayo yamempa vyeo viwili kwa wakati mmoja: Luteni na Brigedia. Hata hivyo, picha na maelezo bring back the old days' memories.

    ReplyDelete
  10. Nyirenda alikuja kupandishwa cheo na Mzee Mwinyi na kuwa Brigadier. Siku hizi wanaita Brigadier General. Naamini kulikuwa na uwalikini wa jinsi alivyoondoka jeshini na ndiyo kupelekea Mzee Mwinyi kumpa cheo na heshima hiyo. Sina kumbukumbu Alexander Nyirenda aliondoka jeshini akiwa na cheo gani.

    Wakati JWTZ inaanzishwa Kashmiri alikuwa na cheo cha Major ktk Tanganyika Riffles. Pamoja na hayo Cpt.Mirisho Sarakikya alipandishwa cheo kuwa Brig na kuteuliwa kuwa Mkuu wa kwanza wa JWTZ. Nafasi ya Mnadhimu Mkuu ilikwenda kwa Lt.Kavana aliyepewa cheo cha Major.

    ReplyDelete
  11. Wahindi nao walikuwa katika jeshi sasa Tangayika ilipopata uhuru hawakuwafanyia vizuri kwa kuanza kuwanyanyasa. Lakini wana michango yao, tuwaenzi na wao na sio kuwaita magabachori.

    ReplyDelete
  12. Anon wa Mon Dec 05, 04:34:00 pm 2011 nakuunga mkono ila kama utagundua ktk wiki mbili zilizo pita bwana Michuzi amejirekebisha anajitahidi sana kupost maoni yetu sema tu aongeze bidii aweze kupost maoni mengi zaidi ya sasa najua anakazi nyingine nyingi zinazo msonga ila ankal jitahidi pia ku-balansisha usielemee upande mmoja sote tunakuhitaji.

    ReplyDelete
  13. Kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya - shauri ya tufani ya barafu, mwenge haukuweza kufikishwa kileleni. Uliwekwa chini kidogo na hilo kundi ikabidi lirudi.

    Baadaye, ndipo Mwenge wa Uhuru uliweza kuwekwa kileleni.

    Huyo kanali Mskashimir anaweza kuongezea ukweli wa habari hii!

    Mtanganyika

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...