Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Emmanuel Nchimbi akisoma maneno yaliyoandikwa kwenye Mnara wa kumbukumbu ya Mkutano wa Kwanza wa TANU kitaifa uliofanywa na Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius K. Nyerere mjini Bagamoyo katika harakati za kupigania Uhuru wa Tanganyika baada ya kuuzindua jana. Uzinduzi huo ulifanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili mjini Bagamoyo alipoenda kuzindua Mnara wa kumbukumbu ya Mkutano wa Kwanza wa TANU kitaifa uliofanywa na Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius K. Nyerere Bagamoyo mwaka 1954 wakati wa harakati za kupigania Uhuru wa Tanganyika.( Kulia) ni Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Martin Shigella.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi akizungumza na wana CCM wa mjini Bagamoyo baada ya kuzindua Mnara wa kumbukumbu kumbukumbu ya Mkutano wa Kwanza wa TANU kitaifa uliofanywa na Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius K. Nyerere Bagamoyo mwaka 1954 wakati wa harakati za kupigania Uhuru wa Tanganyika.
Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM-UVCCM Mkoa wa Pwani akizungumza na wana CCM wa mjini Bagamoyo wakati wa Uzinduzi wa Mnara wa kumbukumbu ya Mkutano wa Kwanza wa TANU kitaifa uliofanywa na Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius K. Nyerere Bagamoyo mwaka 1954 wakati wa harakati za kupigania Uhuru wa Tanganyika uliozinduliwa jana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi akimuwakilisha Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi akipanda mti katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo katika maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Bagamoyo wakicheza kumkaribisha Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi alipokwenda kuzindua Mnara wa kumbukumbu ya Mkutano wa Kwanza wa TANU kitaifa uliofanywa na Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius K. Nyerere mjini Bagamoyo katika harakati za kupigania Uhuru wa Tanganyika.Picha na Lydia Churi wa Idara ya Habari-MAELEZO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hivi hakuna watu wengine waliokua katika chama cha Tanu Jamani? Maana kila siku ni Nyerere tu ndo tunasikia, kama ni kumbukumbu wako wengi waliochangia nchi hii kupata Uhuru jamani.

    ReplyDelete
  2. sasa huo mnara wenyewe mbona hamna picha??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...