THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Archive for July 2011

daraja la mto malagarasi

Habari za leo Mjomba Ankal,
Niko safarini kuelekea Kigoma. Nikapata taswira hizi za daraja la Mto Malagarasi. Picha ya chini ni sehemu linakojengwa daraja jipya. Hapa ndipo waheshimiwa wetu walipokuwa wanarushiana vijembe kuhusu wapi ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami uanzie.
Mdau Rajab.


katibu mkuu wa SID Tawi la tanzania June Warioba aongea


salaam za mfungo mtukufu wa ramadhani toka kwa rais wa zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Ali Mohamed Shein, akisoma risala ya kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na kuwatakia wananchi kheri kati mfungo huo kwasalama,pia kuwataka wajitahidi katika kufanya ibada kwa wingi,kuzidisha imani katika jamii.Picha na Ramadhan Othman Ikulu - Zanzibar.


VODACOM YAJA NA MUONEKANO MPYA WA HUDUMA YAKE YA M-PESA

Afisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Bi. Mwamvita Makamba wanne kutoka kushoto na Mkuu wa kitengo cha huduma za kifedha wa kampuni hiyo Bw. Jacques Voogt kushoto kwake,wakishikana mikono kuashiria uzinduzi rasmi wa muonekano mpya wa huduma ya Vodacom m-pesa kwa wateja wake wote nchini ambayo inaendana sambamba na kauli mbiu ya "Kazi ni Kwako" kwa kuihusisha huduma hiyo na kazi anazozifanya 'Superman' za uharaka, usalama, uhakika na utayari wake wa kusaidia jamii wakati wowote ule na mahali popote pale.
Wafanyakazi mbalimbali wa Vodacom Tanzania wakiwa kwenye mfano wa vazi analovaa"Superman" wakati wa uzinduzi rasmi wa muonekano mpya wa huduma ya Vodacom m-pesa kwa wateja wake wote nchini ambayo inaendana sambamba na kauli mbiu ya "Kazi ni Kwako" kwa kuihusisha huduma hiyo na kazi anazozifanya 'Superman' za uharaka, usalama, uhakika na utayari wake wa kusaidia jamii wakati wowote ule na mahali popote pale.
Afisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Bi. Mwamvita Makamba akimsikiliza kwa umakini,Mkuu wa Kitengo cha huduma za kifedha wa Vodacom Tanzania Jacques Voogt akiongea wakati wa uzinduzi rasmi wa muonekano mpya wa huduma ya Vodacom m-pesa kwa wateja wake wote nchini ambayo inaendana sambamba na kauli mbiu ya "Kazi ni Kwako" kwa kuihusisha huduma hiyo na kazi anazozifanya 'Superman' za uharaka, usalama, uhakika na utayari wake wa kusaidia jamii wakati wowote ule na mahali.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa kwenye uzinduzi rasmi wa muonekano mpya wa huduma ya Vodacom m-pesa kwa wateja wake wote nchini ambayo inaendana sambamba na kauli mbiu ya "Kazi ni Kwako" kwa kuihusisha huduma hiyo na kazi anazozifanya 'Superman' za uharaka, usalama, uhakika na utayari wake wa kusaidia jamii wakati wowote ule na mahali popote pale.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini wakati wa uzinduzi rasmi wa muonekano mpya wa huduma ya Vodacom m-pesa kwa wateja wake wote nchini ambayo inaendana sambamba na kauli mbiu ya "Kazi ni Kwako" kwa kuihusisha huduma hiyo na kazi anazozifanya 'Superman' za uharaka, usalama, uhakika na utayari wake wa kusaidia jamii wakati wowote ule na mahali popote pale.


TAIFA STARS KUKIPIGA NA CHAD KOMBE LA DUNIA 2014

Upangaji makundi ya mechi za mchujo kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil ulifanywa jana (Julai 30 mwaka huu) karibu na ufukwe wa Copacabana jijini Rio de Janeiro nchini Brazil ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) Jerome Valcke.
 
Tanzania (Taifa Stars) imepangwa kundi C Kanda ya Afrika ambalo lina timu za Cote d’Ivoire, Morocco na Gambia. Lakini kabla ya kuingia katika kundi hilo Stars italazimika kucheza raundi ya kwanza ya mchujo dhidi ya Chad.
 
Stars ikifanikiwa kuitoa Chad baada ya mechi mbili za nyumbani na ugenini zitakazochezwa kati ya Novemba 11-15  mwaka huu ndiyo itaingia katika kundi hilo la C. Pia mshindi wa kundi C ndiye atakayeingia katika raundi inayofuata kabla ya kupata tiketi ya kwenda Brazil.
 
Stars ni miongoni mwa timu 29 ambazo kwenye viwango vya ubora vya FIFA vya Julai mwaka huu katika Afrika ziko chini ya timu 24 bora, hivyo kulazimika kuanzia hatua hiyo ya kuchujana zenyewe kabla ya kuingia hatua ya makundi ambayo itachezwa kuanzia Juni 1, 2012 hadi Septemba 10, 2013.
 
Kwa mujibu wa viwango vya FIFA vya Julai mwaka huu, Tanzania iko katika nafasi ya 127 wakati Chad ni namba 158. Kwa upande wa Afrika, Tanzania ni namba 33 na Chad 43. Nchi 52 kati ya 53 za Afrika zimeingia katika michuano hiyo ya Kombe la Dunia. Ni Mauritania pekee ambayo haikuthibitisha ushiriki wake.
 
Timu 10 za juu kwa ubora barani Afrika ambazo zimeongoza makundi 10 ya Afrika katika upangaji ratiba ni Afrika Kusini, Tunisia, Cote d’Ivoire, Ghana, Burkina Faso, Nigeria, Misri, Algeria, Cameroon na Senegal.
 
Afrika ina nafasi tano kwenye fainali za Kombe la Dunia, huku Ulaya ikiongoza kwa kuwa nazo 13.
 
Boniface Wambura 
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)


Uchaguzi Mkuu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Iringa

Rais wa muungano wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Kenneth Simbaya akifungua mkutano mkuu wa uchaguzi ndani ya klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) Simbaya ndiye alikuwa mwenyekiti wa IPC kabla ya kuamua kustaafu nafasi hiyo ,kushoto ni katibu mtendaji wa IPC Frank Leonard na kulia ni weka hazina wa IPC Sulemani Boki
Baadhi ya wanachama wa IPC wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi waliochaguliwa kuongoza IPC.Picha na Francis Godwin. Kwa habari zaidi pamoja na mapicha kibao BOFYA HAPA


UFUNGUZI WA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM MJINI DODOMA LEO

Mwenyekiti wa CCM taifa, Jakaya Kikwete, Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar, Aman Abeid Karume (wa tatu kushoto), Rais wa Zanzibar, Dkt Ali Mohamed Shein na Mwenyekiti wa CCM Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi (kushoto), Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Pius Msekwa (kulia) na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Willson Mukama, wakiwa katika ufunguzi wa Kikao cha Kamati kuu kilichofunguliwa leo Julai 31, katika Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika ufunguzi wa Kikao cha Kamati Kuu  kilichoanza leo Julai 31, 2011 katika Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma. Katikati ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Picha na Muhidin Sufiani-OMR


SERENGETI FREIGHT FORWARDERS
        WAZEE WA KAZI
 TO SEND DOCUMENTS TO EAST AFRICA BY DHL
£25 ONLY
YOU CAN ALSO SEND PARCELLS BY DHL WITH US
SALOON CARS TO MOMBASA/DAR £720
4X4 TO MOMBASA/DAR £800
Contact us for more info;
CHRIS LUKOSI 07903828119
SIMON LOUIS (MOHSIN) 07950689243
BRIAN (BABA NJOROGE0 07795160757
Unit 21 Harbour House,
Coldharbour Lane, Rainham, RM13 9YA
    Tell  (+44) 01708550434    Fax  (+44) 01708550434


LICHA YA CHANGAMOTO NYINGI JWTZ YAONESHA USHUPAVU MKUBWA DARFUR

Kamanda wa Majeshi ya UNAMID- Luteni Generali Patrick Nyamvumba (kulia) akiwa na Maj.  Wilbert Ibuge, Mwambata Jeshi wa Tanzania katika  Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa wakati Maj Ibuge alipotembelea Darfur mwaka jana  viliko vikosi vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ)
Na Mwandishi Maalum
New York

Kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) kinachoshiriki katika operesheni ya kulinda amani katika  jimbo la Darfur, nchini Sudani – yaani Tanzania Battalion (TANZBATT) kama kinavyojulikana huko Darfur na Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York - kimeonesha ushupavu mkubwa, licha ya kukabiliwa na mazingira magumu na ya hatari kioperesheni, likiwemo suala la uhaba wa zana za kisasa za kijeshi.

Hayo yameelezwa na Kamanda Mkuu anayeongoza Vikosi vya Mseto vinavyoundwa kwa pamoja na  Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa maarufu kama UNAMID, Luteni Jenerali Patrick Nyamvumba wakati alipokuwa akizungumza  mwishoni mwa wiki na wajumbe wa Kamati Maalum ya Umoja wa Mataifa ya Ulinzi wa Amani (maarufu kama C-34) katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, New York.

 Wajumbe wa C-34  ni wale ambao ama nchi zao zinatoa wanajeshi, polisi, askari magereza au raia wao kama waangalizi katika operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa (UM). Tanzania ni mwanachama wa Kamati hiyo.

Mkutano huo uliwashirikisha pia makanda wakuu wengine (15) wanaoongoza vikosi vya  kulinda amani vya UM katika maeneo mbalimbali duniani.  Baadhi yao makamanda hao pia walitoa taarifa kuhusu maeneo yao ya majukumu.

Luteni Jenerali Nyamvumba, ambaye ni raia wa Rwanda, aliwaeleza wajumbe wa Kamati hiyo kuwa TANZBATT ni kati ya vikosi katika uongozi wake ambavyo vimeonesha umahiri mkubwa na ueledi wa hali ya juu sana katika kutekeleza majukumu ya kulinda amani Darfur, likiwemo jukumu zito la kuwalinda raia wasiokuwa na hatia ambao daima hujikuta ni wahanga wa migogoro na machafuko.

“Waheshimwa wajumbe,  niseme kwamba  kwa kweli wanajeshi wetu wanafanya kazi katika mazingira magumu sana.    Kwa mfano mwishoni mwa mwaka jana,Wanajeshi wa Tanzania, licha ya  mazingira magumu na ya hatari, uhaba wa zana za kisasa za mawasiliano katika eneo lao la majukumu huku wakikabiliwa na taarifa duni za kiintelejensia kutokana na mazingira magumu ya kioperesheni Darfur, bado waliweza kufanya kazi kubwa yenye kutukuka ya kuwalinda raia na mali zao katika eneo la Khor Abeche”. Akaeleza  Luteni Jenerali Nyamvumba.

Eneo la Khor Abeche ndipo yaliyopo Makao Makuu ya  TANZBATT. Mwisho mwa mwaka jana kulitokea mapigano makali yaliyodumu kwa muda wa takribani siku 10.

Mapigano hayo yalihusisha wanajeshi wa serikali  ya Sudan na  kikundi cha wapiganaji  kijulikanacho kama  SLA- MINI MINAWI kinachoipinga Serikali ya Sudani.

Mapigano hayo  yalikilazimisha kikosi cha Tanzania kuingilia kati kuwaokoa raia ambao licha ya  wengi wao kuuawa na wengine  kujeruhiwa lakini pia nyumba na mali zao zilichomwa moto.

Kwa ushupavu mkubwa, TANZBATT kiliingia katika maeneo ya wananchi, licha ya uhaba wa taarifa za kiintelenjesia na mawasiliano na Makao Makuu ya Sekta ya Kusini yaliyoko Nyala, hivyo kujiweka katika hatari kubwa wao wenyewe, lakini wakiwa na nia ya kuwaokoa na kuwalinda raia waliokuwa hatarini.

Kwa ushupavu mkubwa, kikosi hicho siyo tu kilisaidia kuzuia mapigano yasiendelee kati ya pande mbili husika, lakini pia kiliokoa maisha ya raia na mali zao zilizoweza kuokolewa, kuwapatia hifadhi na huduma za  malazi, chakula na madawa na kuhakikisha usalama wao ndani ya kambi yao.

Kamanda Mkuu wa  Vikosi vya UNAMID, Jenerali Nyamvumba, anasema kuwa  vikosi vya  UNAMID  ambavyo kwa asilimia 85 vinaundwa na wanajeshi kutoka nchi za afrika, vinakabiliana na uhaba mkubwa wa vitendea kazi kama vile vyombo vya mawasiliano vya kisasa pamoja na vya ukusanyaji habari za kiintelejensia.

“Vikosi vyangu vinaundwa na Waafrika, na pengine  hii inachangia sana kuwa na tatizo kubwa la vifaa, labda kama kungekuwa na wazungu ndani yake hali ingekuwa tofauti…” Anasema Luteni Jenerali Nyamvumba kwa masikitiko makubwa.

Akaongeza kuwa licha ya dhamana ya awali ya vikosi vya UNAMID ya kulinda amani kwa hali ya kawaida,  vikosi hivyo vimeongezewa dhamana nyingine nzito ya kuwalinda raia, kama waliyolazimika kukabiliana nayo TANZBATT. Na hii inatoa changamoto nyingine kubwa kwa vikosi hivyo.

Jenerali Nyamvumba alisema kuwa  dhamana hiyo ya kuwalinda raia ni mpya ambayo inawahitaji askari wake kubadilika  kimtazamo na  kiutendaji  na kujielekeza hilo jipya la jukumu la  kuwalinda raia, jukumu ambalo kwa hakika ni nje ya majukumu yao ya msingi na asilia.

“Hii ni dhana mpya ambayo haikuwamo katika makubaliano ya awali. Pia ni changamoto kubwa sana kwetu, kwa sababu sasa vikosi vyetu vinalazimika kwenda katika  makazi ya watu yanapotokea machafuko ili kuwalinda”. Anasema Jenerali Nyamvumba.

Akaongeza pia kwamba, kibaya zaidi, vikosi vyake  vinakuwa havina taarifa za kutosha za kiintelejensia, kwa kuwa hawana vifaa vya kisasa hivyo kufanya majukumu yao kuwa magumu zaidi.  Kama kwamba hiyo haitoshi, hata vifaa vya kisasa vya mawasiliano hawana.  Hili ni tatizo kubwa sana.

Akielezea changamoto nyingine zinazovikabili vikosi vya  kulinda amani  chini ya mwamvuli wa UNAMID, Kamanda huyo anazitaja kuwa ni pamoja na  mafunzo zaidi kwa askari na maafisa wanaopelekwa katika operesheni hizo.

Anafafanua zaidi kwa kusema kuwa, operesheni za kulinda amani hivi sasa zimebadilika mno na zinachangamoto kubwa tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.

“Ni lazima tubadilike kifikra na kimtazamo. Mabadiliko haya lazima yaanzie katika Idara ya Operesheni za Kulinda Amani ya UM (maarufu kama DPKO), ndani ya nchi zinazotoa askari wao na kwa askari wenyewe na maafisa. Operesheni hizi zimebadilika sana, changamoto ni nyingi na kubwa. Hivyo, ombi langu ni kwamba askari na maafisa wanaopelekwa kwa ajili ya operesheni hizi wapatiwe mafunzo zaidi yakiwamo yale yanayohusu  ugaidi na  masuala ya intelejensia.

Tanzania ina kikosi kimoja katika UNAMID chenye askari na maafisa 800 na nyongeza ya Kombania ya wahandisi 75   wenye jukumu la ujenzi wa  makambi katika UNAMID.

Kikosi hicho kimegawanyika maeneo mawili: yaani Khor Abeche (yaliko Makao yake Makuu) na eneo la Muhajeria walipo wanajeshi wengine. Kombania ya wahandisi wa kijeshi wanalo jukumu la ziada kufuatia maombi ya UM ya kuhudumia eneo zima UNAMID kwa ujenzi.


burudani ya rusha roho na belly dance ya kundi la SOUNDS OF TARAAB jijini New york yafana

  kikundi cha SOUNDS OF TARAAB kikitumbuiza jijini New York

Viongozi wa jumuiya ya Watanzania New York, Marekani, wakiwa meza kuu na mgeni rasimu ambae ni balozi wetu kwenye Umoja wa Mataifa, Mh. Ombeni Sefua (wa pili shoto). Kulia  ni Mjumbe wa Jumuiya Bwana Chiume, wa pili ni Mwenyeketi wa Jumuiya  Bwana Hajji Hamis na kushoto ni  afisa wa ubalozi  New York Bwana Mero wakiwa katika burudani hiyo murua kabisa
 Mwimbaji wa Sounds of Taarab akirusha roho mashabiki kwa mipasho
 Belly dancer wa Sounds of Taarab akionesha umahiri wake wa mambo ya kimwambao
 Kama kawa mduara ulipigwa na kupagaisha
 Mweka hazina na mratibu wa mpango mzima wa jambo hili kutokea Mzee Temba akiwa na baadhi ya wadau waliohudhuria shoo hii. Picha na Ny Ebra wa Globu ya Jamii, New York City


matukio mbalimbali toka mkoani morogoro

Baadhi ya Viongozi wa Sekretarieti ya Mkoa na watendaji wa Wilaya mkoani Morogoro katika usikuvu wa elimu dhidi ya mapambano ya rushwa.
Katibu Mkuu Tamisemi, Hussein Katanga , akifafanua jambo kwenye ufungaji wa Kikao cha kazi cha Maofisa Elimu wa Mikoa na Wilaya za Morogoro
Mfanyabiashara wa maharage ,wa Chanjale , Gairo,akionesha magunia yake mengi ya mahinsdi mbele ya mkuu  wa Mkoa wa Morogoro, Mh.  Issa Machibya, ( suti nyeusi) aliyewatembelea. Hata hivyo wakulima wanalanguliwa gunia moja kwa sh 18,000 na wafanyabiashara ambao huenda kuuza kwa bei kubwa zaidi
Mzee wa Kata ya Chanjale, Tarafa ya Gairo, Wilaya mpya ya Gairo, akitoa kero zake wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya ( hayupo pochani) kuhusu barabara na elimu
Ofisa wa Dawati wa Elimu kwa Umma, wa Takukuru Mkoa wa Morogoro, Bi. Mercy Manyalika akitoa mada ya wajibu wa viongozi wa Mkoa wa Morogoro katika mapambano dhidi ya Rushwa
Mkuu wa Mkoa wa morogoro Mh. Issa Machibya akijichanganya na wahudhuriaji wengine waklatio ofisa wa Dawati wa Elimu kwa Umma, wa Takukuru Mkoa wa Morogoro, Mercy Manyalika akitoa mada ya wajibu wa viongozi wa Mkoa wa Morogoro katika mapambano dhidi ya Rushwa. Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii, Morogoro


Dodoma mabingwa wa pool taifa 2011

Mgeni Rasmi katika Fainali za Mashindano ya Mchezo wa Pool Taifa ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe Mh. George Simbachawene (kulia) akikabidhi kombe la ubingwa wa Taifa wa Mashindano ya Safari Lager kwa Nahodha wa Timu ya Pool ya mkoa wa Dodoma ambao ndio mabingwa wapya wa mchezo huo kwa mwaka huu.
Mgeni Rasmi katika Fainali za Mashindano ya Mchezo wa Pool Taifa ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe Mh. George Simbachawene (kushoto) akikabidhi kitata cha sh. mil 5 kwa kiongozi wa timu ya mkoa wa Dodoma ikiwa ni zawadi ya ubingwa wao huo walioupata usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Kilimani Club,mjini Dodoma.
Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscer Shelukindo (kushoto) akikabidhi kitata cha sh. mil 3.5 kwa kiongozi wa timu ya mkoa wa kimichezo wa Ilala,ikiwa zawadi ya ushindi wa pili walioupaka mkoa huo.

Mgeni Rasmi katika Fainali za Mashindano ya Mchezo wa Safari Lager Pool Taifa ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe Mh. George Simbachawene akiwa pamoja na viongozi wa mchezo wa Pool na viongozi wa TBL wakifuatilia moja ya michezo ya Fainali za Pool za Taifa kati Ilala na Dodoma iliyokuwa ikifanyika kwenye ukumbi wa Kilimani,Mjini Dodoma Usiku wa Kuamkia leo.
Kuona picha Zingine


just in: Mstahiki meya wa Songea Ali saidi Manya afariki dunia leo

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea, Ali Saidi Manya ambaye pia ni Diwani wa kata ya Lizaboni (pichani ) amefariki dunia leo katika Hospitali ya Misheni Peramiho.

Taarifa za Msiba huo zimetangazwa na naibu Meya wa Manispaa ya Songea Mheshimiwa Mariam Dizumba na kupokelewa kwa mshtuko mkubwa na wakazi wa manispaa ya Songea na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.

Naibu Meya Dizumba amesema mazishi ya Mstahiki Meya Ali Saidi Manya yatafanywa nyumbani kwake Lizaboni Manispaa ya Songea Siku ya Jumatatu Tarehe 1 Agosti 2011.


mambo yalivyokuwa siku ya Tamasha la 17 la Mzanzibari

WATOTO wa skuli ya Kidutani wakicheza beni (mbwa kachoka) katika sherehe za uzinduzi wa Tamasha la Mzanzibar la 17 lililofanyika katika ufukwe wa pwani ya Nungwi hivi karibuni.
Kwa mapicha zaidi BOFYA HAPA


dereva na abiria wake zenji

WANAFUNZI wakiwa katika  baskeli wakitoka skuli  mitaa ya Michenzani mjini Unguja. Hakika uchukuwaji wa abiria kama hivi unaweza kuleta madhara kwa watumiaji wa chombo hicho, anasema mdau Othman Mapara aliyetuletea taswira hii ya Mwezi. 


WANAFUNZI WA SKULI YA SEKONDARI YA VIKOKOTONI, Zenji, WAKIUKARIBISHA MWEZI WA RAMADHANI

 SHEIKH Mselemu Ali akitowa  mhadhara  kwa Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Vikokotoni  kwa ajili ya kutoa mafunzo ya Mfungo wa Ramadhani, unaotarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi wa Nane. 
 WANAFUNZI wa Skuli ya Vikokotoni wakimsikiliza . Mselem Ali akitowa  mawaidha  ya dini ya Kiislam kwa Wanafunzi hao ikiwa ni moja ya Maandalizi ya kuukaribisha mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kutowa mafunzo ya dini, mdahalo huo umeandaliwa na Uongozi wa skuli hiyo uliofanyika katika viwanja vyao. 
                                         


madaktari bingwa wamtembelea rais wa zanzibar ikulu ya pemba

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Madaktari Bingwa kutoka taasisi mbali mbali duniani ambao wako kisiwani Pemba kuazimisha miaka 11 tokea kuanzishwa kwa ‘Maabara ya Afya ya Jamii’ (PHL), huko Ikulu ndogo ya Chake chake Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Madaktari Bingwa hao katika  Ikulu ndogo ya Chake chake,Pemba.Picha na Ramadhan Othman-IKULU,Pemba


Kikundi cha mchiriku cha jagwa music toka tandale chawasha moto denmark

Mpiga kinanda wa muziki wa Mchiriku wa Jagwa Music group toka Mwananyamala Kisiwani Kwa Jolijo,  jijini Dar es salaam,  kikitumbuiza usiku wa kuamkia leo katika jijini Copenhagen, nchini  Denmark,  ambako wamepagawisha wapenzi wa muziki wa mchiriku isivyo kawaida. Karibu kila mwaka kundi hili hualikwa katika matamasha mbalimbnali ughaibuni. Wao hawana makuu, vvyombo vyao ni hicho kinanda, ngoma, filimbi na kiti cha kukalia ambacho hufanywa percussions. Wakianza hakuna anayebaki ameketi na wana uwezo wa kupiga muziki usiku kucha bila kuchoka
Add captionMwimbaji wa Jagwa akighani na kumfanya mshabiki ashindwe kujizuia
Mnenguaji wa Jagwa Music band ilibidi ashikiwe kiti
Mcheza show wa Jagwa akifanya vitu vyake.


mkutano wa SID World Congress 2011 waendelea washington DC

Katikati ni Makamu wa Rais wa Chama cha Maendeleo ya Kimataifa (Society for International development -SID), Balozi Juma Mwapachu akiwa kutoka shoto na Ankal, mjumbe kutoka Uganda, Sunday shomary wa Idhaa ya Kiswahili ya Voice of America (VOA)  na Lukas Mkami a.k.a DJ Luke Joe wa Globu dada ya Jamii ya Vijimambo wakati wa mapumziko leo katika hoteli ya Omni Sherham jijini Washington DC.


masoud kipanya katika maandalizi ya mwisho ya kuzindua albamu yake marekani

Masoud Kipanya (wa pili shoto) akiwa na Dj Luke Joe 'Vijimambo', Mweka hazina na SID Tanzania Chapter  Da'Yasmin Chali, Sunday shomary wa VOA na Katibu Mkuu wa SID Tanzania Chapter Da' June Warioba jijini Washington DC
javascript:void(0)
Masoud Kipanya  akiwa studio jijini Washington DC akikamilisha albam yake ya 'Upuzi wa Kipanya' anayotarajia kuizindua jijini Dallas agosti 6, 2011 na siku itayofuata atazindua tena jijini Houston.
Kipanya akionesha kava ya albamu yake


The Omni Shoreham hotel, washington DC, in a nutshell


tamasha la fiesta ndani ya lidaz klabu jijini dar usiku huu lanoga

Jukwaa lilivyokuwa linaomnekana kwa mbali. Chini ni Msanii Ludacris akimwaga Lazi usiku wa kuamkia leo viwanja vya Leaders Club, Kiondoni, jijini Dar es salaam katika shoo ya hitimisho la Tamasha la Fiest. Picha na Kajuna Son na Michuzi Jr


Palikuwa hapatoshi

DJ wa Ludacris akifanya mambozzzzz

Msanii mahiri wa Kike kutoka nyumba ya vipaji THT,aitwaye Lina akicheza jukwaa na mmoja wa madensa wake kwa namna ya kipekee usiku huu,ambao shangwe za hapa na pale ikiwemo miluzi kibaoo.
Nyomi la Watu
Kijana mdogo hivi lakini mambo yake ni makubwa awapo jukwaani,anaitwa Beka Boy kutoka nyumba ya vipaji THT akiimba jukwaani.
Msanii wa kike Mwasiti pamoja na msanii mwingine anayeibukia vilivyo katika anga ya hip hop bongo,Gozilla wakilishambilia jukwaa la Serengeti Fiesta 2011 usiku huu.
Wakazi wa jiji la Dar ambao wametoka kila kona wamejitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2011.
Msanii mwimbaji na mtunzi kutoka THT aitwaye Amin akiwa na kundi lake wakionyesha umahiri wa kucheza jukwaani kwa namna ya kipekee kabisa usiku huu.
Msanii mahiri wa kizazi kipya Ben Paul akiimba kwa hisia jukwaani usiku huu.

Pichani ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Serengeti Breweries Limited,Tedd Mapunda,Mkurungenzi wa Masoko wa SBL,Ephraim Mafuru pamoja na Mdau wakiwa wamepozi huku wakifuatilia tamasha la Serengeti Fiesta likiendelea jukwaani usiku huu kwenye viwanja vya Lidaz Clud,Kinondoni jijini Dar.
Umati wa watu uliofurika usiku huu ndani ya viwanja vya Lidaz Club,wakishangilia majotro yanayaoendelea hivi sasa,ama kwa hakika ni full kujiachia watu ni wengi na ulinzi upo wa kutosha kabisa.