Ankaal Assalam Alaykum,

Natumaini unaendelea kama kawaida kutublogua hapa kwenye blogu yetu huku ukiendelea kula ubaridi wa huko Swiss.

Tuachane na haya hebu hapa wadau tupate kushauriana hili jambo la mgomo unaoendela wa madaktari wetu hapa Tanzania.

Binafsi nafikiri hawa madaktari wanaoendelea na mgomo hawaikomoi serikali yetu ama viongozi bali wanatuumiza sisi wanyonge ambao Hospitali zetu ni zile za umma.

Wadau hivi nitajiwe hapa mtandaoni kuna kiongozi gani mkubwa ambaye amepata kuugua yeye binafsi akahudumiwa hospitali mathalan Mnazi Mmoja,Mwananyamala n.k?

Wote wakitokea kuumwa basi hospitali zao ni Aga Khan, Lugalo ya Jeshi ama moja kwa moja nje ya nchi.

Imekuwa tamaduni iliyozoeleka kwa wakubwa kupata matibabu nje ya nchi na si wa serikali ya CCM tu bali hata wa vyama vya siasa vyenye nguvu kama Chadema,ni karibuni tu Mhe.Zitto Kabwe ameuguwa na katibiwa Aga Khan na India si yeye tu Profesa Mwandosya na Dokta Mwakyembe matibabu yao yalifanyika nje, ninaamini pia watanzania wengi wanayapata kila siku na wanashindia katika vijihospitali ambavyo kupata matibabu ni dili na hata dawa utaambiwa hakuna lakini mbaya zaidi hao hao madaktari ambao si haba tunawategemea leo hii wanagoma mgonjwa anateseka.Hao viongozi wanaowashinikiza wakae mezani wote wakiumwa hata mafua tu wanatimkia Ulaya na India.

Mbaya zaidi kuna watu upande wa pili wanataka kuingiza siasa katika hili mfano mmojawapo juzi Mhe Mnyika amezungumza kwa anachokiita ni tamko la CHADEMA kuwa anaunga mkono na mbaya zaidi anadai Mkuu wa nchi yupo nje asingeenda angebaki kutatua suala hili,binafsi najiuliza kwani Rais ndio anafanya kazi zote peke yake?

si amewateuwa Mawaziri na viongozi mbalimbali kumuwakilisha?Mhe.Mnyika aache utoto na usiasa katika hili alete hoja za msingi kwa maslahi ya watanzania na aige mfano wa vijana wenzake kama Mhe Zito ama Mhe Januari sio kila kitu siasa tu uonekane unajua kuongea.!

Huyu ni kiongozi wa jimbo ambalo nina imani pia kuna wagonjwa wengi ambao wameathirika na maradhi na wamekosa huduma kwa ninaouita ujinga wa hawa madaktari wetu ambao wote wamesoma kwa kodi yetu walalahoi hakuna hata mmoja amesoma kwa gharama yake au gharama ya kiongozi wa nchi lakini leo hii sisi tuliowasomesha wanatuua kwa ugomvi wao na watawala .

Watanzania tunakatwa kodi zetu kuwasomesha wauaji! ni hatari sana kutengeneza kundi hili la wauaji ambalo halifai hata kidogo kuungwa mkono hata kama wana hoja za msingi hawakupaswa kutufanyia hivi sisi wanyonge.

Leo madaktari ambao kwa namna moja ama nyingine ni watu muhimu kwa jamii wanagoma na watanzania wasio nacho wanateketea na baada ya siku 2 wanafuta mgomo wao baada ya kumaliza tofauti zao na serikali,je na walimu ambao ndio daraja kuu nao wakigoma tunasemaje?na baada ya hapo watagoma watu wa vyombo vya usalama.

Leo hii mtanzania wa kawaida kipato chake ni kidogo sana kwa siku na achilia mbali mshahara anaopata toka sekta binafsi unaishia katika kununua vifaa vya shule kama box ya rimu na madaftari kisha anakumbana na nauli za daladala kwenda kibaruani anakuwa na subira lakini huyu Daktari anayegoma ukiangalia kima cha chini kama kuna wanaopata chini ya Tsh 500,000 sidhani bado hawaridhiki na hilo wanaleta ukatili wa kugoma je huyu mwalimu anayehangaika na chaki kwa muda wote mpaka wanatoka madaktari hawa mbona amekuwa na subira?

Ningeomba Mheshimiwa Waziri Mkuu awatimue madaktari wote waliogoma na jeshi letu lenye wataalam mbalimbali lichukue nafasi kwa muda kutoa matibabu kwa wagonjwa ama iundwe timu maalum ya kuokoa janga hili linalotukuta walalahoi kisha madaktari hawa wote wafutiwe leseni zao za udaktari na wabaki majumbani tu wakijitibia wenyewe na ama zaidi basi waliohusika na mgomo huu wa uuwaji washitakiwe katika mahakama zetu kwa kosa la mauaji kwa watu wasio na hatia.Pia jamii ya watanzania Misikitini na Makanisani wawalaani madaktari wote hawa kwa Mungu.

Nawakilisha

Wabillah Tawfiq Nangoja majibu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 94 mpaka sasa

  1. Ndugu yangu, asante sana kwa ujumbe wako. Naona kazi uliyotumwa ya kuwavuruga madaktari umeifanya. Kilichopo ni kuwa madaktari hawatatetereka kamwe kwa hoja yako hii mufilisi. Endelea kutetea utendaji mbovu wa viongozi wako wa nchi hii, kwa utaratibu uleule wa "ndiyo mzee" kwa kila kitu

    ReplyDelete
  2. Mimi nawa support madaktari kwa 150%. Ni wananchi wa kawaida haswa wenyekipato cha chini unawaongelea ndio wako wengi Tanzania na ndo walioiweka serikali hii inayojali matumbo ya wachache badala ya kuthamini mchango wa watumishi wa umma kama walimu, madaktari, manesi n.k ambao wanafanya serikali ithaminike.
    Ona leo hii wabunge wanajiongezea posho ya almost 300% alafu watumishi wenzao wakiomba nyongeza ya posho 30% wanafukuzwa. Mimi binafsi ni mfanyabiashara mwenye hela ya kujitibu private ndogo ila inaniuma kuona watu wanasoma 7 yrs alafu wanafanya kazi from 8 to 8 na wanaishia kuwa na maisha duni.
    Madaktari endeleeni kugoma mpaka hao maskini wanaodanganyika na kanga na wali wakati wa uchaguzi wasaidie kuwaondoa mafisadi na hela zinazoibiwa na hao wezi zitumike ku fund nyongeza yenu.

    ReplyDelete
  3. Mimi nawa support madaktari kwa 150%. Ni wananchi wa kawaida haswa wenyekipato cha chini unawaongelea ndio wako wengi Tanzania na ndo walioiweka serikali hii inayojali matumbo ya wachache badala ya kuthamini mchango wa watumishi wa umma kama walimu, madaktari, manesi n.k ambao wanafanya serikali ithaminike.
    Ona leo hii wabunge wanajiongezea posho ya almost 300% alafu watumishi wenzao wakiomba nyongeza ya posho 30% wanafukuzwa. Mimi binafsi ni mfanyabiashara mwenye hela ya kujitibu private ndogo ila inaniuma kuona watu wanasoma 7 yrs alafu wanafanya kazi from 8 to 8 na wanaishia kuwa na maisha duni.
    Madaktari endeleeni kugoma mpaka hao maskini wanaodanganyika na kanga na wali wakati wa uchaguzi wasaidie kuwaondoa mafisadi na hela zinazoibiwa na hao wezi zitumike ku fund nyongeza yenu.

    ReplyDelete
  4. wacha wagome serikali imeshindwa kuwajali madaktali wake mpaka inaruhusu wananchi waende loliondo amabako inajua hakuna tiba yoyote zaidi ya utaperi, sasa kama babu anatibu na viongozi na wananchi wote wamepata kikombe kuna haja gani ya kwenda hospitali? wabunge wamejiongezea $ 200 kwa siku wanapokuwa kwenye vikao je ni $ ngapi wameongeza kwa madaktali walimu police na wafanyakazi wengine wa serikali? ninawapongeza wote madaktali kwa kugoma mtu akizidiwa aende loliondo babu haja goma kutoa tiba. Nawakilisha....

    ReplyDelete
  5. Mdau umetoa maoni na tunalazimika kuyaheshimu.
    Siamini kwamba kuna daktari hata mmoja anayegoma kwa nia ya kumkomoa mtu yeyote au taasisi yoyote. Madaktari wanagoma kwa sababu wao ni watu kama sisi na wanapata matatizo kama sisi. Watalipia vipi watoto wao ada za shule kama hata pato lisilo na nyongeza hawalipati hata kama wangependa liongezwe?
    Tunaweza tukajidanganya kwamba vigogo wote wanatibiwa hospitali za binafsi au nje ya nchi lakini kama na wao ndivyo wanavyofikiria basi wanajidanganya. Mama zao na baba zao wengi wapo mikoani na wanategemea hospitali hizi hizi tunazozitumia kama kituo cha kwanza kabla hawajaenda kwenye hospitali za binafsi. Mgomo unatugusa wote.
    Nikumbushe wadau pia kwamba hawa madaktari hawajasoma bure kihivyo. Serikali itawadai wengi wao walipe mikopo waliyochukua ili wasome, tena kwa nguvu na vitisho. Watadaiwa kwa nguvu kuliko nguvu inayotumika kupambana na mafisadi wanaotuingiza kwenye mikataba ya hovyo; mafisadi waliosoma bure enzi za Mwalimu.
    Sisemi kwamba naunga mkono au naupinga mgomo huu maana kuna mambo mengi hatuyasikii kuhusu kinachoendelea. Ambacho nasita kukifanya ni kuwalaani hawa madaktari. Kama tunataka kulaani watu basi tuwalaani wote waliotuingiza kwenye mikataba ya hovyo ya madini, tuwalaani wote wanaokula hela za Richmond, waliokwapua hela za EPA nk. Hao ndio wauaji maana kama wasingetutia hasara taifa lingekuwa na hela za kuwalipa madaktari, walimu, manesi na wafanyakazi wote wanaojenga nchi hii kwa bidii. Serikali ingekuwa ina hela za kuhudumia hospitali zetu.
    Suala la JK kwenda ng'ambo sio geni wala tusilizungumzie kwa kushangaa. Tulipompigia kura tulitakiwa kulitarajia hilo. Watu walikufa kwa mabomu yetu wenyewe huko Mbagala yeye akatimkia ng'ambo, itakuwa mgomo wa madaktari?
    Nawasilisha.

    ReplyDelete
  6. Nakuunga mkono kabisa. Hakuna hata kigogo yeyote anayejua matatizo ya madaktari na hospitali zetu. Wao wanaenda India au South Africa. It is the only country in the world iwht Medical attaches in India etc etc. Labda na wabunge nao wangegome maana Pinda hajasaini ma-allowance yao. It is a joke. The govt should settle this immediately. Wabunge wanalipwa hela nyingi sana ndio maana unaona maprofesa, waganga etc wameacha kazi zao na kuenda kwenye siasa. Come on Pinda, tell us the truthe. Look at the Harambee they are conductionf, they give away millions.

    ReplyDelete
  7. Hawa ndio wale Masaburi anasema wanafikiria kwa kutumia makalio.. Umesoma vizuri wanachokidai maDr? Umefuatilia kauli zinazotolea na viongozi wako ambao unasema hata kama Vasco Dagama hayupo wanatakiwa kutekeleza wajibu wao waliopewa? Kaa ukijua hao MaDr hawalalamikii posho pekee bali uboreshwaji wa mfumo mzima wa afya, ushajiuliza kwa nn hata hao unaosema wanaumwa mafua kwa nn wanaenda ng'ambo? Unahisi hakuna MaDr au ni huduma mbovu ambazo mlalahoi wa kawaida anaipangia foleni? Ndio tunajua kuna watu wanaathrika na mgomo huu lkn kaa ukijua hata maDr wakiwepo wodin na huduma ni mbovu wataendelea kufa? Ushaawahi fika mwaisela, sewahaji, Kibasila ukaona mafuriko ya wodi na watu wengine kulala uvunguni mwa kitanda? Anza kuilaumu uongozi wa serikali yako kwanza kwa kuweka sera na kutokuzitekeleza, hivi unahabari kuwa hao unasema ni wauaji walikaa 3month bila mshara na walikuwa wanaingia wodini? au ulitaka wao wafe kwanza ili wagonjwa wajitibu? Next time njoo ukiwa umefikiria na kichwa ulichopewa na mungu kwa kufikiria na sio hicho kichwa chako ndani ya pant,...!

    ReplyDelete
  8. Huna adabu na hujui ulisemalo! Madaktari wanapigania siyo maslahi yao tu, bali pia kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa kawaida wasio na uwezo! hao viongozi wa serikali hawatibiwi katika hizo hospitali zetu kwa sababu wanajuwa hamna kitu huko ndio maana wanaenda private na nchi za nje! Nilitegemea wananchi muwaunge mkono madaktari katika hii vita kwani matokeo yake ni kwa faida ya wananchi wote. Katika vita lazima watu watakufa,bila kufanya hivi basi mutaendelea kufa na kupata huduma duni milele! huu ndio muda wa kufanya mageuzi wananchi katika sekta ya Afya, tuwaungeni mkono madaktari katika vita hii!

    ReplyDelete
  9. kaka michuzi tunaangalia ugumu wa kazi ,huwezi fananisha mwalimu wa shule ya msingi aliyemaliza form four akaenda crash program na kisha kuanza kufundisha ,eti ajifananishe na daktari mimi binafsi sikubaliani na hili,daktari ambaye amesoma masomo magumu si chini ya miaka mitano.na pia hii kazi kaka ni risk kubwa ni vile jamii haielewe na ngumu kuelimisha katika hili,everytime ua treating a patient is risk ,coz u never know some have TB n lots of airtransmitted diseases but point yangu ya msingi ni kwamba hakuna uwiano katika ugumu wa kati ya daktari na ualimu.
    AHSANTE.

    ReplyDelete
  10. hujui unachokisema bwana mdogo! Mungu akusamehe sana. maskini unaandika andika tu ovyo ovyo huna hoja na sijui michuzi nawe unachuja au unabandika tu? mi nawaunga mkono madaktari km huruma wanayo ndo mana wametibu watu muda wote kwa hali ngumu, km kufa serikali ndio inaua saana, wacha wagome ili wapumbavu kama wewe mjue ni jins gani serikali yenu ilivyo chafu ili mjiunge nao kutatua tatizo, wana madai ya msingi sana, GOMEENIIIII BULLSHIT

    ReplyDelete
  11. hivi ndugu uliyeandika hii habari uliweza hata kufikiri kabla ya kuanza kumwaga wino wako na kuandika mambo haya!!? je unajua ni miaka mingapi daktari anasoma mpaka kuweza kupata cheti cha kuitwa daktari?, je unadhani hawawezi kusoma kozi fupi kama za bank na kukusanya mshahara mnono kama wenzao? je unajua kuna magonjwa mangapi ya kuambukizwa ambayo yanaweza wakuta katika mazingira ya kazi zao? je kuna lawama ngapi zinazowakuta toka kwa raia wakati vifo vinavyotokea huku raia wasijue hata uhaba duni wa vifaa kuwa nao unachangia? je wajua kuwa ndo kazi inayoongoza kwa kuchukuliwa wake au waume zao kutokana na ubize walio kuwa nao?...kifupi madaktari hawathaminiki nchini kama wanavyosaminiwa kwa nchi za wenzetu na kamwe usifikilie tu kumfukuza kazi daktari ni raisi tu kama kubadirisha nyanya sokoni...udaktari si kazi ya kitoto ya kuleta bra bra. kama madaktari hawatapata motisha toka serikalini ni vipi tutaweza washawishi vijana wa kesho kujiunga na udaktari wakati wakijua kabisa ni kazi isiyo na maslahi..mwishowe wote tutakimbilia kwenye biashara na hospitali zikabaki hazina watu.KWA PAMOJA TANZANIA INAWEZEKANA.

    ReplyDelete
  12. ndugu kama unaandika hivi kwasbb unafikiri kila daktari kasomeshwa na kodi yako nataka nikwambiw wapo walojisomesha , kwa hiyo go to school and learn more ili siku ingine uje na hoja ya muhimu, walimu walishagoma zamani kama unafikiri hawakugoma, ndo mana hata elimu kila kukicha inadidimia, sema hawa madaktari wakigoma effect inaonekana haraka, ni watu muhimu kwa namna yoyote ile na tuna wahitaji kazi yao ngumu kwa hiyo lazima waboreshewe mishahara na sehemu za kazi, watu wanalala wanne kitandani wengine chini, daktari anafanya kazi kama yuko sokoni dawa hazipo vifaa vinaharibika habitengenezwi, hiz kero zote hajasababisha daktari bali ni serikali yako! nafikiri huyu aliyeandika ana mental disorder, angekaa achambue system zaidi

    ReplyDelete
  13. Jamani madaktari wakigoma wanaonekana wamefanya dhambi. Kama serikali ingekuwa makini wangemaliza tofauti zao katika mazungumzo lakini serikali yetu ni kichwa maji, haitaki ushauri. Wanasingizia kuwa wanalipwa mshahara mkubwa kuliko watumishi wengine. Kama serikali inaona mshahara ni mkubwa mbona wabunge walijiongezea posho kwa madai kuwa maisha ni magumu wakati mtanzania wa kijijini ndiyo ana maisha magumu kupindukia. Hilo wewe mdau hukuliona, au baba/mama yako ni mbunge? Serikali yetu ni jeuri haiwajali waliopo chini. Mifano ipo; walimu kutolipwa stahili zao na wakigoma wanatishiwa kufukuzwa. Matokeo walimu hawafundishi na shuleni wanakwenda lakini hilo hamlioni kwa sababu mwanafunzi anakufa kielimu. Anayekufa kimwili ndiyo mnaona madaktari hawana utu. Wasio na utu ni serikali, tukishawapatia ulaji kwenye kura wanatusahau mpaka uchaguzi mwingine. Wapo wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, hawakulipwa mpaka walifikia kulala barabarani pale Salender Bridge. Sijui kama wameshalipwa na wengine mpaka mauti yamewakuta bila kupata haki yao. Serikali yetu inajifanya kiziwizi haisikii vilio vya watu wake. Waacheni madaktari wagome kwa kuwa serikali yetu ni sugu na migomo. Halafu hao madaktari wa Jeshi unaosema wapo wangapi ukilinganisha na idadi ya wagonjwa hap Tanzania. Iambie serikali unayoitetea iache kiburi izungumze na madaktari. Huyo Waziri wa Afya hafai kwanini anakaa kuzungumza na waandishi wa habari wakati waliogoma wapo hapo hapo Dar. Inaonyesha serikali ina makosa na imeona kuzungumza na vyombo vya habari ndiyo mtindo wa kumaliza kero.

    ReplyDelete
  14. A crap hoja i have ever read....doctors have been taken advantage by their employer(govt) for so long.they work under very poor conditions....they have exhaust all other means to better their working conditions...they hsve been volunteers for do long

    ReplyDelete
  15. Alaykum Salaam,

    HIJA YA HAJA:

    Lawama ziwafikie wote pande mbili,yaani MADAKITARI na SERIKALI.

    Walitakiwa watafute njia muafaka ya kufikia malengo, wao Madakitari kudai Mafao yao bila kuathiri huduma muhumu kwa Umma na Serikali kufikia Maazimio yao ya Kiutawala bila kuwaumiza Wananchi.

    ReplyDelete
  16. Acheni ubabaishaji,hilo jeshi lina wataalam wangapi wa afya?Tatueni mambo ya msingi/wekeni mazingira mazuri ya kufanyia kazi.Bongo hii,kila kitu siasa.

    ReplyDelete
  17. MDAU NIMEPENDA SANA COMMENT YAKO HII HUYO DOGO MNYIKA KIMBELE MBELE SANA MGOMO CHUO KIKUU YEYE MUHIMBILI YEYE NA KUMLAUM JK BASI HAKUNA HATA JAMBO ASILO TUPIWA LAWAMA HAO MAWAZIRI WANA FANYA NINI HAKIKA HAO MA DOC WANA KOMOA WANYONGE NA UKIWA NA PESA YAKO UKIENDA HOSPITAL PRIVATE UTA WAKUTA HAO HAO WALIOGOMA WANA FANYA KAZI WAPUUZI WAKUBWA WEZI WA FADHILA FUKUZA WOTE KAZI FUNDISHA ADABU HUO SIO MGOMO HUJUMA ZA SIASA KUMUANGUSHA JK NA ZINATOKA HUMO HUMO KWENYE VYAMA VYAO KAMA SI CHADEMA BASI CCM INAYO GAWA MAFUNGU

    MDAU USA

    ReplyDelete
  18. wananchi wasio na hatia wanaumizwa na serikali hawaumizwi na madaktari.

    hii sasa ni vita kati ya serikali na madaktari na wanaoumia (wasio na hatia) ni collateral damage - inatokea kokote vitani hii (na madaktari kwa wito wao wamekuwa waki-minimize hii angalau kwa kuendelea kuhudumia wagonjwa wenye dharura - bado unasema ni wauaji?

    pesa ya kusomea tuliyokopeshwa tumeshairudisha kwa kufanya kazi katika mazingira magumu na kunyonywa (kwa mshahara na marupurupu madogo)

    ReplyDelete
  19. punguza hasira,hasira hasara la muhimu ni busara zaidi kutumika kwani unvyofikiri kuwatimua ni hoja?common sense is not common to all jaribu kufikiri upya

    ReplyDelete
  20. Nakupongeza kwa uzalendo wako..kiukweli hawa madaktari wamekosa uzalendo ktk nchi hii.Moja kwaninavyo fahamu mimi kila taaluma ina ETHICS zake,migomo nikinyume na ETHICS kwasababu hawa madaktari wanakula kiapo ndipo wanapata kazi hiyo.Pili wamesahau kuwa pesa wanazotaka kupewa zinatokana na walipa kodi ambao leo hii wanagoma kuwatibu sasa je wakifa hawa hiyo pesa wanayotaka iongezeke itatoka wapi na watu ni wagonjwa???.Tatu nina uhakika hata wakipewa milioni kwa wiki haitawatosha maana kipato kikubwa hupelekea matumizi makubwa pia..kumbe hiyo ni tamaa tu ambayo wanatakiwa waichunge hii tamaa na kurahisisha mahitaji yao kama ni swala la kuongeza kipato njia zipo nyingi sio lazima mshahara na posho(ujasilia mali ni moja wapo,ukiondoa rushwa).Nne ktk swala la kudai haki kunanjia na utaratibu maalumu sio vema kutumia njia ambayo itazuia watu wengine wengi kukosa haki zao za msingi,hapa naona huu mgomo unazuia walipa kodi kutopata haki yao ya kutibiwa..kitu ambacho ni kinyume na haki za binadamu.Tano ninaunga mkono hawajamaa kama wasipoludi kazini basi huo ndio uwemwisho wa kazi yao.MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  21. Naunga mkono hola kwa 60% ungemalizia kabisa na way out. Je hoja za Madaktari zina msingi ama la! Na hao waalimu wafanyeje? Lakini ni bora kutizama pange zote za tanzania, nikimaanisha mijini na vijijini, mi nimetembea sana na nimeona mambo ndani ya vijiji na miji kwa hawa hawa wafanyakazi wa umma especilly waalimu na doctors

    ReplyDelete
  22. Huna akili hata robo wewe!! U have missed the point big time

    ReplyDelete
  23. Mtoa hoja anatoka povu bila hoja za msingi.Siku nyingine 'Usiwakilishe'(represent) hoja 'UWASILISHE' (present).Ndugu mtoa hoja, hivi kuna mantiki gani ya kisomi kumlipa mbunge laki 2 kwa siku ili akashauri watu wafunge milango wapigane bungeni, au akashauri wenye virusi vya ukimwi wawekwe nembo, ilhali daktari anayeokoa maisha ya watu (wewe unamuita muuaji) akilipwa posho ya elfu 10 kwa usiku mmoja anapokuwa kazini? Kuna mantiki gani mkurugenzi wa taasisi mojawapo ya serikali au mkuu wa idara fulani katika wizara kupewa mafuta lita 250 kwa mwezi ilhali daktari anaachwa bila hata lita 1 ya mafuta ili ahudumie wagonjwa wetu usiku wa manane? Mambo mengine si ya kukurupuka na kuanza kuwatukana na kuwakejeli madaktari, madaktari ni watu wazima wenye akili zao timamu, wenye utashi, wenye mahitaji kama mimi na wewe. Wasipolipwa stahili zao wataishije? Ingekuwa ni wewe hujalipwa stahili zako ungeishije? Udaktari ni ajira kama zilivyo nyingine, si WITO pekee. Tusitumie kigezo cha 'UDAKTARI NI WITO' kubana haki zao za kudai stahili zao. Kwa serikali nyingine SIKIVU, ingekuwa imeshawalipa madai yao na kusitisha migomo isiyo ya lazima. Lakini kwa serikali yetu iliyojaa wachumia tumbo na vilaza, wanatumia mabavu kubana haki za madaktari hawa na wafanyakazi wengine. Kwa namna hiyo hatuwezi kufika tunakotarajia kamwe. Msishangae siku chache zijazo wakagoma wengine ambao si madaktari. Kazi ipo

    ReplyDelete
  24. wewe utakuwa umetumwa na serikali na ni miongoni mwa mafisadi mnaoula jasho letu. Bila kugoma unadhani haki yao watapata wapi. Kila anayegoma lazima kuna wanaoadhirika. n***o

    ReplyDelete
  25. Nakuunga mkono mtoa hoja, walichofanya madaktari sio ubinadamu,maana kuna njia nyingi za kudai maslai bila kuathir watu wengine? inasikitisha sana

    ReplyDelete
  26. Mdau uelewe kwamba ni lazima haki itendeke kwa pande zote, inawezekana njia waliyotumia madaktari haikuwa sahihi lakini ni muhimu tukaelewa kwamba hoja zao ni za msingi hasa ikizingatiwa kwamba wanaona serikali inatumia pesa nyingi kwa shughuli ambazo hazifai kupewa kipaumbele (wote tunafahamu shughuli hizo) wao wanaambiwa serikali haina fedha. Madai yao ya kupewa TZS 10,000 kama posho ya "on call" ww ungeambiwa uamke usiku kwenda kazini kwa pesa hiyo ungekubali wakati unajua mamilioni yanatumika kwa mambo ya hovyo? Lazima serikali ifahamu kwamba daktari hawezi kulazimishwa kufanya kazi maana kazi hiyo inategemea utaalamu wake na utashi sio kulazimishwa. Naona kuna janga kubwa linakuja kimya kimya ambalo serikali imeamua kulitengeneza kama wataalamu hawa watalazimika kwenda kazini bila utashi wao. Kwa kuwa viongozi wetu hawatibiwi ktk hospitali hizi hawajali yatakayotokea.

    ReplyDelete
  27. Sawa kabisa naungana nawe. Sisi watu wa hali ya chini, tunategemea huduma toka hospitali za serikali, Je wagonjwa wanahatia gani? Asante kwa hoja hiyo, na naungana na Waziri Mkuu pia, hata waliostaafu pia waitwe waungane na Madaktari hao wa Kijeshi.
    Mama G.

    ReplyDelete
  28. Sheikh naona umetumia jazba kubwa sana,lifatilie hili suala kwa umakini utaona serikali ndio ina makosa,sbbu madaktari hajakurupuka kugoma tatizo lipo kwa Katibu na Naibu wazir wa Afya,walionyesha dharau za wazi kwa Madaktari.

    ReplyDelete
  29. Nawewe inabidi ujadiriwe ,Kama unajua Rais anawawakilishi wake kwanini akuwatuma wamwakilishe mkutanoni? Naye kama mkuu wa nchi atatue matatizo ya ndani kwanza.

    ReplyDelete
  30. Kla mtu ana uoni wake katika hili nami pia ningependa kuwaunga mkono madakitari kwa mgomo wao na pia kuwashauri wafanyakazi wa idara zengine za serikali kama vile walimu kuwaunga mkono.........hivi juzi tu waheshimiwa wabunge wamejiongezea posho kutoka 70,000/= hadi kufika 200,000/= huu ni uungwana kweli wakati mwalimu anapata chini ya hapo kama mshara wa mwezi na mbunge anapata hiyo kama posho!? jee huu sio kinyume na uungwana halafu huwa wanashinikiza tu na yanatekelezwa tena bila hata kujadiliwa...kama haitoshi waziri analipwa mshahara kama waziri na posho na marupurupu mengine halafu analipwa kama mbunge mshahara na marupurupu mengine jee hiyo ni sawa halafu kuna wabunge hawana taaluma yeyote ukilinganisha na hadhi wanayopewa ukilinganisha na "maprofesheni dokta wetu" ambao mgomo wao unaonekana kituko....nawasihi endeleeni na mgomo mpaka mupate haki yenu ya msingi wanajeshi madokata hawawezi kutosheleza huduma za hospitali zote nchi isitoshe wengi wao ni wataalamu wa majanga ya dharura kutokana na mazingira ya kazi zao hawawezi kukaa na wagonjwa kitambo ambacho madaktari hawa wanakaa nao serikali iache kukwepa jukumu itimize wajibu wake iache vitisho...."the right is taken and not given" stand for your right.....kimahesabu idadi ya wabunge na gharama zao ukilinganisha na idadi ya madaktari na gharama zao wanazo hitaji nikituko kuona kwamba serikali huku haitaki lakini kule bungeni ni poa kila litakiwalo linawezekana tena kwa kodi za hao hao madakitari na walimu na watumishi wengine wasiothaminiwa......nasikitika kuona kwamba ndugu zetu wasio na hatia wanapoteza maisha yao kwa hili lakini tusiangalie tulipo angukia tuangalie tulipo jikwaa.

    ReplyDelete
  31. NIMEITAMANI SANA HII HOJA YA HAJA
    mimi ninavyoona katika hili kuna matatizo mengine sio hayo wanayodai madaktari wetu,sababu huu mgomo haukuanzi kwao sasa baada ya maktari wanafunzi kugoma nao wakaleta madai yao,je wakitekelezewa wanaweza kutuambia watanzania kwamba watarudisha roho za waliofariki,je taasisi nyingine zikigoma wao wataweza kutimiza wajibu wao kutibu wagonjwa,mf.tanesco,dawasco,vituo vya mafuta,makampuni ya simu,daladala,na wengineo.wao wasijione bora kuliko watanzania waliojitoa kuwasomesha. nawasilisha

    ReplyDelete
  32. Wabillah Tawfiq, wewe hujawahi kuwa Dactari ndio maana unaongea ongea hayo, Mbunge Mnyika alichosema yuko sawa sana na wala hajaonesha utoto bali ukomavu wa fikra, raisi ndio ana wasaidizi wengi lakini kauli yake moja ina nguvu zaidi ya wasaidizi wake elfu moja. Kama ilimlazimu kwenda huko basi angalau angezungumza lolote kuhusu hili ili tujue raisi anamsimamo gani juu ya hili, kuliko kuwahi kwenda kukaa na watu ambao nchi zao hazina migomo na madaktari wanalipwa mishahala ya juu sana. Kama ningekuwa raisi leo, ningefanya juu chini Waalimu, Askari, Wanajeshi, Wanasheria na Madaktari wanalipwa mishahara ya juu kuliko mtu yeyote katika nchi hii, hata wabunge wangetamani kwenda kufundisha primari halafu tungeona nani atagoma.
    Alpha Amboklie.

    ReplyDelete
  33. unasubiri majibu ya nani wakati unaandika pumba tu!!
    na uanze kulaaniwa wewe na huyo mungu, deluded,pathetic,short sighted guy uliyekuwa fooled na watawala wako.
    nchi haiwezi kuendelea kwa kuna na myopic pipo kama wewe.

    ReplyDelete
  34. Pole ankal kwa kusoma sana hizi hoja zetu ila mimi nataka kumjibu huyu jamaa aliyepinga mgomo wa madaktari na kuomba tuwalaani.

    pole sana ndugu yangu unaonekana umeumia sana, lakini mimi kwa upande wangu nawasapport hawa madaktari kwa huu mgomo, kwani huoni hayo mambo yanyoendela au ndio umeziba masikio?
    juzi juzi tu hapa wabunge wameongezewa posho %zaidi ya 130, sikukusikia ukisema kitu hapo inamaana na wewe ni mmoja wao!
    madaktari hawakuwa na sababu ya kugoma kama wangepewa stahiki zao ambazo serikali inauwezo wa kuwapa, kunasababu gani ya kuwaongezea wabunge posho kama ile, wakati hapahapa katika hii blogu kuna picha ya wanafunzi wa shule ya msingi wameonyeshwa na jengo lao la shule halitamanishi hata kidogo,
    kiongozi alipaswa kuingilia kati kama mawaziri wake wameshindwa kusuluhisha kwanini aondoke, nia njema kabisa ya madaktari ni kuungana na watanzania wote kuwaondoa mafisadi, nani alikuambia serikali inakaa kusuluhisha kwa amani namna unayotaka wewe? umeona wapi, kwanza kiongozi wahi na chama chake angetupa moyo sana kama asingepitisha zile posho lakini ona kilichootkea sasa, hapo nani anaumia zaidi? laana inamkuta mtu ambaye amekosa kaka, na sasa hawa hatutawaombea laana ila tunaomba kwa Mungu amuongoze raisi wetu afunguke masikio na ktusikiliza sisi wananchi kwani ndio tuliomuweka madarakani. Binafsi sipendi hata kidogo machafuko kwani nimeona hali inavyokuwa mbaya. hali ya mtanzania inakuwa mbaya kila iitwayo leo angali umeme, maji, mafuta, gesi kila kukicha wanapandisha tu kiholela sasa utasema hapo kuna serikali kweli??
    ni mimi mdau mwenye uchungu na nchi.MSUMARI

    ReplyDelete
  35. Umesema kweli, kuna njia nyingi za kudai na serikali ikashikwa pabaya kuliko kukomoa wagonjwa. Hao madaktari wakiugua hawatibiwe kwenye hospitali zetu, wanaenda binafsi na nje ya nchi.

    ReplyDelete
  36. Mdau hoja yako imejaa jazba. Madaktari wana madai ya msingi ambayo serikali inapaswa kuyapatia ufumbuzi. Njia waliyotumia ndio yenye utata kidogo lakini me nadhani walitumia njia nyingine zote ikashindikana. Jaribu kusikiliza hoja zao utawaelewa.

    ReplyDelete
  37. Je sababu gani inawafanya wagome hao madactari? Na serikali mbona haisemi imefanya nini kutatua matatizo yao. Isije ikawa ndio yaleyale ya kupuuza madai yao wakijua hawawezi kugoma>

    ReplyDelete
  38. Kama unafikiri kuwa mgomo huu hauathiri wanasiasa basi wewe kwa maneno ya Nyerere ni mjinga (ignorant). Sasa unataka madaktari ndio wawagomee watu wa usalama na walimu? Wagome na wao. Kama hawagomi, basi wameridhika na wanachokipata. Kuna watu wana mshahara wa lakh 2 lakini matumizi ya milioni 5 kwa mwezi. Watu km hawa wana njia nyingine za kuiibia serikali na miposho kibao. Madaktari hatuko ktk nafasi za aina hiyo. Kama unafikiri madaktari wa jeshi ni wanajeshi tu, si madaktari basi wewe ni mjinga tu. Wakichukuliwa kutoka jeshini, na hospitali za jeshi zitaendeshwa na nani?

    ReplyDelete
  39. wewe pumbavu mbona umeme ukipanda hausemi kitu, mafuta yakipanda kimya, wabunge wanaenda bungebeni kusinzia alafu wanataka walipwe laki 2 kwa siku wala husemi,

    Kama wewe mshahara wako mdogo alafu umeridhika, powa myamaza kimya, waache wanao dai haki zao waseme, kuhusu mnyika kutoa kauli ya chadema hilo wewe linakuhusu nini? siasa ni maisha, mbona ccm kuna mambo ambayo hayahusi siasa wanafanya kisiasa? safari za mawaziri na wakuu wa serikali mikoani ni za kisiasa au kiserikali? mbona wanapokelewa kisiasa zaidi na marangi ya kijani?
    Wakuu wa mikoa na wilaya ni viongozi wa kisiasa au serikali, mbona wengi wanafanya mambo yao kichama zaidi, wengine ni wajumbe wa almashauri kuu ya ccm.

    KUNYA ANYE KUKU AKINYA BATA KAHARISHA.

    ReplyDelete
  40. Nakuunga mkono mdau. tatitizo Tanzania tunaendeshwa kisiasa mno, ni kweli waheshimiwa wangine wanaongeaga ili mradi waongee, anayeongoza ni Lema na Mnyika, Zitto bravo zana, hunyamamza au husema stahili!

    Viongozi wa juu na siku hizi wanashindwa kutoa maamuzi kwa kuogopa upepo wa siasa. hii sio sawa.

    hawa madactary, walijikusanya starlight eti wanamsubiri waziri mkuu wakati huo hata hawajamualika, wanategemea eti kwa vile kuna vyombo vya habari basi ujumbe utafika halafu PM aje! utoto gani huu?

    Baada ya kuona kosa lao hilo wakamtumia ujumbe wa kutaka wakutane, akawaambia wakutane J2, wakaja na hoja eti sio siku ya kazi hivyo hawaendi! utoto gani huu?

    ReplyDelete
  41. Nakuunga mkono mdau. tatitizo Tanzania tunaendeshwa kisiasa mno, ni kweli waheshimiwa wangine wanaongeaga ili mradi waongee, anayeongoza ni Lema na Mnyika, Zitto bravo zana, hunyamamza au husema stahili!

    Viongozi wa juu na siku hizi wanashindwa kutoa maamuzi kwa kuogopa upepo wa siasa. hii sio sawa.

    hawa madactary, walijikusanya starlight eti wanamsubiri waziri mkuu wakati huo hata hawajamualika, wanategemea eti kwa vile kuna vyombo vya habari basi ujumbe utafika halafu PM aje! utoto gani huu?

    Baada ya kuona kosa lao hilo wakamtumia ujumbe wa kutaka wakutane, akawaambia wakutane J2, wakaja na hoja eti sio siku ya kazi hivyo hawaendi! utoto gani huu?

    ReplyDelete
  42. kaka nimekusoma. ila kwa upande wangu madaktari nao watu, kazi wakati nyumbani njaa ngumu. hata wewe hapo unapofanya kazi sijui wasipokulipa kwa haki yako sijui kama kazi itakuwa nzuri na utaifanya kwa moyo. wengi wmeumia kutokana na mgomo ila mtatuzi wa suala hili ni serikali ITOE HAKI na sio kuwatimua maana itabidi waanze kusomesha upyaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa. HAKI TU ndio utatuzi, serikali ione umuhimu wa madaktari sasa

    ReplyDelete
  43. inawezekana una point lakini kwa taarifa yako, hiyo hospital ya Lugalo yenyewe ina Doctors watano tu, waliobaki ni clinical officers wasio na uwezo na hata ujuzi wa kufanya kazi hospitali hata ya mkoa, achilia mbali hospitali ya rufaa kama muhimbili. lakini unavyomlipa dr sh 10,000 kwa kufanya kazi overtime usiku kucha wakati watawala wizara ya afya unawalipa 70,000 kwa kukaa kikao kimoja cha masaa mawili unategemea nini? unahitajika usawa

    ReplyDelete
  44. Madaktari wanaogoma ni mafisadi wauaji wa wazi wazi hata baada ya kupigiwa magoti na Waziri Mkuu wamengang'ania hoja zao ambazo si za ajabu na zinazungumzika. Huko ndiko tuliko. Pesa tu. Nongwa imekuwa wabunge kuongezewa posho. Fihi, wivu, chuki, husda, roho mbaya, uchawi wa kisasa. Yawezekana wanatumiwa.

    ReplyDelete
  45. Ninaamini huyu mtoa mada hajui anachokisema au katumwa awasemee watu fulani!

    Nchi yetu imefika mahala ambapo hakuna jinsi inabidi kutumia nguvu ya Umma pamoja na migomo ili serikali iweze kutambua kwamba watu wamechoka wanahitaji maisha bora.

    Kusomeshwa kwa kodi za watanzania sio hoja, hoja ni kwamba Serikali inawajali na kuwapa stahili zao kama mikataba yao inavyosema? Kwa kweli mimi ninawaunga mkono hawa madaktari kwani watafungua macho kwa tasnia zingine kuiga mfano wa kudai haki zao kwa mwajiri wao aliyeweka pamba masikioni!

    Asakri jeshi wana maduka yao ambayo bei yake ya vitu iko chini, vivyo hivyo kwa polisi...madaktai wanabanana na watu wengine katika maduka ya kawaida hivyo kusema kuwa fani yao ni wito sio kweli! Wanayo mahitaji sawa na watu wengine.

    Mh. Waziri Mkuu alinukuliwa akitetea posho za wabunge...kwa kweli simuelewi na sitamuelewa hata kidogo. Kipaumbele ni kipi hapa?

    ReplyDelete
  46. sijaamini kama na wewe unasupport upuuzi wa serikali,hivi kwa akili yako matatizo wanayoyapata makazini yanaweza kulingana na pesa wanayopata,wanajitoboa,wanakunywa arvs kisa tu alikuwa anamtibu mgonjwa,na hata hiyo hela ya risk hawapewi,put urself in their shoes

    ReplyDelete
  47. jambo usilolijua ni kama usiku wa giza...ungekuwa unajua shida wanazopitia madaktari usingesema hayo ulionena,,,kwenye every fight 4 liberation sacrifices have to be made for changes to take place,,kama wao walioko bungeni wameweza kujinufaisha huoni its only fair kwamba na madaktari wana haki ya kuongezewa posho,,ikiwezekana hata na walimu wagome sababu hii nchi inaendeshwa kwa mfumo duni and unless piple take action tutaishia pabaya,,i totally support them doctors,,4 being a doctor's wife,,,i surelly know what they go thru kila siku

    ReplyDelete
  48. Nadhani fomu za mikopo ya elimu ya juu ziangaliwe upya maana tunawakopesha/kuwasomesha watu ambao hata shule haijaisha sawasawa tayari wameshakuwa mabosi na wanataka maslahi ya ajabu. Wanataka nyumba, magari, mishahara minono n.k. kwa hiyo hii nchi watu ni madaktari tu wengine takataka. Je hawa chekechea wa udaktari kama wanataka 3.5m je super Specialist alipwe ngapi? Bora kutibiwa na mitishaba kuliko madaktari wa aina hii.

    ReplyDelete
  49. ni hivi, serikali ifute ufadhili kwa fani za udaktari wa binadamu ili wajisomeshe wenyewe uone mziki wake??? Hivi tu mnawasomesha hawatoshi je mkifuta ufadhili itakuwaje?? kusoma tu hayo masomo yake inahitaji moyo..nadhani mngewapongeza kwa kuamua tu kujitosa kwenye miso hiyo y mateso. sasa mnawakatisha tamaa...na nyie madaktari mbona bado vijana sana??? akili mnazo nyingi tu...,liyosoma hamwezi kuyasahau...acheni hiyo taaluma mfanye mambo mengine..kwani matajiri wote nchi hii na duniani ni madaktari...tatizo mnauona udaktari tuuuuu..kuna mambo kibao ya kufanya...mkishindwa kwa hili basi hamtaweza tena...Halafu nchi kusomesha wataalamu siyo ombi ni hitaji lake la msingi kwa manufaa ya nchi na siyo eti tumewasomesha....sasa msingewasomesha wataalamu huduma kwa wananchi mnaowatalwala kwa ahadi kibao mngezitoaje??? mimi nadhani KUNA HAJA YA MAPINDUZI YA FIKRA......

    ReplyDelete
  50. Wewe bado una hoja za kukumbatia ujinga na ubinafsi. madaktari wanahaki ya kugoma na leo hii unawaona wauwaji lkn hujawahi kuwaita waponyaji unapopata huduma kutoka kwao.Serikali yako ni ya kijinga na ubabe wa kipuuzi, tena usithubutu kutoa kauli zako za kiupendeleo km hizi...mwanasiasa mkubwa wee! nyie nyie ndio mnaoshangilia nchi yetu inamegwa na mafisadi kila siku watu wakitaka haki mnasema wanavunja amani...sioni msimamo wako ktk hili.Km raia wanajua wanaumia waonyeshe mchango wao kusaidia nia ya madaktari ambao wasaidia sio kuwasaliti kama unavyofanya ww.Hii ni vita ya nchi nzima madaktari ni sample tu...kwa taarifa yako hiyo unayoiita serikali IMESHAKUSALITI siku nyingi.

    ReplyDelete
  51. Mimi naona haya madai ya madaktari wetu sasa yana utata. Mwanzo niliyaona ni ya msingi kabisa lakini jinsi siku zilivyoenda nimeanza kuhisi harufu fulani kama ya ki-harakati harakati vile.

    Kwanza walianza madaktari walio kwenye mafunzo ya vitendo na baadae chama chao ambacho kinawahusisha madaktari wote kikachukua jukumu lakini hapa mwishoni mapinduzi yakatokea sasa wanaoongoza hizo harakati zao wanajiita jumuiya ya madaktari. Kiongozo anayeongoza hizo harakati za hawa madaktari wetu ambao ni waajiriwa wa serikali kwa mujibu wa mtoto wa mkulima si mwajiriwa wa serikali. Inasemekana miaka ya nyuma alifukuwa akiwa mafunzoni na baadae alisamehewa na raisi lakini hakurejea tena kumalizia mafunzo. Hivyo pamoja na kuwa hayupo kwenye orodha ya waajiriwa wa serikali vile vile hakuhitimu huo udaktari wenyewe. Inasemekana ana NGO yake inayoshughulika na Ukimwi. Sasa ndipo ninapochanganyikiwa mtu ambaye si daktari na so mwajiriwa wa serikali anaongozaje harakati za kudai haki za madaktari wa serikali?

    Hivi hapa Afrika kuna nchi ambayo uchumi wake unaruhusu daktari ambaye anaanza kazi kulipwa 17,000,000? Kama ingekuwa inawezekana ningeanza kumfua mwanangu wa chekechea na PCB ili hapo baadae ale kiulaini!!!

    Ingekuwa enzi za mwalimu huyo kiongozi wao angekuwa ashakatwa na kupelekwa central shimoni kupata dawa yake, na akitoka angeenda kumhadithia mkewe

    ReplyDelete
  52. kwa mtazamo wangu mm naona haujui unachokiongea, ni vema ungefahamu kiini hasa cha matatizo haya, kama serikali itaendelea kutumia Kodi zetu kupeleka familia zao na wao wenyewe kwa matibabu nje ya nchi ilihali kuwa kuna Madaktari waliosomeshwa na hizi pesa zetu wakikosa maeneo bora ya kufanya kazi na pia kukosa maslai yanayoendana na kazi zao.. madaktari wana haki ya kufanya hivi na yote yatakayotokea ilaumiwe serikali kwa kushindwa kusiamamia vema utekelezaji wa hudumu muhimu kwa wananchi... Mhe. Pinda ajibu Hoja na sio kutisha watu.
    Mwanaharakati.
    Iringa.

    ReplyDelete
  53. KIJANA UMEKURUPUKAA TENA UPO UPANDE WA SERIKAL.LEO MADR BONGO WANAZALAULIWA SANAA KANA KWAMBA HAWANATHAMANIII HOSPITAL ZETU ZIMEKUA CHAFUU YA JAMAA WANAPIGA MZIGO KWENYE RISK KUBWA SANAA NA HAO JAMAA KWENDA KUTIBIWA NJEE NI DHARAU KUBWA SANAA KWA MADR WA BONGO YANI HAWANAUWEZO AU WAPO CHINI YA KIWANGO NA HUO MSHAARA UKIULINGANISHA NA DR HAUFAI KABISAA NJO HUKU ULAYA UONE DR ANAVYO SAMINIWA NA SERERKALI NA VIWANGO VYA HOSPITAL,NCHI MASKINI WAKATI MADINI KILA SIKU YANAIBIWA..ALAFU NGESOMA HII KOZI UNGEONA MZIKI WAKE..MNAYOYAFANYA MTAJUTAA TZAMENI MALAWI..MDR WOTE WAMEKIBIA NCHI NZIMA INATAKRIBANI YA MADR 150 TU..

    ReplyDelete
  54. wewe mdau uliyoandika hii mada, kweli umechemsha.Hivi unaposema kuwa hawaikomoi serikali (yaani viongozi) bali wanawaumiza wananchi, ni kweli unavyosema, lakini ujue kuwa wananchi haohao ndiyo waliowachagua viongozi haohao wabovu ambao hawawajali wananchi wao.kwa hiyo hilo ni fundisho kwa wananchi kuwa wasiwachague tena viongozi hao wabpovu.Pili wananchi haohao ndiyom hawawachukulii hatua viongozi wao hata kuwauliza tu hadharani kwa nini wao wakiumwa wanakimbilia nje ya nchi kutibiwa na siyo Muhimbili???hebu wawaulize tupate kusikia majibu yao.Kuwafukuza madaktari na kuwanyanganya leseni zao si jibu la matatizo, na wewe mdau unasema eti jeshi letu lina wataalamu, yaani madaktari, ambao waje kuwasaidia kuchukua nafasi za hao madaktari, kwa kweli unanichekesha sana, eti kuna wataalamu!!!!!!!! ama KWELI ALALAYE USIMUAMSHE, UKIMUAMSHA UTALALA WEWE.Rey.

    ReplyDelete
  55. Sidhani kama huyu mtu anelewa kiini cha mzozo huo! nafahamu fika kuwa tunategemeana hata kwa yule anayeuza nyanya kule sokoni.

    Suala sio nani kasomeshwa na nani, suala ni kwamba haki za msingi za mtu ni zipi hasa! sio suala la siasa hapa! leo tunashuhudia madaktari wengi na wahandisi wapo nchi za kusini mwa afrika wakifanya kazi huko wakati sisi tunaimba wimbo wa kuwafanya wao kuwa wazalendo kwa lipi hasa!

    Ama unafikiri ni nani anayetaka kumuhudumia mtu kisha apokee na rushwa ikiwa kama sehemu ya ujira wa kazi yake! Naona wameshazalilishwa vya kutosha kinachotakiwa sasa ni kuchukua hatua.

    Wafanyakazi wa Tanzania leo wanapata mzigo mkubwa wa kulpa kodi kadhaa kuanzia mishahara mpaka kwa wakati wa manunuzi mbalimbali, wakati wale wengine wanaojiita sekta isiyo rasmi wananeemeka kwa kutokubanwa kwao,nani mwenye magari mazuri ama nyumba nzuri leo na mitaki kedekede kama sio wafanya biashara? Nafikiri umefika wakati wa watu kupanga bei za taaluma zao, wengine Bungeni kule wameshaonyesha mfano!

    ReplyDelete
  56. Nakubaliana na wewe mtoa hoja.

    Kinachonisikitisha ni kuwa baba, babu na bibi zangu kule kijijini wamekatwa kodi zao ili kufundisha hawa jamaa bure, elimu ya chuo kikuu kwa miaka mitano. Leo hii wao ndiyo wamewapa mgongo - masikini weeeee!

    Madaktari kuweni na ubinadamu, ni kweli baadhi ya madai yenu ni sawa lakini mumesahau kwamba nyinyi hamuwezi kujifanya muko free sana kwani mumesomeshwa kwa fedha zetu sote walipa kodi.

    ReplyDelete
  57. Wilson KashalabaJanuary 30, 2012

    Mtoa hoja naomba unapokuwa unatoa hoja usijifikirie wewe tu. Ni kweli kwamba wanachi wanapata shida kutokana na mgomo wa madaktari, ila kumbuka kuwa kabla ya huu mgomo serikali ilileta mambo ya siasa katika taaluma ya Udaktari. Jambo la muhimu ilikuwa ni Serikali kuwalipa malipo waliyokuwa wanadai Wanafunzi madaktari na baada ya hapo kusingelikuwa na Mgomo wowote. Walichokosea Waziri wa afya, Naibu wake na Katibu Mkuu wa Wizara ni kuwadharau wale vijana halafu wakatoa maamuzi ya kipumbavu eti wakawaondoa Pale Muhimbili na Hapo Madaktari wote wakaona wamedharilishwa. Mimi maoni yangu kwa wanajamii ni Kuwa Viongozi wetu waache kuyachukulia mchezo mchezo matatizo ya watanzania kwa kufanya maamuzi ya kisiasa. Sasa kama walikuwa hawana Pesa ya kuwalipa hiyo pesa waliyolipia timu nzima ya Rais Kwenda Uswisi wameipata wapi? Hivi ni lazima kwa Rais wetu kwenda kwenye kila mkutano anaoalikwa? Mbona marais wenzake wanatuma waakilishi? Tuwe wakweli na Tuilekebishe Serikali
    yetu na Siyo kuwalaumu Madaktari.

    ReplyDelete
  58. Hujui unachokiongeaa na wasiwasi hata na uwezo wako wa kupambanua mambo. Utafukuza madaktari unafikiri ni kitu rahisi? Nchi inayokabiliwa na uhaba wa madaktari ukifukuza utapata wapi mwingine? Acha kuongea na bila kutumia common sense. Reason kijana sijui ndo mzee. Hawa jamaa wakiamua kwenda nje ya nchi wanahitajika sana na je mtawalaamu kwa kwenda kutafuta green pastures? Nashauri wakiwatimua nendeni kusini mwa jangwa la sahara South africa na Namibia madaktari mnahitajika sana na kuna green pastures nzuri sana. Kama kiongozi hajali mwananchi akifa ya nini daktari ajali. Acheni unafiki. Tatizo ni viongozi wenu wanasiasa wasiokuwa na uzalendo na nchi na wala msitake kuwafanya madaktari waonekane wabaya mbele ya wananchi

    ReplyDelete
  59. Ndugu fahamu chokochoko yote hii imetokana na posho za Waeshimiwa Wabunge.Maisha magumu kwa wote.

    ReplyDelete
  60. Napenda kutoa mchango wangu na mtazamo wangu juu ya hili swala la mgomo wa madaktari....Mimi naweza sema alichosema muweka hoja ni sawa kwa upande mwingine wa coin,ila tukirudi huo mwingine wanahaki,kama kwa mtizamo huu umekubali mbona hukusema posho za wabunge zisiongezwe na baadala yake zikaongeze majengo hospitalini na madawa ambayo yangeongeza ufanisi wa madaktari?Hivi inafurahisha uende hospitali dokta agundue ugonjwa halafu akwambie dawa hamna au ulale chini?Kama sio kuwaaibisha hao hao madaktari ni nini?Wao huingia kazini usiku kucha na kuchukua risk ya magonjwa wote,ila kwanini sasa isifike wakati serikali ilipatie hili nalo ufumbizi wa haraka?Ni hayo tuu mdau.

    ReplyDelete
  61. Mtoa mada wewe ni CCM na wacha kuleta siasa zako vile vile.Huwezi kusema kodi za watanzania zinawasomesha wauaji huu ni unafiki.Umeyapitia madai ya Madaktar ukaona wanachodai?Km ungekua mzalendo na mwenye busara unapaswa kuilaumu sekali kwa sababu pamoja na madai mengine ya madaktari lakini pia yapo madai yakutaka vifaa bora na mazingira bora yakuwatibu wagonjwa mfano mashine za vipimo na vitanda ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
    Ninachokiona hapa kwenye hoja yako ni u CCM wako,mm nakubaliana na ww kuhusu mnyika kwamba amekosea lkn hata na ww siasa inakusumbua.Madaktar hawakugoma ili kumnufaisha yoyote katika wanasiasa bali wanataka sekta ya afya iboreshwe kwa ujumla wake km utayaangalia madai yao kwa umakini.
    Hivyo basi na ww acha utumwa wakichama bali yaangalie mambo ukiwa na ubongo huru usiofungwa na mapenzi na chuki binafsi.Unalaumu madaktari wanauwa wanyonge lkn hulaumu wanaotoa kauli za kejeli kwa madaktari wala huhoji kwanini hao viongozi waserikali wasitibiwe ktk hospitali za bongo.Hii ni kwa sababu hao mawaziri wanajua wazi udhaifu wa sekta ya afya tz ndio maana wao hawatibiwi hapo.

    Mdau Ubatani.

    ReplyDelete
  62. Nakubaliana nawe mdau kuwa mgomo wa madaktari umewaumiza zaidi wenzetu ambao wanategemea zaidi hospitali za serikali na mbao hawana uwezo wa kwenda kwenye hospitali za kulipia. Ukiangalia migomo wanayofanya wenzetu, nchi zilizoendelea, na hasa kwenye sekta muhimu kama hiyo ya afya, transport, etc migomo yao huifanya kwa muda mfupi kwa mfano hugoma kwa siku moja hadi tatu, lakini baada ya hapo hurudi kazini na kuendelea shughuli kama kawaida. Kwa vile nia ya kugoma ni kuonyesha umuhimu wa wafanyakazi wa sekta hii ambapo kutokuwapo kwao hata siku moja kazini kunaleta upungufu mkubwa. Hiyo migomo ya siku chache inaleta impact kubwa na inakuwa kama taser gun kwa serikali kuwakumbusha kuhusu kuto-take ajira za zao for granted. Kuweka migomo ambayo inakuwa indefinite kwa kweli inawaweka madaktari katika muonekano mbaya kwa jamii hata kama madai yao yalikuwa yana haki zote.

    Lakini kwa upande mwingine, nadhani serikali nayo inabidi ijifunze kutokana na mgomo huu, kwani kama wahusika serikalini wangeshughulikia madai ya wahusika mapema, bila shaka tusingefika hapa. Mwanzoni, kwa uelewa wangu, shida ilikuwa kucheleweshwa posho za interns, ambayo ikasababishia wao kugoma. Mgomo wa madaktari haukuwepo wakati huo. Lakini cha kujiuliza ni kwanini posho zao zichelewe? Wao on daily basis wana-deal na pyschological stresses za kuwahudumia wagonjwa ambao wengine ni mahututi, sasa iweje umuongezee stress nyingine ya kutojua yeye au familia yake atakula nini eti kwa vile posho imechelewa? Sidhani kama posho za viongozi, wabunge zinacheleweshwa kwa namna hiyo. Kwa nini? Ni kwa vile wanathaminiwa. Seriously serikali inabidi kujifunza na sakata hili na kuwachukulia wahudumu wake wa serikali kwa umuhimu unaostahili na sio kusubiri mpaka crisis itokee.

    Binafsi nilikuwa na-sympathise na madaktari kwa siku zile chache za mwanzo, lakini sasa naona unakuwa ni ukatili wa hali ya juu kuendelea na mgomo indefinitely given wagonjwa wasiokuwa na hatia wanazidi kupoteza maisha na ndugu zao kuwa tortured psychologically. Put yourselves in their shoes, how does it feel to see your beloved one dying needlessly and you can do nothing about it?? Unamtoa mahala ambapo ulitegemea maisha yake kuwa saved, na kumrudisha nyumbani unamuona akifa ukimuangalia, na huna uwezo wowote.. Just think about it..

    ReplyDelete
  63. Kaka hicho ni kilio cha samaki.

    Kwa akili ya kawaida tu,ukichukua madaktari wa jeshi wakahudumu hospitali za kawaida bado tatizo linakuwa palepale kuwa madaktari wamegoma. Kila siku tunalia kwamba tunaupungufu wa madaktari,leo hii anakuja mwanasiasa anatangaza eti madaktari wanajeshi wahudumie wagonjwa!Hao madaktari wa kijeshi si wapo mda wote lakini bado ukiwaweka hao pamoja na waliogoma bado hawatoshi.Au mnataka kutwambia kusipokuwa na mgomo madaktari wa kijeshi hawahudumii wagonjwa na badala yake wanajikita kulenga shabaha?
    Hapa ishu ni Serikali kuwasikiliza hawa jamaa na kuacha jeuri za kitoto kwamba eti mtaleta wanajeshi.

    Otherwise tumwombe Mungu tu tusiugue katika kipindi hiki manake ukithubutu tu imekula kwako
    !

    ReplyDelete
  64. Wewe mtoa mada ni mnafiki tu.Mimi sio dkt but madaktari wana haki ya kudai maslahi na malimbikizo wanayoidai serikali.Kwanini serikali isiwalipe malimbikizo na mishahara at least unaoendana na hali ya maisha ya sasa ukizingatia wanafanya kazi muda mwingi, yenye lawama na kwenye mazingira hatarishi. Pia madai yao kama ni hela ndogo sana ukizingatia na usumbufu wanaoupata.Yes, ni kweli mnyika nae ni mnafiki kama wewe coz anataka kupata umaarufu usio na tija kupitia vitu kama mgomo badala ya kufuanza na matatizo ya jimboni kwake.
    Matatizo yote haya yanaletwa na uwajibikaji mbovu wa serikali coz serikali inawekeza kwenye politics badala ya kuwekeza kwenye elimu, health, miundo mbinu na mengineyo ya msingi.Ni serikali ya kifisadi coz ina-neemesha wachache walioka kwenye "system".Haya matitazo ya mgomo wa dkts na walimu hayajaanza leo, na serikali haionyeshi dalili zote ya kukabiliana na matatizo haya.cha msingi ni kuindoa hii serikali isiyotujali. Na ukiangalia kwa makini utaona walalahoi wengi ndio waliingiza madarakani halafu leo tunalamika. Sasa tunamlalamikia nani ? Acha tufe mpaka tushike adabu labda kizazi kijacho ndio kitaamka. serikali imeingia madarakni kwa 80% za walalahoi.

    ReplyDelete
  65. Mungu akusamehe maana hujui ulisemalo
    na mbaya zaidi hujui jinsi ya kuwakilisha mawazo.

    ReplyDelete
  66. kwa uelewa huu watanzania we have a very long way to go!

    Mungu wabariki Watanzania
    Mungu ibariki Afrika.

    ReplyDelete
  67. Ni hoja isiyona mshiko. Serikali inatakiwa kuwasikiliza madaktari na kushughulikia matatizo yao haraka. Mbona ikusherewa kuwaongezea wabunge posho from 70000-200,000tsh?. Hao madaktari wa jeshi/polisi mnaowataka kuingia kazini wako wangapi? je watatosheleza hospitali zote Tanzania?. Unamfananisha Daktari na mwalimu wapi na wapi? That why hata Pinda kawapiga mkwara jana akidhania anaongea na walimu-ameshamsha sana na amejidhalilisha sana. Na ameonyesha anaupeo mdogo.

    Unamshauli pinda awatimue madakaktari wote waliogoma, je hapo atakua ametatua tatizo au anazidisha tatizo? Ubabe hautasaidia wanaokufa ni raia, kwa kutokua na serikali sikivu.
    Hoja yako ni ya enzi za mwaliu, kwa sasa watanzania sio mabwege tena, hawadanganyiki. All the best madakatari endeleeni kudai chenu, watanzania wote tupo nyuma yenu.

    Sitashangaa michuzi ukiiminya hoja yangu kwa sababu upo upande wa serikali ni poa tu, but message sent.

    ReplyDelete
  68. mmmh fanyia uchunguzi kwanza hili swala...dont be biased

    ReplyDelete
  69. Naungana na mtoa hoja katika blog kulaumu madaktari kwa mgomo.

    Watafute njia bora zaidi ya kudai maslahi si kugoma.Kugoma kwa daktari ni kuua.Si busara ,si busara,tusiende huko iwe ni aibu na waambeni radhi wanachi.

    Anayewaunga mkono anashiriki siasa mbovu na mitaani.Katika serikali kila mtumishi anaumuhimi wake.Bahati mbaya serikali iliingia dosari ya kuweka mapato tofauti ndo maana jeuri hii inatokeza.

    Hatukushindwa kusomea udaktari bali tulichagua fani nyingine,na wao walichagua udaktari si kuwa ni bora zaidi.

    Tunasubiri hatua na kinidhani dhidi ya mgomo.Mnasema rais akatishe safari kwa ajili gani?Raisi hana wawakilishi wanaomsaidia kazi hadi uvunje safari kwa sababu ya mgomo wa daktari!Waaacha hizo siasa.

    ReplyDelete
  70. iNAONYESHA UNAUTAPIAMLO WA KUFIKIRI - YOUR GROSS MIND DEVELOPMENT IS VERY POOR. THINK BEFORE YOU RIGHT

    ReplyDelete
  71. Ukiwa huna ndugu rafiki,mke,mume,mtoto,mchumba,mpenzi,nk ambaye amepatwa na adha ya kukosa huduma za hawa watalaam unaweza usimwelewe anachotaka kusema huyu mtoa mada.Lakini kama umeuguza halafu ukaenda hospitali na usikute daktari ndiyo utamwelewa anachosema huyu mdau.Serikali ilitatue hili tatizo haraka tafadhali

    David V

    ReplyDelete
  72. wauaji gani? ilaumu serikali yako inayojua kulipa wasiofanya kazi pesa nyingi na wanaofanya kazi wanakandamizwa..kwa hiyo we unaona ni bora wabunge na vigogo wengine serikalini wanaopiga porojo na kuiingiza nchi kwnye matatizo ndiyo wana haki ya kula kodi zetu? na wasiwasi na iq yako na uelewa wako wa dunia ya sasa? wewe huwezi kusurvive kwa mawazo ya kipuuzi kama hayo.

    ReplyDelete
  73. UTUMBO!!!!!!!!

    ReplyDelete
  74. Ulichosema ni sahihi ila hukuangalia upande wa pili.

    Serikali inabagua watumishi wake ndio maana wengine wanaona wanaonewa, angalia mifano ifuatayo kwa watu wenye elimu sawa na daktari yaani digrii moja.

    1. Tutorial assisatnt chuo kikuuu analipwa mpaka 900,000/=
    3.Ecologist wa TANAPA wanalipwa mpaka 1m.
    3. BOT sijuai wnalipwa sh. ngapi ila wanapewa mkopo wa nyumba mpaka million 50-70

    4. TRA wanalipwa zaidi ya 1.5M.

    5.Kuna taasisi nyingi za serikali wanatoa mikopo ya nyumba mf. Taasisi ya elimu unapewa mkopo wa material ya ujenzi.

    6.Hao wote wanalipwa posho nzuri tu.

    Kimsingi siungi mkono mgomo lakini kuna umuhimu wa serikali ku-balance keki ya Taifa, haiwezekani kukawa na tofauti kubwa kiasi hicho kwa watu wenye elimu sawa.

    Kusema wamesomeshwa bure sui hoja kwani wengi wao wamekopeshwa na bodi ya mikopo ila viongozi walio madarakani ndio0 wote wamesomeshwa na kodi za walala hoi.

    Serikali ina uwezo huo kama ikadhibiti mapato yake hasa ya migodi, ikapunguza rushwa katika ulipaji kodi, ikasimamia ipasavyo ukusanyaji wa mapato, ufisadi na wizi ukadhibitiwa serikali kuu na serikali za mitaa, IKADHIBITI MATUMIZI YAKE N.K Pesa hiyo ni ndogo sana wanyodai hawa madaktari ambao wamesoma masomo magumu kwa miaka isiyopungua sita.

    ReplyDelete
  75. Huna akili wewe, na kama unafikiri watu wanaogopa jeshi au kufutiwa ajila basi waendelee na hilo suala.
    Tumechoka kunyanyswa na tunataka suluhisho la kweli la matatizo yetu na si kutubabaisha na siasa zako zisizo na mbele wala nyuma kwani umekaa kuwateteta viongozi wauaji na kutumia maneno ya kupandikisha chuki za watu juu ya madaktari. Bila shaka wewe ni kibaraka uliyetumwa na hawa viongozi wanyonyaji

    ReplyDelete
  76. Hujui unachoongea wala kutetea, Madaktari wa sasa wanajisomesha kwa kupewa mkopo ambao ni deni linalolipwa, pili anachoongea mnyika yukosahihi kwa 100% kwani kinachodaiwa ni cha msingi, tatu mbayuwayu na makundi mengine tayari yapo kwenye mgomo wa kimya kimyaambaoathari zakenikuporomoka kwa elimu na uchumi wa nchi. Unaweza kumlazimisha Ng´ombe kwenda mtoni lakini si kunywa maji. Kinachodaiwa na madaktari ndicho kinachodaiwa na watumishi wote, angalia fedha wanayofisadi wanasiasa ndipo uhukumu wataalam wanaokaa darasani.

    ReplyDelete
  77. Ndugu yangu nakupa pole sana kwa kuandika maoni mengi juu ya ndugu zetu madaktari. Kuna uliyosema nakuunga mkono, ila kuna mengine kwa mtazamo wangu mimi wana haki ya kugoma. Madaktari wetu wanafanya kazi kwenye mazingira magumu sana. Mfano ungekuwa wewe ndio Daktari mshahara wako wa miezi mitatu hupati ungefanya kazi? Hawa watu wanadai haki yao ya msingi kabisa, wanaona jinsi nchi yetu inavyokwenda sasa, wameamua kufanya hivyo ili kilio chao kisikike. Miezi mitatu bila mshahara si unajenga mazingira ya rushwa iendelee? Wataishi vipi watu hawa? Viongozi wanalipana posho na mishahara mikubwa sana! Serikali au sijui Serekali inapoteza imani kwa watu wake kwa kuwa haitaki kuambiwa ukweli! Hii ni hatari sana kwa watu maskini ambao ndio wengi, yani asilimia 95 ni maskini wa kutupwa! Kila kiongozi ameweka maslahi yake kwanza kuliko kuangalia jamii inayomzunguka itajikomboa vipi! Labda ndugu yangu una kinafasi kidogo kinachokuingizia pesa basi unaona maisha ni sawa kabisa? Dunia hii watu wote ni sawa na mahitaji anayopata mkuu wa nchi ndio na watu wote wanahitaji kama hayo. Wenzetu wanaoleta ukoloni mambo leo hapo nyumbani, huku kwao watu wote wanapata huduma zote kama hao viongozi wao, na mtu akifanya uzembe anaondolewa haraka sana kwa manufaa ya nchi. Ukimnyima Dr huduma unataka nini si watu wako wapoteze maisha? Nchi nzima ilitakiwa kuandamana kudai Madaktari wapewe haki zao wanazodai. Kweli wanaokufa ni maskini na ndugu zetu si ajabu hata mimi naweza kuumwa nisitibiwe! Lakini bora Punda afe mzigo ufike, ili kesho yasitokee tena makosa haya, kumbuka tu huwezi kushindana na sauti ya uma, katika uma mkubwa basi hapo Mungu yupo na uma huo.

    ReplyDelete
  78. Umeongea ukweli kabisa mdau, ila wa kulaumiwa ni serikali na si madaktari. Wabunge, mawiziri na viongozi wa serikali hapa Tanzania wanapata mishahara na marupu rupu makubwa kuliko madaktari, ulizia nchi za wenzetu. Ni kikikutajia nchi chache tu kama uingereza, South Africa, Botswana na Ruanda, ni kinyume kabisa madaktari ndio wanaolipwa vizuri. Uongozi wa Tanzania unazidi kufanya madudu kila kukicha. Yaani badala ya kuwekeza kwenye sector ya Afya na kuboresha mfumo mzima wa utoaji wa huduma za Afya wao wanaona bora kukimbiza wagonjwa India hii ni aibu kwa taifa. Nilibahatika kumwona Mh. Mwandosya akihojiwa ITV, yeye alisema watu walikuwa wanashangaa wimbi la wagonjwa kutoka Tanzania kwenda nchini India, akadai ati serikali inawapenda watanzania. Amini usiamini nililia siku hiyo kwa uchungu na kwa mara ya kwanza nikaamini kuwa hatuna wawakilishi. Maana nilikuwa namwona Mwandosya kuwa kiongozi mwenye upeo wa juu na ni kati ya viongozi niliowapenda sana. Sikuamini Mh. Mwandosya alishindwa kutambua kuwa machoni pa watu wa nje tunaonekana ni taifa la ajabu kutumia fedha nyingi kupeleka wagonjwa India badala ya kuboresha huduma za Afya nchin kwetu, hasa ukizingatia kuwa miaka 50 ya uhuru imepita na huduma ndio zinazidi kuzorota. Watanzania tuzidi kumwomba Mwenyezi Mungu afungue macho ya viongozi wetu ili warudishe upendo uliopotea kwa wananchi wao. Kumdharau daktari na kumnyima haki zake za msingi kunachangia kwa kiasi kikubwa kuzorotesha huduma za Afya Tanzania. Mungu ziweke mahala pema peponi roho za watanzania wenzetu waliofariki dunia kutokana na mgomo wa madaktari. Poleni sana madaktari, kwa vile kwa mwenye upeo mdogo atawaona nyie kama ndio mliosababisha vifo hivyo.

    ReplyDelete
  79. Mimi nafikiri ndg wakigombana chukua jembe ukalime na wakipatana chukua kikapu ukavune, naunga mkono hoja yako ndg yangu lakini hii inavyoonekana ni kama ugomvi wa baba na mama ndani ya nyumba wakati watoto hawajui kinachoendelea, watalala na njaa kama sio kukatisha masomo yao. Nionavyo mimi serikali isichoke kutafuta muafaka wa jambo hili. serikali isitumie nguvu maana athari za ubabe ni mbaya kuliko kitu kingine hapa duniani. Leo serikali imeamua jamaa warudi kazini na ukijua fika kabisa kazi ya udaktari ni ya wito ya kujituma sio kusukumwa kama kubeba zege, hapo unadeal na mgonjwa ambaye ni mtu anayesikia maumivu. Je jamaa wakirudi makazini na kutembea na nguo zao nyeupe kutibu watu utasemaje watapokea mshahara wao mdogo kama wanavyodai huku wagonjwa wakifa kama sio kuteseka. Naomba sana mimi ni mtanzania kama wengine, angalieni jinsi ya kufanya bila kutoa vitisho hao sio watoto wadogo pia wana akili na matatizo kama wengine.

    ReplyDelete
  80. sehemu kama hii ni sehemu inayohitaji kuweka habari zenye uchunguzi wa kina kabla ya kuandika chochote ili kila uandikacho kiheshimiwe na wasomaji.
    Kwanza unapoongea kuhusu waalimu na kuwalinganisha na madaktari sijui unatumia vigezo gani vya ufananaji na utofauti
    Mwalimu anaingia kazini asubuhi anatoka jioni, kila siku anakula chakula cha jioni na familia yake, analala kwake tena usingizi mzito, vipi nao madaktari na wahudumu wa afya wangefanya hivyo?
    unajua ni ndoa ngapi zimevunjika kutokana na kazi ya udaktari?
    daktari anaingia risk kumuokoa mgonjwa na hata baada ya kujikinga bado anaijiweka kwenye hatari ya kupata maambukizi ya magonjwa mbalimbali, nani anaemhudumia au kumlipa fidia pindia apatapo maambukizi hayo yaliyosababishwa na kazi yake?
    kama waalimu wanaridhika na wanachokipata ni kwa sababu kinawatosha ingekuwa sivyo wangepigania haki zao na hiyo isitumiwe kama justification kuwazuia wanaodai haki zao kufanya hivyo.
    umesema madaktari wote na hamna hata mmoja ambaye hajasoma kwa kodi za wananchi, hizo takwimu umezipata kwenye chanzo kipi cha taarifa?Nadhani hujapitia hata taarifa ya waziri wa afya wakati akijibu hoja za madaktari labda kauli yako ingebadilika.
    ushauri wako wa serikali kuwafukuza madaktari na kuwafutia leseni umezingatia upeo wako wa kufikiri nadhani maana nadhani una takwimu sahihi za wataalamu wa afya wanaohudumu katika jeshi na ni wa ngazi zipi, na mahitaji halisi ya wataalamu na wa ngazi zipi wanaohitajika.
    Huyo Mungu anaeombwa kuwalaani madaktari lakini awabariki wanasiasa wanaoifanya mioyo yao kuwa migumu Ni yupi?miungu ipo mingi ututajie ya kwenu.
    Labda nikupe kisa kimoja,Muhimbili ilikuwa na daktari mmoja ambaye sasa ni marehemu ambae alikuwa ni profesor katika surgery(upasuaji. alijitoa maisha yake yote kuhudumia wagonjwa na alikuwa akikaa wodini na theatre hadi usiku saa nyingine hata kukosa muda wa kula mchana. daktari huyu aligundulika na uvimbe wa cancer katika kongosho lake iliyomuhitaji kufanyiwa upasuaji nje. pamoja na umuhimu wake katika taifa serikali ilishindwa kugaramia matibabu hadi kupelekea yeye kuuza nyumba.
    baada ya matibabu yake aktari huyu bado aliendelea kujitoa hususani kufundisha madaktari lakini muda mwingi aliutumia kuhudumia wagonjwa huku akiishi kwenye nyumba za muhimbili maana hana nyumba tena. baada ya miaka kumi lile tatizo la awali likajirudia, na kwa wakati huu hakuwa na cha kuuza ili akatibiwe. Yule daktari mpaka umauti unamkuta alikuwa anajifungia ndani na hataki kuonana na mtu yeyote. Swali linakuja kama hao wanaolazimisha watu warudi makazini wangekuwa wao serikali ingewatelekeza kama alivyofanyiwa professor huyu?
    Ni vizuri ukatumia muda wako wa kutosha kuenda katika undani wa jambo hili na sio kusikiliza hadithi za vijiweni kabla ya kuandika makala kama hiyo, tafuta vielelezo vya kutosha kuhusu hali halisi ya afya tanzania, changamoto zinazowakabili watoa huduma hizo, muda wanaoutumia kazini na ulinganishe na viwango vya shirika la kazi duniani kuhusu masaa ya kazi yanayoruhusiwa kwa mfanyakazi,chunguza kuhusu uwiano wa daktari na wagonjwa na upate takwimu ni wagonjwa wangapi anaruhusiwa daktari mmoja kuwahudumia kwa siku. baada ya hapo oanisha masaa ya kazi, idadi ya wagonjwa, ugumu wa kazi, mazingira hatarishi na ulinganishe na kipato cha huyu daktari uone kama vinawiana ili ukiamua kuandika makala kama hiyo uwe na vigezo vya kuzungumzia na sio bla bla.

    ReplyDelete
  81. Jamani, hivi serikali yetu kwanini inaonyesha weakness kama hii. Two weeks ago hapahapa michuzi, kabla hata ya mgomo kuanza nilisema serikali ichukue hatua kuondoa elements (watu) wanaochochea migome kwenye utumishi wa umma. Nilicomment kwamba watu kama kina DR. NAMALA MKOPI na huyu DR ULIMBOKA ni kazi ya serikali kuwa-eliminate (elimination) kabla hawajaleta madhara kwa public nzima. Nikatoa mfano kwamba katika nchi kama Rwanda, ujinga kama huu usingetokea, wale wachochezi kama kina DR, NAMALA MKOPI, RODRICL na mwenzake ULIMBOKA wangekuwa wameshakuwa eliminated kuzuia kansa ya mgomo isisambae nchi nzima. Kwani watu wangapi wameshakuwa eliminated nchi hii kwa kutishia maslahi ya wengi. yaani people are dying kwa sababu ya watu hawa wawili, usalama wa taifa mko wapi? where is our intelligence service jamani? WHY? Mbona kama mnakumbuka wale waliokuwa wanachochea maandamano ya waislamu wamepotezwa, watu wangapi wamepewa sumu na tumeona?, watu wangapi wamepata ajali za utata na tumeona?, watu wangapi wamepotea kimiujiza na tumeona na tumeshazoea, sembuse hawa madokta wawili, DR. NAMALA MKOPI na DR. ULIMBOKA, hawa inashindikana nini kuwaeliminate nchi irudi kama kawaida tuendelee na biashara zetu? hivi ingekuwa RWANDA mnadhani KAGAME ANGEVUMILIA MAMBO KAMA HAYA? INANIUMA SANA KAMA FORMER INTEL. SHOULD I ACT ALONE?

    ReplyDelete
  82. wewe michuzi ni mnafiki weka comment za watu hata kama zina negative that is the meaning of comments. don`t expect positive comment only. kama hutaki funga kipengere cha comment.

    ReplyDelete
  83. Umetumwa? Ushindwe na ulegee

    ReplyDelete
  84. Kwa jinsi ulivyoongea ujinga sishangai kutoona jina lako mwisho. Umeweka ushabiki badala ya hali halisi iliyopo mezani. Serikali ilijitoa kwenye kufanya biashara ili isimamie huduma za jamii ikiwemo Afya. Sasa inaposhindwa lazima iwajibike kwa mfano madaktari walilazimika kufikia hatua hii baada ya kupuuzwa na viongozi wa wizara ya afya bila sababu maalum. Waziri Mkuu nae anakuja badala kutatua tatizo anaishia kuchonganisha madaktari na wananchi.

    Kifupi ni kuwa kilio cha madaktari si chao peke yao, hata sisi walalahoi tunaolala mzungu wa nne pale amana na kwingineko tunawaunga mkono. Na mnapotokea watu wenye akili ya kuku kama nyinyi ambao mnaona mnapodoa na wakati huo huo mnapekua kusaka chakula kilichopo ni aibu. Rais wetu amekuwa Rubani sasa, safari 322 ndani ya miaka 7 ya utawala ni aibu, hakuna faida kama hela anazoomba zinaishia kumsafirisha yeye na kundi lake. Namaliza kwa kusema mtu yeyote asieona umuhimu wa mgomo huu basi tuna mashaka nae, na serikali isipokuwa makini katika hili basi litaishia mtaani.

    ReplyDelete
  85. 1. Yanapokuja mambo ya msingi hasa uhai wa wananchi RAIS lazima awe mstari wa mbele kushughulikia. Katiba inamlazimisha kufanya hivyo. Katiba haimlazimishi RAIS kwenda nje ya nchi kama ndani ya nyumba yake kuna shida tena ya watu kufa!

    2. Kuna tatizo la mfumo hapo ambalo mwandishi unashindwa kulielewa na kulichanganua. Kwa nini viongozi wa serikali wakuu wa serikali wanatibiwa nje ya nchi? Baadhi ya majibu unayo. Mengine ndio madaktari wanadai (vitendea kazi na mazingira bora ya kazi) nahati mbaya wewe hutaki madaktari wadai vitu kama hivyo. Kimsingi baadhi ya madai ya madaktari siyo kwa ajili yao, ni kwa ajili ya wagonjwa.

    3. Madaktari ni binadamu kama wewe - ni wazazi na pia wana majukumu ya kijamii na kifamilia. Gharama za maisha zimepanda na hili linajulikana hata na serikali yenyewe (ndio maana RAIS kasaini nyongeza ya posho za Wabunge). Watumishi wakidai haki zao hawasikilizwi. Wafanyeje sasa? Ni kweli baadhi ya madaktari wamesoma kwa kodi za Watanzania. Swali la kujiuliza ni mlipa kodi ni nani? Baba na mama zetu ndio wanaolipa kodi ambao pia ndio wazazi wa madaktari haohao. Na zaidi ni jukumu la serikali kugharamia elimu hasa ikizingatiwa kuwa elimu ni "public good".

    4. Watumishi wa serikali wanafanya kazi katika mazingira magumu sana. Ndio maana wengine wanafikia hatua ya kudai rushwa ya Sh 1000 ili kuziba pengo la bajeti. Kibaya zaidi wana kula rushwa kutoka kwa wa-Tanzania wa hali ya chini sana. Lakini yote hii ni sababu ya mfumo ambao serikali imeukumbatia.

    5. Serikali ndio ishtakiwe kwa kuwatesa madaktari waliopo katika mafunzo hivyo kuvunja mkataba.

    ReplyDelete
  86. hoja uliyotoa ni nzuri,lakni hebu tiangalie upande mwingine. nikimaanisha na upande wa uongozi walioshindwa kuelewana na madaktari hadi ikapelekea kugoma,binafsi sitetei mgomo lakni sizani kama Hawaii wataalamu waliamka tu wakaanza kugoma kunasababu. Ni kawaida yetu siye tulio katika management hatutaki mazungimzo hatutumii hekima na maarifa tunataka mabavu kunyamazisha walio chini pale tunapokutana na challenges na matokeo yake ndio hii migomo hata vyuoni ni sababu hizihizi unazoziona kwa madaktari. tunajua wakigoma kwa kuwa wao ndio wanaonekana kwa jamii,wataonekana wao ndio kwenye hatia na hukumu itatolewa juu yao, lakni wewe uliyeshindwa kuwatatulia matatizo yao utapewa promotion kama si kuamishwa idara.
    Ushauri wangu kwa serikali hizi hatua zichukuliwe pia kwa upande wa managment kama kuna mtu alishindwa wajibu wake hadi ikapelekea madhara haya naye aadabishwe hapa nadhani haki itakuwa imetendeka. la hii hali itaendelea kujitokeza hata kama wakiondoa madaktari wote wakaja wapya na iko siku watafanya yaliyotokea leo,na wakuumia tutakiwa mimi na wewe.
    Swala la msingi wananchi hawataki kuona migomo kama hii ikijitokeza tena.

    ReplyDelete
  87. Ivi wewe ndugu unaesema madaktari wote watimuliwe alafu wawekwe wanajeshi umeshawahi kwenda tibiwa hospitali za jeshi au unasema tu. Madakatari wa kijeshi na manesi wao hawana la kupoteza kwani kwao ni kama vile wana ajira mbili hawezi kujiumiza mwili,kichwa na nafsi kukutibu wewe kwa ukamilifu ili apate ugali wake, yeye bado anaajira yake kama askari. Wanao pata matibabu mazuri kwenye hospitali za jeshi ni wale wakubwa wenye nafasi zao sio mtu hohe hahe kama mimi na wewe, maana unamwona daktari na bado unaambiwa dawa na vipimo hakuna.

    Mgomo huu wakulaumiwa ni serikali tusiwalaume madaktari kwani wao ni wahitaji kama mimi, wewe na hawa mafisadi wetu.

    ReplyDelete
  88. michuzi usibanie maoni: ni kwamba, nchi kuwasomesha wataalamu ni jukumu la msingi la nchi husika ili wananchi wake wapate huduma...hapa ndipo watanzania wasipoelewa kutafakari mambo. sasa si msitishe ufadhili wa udaktari ili anayetaka ajisomeshe..ili tusomeshe wana siasa tu halafu ukumwa utajijuu..ya nini kuwasimanga watoto wa watu waliojitoa mhanga kukesha na kupata risks kwa wajili ya kuokoa maisha ya binadamu ambaye haoni taabu kukabidhi maisha yake mikononi mwa mtu ambaye hana hamasa na kazi yake..eti ukifa ni mapenzi ya Mungu..ndiyo maana vifo na ulemavu kibao huku kwetu na pia makanisa na ibada zisizo rasmi ni kibao ili kujifariji...ACHENI KUFADHILI FANI YA UDAKTARI FADHILINI SIASA ILI DAKTARI AJISOMESHE KWA FAIDA BINAFSI..SIYO OHHH TUMEKUSOMESHA...KWANI SI NYIE MNAWAHITAJI?? MBONA MNALIA UPUNGUFU UPUNGUFU..KASOMENI WENYEWE

    ReplyDelete
  89. Pande zote MBILI hazikutumia busara,,,WADAI na WADAIWA.

    Matokeo yake vi HASARA KWA WASIO NA HATIA (YAANI WANANCHI)

    ReplyDelete
  90. Mimi nimeolewa na daktari, sijasoma kama mume wangu, lakini mshahara wangu na marupuprupu yangu yanazidi yale ya mume wangu. Ajabu kazi zake ni ngumu zaidi ya zangu, na mara 2 kwa wiki anakuwa zamu kwa maana usiku hatulali maana ni kugongewa kwa ajili ya emergency au wagonjwa waliozidiwa. Jamani serikali inakosea sana. Mdau wa 11:44 hujui unachongea hivyo usiwe unachangia mada.
    Namwonea huruma sana Waziri mkuu kwa uamuzi aliotumwa kutoa, zamani alikuwa anaongea vizuri kwa vile alikuwa anasema kile cha haki kwa utashi wake, lakini siku hizi anaongea kile alichotumwa kuongea na hii inamfanya kuongea kwa uoga, aibu na kutojiamini kwavile kwa utashi wake anajua anachoongea hakimpendezi Mungu ila anafanya hivyo kwa vile anaiogopa system iliyomweka kwenye uongozi. Tumebaki na Magufuli tu ambaye ana hofu ya Mungu, hayupo kumpendezesha mtu kwa unafiki yupo kwa ajili ya maslahi ya wananchi na maendeleo ya nchi. Nakumbuka alipopandisha bei ya kivuko na kutoa utani wa kupiga mbizi, viongozi wanafiki wanaotaka kuwapendezesha wananchi kwa ujinga wakawa wanatetea ujinga. Kama kwa miaka 14 kivuko cha Kigamboni hakijapandishwa bei, pia ni kivuko pekee ambacho kilikuwa na bei ndogo sana ukilinganisha na sehemu nyingine(mfano pangani kwa wakulima kivuko ni sh. 200 miaka mingi, mwanza 500). Kwa kujua kuwa hajamkosea Mungu na hayuko kwa ajili ya unafiki alishikilia alichoamini na hakubadili msimamo wake. Narudia tena wadau, tukazane na kumwomba Mungu atupe viongozi kama Magufuli, la sivyo migomo itazidi sana nchini. Hii ni kwasababu ya uchoyo wa kujilimbikia mali viongozi wetu, na mbaya zaidi tumewapa uongozi watu ambao baba wa Taifa wakati wa uhai wake aliwakataa. Hii ndio faida yake! Asiyesikia la mkuu huvunjika guu, acha tuvunjike, imekula kwetu. Kwa mwenye upeo mdogo ataona kama nimechanganya mada, hapana, kwa ufupi ni kuwa uongozi mbovu ndio umepelekee nchi yetu kufika mahali tulipo. Leo hii daktari anafikiria ni heri na yeye akawe Mbunge, umeona wapi upuuzi kama huu !!!Sisi tunalumbana kwenye hapa wao wanahesabu siku kwenda kulamba laki 3 na nusu kwa siku. Sijui kwa kazi gani wanayofanya!!!

    ReplyDelete
  91. Mimi nawa support madaktari kwa 150%. Ni wananchi wa kawaida haswa wenyekipato cha chini unawaongelea ndio wako wengi Tanzania na ndo walioiweka serikali hii inayojali matumbo ya wachache badala ya kuthamini mchango wa watumishi wa umma kama walimu, madaktari, manesi n.k ambao wanafanya serikali ithaminike.
    Ona leo hii wabunge wanajiongezea posho ya almost 300% alafu watumishi wenzao wakiomba nyongeza ya posho 30% wanafukuzwa. Mimi binafsi ni mfanyabiashara mwenye hela ya kujitibu private ndogo ila inaniuma kuona watu wanasoma 7 yrs alafu wanafanya kazi from 8 to 8 na wanaishia kuwa na maisha duni.
    Madaktari endeleeni kugoma mpaka hao maskini wanaodanganyika na kanga na wali wakati wa uchaguzi wasaidie kuwaondoa mafisadi na hela zinazoibiwa na hao wezi zitumike ku fund nyongeza yenu.

    ReplyDelete
  92. Nimeshawi kusema ya kwamba kuna jamaa, usalamaa wa taifa(wabovu)au wamewekwa maalum, au basi wanapitia kwenye mitandao kuchonganisha. Wengine wanaandika kama hawana elimu au nimavuvuzela tu. Hawaeleweki. Inabidi kupima, kweli jamaa zimo timamu kutoa hoja ya namna hii? Na huyu jamaa aliyetoa hojaa hii ni mmoja wao. Au ametumwa kupima, maana anaongea pumba.

    ReplyDelete
  93. Mawona upo juu sana!!! Kweli wananchi imekula kwao kama nilivyosema hapo awali. Na kubaliana nawe kanga na visimu vya torch ndio vinawatokea puani sasa. Ajabu watu wanasahau kabisa, ikifika tu karibu na uchaguzi wakitupiwa hivyo vizawadi tu wanachanganyikiwa. Madaktari endeleni kugoma mpaka kieleweke, poleni sana, mlikuwa wastaarabu miaka yote lakini nanyi mmechoka sasa. Yaani mishahara yenu ni midogo sana, heshima ni hilo jina la udoctor! Seriklai itaue tatizo hili haraka sana, wale unaowapa vikanga wanapata shida sasa, wasaidieni tafadhali.
    Namshukuru Mungu kwa kwa kiasi fulani watu wamefunguka kidogo, nimeshangaa watu wakihijiwa kuhusu mgomo almost 90% wanawatetea madaktari. Mungu ibariki Tanzania, tufike mahali sas themani ya elimu ionekane, na si siasa za bla bla!

    ReplyDelete
  94. Ngombare wewe mwenyewe unastahili kuwa eliminated, bora ukae kimya kulikokuandika ujinga mliokuwa mnafanya na serikali zenu zilizopita za kidikteta. Ni kalne mpya hii badilika na unaweza kuuliwa mwenyewe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...