Mkuu wa mkoa wa Tanga Luteni (Mstaafu),Chiku Gallawa akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu Konstebo Henry Nyang'ombe askari wa kikosi cha Kutuliza Ghasia mkoani Tanga (FFU) aliyefariki na mwenzake Koplo Jeggy Kangaga wakati wakiwa katika msafara wa Makamu wa Rais, Dkt Mohamed Gharibu Bilal alipokuwa na ziara ya siku nne mkoani Tanga, Mwenye kanzu ni Mwenyekiti wa CCM Mkoani Tanga Bw. Mussa Shekimweri.
Kamanda wa Polisi mkoani Tanga,SACP Constatine Masawe akitoa taarifa ya ajali kwa waombolezaji waliofika katika kambi ya kikosi hicho cha FFU kilichopo eneo la Majani Mapana Jijini Tanga. wengine waliokaa kwenye viti kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Dkt Ibrahim Msengi, Mkuu wa wilaya ya Lushoto Sophia Mjema na Mkuu wa wilaya ya Korogwe Bw. Erasto Sima.
Askari G1752 Konstebo Henry Nyang'ombe (25) ambaye alijiunga na jeshi hilo mwaka 2008 alisafirishwa kwenda kijijini kwao Makongoro kilichopo kata ya Buturi wilayani Mara kwa mazishi.
Askari E 1192 Koplo Jaggy Kangaga (43) ambaye alijiunga na jeshi hilo mwaka 1987 kabla ya mwaka 2008 kupandishwa cheo na kuwa Koplo alichokuwa nacho hadi mauti yalipomkuta, alisafirishwa kupelekwa kijijini kwao Mwakisandu kilichopo wilayani Meatu mpakini mwa Maswa.
sehemu za waombolezaji wakiwemo askari wa kikosi cha polisi cha FFU wakiwa na hudhuni kuondokewa na wenzao hao, wakifuatilia kwa makini taarifa mbalimbali zilizokuwa zikisomwa katika msiba huo.
Mkuu wa wilaya ya Korogwe Bw. Erasto Sima akijaribu kuwabembeleza ndugu za marehemu mara baada ya kutoka kutoa heshima zao za mwisho kisha kulipuka kwa kilio kutokana na huzuni za kuondokewa na ndugu zao hao. Kulia kabisa ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Bi Zipora Pangani.Picha na Mashaka Mhando, Tanga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Vifo vya ghafla mara nyingi huwa vinaleta mshtuko mkubwa.Poleni kwa wanafamilia na jeshi la Polisi kwa ujumla.Halafu Bw.Mashaka hii habari umeileta nusu nusu.Chanzo cha ajali kilikuwa ni nini?Mwendo kasi,kona kali,kupasuka tairi,n;k.Na hawa marehemu walikuwa nyuma ambako huwa wananing'inia??Askari wengi huwa nawaona wananing'inia juu bomba ya hizi gari zao za patrol..Hiyo si salama hata kidogo..Hata hizo pick up zinatakiwa kuwa na viti vyenye mikanda huko nyuma kama mnaamua zibebe Abiria.Mnatakiwa kukaa ndani siyo kuning'inia kwenye hizo bomba.Hamko vitani kama JWTZ.USALAMA KWANZA!

    David V

    ReplyDelete
  2. kifo sio mchezo jamani,poleni sana akina Ras Makunja,tunaona jinsi gani?udhuni na ukiwa ulivyowashika wapiganaji wetu akina ras makunja,poleni sana

    ReplyDelete
  3. Poleni wafiwa. Ukweli ni kwamba hilo gari lililopata ajali lilikuwa katika mwendo kasi. Nilikuwa naendesha kutoka Moshi kuja Dar es Salaam na nililishuhudia kwa macho yango jinsi lilivyokuwa linakimbia. Sikushangaa nilipolikuta limepinduka.

    ReplyDelete
  4. Sawa mdau ila chanzo cha ajali ni gari la Polisi lenye namba za usajili PT 200 lilishindwa kufunga breki kwa uharaka na eneo lenye la Ndulu pana kona basi dereva likamshinda likapinduka kwenye korongo na asakri hao wawili wakafa papo hapo na wengine wanne kujeruhiwa. Suala la kuning'inia hiyo ni suala la kipolisi lakini kimantiki tu askari anapokuwa kwenye misafara ya viongozi lazima akae kwa mtindo huo, kwa ujumla ilikuwa bahati mbaya. Mhando

    ReplyDelete
  5. Naona hukuelewa anasema tatizo ni mwendo kasi, mwendo kasi ni hatari uwe msafara wa raisi or wa nani, mwendo kasi na hizi barabara zetu ambazo zinajengwa bila signs za barabarani nalo pia ni tatizo

    ReplyDelete
  6. Poleni sana Watanzania wenzangu pamoja na familia za wafiwa. Imenisikitisha sana ila ningependa kutuo maoni yangu ya kuhusu kubadilisha aina ya magari yanayotumiwa na polisi. Mimi ni Mtanzania ambaye nimesafiri sana nje ya nchi , nchi zote za ulaya na asia na marekani hawaruhusu watu wenye pick up kupakia watu nyuma. Ningependa kulishauri jeshi la polisi Tanzania kununua Hiace kwa ajili ya kubeba polisi wanaokuwa kwenye msafara wa viongozi wa kitaifa kuwaweka nyuma ya gari pick up ni kuhatarisha maisha yao sio vizuri na wala sio ubinadamu maana nao wana takiwa wakae kama viongozi kwenye gari na kufunga mikanda tujali Human Right yao maana tunahatarisha haki yao ya Kuishi.
    Tusiendele kutumia aina ya magari kama vile askari walio vitani hata askari wanao patrol mjini wanatakiwa watumie Van au Hiace sio kusimama nyuma ya gari likipata ajali kuna asilimia zaidi ya 90 ya kupoteza maisha au kuvunjika viungo.
    Tukumbuke kuwa wana famila zinawategemea kama Watanzania wengine walivyo.
    Asante sana
    Mtanzania Ughaibuni

    ReplyDelete
  7. Je dereva nae anashikiliwa kwa uzembe na kusababisha vifo? Kina ras makunja poleni kumbe mjue mauti ni kwa kila binaadamu hakuna aliye juu ya sheria.

    ReplyDelete
  8. na huyo makamu wa rais akaendelea na shughuri zake ndivyo? sasa hivi kajifunza nini? NEXT TIME NAYEYE AJARIBU KUNING'INIA .maana hao ni watu waliokuwa wakilinda usalama wake ndungu na jamaa na wapa pole sana kwa kupotelewa na wapendwa wenu, ningekuwa mimi ni ngefungulia mashtaka polisi pamoja na serikali yake walishindwa kumpa elimu ya barabarani huyo dereva.napia kama yu hai afunguliwe mashtaka.na ndugu wa hawa jamaa walipwefidia.

    ReplyDelete
  9. May CORPSES of these CORPS, rest in Eternal PEACE!

    AMEEEN!!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...