Habari ya kazi uncle Michuzi ..
Bila shaka unaendelea na kazi kama 
kawaida ya kulijenga Taifa letu...na kheri ya mwaka mpya..

kwanza kabisa kaka mimi naomba unibandikie Tangazo langu kwenye  blog yako,,,Jina langu naitwa Rose umri wangu ni 29 naishi ughaibuni kwa sasa ni kwa masomo,,,napenda kupata marafiki wengi iwezekanavyo.

Me sibagui rangi wala dini  nachopenda wale ambao wako serious  kidogo...ili kubadilishana mambo ya hapa na pale ya kimaisha ,,kwa wale watakao kuwa serious naomba waniandikie e-mail  
rose557790@yahoo.ca  nitajibu haraka niwezavyo.. 
ASANTE
Rose

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Huyu binti simuelewi, yeye anatafuta marafiki au anatafuta mume, awe muwazi ili tuweze kumsaidia vilivyo, maana sisi wengine tuko serious katika kuoana siyo urafiki, sidhani kama urafiki unahitaji u-seriousness wowote, be clear and straight Rose, we will be there to help you don't feel shy.

    ReplyDelete
  2. nenda fesibuku... utapata marafiki alfu...

    ReplyDelete
  3. Mtu akibadilisha mawazo hahitaji kuwa "serious"!!

    ReplyDelete
  4. Hey rose! I like ur hand writting

    ReplyDelete
  5. Sawa Rose kabla ya wewe kuandikiwa e-mail na wandugu, nafikiri wengi watakao andika watagusia AGENDA YA MAHUSIANO NA NDOA, kulingana na wasifu pia umri wako na taswira ya pendekezo lako hili, kabla ya watu hawaja chapa key board za computer zao je hapo unasomeka vipi?

    Mdau

    Dar Es Salaam.

    ReplyDelete
  6. Sawa Rose kabla ya wewe kuandikiwa e-mail na wandugu, nafikiri wengi watakao andika watagusia AGENDA YA MAHUSIANO NA NDOA, kulingana na wasifu pia umri wako na taswira ya pendekezo lako hili, kabla ya watu hawaja chapa key board za computer zao je hapo unasomeka vipi?

    Mdau

    Dar Es Salaam.

    ReplyDelete
  7. Rose bado hasomeki tuma picha watu watasimini mada yako mdada... lakin wewe rose hujui kuwa kuna mitanda ya jamii km facebook,taggede,badoo nk ingia humo post u seriousness wako humo

    Madau maarufu Blogger
    dar

    ReplyDelete
  8. Jamani dada Anataka mwanaume wa kumuoa kashaona kakaa nje umri unakwenda anataka ajinusulu kutoka katika kitanzi cha upweke .Ila dadangu umestuka muda muhafaka we andika unatafuta mume watu waelewe sio dhambi kujieleza tena mie nakupa pongezi sana maana umeonyesha ujasiri.Tuache kasumba za mwanaume ndio anatongoza hapana mwanamke nae awenauwezo wakutongoza maana unaweza kuta kampenda mtu alafu anashindwa kumweleza kisa mila na desturi hairuhusu mi nafikiri ili limepitwa na wakati.

    ReplyDelete
  9. hapo canada kuna jamii ya wa TZ. Si ujinge na jamii tu.

    mdau wa Musa hasani (msasani)

    ReplyDelete
  10. Nhee Da Rose nadhani anasomeka vizuri kutokana na azma yake jinsi alivyoileta kwetu.

    La msingi ni watu kuanza kutuma CV's zao ( Taarifa za Wasifu kwa watakao taka mahusiano naye iwe ndoa au urafiki...??? ,ili mwenyewe achague ),,,inaeleweka kwa maadili yetu Mwanamke ameumbiwa na aibu.

    Zitamwagika CV katika e-mail in box yako hadi balaa!

    Isipokuwa Rose umelilia chai wewe mwenyewe usije kulalamika unaungua!

    ReplyDelete
  11. Rose , kuwa muwazi unataka kuolewa?

    Hapa nyumbani pana Wanaume kibao watu wastaarabu wametulia kwa heshima zao, shughuli zao na pesa zao isipokuwa utata na changamoto ni kuwa madadaz wengi huku wamekuwa ''Micharuko'' sasa Wajanja wengi wanakuwa wagumu kuingia hii mikenge!

    Sasa kama wewe ni Mwanamke unaejiheshimu na mwenye mwelekeo wa maisha utakuwa unafaa sana!

    ReplyDelete
  12. Hiyo jamii ya Wa Tanzania hapo Canada Da Rose inawezekana amesha wachambua na akaona karibia Wanaume wote ni ''Makachala'' walio walio wengi awakiwa nje wanakuwa Wasela , unajua watu wanapokaa pamoja wana onana kinyaa kutokana kujuana nyendo zao, ndio maana ametugeukia huku nyumbani Bongo apate Mwanaume wa asilia!

    ReplyDelete
  13. naona rose hauko serious hiyo e-mail yako mbona haieleweki ni rose557790@yahoo.ca

    ReplyDelete
  14. Weye Rose weye ni kweli wataka mume weye au watucheza shere?

    ReplyDelete
  15. nenda mitandao ya kijamii binti

    ReplyDelete
  16. JAMANI SI HIVO MNAVOFIKIRI TATIZO NI KWAMBA WATU WENGI HATUNA UELEWA KWAMBA VYOMBO KAMA HIVI VINAWEZA KUTUKUTANISHA NA WATU MBALI MBALI SO SIO KOSA LENU KULAUMU AU KUHISI VITU TOFAUTI NAHITAJI MARAFIKI NAJUA FB KUNAKUUNGANISHWA NA MARAFIKI PIA ILA HATA HII BLOG NI NZURI PIA NASHUKURU KWA WALE WALIONI INBOX. NAJUA KATIKA MAISHA HAWAKOSEKANI WATU KAMA NINYI HAPO JUU SO NEVER ...MIND KWA YALE kwa bhati mbaya MLIYOYAFIKIRI...pia kwangu umri wangu haujaenda wapo walioolewa wado lakini mpaka sasa hawajabahatika kupata yale waliopangilia so si kigezo cha umri asante

    ReplyDelete
  17. aah rose unaniumiza na maneno yuangu roseeeeee koh koh koh....

    ReplyDelete
  18. NAHITAJI MARAFIKI WA JINSIA MBALIMBALI MBONA MNASTICK KWENYE WANAUME NASHUKURU MUNGU NIMEPATA TENA WENGI TU WADADA NA WAKAKA ..NAOMBA TUWE WASTAARABU TUENDANE NA UTANDAWAZI ASANTE,,SIJABAGUA DINI WALA RANGI YA MTU UMRI AU JINSIA.HIYO NDO E-MAIL YANGU ULITAKA E-MIL GANI ACHA HIZO

    ReplyDelete
  19. Dear Rose njoo Canada, huko UK sijui bongo au US kote choo, hakuna kazi wa elimu huko kuna siasa na kudai usawa, vijana wengi hawana kazi hivyo ukienda huko ,usinunue kigali ukakiegesha mitaani, si ajabu usiku ukakuta kimechomwa moto, kwa madai kwamba vijana wanataka usawa, huko UK na US bongo !!! nako miundo mbinu hakuna, sasa kama utapata mtu ana nyumba jangwani-sahuri yako tutakuona kwenye michuzi umeshika gogo la nazi.

    ReplyDelete
  20. Ila pia hiyo email adress nadhani ameikosea.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...