Katika kuboresha huduma zake, NMB imeanzisha makakati wa kutoa huduma kwa wafanya biashara wakubwa, serikali na makampuni makubwa uitwao NMB Business Center.
Katika mwendelezo huo,NMB imefungua kituo kiitwacho Kariakoo Business Centre, hivyo wafanya biashara watapata huduma katika mazingira yaliyo boreshwa zaidi.
Kariakoo Business Centre ni ya pili baada ya Arusha Palace Business Center iliyofunguliwa huko Arusha katika jingo la Arusha Palace Hotel.





Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Mark Wiesing, alisema ” NMB imenuia kuendelea kuboresha huduma zake zaidi, Business Center zitawezesha wafanyabiashara na makampuni kupata huduma bora kwenye eneo lililoboreshwa zaidi”. Mark Wiessing aliwashukuru wateja wa NMB kwa kuendelea kutumia huduma za NMB na kuahidi kuendelea kuboresha zaidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. mara kadhaa nimeshaandika kutaka kiswahili kienziwe na sisi watanzania hususan wa fani ya habari...na katika niliyoyatilia mkazo ni neno BORA . Hili neno sio kitenzi . huwezi kulinyambua . ni kama vile neno nzuri ..huwezi kusema imenzurishwa au manzurisho ...inakera kwa mtu anaekifahamu kiswahili sawasawa kuona hata watu wenye heshima katika fani ya habari kama kina michuzi na wengine wanakibananga kiswahili lugha amabayo wenapaswa kujivunia kuwa ni ya taifa na wenyewe ni watanzania.

    ReplyDelete
  2. habari brother michuzi. mimi ni mdau wako na napenda kusoma blog yako na nafurahi inavyotupa habari mbalimbali ...keep it up and big up sana tu. ila kuna jambo la lugha nakuombeni sana tukienzi kiswahili....hasa nyie wanahabari ...juzi niliandika maoni hapa kwenye habari hii lakini sijayaona yametolewa sasa sielewi kuwa kaka michuzi umenibania kwa sababu nilikukosoa kuhusu matumizi ya lugha au labda hujanibania ni mambo tu yameingiliana ...anyway sote ni wananchi tunajenga taifa moja ...nia yetu ni kusonga mbele kimanufaa zaidi. sorry kama nimekuuzi ila tujaribu kuwa fasaha katika lugha yetu wenyewe ...wazungu wanakuja wanaisoma lugha yetu na wanatushinda ...kwa hiyo nasi hatuna budi kukienzi kiswahili ....tusitumie maneno mabovu kama maboresho na uboreshaji .

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...