THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

msaada tutani: Swali kuhusu uwanja wa Emirates

Asalaam aleykum Kaka Michuzi

Sisi hatujambo na tunashkuru kwani tumeshinda ushindi mnono dhidi ya ya wale jamaa vijana wa 'arri redknap' . Lakini kama ujuavyo kumetokea mzozo mkubwa kiasi cha kwamba tumeona hili suala tulilete kwako labda waweza kutusaidia kupata ufumbuzi. Maswali yenyewe ni:

1. Je Arsene Wenger ndiye aliyevumbua/aliyekuja na idea kwa jamaa wa FIFA kuwa kwenye magoli ya viwanja vya mipira yafungwe nyavu?

2. Je Arsene Wenger alipatent hiyo idea au aliamua kuitoa tuu kusaidia soka duniani?

3. Je ni kweli uwanja wa Emirates ndio uwanja pekee UK wenye msikiti/prayer room ? 

Kwa sasa maswali ni hayo tuu. Ina naomba uwafikishie salaam wale wapinzani wetu wajadi kutoka Morogoro, Vingunguti kiembe mbuzi, Mbezi Louis, Mbagala kuu, Ilala kwa waPemba na kwa barafaa, Pemba mnazi, Kibugumo,  Buguruni kwa mnyamani na bila kusahau ndugu zetu wa karibu kutoka Mwananyamala kisiwani.

Ni mimi Arsenal mwenzenu wana Imarati

Mr Arsenal.Kuna Maoni 16 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  Kweli wewe ni mr.Arsenal maana jinsi ulivyoweza kuolozesha makina hayo sikuamini macho yangu

 2. Anonymous Anasema:

  Assalam aleykum Ankal,

  Kwanza Kabisa Hongera Ankal kwa ushindo mnoooono wa bwawani.

  pili, naomba kuchukua fursa hii kujibu maswali haya ya mdau Mr Arsenal . Atambue kuwa nyavu hazijagunduliwa na yule mzee aliyetandikwa 7 kwa kagoli kamoja na Blackburn siku chache zilizopita . Nyavu zimegunduliwa na mtaalamu Engineer toka kwa timu makini ya Ankal akiitwa John Alexander Brodie bonyeza hapa

  tatu, kuhusu suala la prayer rooms, wazee wa kazi na mabingwa wa all time Man United ndio wa mwanzo kuwa na prayer rooms katola old trafford bonyeza hapa

  mwisho, naomba kuwashukuru ndugu zangu wa chamanzi, kimanzichana, Mbezi gongoni, Ruvu, kwa mnyamani, Aiport na wazee wa Mwananyamala kisiwani kwa msaada wao mkubwa wa kutafuta ufumbuzi huu.

 3. Anonymous Anasema:

  I cant wait kusoma majibu toka kwa Bantu ya timu yake

  Hivi kweli huu ushabiki wenu wana Emirates tena umezidi


  sasa tushajua kuwa Ankal deep down naye ni Emirati tuu japo ngumu kwake kuachana na clabu ya mabaguzi

 4. Anonymous Anasema:

  Nadhani aliyejibu hoja hapo juu hakuwa sawa au kwa kusudi tuu kaamua kupotosha ukweli

  1. Kuhusu Arsene Wenger kuvumbua nyavu magolini ina chembe ya ukweli kwa sababu kuna tofauti ya majina na pia kuna issue kuwa wanatoka kwenye ukoo mmoja ndio maana watu wengi wanaamini kuwa ni Wenger. Lakini masha khof hapa ni kisiwa cha kupeana habari na kuwekana sawa naamini kadri muda unavyozidi kwenda tutaendelea kuhabarishana lakini nashauri kwa sasa tuamini hilo la Arsene kama mvumbuzi.


  2. Suala la Msikiti ndani ya Emirates nadhani halina mjadala kwani Arsenal kwa kias fulani kwanza iko sponsored na Waarabu waislam toka Dubai na ishawahi kuwa na wachezaji wengi waislam kama vile Abou Diaby, Kolo Toure , Lassana Diara , Eboue, Robin Van Persiem Thiery Henry na bila kusahau kuwa hata huyo wenger mwenyewe inasemekana naye ni muislam ndio maana mle ndani ya Emirates kuwa Msikiti

  na picha hii hapa:

  Mwisho ningependa salaam ziwafikie arsenal wenzetu waliopo:

  Changombe kisarawe
  Uyui, Tabora
  Bweni, Mafia
  Mangesani kwa shaabudu, Bagamoyo
  Mbezi,Mkuranga
  Bwejuu, Zanzibar
  bila kuwasahau watu woooote wa friends of Arsenal pale K-Teashop na kule kwa ankal CHAAAZ kinondoni

 5. Anonymous Anasema:

  Leo wameshinda imekuwa tabu hakulaliki!! hebu mkicheza na Man utd fanyenyi kama hivyo basi!! na jitahidini mchukuwe cup!!

 6. Anonymous Anasema:

  je kuna kanisa uwanjani hapo?

 7. Anonymous Anasema:

  Henry ni mwislamu tokea lini?
  Van Persie kuoa Mmorocco ndio amekuwa Mwislamu? Mnaamini sana youtube..
  Ndo yaleyale ya Michael jackson Mwaislamu.

 8. Anonymous Anasema:

  Wadau,

  PANA MASUALA MATATU NI VIGUMU MTU KUJUA UNDANI WAKE:

  1.Imani ya DINI,
  2.Msimamo wa KISIASA,
  3.Siri ya NDANI YA MOYO WA MTU (NIA)

  UFAFANUZI:
  Tutabishana sana isipokuwa jibu analo muhusika na Siri yake ya ndani moyoni mwake:

  1.IMANI YA DINI:
  Pana watu suala la Dini na Msimamo wa KIIMANI inabaki kuwa ni SIRI kubwa ya maisha yake, mfano wapo watu hawapendelei kujulikana wapo ktk Imani gani (Kwa undani),,,ingawa inaonekana siri kwa kitu kama hiki ni dalili ya UNAFIKI'',,,,imeshatokea mara nyingi watu wakavutana sana baada ya Kifo kutokea isijulikane Marehehu azokwe kwa Imani gani kwa vile mwenyewe aliweka ni siri.

  2.MSIMAMO WA KISIASA:
  Ni mara nyingi ktk vyama vya Kisiasa kunakuwa hakukaliki kwa watu kushukiana kuwa na Itikadi za vyama vingine, ingawa wakati mwingine inakuwa sio kweli, Pana wakati mwingine mnakuja kushituka mwenzenu anapandishwa Jukwaani na kuvalishwa koti la chama kingine, Kumbe lohhh mlifikiri mpo pamoja kumbe jamaa sio mwenzenu!

  3.SIRI YA NDANI YA MOYO WA MTU (NIA)
  Siri ya mtu ni kichaka, inakuja fahamika baada ya kitendo kutokea ndio inaeleweke mtu yule kumbe nia yake ilikuwa ni kadha wa kadha!

 9. Anonymous Anasema:

  kama henry na van persie wakiwa wasislam wewe unawashwa na nini? chuki zengine bwana hovyoooo...!

 10. Anonymous Anasema:

  Actually sio siri uislamu unapanuka sana ulaya na asia, na ndio maana ukristo sasa unakuwa exported to afrika. Kuna mtu amekwenda Korea na kukaa kule kama mwaka, anasema kuna makanisa mengi lakini hayana watu. Wakorea wana dini yao ya asili. Wamejaribu kuwapata kidogo lakini bado hawana utamaduni wa kwenda kanisani jumapili. Wamarekani wameyajenga kwa fujo. Uislamu unakubalika ulaya sana. Watu wanataka kujua huu uislamu ni nini na hii Quran ni kitabu cha maajabu gani. Wengi Wakisoma wakiridhika wanaslim. Vijana wengi wanaslim uingereza, Marekani ujarumani na Hispania. Tafuteni, Someni elimikeni sio mnabwabwaja tu. Makanisa mengi ulaya hasa uingereza yamekuwa misikiti, unakatwa msalaba juu unawekwa mwezi, hii sikuambiwa nimeona kwa macho yangu. Padri anasema kuliko kumuuzia mtu akafanya BAR bora umuuzie mtu atakaendeleza kanisa kuwa nyumba ya ibada. Hawooooooo kaageni hivyo hivyo. Islam is spreading slowly but surely.

 11. Anonymous Anasema:

  Kuhusu Prayer Room au Msikiti, najua kuwa viwanja vya Emirates, Ettihad Stadium (Man City), White Hart Lane (Tottenham, ambako Waislamu na Wayahudi wanatumia chumba hicho kimoja kwa ibada), Stamford Bridge (Chelsea) na Bolton vyote vina misikiti au Prayer Rooms.

 12. Anonymous Anasema:

  Timu zote za Uingereza zina misikiti kutegemea na wachezaji wao wanaoswali (Anelka, Kolo Toure, Yaya Toure, Kabul, Armanda Traore, n.k.). Barcelona na Real Madrid pia ina vyumba vya kusalia kwa ajili ya kina Seydou Keita, Eric Abidal, Mesut Ozil, Benzema na Diarra, wakati Bayern Munich ilibidi imtengee Frank Ribery (Bilal) chuma maalum cha kuswalia

 13. Anonymous Anasema:

  Baadhi tu ya wachezaji wakubwa waliotoka Ukristo na kuwa Waislamu ni Anelka, Henri, Van Persie, Franck Ribery, Eric Abidal, Armand Traore na Fred Kanoute. Trend hiyo inaakisi ukweli wa kuwa vijana zaidi ya 8,000 UK na 20,000 Ufaransa wanasilimu kila mwaka. Huko USA idadi ni 70,000 kwa mwaka. Kina Chuck D, Ice Cube wamekuwa Waislamu siku nyingi. Waislamu wapya ni kina Snoop Dogg.

 14. Anonymous Anasema:

  Kaazi kweli kweli hata chuoni kwetu kuna Prayer room ambayo mtu wa imani yoyote ile anaruhusiwa kuingia na kufanya ibada zake between classes. Vile vile kuna Islamic centre pembeni kabisa ya mabweni na madarasa ambayo siku ya Ijumaa watu hujaa mpaka zinafanywa ijumaa mbili kwa sababu medical school ina hospitali kubwa kwenye huu mji (University hospital)ambako kuna waislam wengi wanafunzi na madaktari pia kutoka Afrika na Asia.

  Lakini hapa shuleni hakuna kanisa, ila yapo mtaani na haka kamji kana makanisa kibao lakini machache tu yanatumika mengine ni majumba ya makumbusho!

  Na unaebisha kuhusu Henry nafikiri umesahau kuwa huyu ametokea France ambako inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya waislamu huku Europe.

 15. Anonymous Anasema:

  Ndugu zangu uwe muisilamu, mkatoliki,anglikana,lutherand nk haikusaidii chochote kama huna uhusiano mzuri na Mungu.Nashangaa mdau mmoja hapo juu anashangilia kuhusu kuenea kwa uisilamu sehemu nyingi.We binafsi inakusaidia?kama moyo wako ni mchafu yaani hauko vizuri na Mungu hata ukiwa na dini yenye mapembe haikusaidii kitu na mbinguni huendi maana Mungu haongeki wala hapokei rushwa na hasemi uongo wala hajawahi kusema uongo.Kama amesema usizini,usiibe nk na wewe unayafanya hayo mwisho wako ni jehanamu kwenye moto mwa milele.Mdau hapo juu unaeshangilia dini yako kuenea sehemu nyingi unapoteza muda, ingekuwa vyema kama ungeshangilia watu wengi kumkiri na kumpokea Bwana Yesu maana amekaribia kurudikuwachukua watakatifu waliomwamini na kumfuata sio wale wanaoamini dini zao huku wakimkana Bwana Yesu.Kutomkubali Bwana Yesu ni kutomkubali Mungu pia.Dini yako haikusaidii kitu kama bado unaendelea kuishi dhambini.

 16. Anonymous Anasema:

  1. wenger hajagundua nyavu, nyavu is as old as football itself.
  2.nani anahamua kuisaidia tu FIFA na multi-billion patent?
  3. whats the relevence of religion, race or creed in sports? seriously, proud to have a mosque?
  4. lets spend same effort and time in developing our country