Mdau Abdi Mchopanga akiwa amepozi na mkewe Aziza safi kabisa usiku huu.
Bibi Harusi,Dada Aziza akiwa amepozi  na ua lake safi kabisa usiku huu,wakati hafla ya mnuso huo ikiendelea hivi sasa ndani ya ukumbi wa Water Front jijini Dar.
Maharusi,Abdi Mchopanga na Aziza wakichangamkia msosi usiku huu.
Maharusi na wapambe wao wakichangamkia mnuso safi kabisa.
Bibi harusi akikabidhi keki ya upendo kwa wakwe zake kwa heshima kubwa kabisa.
Bwana harusi nae akikabidhi keki kwa wakwe zake.
Mc Luvanda akitoa maelekezo mafupi kwa maharusi mbele ya wageni waalikwa (hawapo pichani) waliofika kushuhudia mnuso huo wa nguvu unaoendelea hivi sasa ndani ya ukumbi wa Water Front,jijin Dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

 1. hapo juu uncle michuzi angalia kingereza mbona lugha gongana italeta madhala katika ndoa MY WIFE

  ReplyDelete
 2. yani bwana harusi alivyomuona dada wa shampeni amefurahi haswa ila picha zingine zote amenuna

  ReplyDelete
 3. Mdau anony wa Sun Apr 01, 01:50:00 AM, hiyo lugha ya MYWIFE au barabara ya Morogoro road huwa ni lugha za humu jamvini hivyo waliomo humu wanajua it is kind of jokes at the same time unapata na habari

  ReplyDelete
 4. Ndoa ya Kiislamu? Mbona majina ni ya Kiislamu but ndoa imekaa kama ya akina John, Peter, Alex, Marie,Anna, Eliza etc????????

  ReplyDelete
 5. Mabrouk!!

  ReplyDelete
 6. Anonymous wa sun april, 08:28:00 AM 2012 napenda kukujibu tu mimi kama wengi hapa hatuwajui maharusi wanafuata dini gani lakini kwa majina tu nadhani utakuwa unakosea unaposema ni majina ya kiislamu kwani majina hayo sio ya kiislamu bali ni ya kiarabu. Kuna tafauti kubwa baina ya uarabu na uislamu. Kuna waarabu wengi ambao sio waislamu na majina yao ni kama ya waarabu wengine. Uliza waliopo nchi kama palestine, egypt, iran, iraq, jordan na kwengine watakuthibitishia hili. Infact hata waisrael ni taifa moja kati ya mataifa ya waarabu ingawa wako tayari kufa kuliko kukubali hilo.

  ReplyDelete
 7. Mkae ,muishi milele na milele ,mpendane,heshima, bado vijana msirubuniwe na vichochezi , mmependeza sana , nakuombeeni kila la kheri na baraka muwe na mafanikio mema, mpate watoto wema na wawe viongozi wa nchi yetu kwa sisi ambao tutakuwa wazee tayari miaka hiyo, Inshallaah mwenyezi awajalie ! Ameeen

  ReplyDelete
 8. wadau msshituke sana Bwana na Bibi Harusi ni waislam safi na ndoa ilishafanyika ijumaa hii hyo nikama party hiv kwaajili ya kufurahi pamoja na ndugu jamaa na marafiki nk

  ReplyDelete
 9. Yapo Majina Yaki Arabu na Yapo Majina ya Kislamu juwa hilo japo kweli wapo watu Waarabu ambao sio waislamu ila wanatumia wapo majina yao ya Kiarabu na ya Kiislamu kama Ilivyo Kama ilivyo majina Ya Kikristo wapo warusi Waislamu wanatumia majina yao na majina ya Kikristo ila Hao wana Harusi ni Waislamu. Harusi ni Harusi walivyoona wamependa ndio sawa kwao, Kwani hata Kikristo kuna mambo mengi hakuna ila tunaongezea chumvi sababu ya Life ya Kigiriki na Ki Roma.

  ReplyDelete
 10. Mtume Mohammad alituusia kwamba mtafuata kila kitu wanachofanya na hiyo ndio furaha yao, kumbe wanatueleza jahanna. Furaha ni kitu kingine lakini kuiga kila utamaduni mpaka unakuwa kama wao sio vyema. Wazww wa Bwana harusi wamevaa kiislam kabisa. Ila nafikiri bado masheikh wafanye kazi kututoa waislam kutoka utamaduni wa kuiga huu sio mzuri.

  ReplyDelete
 11. Anony wa 08:28 elimika kidogo. Utamaduni wa kufanya sherehe za harusi ukumbini si wa wakristo pekee ni kwa watu wa dini zote pamoja na waislamu. Kinachomata ni uamuzi, fedha na mipango tuu.

  ReplyDelete
 12. Maashallah mumependeza kweli kweli lakini ni kweli angalau bi harusi angefunika hayo mabega.

  Hiyo ni kwa mila za kiislamu nakubaliana na wengine hapo juu tusiige kupita mpaka.

  Hata hao wakristo siku hizi wakienda kanisani basi hufunika hayo mabega.

  Otherwise nawatakieni ndoa njema muishi muzae watoto waje kuwasaidia uzeeni.

  ReplyDelete
 13. Mashallah !

  Muwe na Ndoa ya amani asali kwa maziwa kwa matabasamu lukuki nyusoni milele na milele ugomvi,kulaliana 'Mzungu wa nne' na talaka mwiko !

  INSHALLAH !

  AMIIIIIIIIIN!!!!!!

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...