Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin William Mkapa akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki kwa tikeki ya CCM,Sioi Sumari kwenye Mkutano wa Kufunga Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo hilo uliofanyika leo katika kijiji cha King'ori kata ya Leguruki.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin William Mkapa akihutubia kwenye Mkutano wa Kufunga Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo Arumeru Mashariki uliofanyika leo katika kijiji cha King'ori kata ya Leguruki.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowasa akisalimia wananchi wa kijiji cha King'ori kata ya Leguruki wakati wa Mkutano wa Kufunga Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo Arumeru Mashariki leo.

kwa picha zaidi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Mkapa zungumzia changamoto zinazomkuta Mtz wa leo, sio historia za uhuru. Zungumzia matatizo ya umeme usio wa uhakika, zungumzia maendeleo ya viwanda huo ndo ukombozi ambao hamjamliza. Zungumzia umaskini wa mtanzania. Kaka Michuzi hili ni ombi kwako uwe una balance habari, ukiweka CCM wanafunga tuwekee na Chadema pia wanavyofunga. we ni mwandishi professional, hautakiwi kuwa bias..jitahidi kubalance habari.

    ReplyDelete
    Replies
    1. muwe mnawakumbusha wapiga picha wenu wawe wanatuma habari mapema

      Delete
  2. Aliyoyazungumza mzee MKAPA sikatai, kazungumza vizuri sana KUHUSU KUWAKOMBOA WENZETU WA NCHI JIRANI NA HII NDIYO TABIA YA WATANZANI YA UPENDO NA UPOLE NA UKARIMU.Sasa kuhusu hayo mashirika aliyoyabinafsisha swali linakuja alikuwa wapi siku zote kuwaeleza watanzania wenzake faida za huo ubinafsishaji au anafikiri watanzania ni malimbukeni ni watu wakuburuzwa tu?!Kwenda kuwaita wenzake wanafiki na wafedhuli maana yake ni nini? Hayo yote aliyoyazungumza kama angezungumza mwanzoni nani angemlaumu?Yeye anasubiri watu waje waulize kwani kazi ya viongozi ni nini? Kwanini yeye asitoe hizo taharifa miaka yote hiyo anakuja kuongea leo hii wakati watu washakata tamaa ya maisha?, na kama anawatukana wenzake hivyo faida ya kuwa na upinzani ni nini? na inavoonyesha basi haina maana ya kuwa na upinzani tuwe na chama kimoja kama mambo yenyewe ndio hayo na kumbuka mzee hao ni watanzania wenzako na niwatu wazima wenye utashi kamili ni waume za watu ni mama za watu ni wachumba wa watu ni baba za watu na ni viongozi wa watu si vizuri kutumia hiyo lugha. kumbuka mzee wangu wapinzani haohao ndio wanalipua uozo wote ulio ndani ya CCM na ndio haohao wanaokijenga chama cha mapinduzi kizidi kuwa imara kila kukicha kutokana na wanavyokikosoa. Mzee mkapa kumbuka hayo yote uliyoyaelezea pasingekuwepo wapinzania wa kukuchachafwa walahi usingezungumza hayo yote na watanzania wasingejua chochote kinachoendelea ndani ya taifa lao. Sasa tuambie hizo faida za ubinafsishaji anaefaidi ni nani? MZEE WANGU ULIMI NI KIUNGO KIDOGO SANA LAKINI MATATIZO YAKE NI MAKUBWA SANA, THINK AFTER LIFE ULIYOWATENDEA WATANZANIA UTAENDA KUYAJIBU VIPI?! UMENISIKITISHA SANA BABA LAKINI NAKUPENDA SANA. WEWE UKIWA KAMA MWANADAMU NAFAHAMU UNAMAPUNGUFFU YAKO ALAFU MZEE HASIRA PUNGUZA MWILI MKUBWA HUO UTAPATA PRESHA BUREEE NA BADO TUNAHITAJI HEKIMA ZAKO.ALAFU HAO CHADEMA USIWAJALI SAAANA MZEE WE WAPOTEZEE TU HAO BWANA WANAONGEZA CHACHU TU YA WATU KUWA MAKINI NA UWAJIBIKAJI. NI HAYO TU.

    ReplyDelete
  3. Ina maana CHADEMA hawaja funga kampeni? hii so sawa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. msiwe wepesi wa kulaumu bloggers. mmejiuliza je wapiga picha wenu wametuma hizo picha hazijawekwa? wakituma nawao zitawekwa presha ya nini?

      Delete
  4. mkereketwaApril 01, 2012

    Mkapa kumbuka tulipo ni wewe umetufikisha hapa! uliuza mashirika yooote ya umma na mengine mligawana bure! nyumba zote! ulibariki ufisadi ambao ndio ulioleta umaskini huu! Leo utatuambia nini? kusema kweli hukustahili hata kusimama jukwaani leo!

    ReplyDelete
  5. Acheni Siasa za Kiukoo na Upendeleo ili muweze kushinda ktk Chaguzi na kutawala.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...