Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu wa CCM, Benjamin Mkapa akizindua kampeni za CCM za uchaguzi mdogo jimbo la Arumeru Mashariki leo katika Uwanja wa Ngaresero. 
 Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akimnadi mgombea ubunge wa tiketi ya CCM jimbo la Arumeru Mashariki, Sioi Sumari kwenye uzinduzi wa kampeni za CCM za uchaguzi huo kwenye Uwanja wa mpira wa Ngaresero leo.
 Pamela Sioi Sumari akimnadi mumewe Sioi Sumari wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo za CCM. 
Edward Lowassa.
Sioi akihutubia kwenye mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni za CCM.


 "Wenzetu alama yao ni hii hapa, haina maana yoyote itoeni", ndivyo alisema Kaaya kisha akakitupa hicho kijiti alichokuwa akionyesha. Kushoto ni mratibu wa kampeni za CCM kitaifa Mwigulu
Nchemba.
Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama akizungumza.


 Wananchi wa Arumeru Mashariki wakiwa wamefurika kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM leo.

Mratibu wa kampeni za CCM, jimbo la Arumeru Mashariki Mwigulu Nchemba akiongoza msafara wa waendesha pikipiki kuingia uwanjani
kwenye uzinduzi kampeni za CCM. Kulia ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Martine Shigella.




Mmoja wa walioshiriki katika kugombea kura za maoni kupata mgombea wa CCM, Elirehema Kaaya (kulia) akimpongeza mgmbea ubunge kwa tiketi ya CCM Arumeru Mshariki Sioi. wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Du, ila ule upande wa 2 kitengo chao cha propaganda si mchezo! ni kama yule waziri wa Sadam wkt ule kuwaambia jeshi la Marekani (au NATO cjui) 'mkiingia Baghdad ndo kaburi lenu' kumbe hamna lolote. Jamaa wanatisha ukichungulia mtandao m1 wa kijamii wanavotiana moyo na kuponda kila kitu. Mbaya zaidi hata ya ukweli wanageuza yanakuwa uongo halafu wanaamasishana na kudanganyana mwisho huridhiiika wenyewe, hawataki ukweli, hawaaprishieti na kwa staili hii nahisi hawatafanikiwa kamwe.Wanatuchanganya cc wapenda mageuzi tusio na ufurukutwa wa chama chochote, hata hatujui ukweli ni upi sbb matokeo huwa tofauti kabisa na walivotuaminisha. Badilikeni jamani, najua mnasoma maana mtandao wenu unaongoza kwa kunyofoa habari na picha toka Michuzi Blog, chukueni na hii comment mfanyie kazi.

    ReplyDelete
  2. Hivi jamani huyu mgombea ni SIOI au SIYOI? Mi vyombo vya habari vinanichanganya kweli! Big up CCM kwa uzinduzi wa kishindo anyway!

    ReplyDelete
  3. Waswahili wanasema " Kwa kila Azidiye zaidi huzidiwa " Mtu anayezidi kujigamba kuwa ni bingwa wa jambo, huja siku naye akajikuta ameshindwa na wengine.

    ReplyDelete
  4. duuh, kazi ipo. hio nyomi ni noma. kwa kweli mdau wa 1 nakuunga mkono maana mm ni mwenzako nayataka kweli mageuzi ya kweli lakn hii ccm bado haitingishiki labda wajiandae kwa miaka 20 baadae lakn kwa sasa hapana.kidogokidogo tu..mbaya ni hio ya kututia matumaini kuzidi uhalisia wa mambo mwisho watu wanaona upuuzi na kuamua kuirudia ccm yao

    ReplyDelete
  5. Mwenzenu nsioni ni kwa namna gani CHADEMA na washiriki wenzake wanaweza kupona hapa, ingawa ninaelewa kuwa mwisho wa habari akina Mbowe watalalamika kuibiwa kura kama ilivyozoweleka!!

    ReplyDelete
  6. watanzania wanasikitisha sana jamani vumbi lote hilo mgombea akipita na kushinda uchaguzi wanaanza kulia njaa hehe kweli mmelogwa na mchawi mwenyewe kafariki sasa hapo kazi ipo.

    ReplyDelete
  7. Huyo mratibu wa kitaifa anayepanda piki piki akiwa amesimama na hajavaa helmet anatoa picha gani kwa watanzania na ndo kusema kuwa trafik hawakuona hilo tukio!!

    ReplyDelete
  8. Huyo Kaaya hapo umecheza kitoto. Kumbuka unaowaonyesha hiyo manati ni watu wazima!

    ReplyDelete
  9. HAKUNA KITAKACHOIONDOA CCM, KAZI IPO!!

    ReplyDelete
  10. Hili nyomi dogo sana, halikuti lile la CHADEMA.
    CCM hamuwezi mziki wa CHADEMA
    Aaaagh!!!

    ReplyDelete
  11. mkapa ni jembe.na kelele hizi za kejeli na tambo zote bado cku 14.mtanyamaza

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...