Na Mwandishi-MAELEZO-Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho kikwete amesema hatua ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) kujiunga na Mamlaka ya kimataifa ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (IAACA) kutasaidia kupanua wigo Taasisi katika kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa nchini.

Rais Kikwete ametoa kauli hiyo leo(jana) jijini Arusha wakati akifungua mkutano wa watendaji wakuu wa Taasisi za kupambana na Rushwa kutoa nchi mbalimbali Duniani.

Amesema kuwa hatua hiyo ya TAKUKURU kujiunga na IAACA itawasidia kukabiliana na vitendo rushwa kwa usaidizi wa kimataifa pindi watuhumiwa wanapokimbilia Nchi nyingine kwa ajili ya kupata hifadhi ili wasifikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Rais Kikwete amesema hatua hiyo itasaidia kuimarisha vita dhidi ya baadhi ya watendaji ambao wamekuwa wakitumia nafasi zao kujinufaisha na mali za umma na hivyo kurudisha nyuma maendeleo katika baadhi ya miradi ambayo ingetumia fedha fulani kuiendeleza badala inazoishia katika mifuko ya watu wachache.

Hivyo Rais Kikwete ametoa wito kwa nchi wananchama kuisaidia TAKUKURU kwa fedha na vifaa kwa ajili ya kuwasaidia katika vita dhidi ya kupambana na rushwa nchini.

Rais Kikwete ameongea kuwa utashi wa kisiasa ni muhimu katika kufanikisha mapambano dhidi ya rushwa nchini ili vita hiyo iweze kuleta matunda na tija kwa Taifa na wananchi wake .

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Dr. Edward Hoseah amesema kuwa mkutano huo ambao unafanyika kwa mara ya kwanza nchini utasaidia kubadilishana uzoefu na kuwajengea uwezo Nchi wananchama kwa ajili ya kuwa na mtandao utakaosaidia utakaowaunganisha katika kukabiliana na vitendo vyote vya rushwa katika maeneo yao.

Amesema kuwa hatua hiyo itasaidia misingi itakayowawezesha kuwa na malengo ya pamoja na kampeni za pamoja ya jinsi ya kukabiliana na rushwa ulimwenguni .

Aidha Dr. Hoseah amekiri kuwa pamoja jitihada kubwa zilizofikiwa na TAKUKURU katika kupambana na rushwa bado rushwa ni changamoto kubwa ambayo inahitaji ushirikiana kwa wadau wote ikiwemo kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kutoa ushirikiano kwa Taasisi pindi wanapohitaji taarifa.

Amesema kuwa kuiachia TAKUKURU pekee haiwezi kumaliza tatizo la uwepo wa rushwa nchini na hivyo kuwataka wananchi wawe chachu ya kuimarisha mapambano hayo.

Mkutano huo ni mara ya kwanza kufanyika nchini ambpao zaidi ya washiriki 65 kutoka nchi mbalimbali zinashiriki mkutano huo wa siku tatu.

Washiriki hao wanatoka Nchi za vile Morocco , Uingereza, Qatar, Uganda, Romania, Brazil, Austria, india, Belgium , Spain, Ukraine , Malsiyia , Namibia na Mwenyeji Tanzania.

Wakati huo huo Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Dk. Edward Hoseah amechaguliwa kuwa Mwenyekiti Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri juu ya Rushwa ya Umoja wa Afrika kuanzia mwezi Machi mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hamna lolote! Takukuru mnatuyeyusha tu. Kama kweli mko serious na kupambana na rushwa mnashindwaje kuwawekea mitego polisi wa barabarani mkawakamata wakati ni wala rushwa wa waziwazi.

    NENDENI ZENU HUKO!

    ReplyDelete
  2. Mtoa maoni wa kwanza fanya ubadilike maana hizo tabia za kubeza na kukatisha tamaa sio nzuri,watu wanaposonga mbele wanahitaji kupongezwa na kutiwa moyo, hii taasisi sio ya mda mrefu sana na inaonekana kuendelea kuimarika .Matatizo hayawezi kuondoka kwa siku moja ktk nchi yetu kama sisi wenyewe hatutobadilikanwatoaji rushwa qwakubwa ni sisi wenyewe wananchi sasa tumefanya jitihada gani kuiboresha nchi yetu,tupunguze kulalamika tufanye kazi kwa bidii na uadilifu kila kitu kitakua safi maana hao takukuru pia watafanya kazi vizuri kama tutashirikiana na siokutegesheana

    ReplyDelete
  3. Mtoa maoni wa pili tafadhali usiwatetee hawa TAKUKURU. Mtoa maoni wa kwanza yuko sahihi. Trafic police wanalazimishia makosa ili wapewe rushwa. Kwa sababu wana nguvu hata wakikupeleka kituoni lao moja, mtu unalazimkika kuwapa hivyo vijirushwa ili wakuachie uendelee na safari zako. Kwani takukuru hamyaoni haya? Je sio kwamba mnawasitiri kwa sababu lenu moja? Msitudanganye hamna mnachokifanya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...