Ankal Asalam Aleko.

Pole kwa mishughuliko ya kila siku. Mzee tunataka msaada wako kuanika uovu wa pale eapoti ya Julius Kambarage Nyerere. Hivi ninavozungumza sisi ndugu wa Haroun Abdullah Othman aliyefariki huko Ugiriki wiki mbili zilizopita tumekataliwa kuchukua maiti yetu kutoka hapo airport. Tunahangaishwa huku na huko bila mpango maalum. Kuna kila dalili ya maafisa hao kutaka hongo kutoka kwetu ili watupe hio maiti. 

Tatizo ni kwamba hata pesa za mazishi tumefanya kukopa na kuomba huku na kule. Pesa za kuhonga hatuna kabisa!! Maiti ipo chumba cha cargo hapo airport na tuna wasiwasi kwamba itaoza kwa joto la Dar. Hivi ninavyoandika ni saa 11:30 asubuhi. 

Ndege imefika hapa saa saba usiku. Tunatamani kuwaachia hio maiti, tuone mwisho wao itakuwa nini. Jamani hongo mpaka kwenye suala la kifo? Hapa ninavyoandika nina wasiwasi tutachelewa boti ya saa moja asubuhi tuliopanga kupelekea maiti wetu Zanzibar kwa mazishi ambayo yamepangwa yawe saa tano asubuhi. 

Naandika kwa hasira na uchungu nieleze jinsi uonevu kwa watu wanyonge hapa airport.Inasikitisha kuona kwamba watu wanaendekeza ufisadi katika wakati huu mgumu, badala ya kufariji wafiwa wao wanaendekeza ufisadi. Hivi kweli basi watu wamesahau hata utu na kuipa maiti hiyo heshima yake ya mwisho?

Tafadhaili tunaomba msaada wako ili tuweza kutoa hiyo maiti ukweli hasa hiyo maiti imetoka mbali na inakuja kukwama hapo nyumbani ni jambo la kisikitisha tena kusikitisha sana huu ni uozo wa mwisho sio kuwa na mfano.

Mdau,
Dar-Es-Salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. Ili usaidiwe kuwa mkweli na muwazi. Wamewazuia kwa kigezo gani? ninavyoelewa kuna Standard Procedure. je hizo zimekiukwa? Toa maelezo zaidi tulifanyie kazi swala hili...

    ReplyDelete
  2. Mie nina wasiwasi kuwa hao jamaa wanahisi huo mwili una kitu ndani! wacha wafanye uchunguzi then watakupa tu.

    Hata majuzi kuna mwili ulipita hapo toka India na ulikuwa na 'mzigo' wa kufa mtu.

    Poleni sana

    ReplyDelete
  3. Hao sio binaadam ni wadudu na wapo kila eneo la ofisi muhimu kwa wananchi

    ReplyDelete
  4. kuwa muwazi zaidi,sidhani wanataka rushwa, fuata taratibu na punguza jazba. Hii huwapata wafiwa wengi na kuhisi wanaonewa. Tanzania si nchi mbaya kiasi hicho jamani. Tuache uzushi.

    ReplyDelete
  5. Jamani jamani jamani!hiyo ni Laaaaaanna isiyokifani,,Mimi naogopa sana hali tunayoenda nayo huko nyumbani,,Mwenyezi Mungu atuepushilie mbali kuja kutukasirikia akatuletea maafa ya Sodoma na Gomora,,maana hii sasa ni TOO MUCH,EeEEeeehh Pu Pu PU Ruswa mpaka kwa maiti,,jamani tukiendekeza hawa mafisadi wapenda kula jasho la wenzao,,ghalika ikija haichagui jamani,,fisadi na asokuwa fisadi,Inatukumba wote.
    Ina maana wanaanza kuiadhibu hiyo maiti hapa hapa Duniani kana kwamba wao wataishi milele!
    Tuombe sana kwa Mwenyezi Mungu atukinge na hawa watu!

    Ahlam,,UK

    ReplyDelete
  6. Pole sana jamani kwa msiba mzito na usumbufu unaoupata airport. Hapa naona umerusha lawama tu, lakini haujatueleza sababu hasa sababu iliyofanya wacheleweshe kuwapatia. Maana 'hongo' haiwezi kuwa sababu. Hongo ni matokeo ya sababu, ili kuweza kuzima sababu hiyo. Tupe sababu, ndo tutaweza kuchangia vizuri

    ReplyDelete
  7. Nimeisoma kwa machungu sana,poleni wafiwa wote,hiyo ndio Tanzania kama tuijuavyo,ipo siku yataisha hayo manyanyaso.

    ReplyDelete
  8. Mdau pole lakini angalau ungeandika sababu ya maiti kuzuiwa ndipo tungetoa mchango/mawazo ya kusaidia.

    ReplyDelete
  9. kwa hilo la Airport ikiwa maiti inashikiliwa hivyo uliza sasa wafanyabiashara wa kitanzania wanavyokuwa HARRASED utadhani wapo nje ya nchi yao. Ajabu ni kwamba huko nje mnakwenda na mabo yenu bila presha ila ndege ikianza kutua unawaza watu waliojipanga pale pa kuchukulia mizigo, yaani hata mamishen town wanaafadhali. Ni uozo wa kunuka jamanihivi Airport haina MABOSI?

    ReplyDelete
  10. Msipate tabu mdau, nyie wasusieni hiyo maiti huku mkiomba duwaa kwa marehemu na tuone wataushikilia mwili wa marehemu mpaka lini. Haya mambo yanatakiwa kwisha jamani. Najua wataupeleka mwili manispaa ndio hapo nyie mtaenda na kuudai na mtapewa bila wasiwasi. Naungana na wewe kukupa pole kwa msiba uliokukuta ila Molla yupo nasi na atatufariji yote yatakwisha.

    Mdau aliyehuzunishwa

    ReplyDelete
  11. Pole sana mfiwa , kuwa na subira, inabidi utueleze nini ulichoambiwa, wakati mwingine mapungufu yanakuwa upande wetu wananchi tunakuwa wagumu kuelewa na kufuata taratibu, na mara unapoelezwa utaratibu wa kufuata tunadhani yanajengwa mazingira ya rushwa, je utaratibu wote wa customs, documentations nk kadhalika umekamilika, pia kuna taratibu za kufuata hali inapokuwa ikwama kwakumuona msimamizi wa mahala husika, kukimbilia kuandika kwenye blog kama hivi sidhani kama inasaidia sana, badala kukaa kwenye laptop na kuandika uliyoandika ungejaribu kufuata utaratibu ili malalamiko yako yawafikie walengwa ili tatozo lililo mkono mwako lipatiwe ufumbuzi

    ReplyDelete
  12. How low can you get!! Huu sio mzigo au cargo. Huu ni mwili wa binadamu. Mpeni huyu mtanzania heshima anayostahili na muachie akapumzike.

    ReplyDelete
  13. Mola atawalipa hapa hapa duniani wote wanaowatesa wafiwa katika wakati huu mgumu.

    Watanzania tumekuwa na roho mbaya namna hii? Tatizo kubwa ni kuwa viongozi wanayajua matatizo haya na wanayafumbia macho. Matokeo yake watu makazini wanafanya watakavyo na kudai hongo kila mahali.

    ReplyDelete
  14. Dawa ni moja tu, tumieni mobile zenu kurekodi mazungumzo na hao wanaotaka pesa, mkishapat aushahidi mna play mbele yao na muone kama hawatatoa huduma haraka mno na mwisho wakisha wahudumia msisite hapo pelekeni rekodi kunakohusika.

    ReplyDelete
  15. Poleni sana wapigeni kwa hasbia allah waneema alwakil

    ReplyDelete
  16. Walitoa sababu gani?

    ReplyDelete
  17. mdau pole kwa msiba na machungu ya kumpoteza ndugu yetu haroun,nimesoma malalamiko yako lakini hakuna sehemu ambayo umeeleza kwa uwazi kwa nn mnakataliwa kuchukua mwili wa marehemu???
    hapo lazima ziko taratibu ambazo hamjazikamilisha, sio bure tu!

    ReplyDelete
  18. Pole sana ndugu yangu kwa kukumbana na utaratibu ambao umekuchelewesha huku ukiwa na majonzi makubwa.Ninashauri kuwa na subira pamoja na kuwa kweli mipango yenu haikuwa hivyo.Kuna kesi nyingi za watu wenye nia mbaya kutumia miili ya marehemu wetu kuvushia madawa ya kulevya hivyo huenda mamlaka husika zilikuwa zinahakikisha kuwa nyie sio watu wa namna hiyo kabla ya kuwapa mwili wenu.Hata hivyo ndugu yangu , kama mwili umefika saa saba usiku na wewe asubuhi ushaanza kulalamika , hujaonyesha uvumilivu.Tuwe wavumilivu wakati mwingine kuzipa nafasi mamlaka zifanye kazi kwa manufaa ya jamii yetu.

    ReplyDelete
  19. Ndugu mtoa taarifa umetoa taarifa kwa ufupi sana maana hukusema wewe nani unapatikanaje na labda namba za simu wamekukwamisha kwa lipi zaidi umelala mika bila kutoa taarifa kamili ili atua zichukuliwe kwa maofisa hao

    ReplyDelete
  20. Jamani mengi tunamezea Bongo shauri ya njaa, tamaa, ufisadi, and you name it. Ni dhahiri JKN Airport hapa sasa mnavuka mpaka, au miwili.

    ReplyDelete
  21. Jamani poleni sana hakuna mfiwa anapenda kupitia hili. mabosi wa airport lazima muwashughulikie waliokuwa zamu kikazi hii sababu ndege imeingia usiku wao wananyanyasa watu

    Please wafikisheni mahakamani rushwa ife

    mmeishia wapi sasa

    ReplyDelete
  22. Jamani hivyo yupo binaadamu atakaepuka kifo? Hao jamaa wanaotia ngumu na wao si yatawarudia: Watanzania tumekua
    na roho mbaya, hatuthamini utu,
    sisi ni kitu tu; ukiwa nacho basi
    wewe ndo bwana. Immingration hata
    wafanywe nini rushwa hawaachi kabisa. Labda wote futwe kazi.

    ReplyDelete
  23. KWA UCHUNGU MZITO INABIDI NA MIMI NILAANI HIKI KITENDO CHA KUZUIA MWILI WA NDUGU YANGU HAPO UWANJA WA KENGE WA DARESALAAM(NO TYPING ERROR)
    BAADA YA KUUGUA KWA MUDA MREFU NA HATIMAE KUAGA DUNIA JAMHURI ANAHITAJI KUPUMZIKA KWA AMANI NA AMERUDI KWAO KWANI MIAKA MINGI TULIONDOKA ZANZIBAR PAMOJA KUJA KUTAFUTA MAISHA MISRI NA HATIMAE UGIRIKI AMBAKO NDIKO ALIKO AGA DUNIA SASA AMERUDI KATIKA SANDUKU BILA KUFANIKIWA ALILOKWENDA KUTAFUTA MIAKA YA THEMANINI HAO MAHARAMIA WA HAPO MNADANI WANAPORUSHIA NDEGE WANATAKA PESA.

    MIMI SINA HAJA YA KUTAKA KUJUA KAMA WANA WASI WASI NA MWILI UMEBEBA NINI? KWANI KAMA HILO NDIO TATIZO SI WAUCHUNGUZE NA UCHUNGUZI HAUCHUKUI HATA MASAA MAWILI LAKINI HILO SIO LINALOWASUMBUA LINALOWASUMBUA NI PESA.

    IKO HAJA YA KUTANUA UWANJA WA NDEGE WA ZANZIBAR NA SISI TUKIJA KUFA TUREJEE PALE KIEMBE SAMAKI AMBAKO TUNAFAHAMIANA NA MAITI KWA DINI NA DESTURI ZETU HATUIKASHIFU WALA KUICHELEWESHA KUIPUMZISHA KATIKA KABURI LA HAKI.

    KUNA WENGINE WANAZALIWA NA KUTAFUTA MAISHA KWA SHIDA MPAKA WANAKUFA DUNIANI BADO KUNA VIUMBE WANAWAPA SHIDA SIJUI HUKO AHERA MUNGU TUSAIDIE.

    UPUMZIKE KWA AMANI POPOTE WATAKAPOKUWEKA NDUGU YANGU KARABI.

    ASANTENI.

    SUNDAY,USA.

    ReplyDelete
  24. Ankal,

    Ukiweza tunaomba tuwasilishie rasmi lalamiko la wafiwa kwa wahusika.Kama kuna taratibu zilisababisha usumbufu huu na sisi wadau kwa kutumia blogg hii tuelimishwe.

    Wote tupo njia moja, usije ukajikuta DAR Airport unasubili ndege ya saa moja, huku unataka ukazike saa saba, kumbe hiyo haiwezekani.

    Kama ilikuwa ni uzembe tu, basi waliohusika washughulikiwe kikamilifu.

    Ankal blogg yako inafika kila pembe, kwa hiyo DAR Airport wanaweza kuitumia kutufahamisha kinini kiliwasibu wafiwa, na kama ilikuwa ndiyo taratibu, basi na sisi wadau tuelimishwe hizo taratibu.

    ReplyDelete
  25. Hakuna sababu inayohalalisha kudai hongo tumeona mara nyingi maiti zinakataliwa kutoka Muhimbili kama hukutoa hongo, huwa hawakosi sababu ya kukucheleweshea kuchukua maiti yako. Ukweli ni kwamba kutoa hongo nikitu cha kawaida hapa Tanzania ukimnasa mpokea hongo atatoka polisi au mahakamani kwa kutoa hongo. Kilichobaki tukubali nchi imetushinda kuongoza.

    ReplyDelete
  26. may be wamelipenda jeneza la marehemu maana majeneza yanayokuja kutoka majuu mazuri kupita kiasi ukiliuza hukosi hela ya mtaji

    ReplyDelete
  27. Ndugu na jamaa Watanzania wengi mmeonekana kutaka kujuwa sababu, ngoja liwe kwa upande wako ndipo utakapojuwa uchungu wake, sababu gani? Ikiwa taratibu zimefanywa katika serikali ya Ugiriki na wameipitisha na kuitoa ndani ya nchi, ili ndio tatizo letu yarab nafsi yangu na hicho ndicho kinachofanya ufisadi,rushwa kuota mizizi. mzazi wangu pole sana sote tuko safarini katika hii Dunia kaza moyo wapo binaadamu wamepewa majukumu hawajuwi kama wataulizwa kutokana na majukumu yao! wanavipitia vitabu kwa kuimba na kusoma bila ya ufahamu.

    ReplyDelete
  28. Wadau Maoni mengi nimeyasoma na yangu ni haya:

    1.Kama kuna wasiwasi Maiti inaweza kuwa na 'Mzigo wa Madawa' je ingewezekana vipi Mamlaka za Ugiriki (Forodha) ziruhusu mwili kupita Customs Check up bila kuona hili?

    Inafahamika hakuna Forodha ambayo inaweza pitisha kitu bila ukaguzi tena wa Computer au Vifaa vya kisasa na kuwa kila mzigo ukisha kaguliwa hufungwa kabisa kuwa 'sealed' sasa nafasi ya kuweka huo mzigo ktk Maiti ingetoka wapi?

    2.Kama itakuwa ni mgandamizo wa kutaka kupewa Rushwa hao maofisa, itakuwa ni balaa hili sasa, na hakuna kingine zaidi zaidi wanataka pesa za kudunduliza hadi kuzidai RUSHWA MAITI ili kuendea Yadi kununua Magari, kulewa pombe , kuhongea Wanawake na kujenega majumba!

    ReplyDelete
  29. Hii ni rushwa wazi wazi. Chambilecho mzigo umetoka nchi za ulaya unkaguliwa na kuwa sealed na kupakiwa katika ndege labda uwe umeshonwa ndani ya tumbo. Hao madaktari waliogoma juzi waomba rushwa wakubwa, hasa wakihisi kuwa unajiweza weza hivi wanadai, wauguzi ndio usiseme, na wahudumu mgonjwa utamkuta na mikojo kule moi. there is rushwa everywhere na mpaka likupate jambo haliepukiki life threatening utatoa ili kuokoa maisha au mali. RUSHWA IPO BWANA MPAKA LIKUFIKE. HATA WASTAAFU WANAODAI HAKI ZAO WATU WAKIONA ZILE MILIONI HAZITOKI MPAKA UMETOA CHOCHOTE, NACHOCHOTE CHENYEWE SIO ELFU KUMU NA WAO WANATAKA MILIONI. MIE SIONI AJABU AIRPORT. USIONE WATU WANANENEPA BILA MPANGO NA KUJENGA MAJUMBA KAMA HAWANA AKILI NZURI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...