Habari za asubuhi Ankal na timu nzima ya Globu ya Jamii.

Mapema asubuhi hii imetokea ajali mbaya sana katika makutano ya barabara ya chang'ombe na mandela iliyohusisha magari mawili aina Mitsubishi lenye namba za usajili T 987 BDH linalofanya safari zake kati ya Mwenge na Temeke na gari aina ya Suzuki Grand Vitara la Legal Sector Reform Program lenye namba T 305 AEN. Chanzo cha ajali hiyo ni ile namna ya kuvuka kwa staili ya gombania goli ambapo kina mmoja alikuwa anataka kuvuka.Cha ajabu pale kwenye junction kuna taa ambazo ziliwahi kufanya kazi kwa siku mbili tu wakati zilipo wenkwa na kisha wakazizima mpaka leo. Baada ya hapo kila siku lazima zitokee ajali maana kila mmoja ana haraka na anajiona ana haki!
Chakuchekesha baada ya ajali eti traffic polisi sasa hivi ndio amekaa anaongoza magari! Jamaa anafunga geti baada ya farasi kutoweka!

Picha na Mdau
Mohammed H. Shossi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Jamani Nasahngazwa sana kila nikisia imetokea Ajali hapo changombe serengeti A.K.A Machinjoni...Kwani hakuna dereva Dar asie fahamu kwamba hapo ni chinja chinja anatakiwa kua mwangalifu anapokatiza kwenye hayo mataa mimi nakumbuka nikiwa na miaka 6 baba yangu aliwahi kuniambia hiyo sehemu sio nzuri panaitwa machinjoni na nimekua nikipafahamu hapo kwa jina la machinjoni sasa nawashangaa saana hawa medereva honi ambao wanajifanya kua wanajua sana barabara hawataki kuelewa.. TAKE CARE HAPO NI MACHINJONI>> JAMANI UNAPOPITA KUA MWANGALIFU

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 28, 2012

    barabara chafuuuu alama zimechokaa sheria zinanuka rushwa viongozi wananukia mihela

    sirudi huko kwanza hata uraia nishaukana sitoki nchi ya watu wenye ugumu wa kuelewa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 28, 2012

    Hii inchi sijui nani katuroga jamani, hivi ni lini tutakuwa wawajibikaji na wabunifu jamani? hili eneo limekuwa likisababisha ajali kwa miaka mingi sana. Mimi nimesoma hapo kibasila na kumaliza 1994, kwa miaka minne nilokuwepo hapo ajali zilikua zikitokea kila kukicha.
    Unaweza kujiuliza wahusika kwa nini hawabuni namna ya kutatua tatizo lilopo katika eneo hilo jamani? aghaaaa! Kama taa zinawashinda kuziendesha wekeni roundabout watu wajue moja. Poleni sana wote mliopatwa na ajali, Allah Az-Zawajal awaponye upesi inshaallah na muweze kurudi kwenye familia zenu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 28, 2012

    MACHINJONI!!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 28, 2012

    Hii inasikitisha sana, mbaya zaidi Trafick wanakaa pale toka asubuhi ila wanakaa pembeni hata hawashughuliki na magari yanayocross pale, ila wanasubiri tu gari wanazoweza kupewa rushwa siku kwao inakuwa imepita, wanafunzi wa kibasila ndo kabisa maisha yao yapo hatarini. Sijui tunaelekea wapi na kuna maana gani ya kuziwasha zile taa kwa siku mbili then haziwaki tena na hakuna maelezo yoyote kama zina tatizo au ndo ukiona manyoya ujue kashaliwa.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 28, 2012

    Hivi jamani bongo tutamaliza lini hizi ajali ambazo zinaweza kuzuilika. Hao wadau walioathrika katika ajali wana haki kabisa ya kuishitaki serikali kutokana na hili.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 28, 2012

    Jamani waungwana, Nimeisoma Road Traffic Act ya 1973 yote, ambayo ndio sheria ya barabara zetu. Hii inaelezea kabisa jinsi gani Polisi wanatakiwa wasimamie usalama wa barabarani lakini hauifuatwi hata asilimia moja. Wananchi wanaweza kuishitaki serikali katika ishu kama hizi. Jamani wansheria bongo tuungane ili wananchi wapate haki.

    ReplyDelete
  8. Mwangwitwa ChrisMay 28, 2012

    nami napafahamu kwa ajali maarufu kama machinjioni,sio kwamba trafic hawapo wapo kazi yao ni kukamata magari yanayotoka bandarini yaliyobeba makontena wanapewa posho zao mambo yanakwenda hao ni trafic wetu yaani mpaka aibu,sasaajali imetokea ndio utawaona wakimbizana kama wanawajbika kweli

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 28, 2012

    Utakuta mtu kaliachia lorry kutoka bandarini halafu anapiga honi nyingiiii mwendo si chini ya speed 60 utadhni yupo barabara ya porini kumbe yupo mjini. Zile tochi zingetuka pale serengeti naamini zingefanya watu wakapunguza mwendo na kupunguza ajali kabisa.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 29, 2012

    vijan wanaoendesha siku hizi ni walevi. Eti wanamwona mtu au mtoto anavuka barabara na yeye anakuja badala ya kupunguza mwendo anampigia honi mtu mzima/mtoto anashtuka akipigiwa honi. Hicho kitu kinanisikitisha. Au mtu anavuka zebra anapigiwa honi umesikia wapi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...