Meneja mpya wa bendi ya Mashujaa Martin Sospeter (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza kujiunga na bendi hiyo kwenye ukumbi wa Busness Kijitonyama asubuhi hii.Kulia ni King Dodoo ambaye ni Kaimu Meneja wa bendi ya Mashujaa na Kushoto ni Kiongozi wa Bendi hiyo,Charles Baba.

Ifuatayo ni Taarifa ya Meneja huyo Mpya wa Bendi ya Mashujaa.

"Juzi usiku nilishangazwa na kauli ya mkurugenzi wangu wa zamani katika Bendi ya African Stars,Asha Baraka katika vyombo mbalimbali vya habari kuwa amenifukuza kazi kutokana kuhujumu bendi ikiwemo kushawishi wanamuziki kujiunga na bendi ya Mashujaa.

Kwa kweli kauli ile ilinisikitisha sana kutokana na ukweli kwamba Asha nilimchukulia kama dada yangu,kwani nilifanya naye kazi kwa miaka 14 iweje hii leo aje anitolee maneno ya kunichafua katika vyombo vya habari?

Mimi sijawahi kuhusika na mpango wowote wa wasanii wa Twanga kuhamia Mashujaa na wala sikuwa nafahamu mpango huo zaidi ya mwisho wa siku kusikia fununu za chinichini na mwishowe wasanii hao kutangazwa kuhamia Mashujaa.


Leo napenda nitangaze rasmi kwamba nimeachana na African Stars na kujunga na Mashujaa Entertainment na tayari nimeshasaini mkataba wa kazi katika bendi hii".

“Nilipanga nifanye taratibu za kumuaga kutokana na kuwa nilikuwa nafanya kazi kwake bila ya mkataba lakini nimepata bendi hii ambayo tulikaa na kukubaliana mambo mbalimbali.

Mbali na mkataba baadhi ya makubaliano na uongozi wa mashujaa ni pamoja na kunipangia nyumba hali itakayoniladhimu kuhama ile iliyokuwa chini ya Twanga.

Ninaamini nitafanya vema kazi yangu hii mpya kama ilivyokuwa Twanga ambapo nilidumu kwa muda mrefu na kuchangia kufika hadi hapo nilipoachia, hivyo naomba ushirikiano kwa uongozi, wanamuziki, Wadau na hata ninyi mwaandishi wa habari"Mwisho wa taarifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 29, 2012

    Big up martin achana na Asha hana mpango ni mfa maji. Akikosana na mtu hukimbilia ktk media kumchafua na kama ni mkongomani anakimbilia uhamiaji kumchongelea.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 29, 2012

    Sasa naanza kuwa na wasiwasi na TWANGA huenda kuna tatizo kubwa...haiwezekani wanamuziki waondoke kwa staili hii...DADA ASHA TAFAKARI!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 29, 2012

    Nyie Mashujaa kazi yenu kuiba wanamuziki wa Twanga tuuu??? Kwa nini??? Hamna ushujaa wa kuibua vipaji vyenu na kuvikuza?? Mashujaa wa kurubuni wanamuziki wa Twanga!!! Halafu bila aibu mnajionyesha mbele ya hadhara kuhalalisha ulaghai wenu!!! Shame on you!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 29, 2012

    Sasa inaonekana Mashujaa lengo lake si kupata wanamuziki bora tuu kutoka Twanga Pepeta kisima cha burudani bali ni pamoja na kuwachukua hata wafagiaji wa Twanga Pepeta. Mradi tuu wasafirie kwa Nyota ya Twanga.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 29, 2012

    TUSEME HAO MASHUJAA HAWAWEZI KUSIMAMA KWA NJIA NYINGINE MPAKA WATUMIE MGONGO WA TWANGA?. HII NI TOO MUCH NOW. HAWAWEZI WAKATOKA KWA NJIA HIYO, KWANI BADALA YA KUPATA BARAKA ZA WAPENZI WA MUZIKI WATAJIKUTA WANAENDELEA KUPIGIA VITI KAMA ILIVYO MPAKA SASA. WAMEJAZA RUNDO LA WANAMUZIKI LAKINI WATU HAWAENDI KWENYE MAONYESHO YAO

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 29, 2012

    Ha ha ha nadhani ili Masujaa Band Isimame inabidi wamchukue ASHA BARAKA na uongozi mzima wa ASET na wanunue jina la Twanga Pepeta hapo watakuwa wamemaliza kazi na kutimiza azma yao na si vinginevyo.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 29, 2012

    Go dude....go....miaka 14 yatosha sana

    ReplyDelete
  8. Mikausho MikaliMay 29, 2012

    Dada Asha mishahara na mzingira mazuri ya kazi ni muhimu katika management ya ambo lolote lile.Amini nakuambia utabakia na Msafiri Diof peke yake kwani pamoja na talent yale ana tatizo unaloliua kwa undani

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 29, 2012

    wote watatu hapo mbele wanafiki watupu na wala hamna shukrani,twanga ndio imewapa majina mjini,so mnatakiwa kushukuru kwa kila kitu.

    MDAU WA TANDIKA

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 29, 2012

    Uhusiano wa kiutendaji kati ya kiongozi na meneja wa bendi ukoje? Kiongozi kivipi, maana hata meneja ni kiongozi? Au semeni cheo kwa Kiinglishi kitajifafanua chenyewe.

    Sio ishu ila ni inanikera tu. Kama itawaudhi ni sawa kunitukana kwa gharama zenu, ila ninaomba tu kujua maana ninasomea masuala ya uongozi na utawala.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 29, 2012

    Jamani msimtukane mkunga uzazi ungalipo.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 30, 2012

    Na kweli Anony hapo juu umenena, hao wote ni wanafiki. King Dodoo aliletwa hapa nchini na Baraka Msilwa Mwenyekiti wa Twanga na kaishi miaka mingi nchini kwa kumtegemea mpaka kwa working permit. Martin Sospeter naye alichukuliwa kutoka Tanga miaka ya ya 90 na akakulia na kupata umaarufu akiwa anaishi Upanga nyumbani kwa Baraka Msiilwa. Chalz Baba gari yake ya kwanza kuendesha alinunuliwa na Twanga. Wanapaswa kuwa na shukrani na siyo kujishaua kama wanavyoonekana mbele ya wandishi wa habari.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 30, 2012

    Anony wa pili hapo juu si Dada Asha wa kutafakari, ila wewe ndiyo unapaswa kutafakari. Jiulize kwa nini hili wimbi limekuwa kwa bendi moja tuu ya Mashujaa kuwarubuni wanamuziki wa Twanga kwa kuwapa pesa nyingi ambazo wala haziwezi kurudi kwa kutegemeaa biasharaa inayotegemea gate entrance. Hapa lazima kuna pesa chafu inatoka kwa mpigo kuwahadaa hao vijana.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 30, 2012

    Hivi huyo Martin anayeongelewa alikuwa ni Manager anayefanya kazi zipi hapo Twanga?. Najua huyo siyo Mwanamuziki.Role yake haswa ilikuwa nini?. Tunajua Kiongozi wa Bendi (Band Leader)yupo bado na ni Luizer Mbutu, akisaidiwa na Salehe Kupaza. Murugenzi Msaidizi- Omary Baraka, Manager Utawala(Administration), Hasani Rehani, Manger uhusiano na Masoko Amigolas, na Mkurugenzi Mtendaji Asha Baraka hao wote bado wapo chini ya Mwenyekiti wao Baraka Msilwa). Huyu Martin Sospeter alikuwa ni Manager wa nini mpaka tunapoteza muda kujadili hapa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...