Aliyewahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara miaka ya nyuma,Mh. Idd Simba (kulia) akiongea na Wakili Said Hamad El-Maamry wakati alipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo kujibu mashata 8 likiwemo la kudanganya, kughushi na kulitia hasara ya sh. milioni 320 Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA). Mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo pamoja na washtakiwa wengeni watatu akiwemo Diwani wa zamani wa kata ya Sinza, Salum Mwaking'nda.
mtuhumiawa mwingine katika kesi hiyo akiwa mahakamani hapo.
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Sinza, Salum Mwaking'nda akiwa Mahamani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 29, 2012

    yote danganya toto tu ,na muda ilitakiwa wote watuhumiwa wa mali za serikali kupigwa risasi biashara kuisha kuliko kupoteza muda usiokuwa na maana siku itakuja endeleeni labda mkimbie nchi

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 29, 2012

    Kinachomfurahisha huyu diwani ni nini hasa?

    Furaha mpaka anatupa dole tupu!

    Isije kuwa wameiba bilioni kumi lakini wanashitakiwa deni la bilioni mbili tu

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 30, 2012

    Yaani hamna kitu hapa. Maneno matupu tu na mfupa ukiendelea kukomaa.
    Swali kubwa najiuliza wale walioondolewa madarakani kwa ufisadi hivi majuzi wako wapi? Si humo humo wanaendelea kujisogezea. Hizo fedha zote wanazoiba zingesaidia shule, vitabu na madawati. Ila zitawatokea puani we waache tu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 30, 2012

    Sina kumbukumbu kama TAKUKURU wamewahi kushinda kesi yoyote nzito na sababu zinajulikana, wote ni wale wale tunapoteza fedha za walipa kodi tu.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 30, 2012

    anachekelea maaana hao TUKURU wanapoteza muda wao. Tell me which Minister has been jailed for corruption? None as far as I know. Mtu akiiba mkata anafungwa 2 years. Ukiiba mabillion na wewe ni kigogo, utaachiwa tu. Waste of money kuwapeleka mahakamani. Taifisheni mali zao, au ketini nao wajieleze walipata wapi mali zote hizi- peleka jela, nchi inaliwa hiyo, hivi in 10 years time kutakuwa na kituki,mebaki?

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 30, 2012

    Hao CHADEMA wakiingia madarakani kwanza itabidi wajenge majela mepya maana yaliyopo yamejaa. Halafu bora yajengwe Moshi na Arusha. Maana hapa Dar hawataweza kuwalinda, wajanja wengi. Au bora waanze mradi kabisa, maana baba zenu na wajomba zenu wote wapo ambao waliowahi kwenda shule na kuelimika na waliokuwa wamejaa katika vyuo na wanaendelea kuchukua nafasi za elimu, ndio hao hao maana ndio waliokuwa wameshika nyadhifa huko maofisini na wanaendelea watoto wao kupata nafasi humo. Sisi yetu macho. Akina Idd Simba wamefungua Dimba.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...