Waziri wa Fedha Ofisi ya Rais Zanzibar,Mh. Yusuphy Mzee pamoja na Naibu Waziri wa Fedha Tanzania Bara,Mh. Jeneth Mbene wakiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB),Dr.Kwame Donkoh wakati wa mkutaano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) unaoendelea jijini Arusha.

Na Woinde Shizza,Arusha

Watanzania wametakiwa kujitangaza kiuchumi kupitaia mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB) ulioanza jana jijini Arusha ambao umewajumuisha Marais 6 na Magavana wa Nchi mbalimbali za Afrika

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo kikuu cha Dodoma Bw,Juma Mwapachu ambapo alisema kuwa hii ni fursa ya pekee kwa Watanzania kushiriki kikamilifu katika mkutano huu

Bw.Mwapachu alisema kuwa Mkutano huu ni muhimu sana kwa Nchi yetu na unawajumuisha watu mashuhuri na Si vikao vya Magavana tu pia Umoja wa Mabenki ya biashara ya Afrika nzima pamoja na vyombo vya habari Mashuhuri

Aliongeza kuwa katika mkutano huo pia kuna vyombo vya kupima gredi ya Uchumi wa Nchi mbalimbali na mfano Tanzania Uchumi wake umekuwa ukitolea mfano katika mkutano wa Benki ya maendeleo ya Afrika

Alisema kuwa kupitia Benki hii pia wameweza kufadhili ujenzi wa miundombinu ya barabara ya Namanga hadi Arusha na bado wapo mbioni kuhifadhili barabara ya Moshi hadi Holili

“Kweli uchumiu wetu unabadilika kiharaka sana na ukitazama mtikisiko wa kiuchumi 2008-009 ambao kweli kuna nchi ambazo zimetikiswa kiuchumi ”alisema Bw.Mwapachu

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Madini Tanzania Bw.Richard Kasesera alisema kuwa ni fursa adhimu ya kukuza uchumi kwa Mkoa wa Arusha na kuvitaka vyombo vya habari kuwa chachu ya kutangaza uchumi wa Tanzania wakati huu Mkutano unapoendelea

Aliongeza kuwa ni jambo la muhimu kwa vyombo vya habari kuelezea matatizo yetu ya kiuchumi na kuacha kuzipa kipaumbele habari za vurugu za Zanzibar za vikundi vichache na kuzipa kipaumbele habari hizo huko ni kuwanyima watanzania kupata na kuwatia hofu wahisani

Mkutano huu wenye kauli mbiu Afrika katika Ulimwengu wa utandawazi,changamoto na Fursa unafanyika kwa siku 4 na kukusanya zaidi ya washiriki elfu mbili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...