Wadau wakigeuza kuhofia kukwama kwenye bonge la shimo na maji machafu karibu na kituo kidogo cha Polisi Mabatini maeneo ya Sinza jijini Dar es salaam. Barabara hii na nyingine nyingi za pembeni zikifanyiwa ukarabati wa uhakika zitapunguza mno foleni ya magari kwenye barabara kuu. Mh Mbunge Iddi Azan na madiwani wa Kinondoni mpo?
Home
Unlabelled
barabara ya sinza mabatini inahitaji kufanyiwa ukarabati
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Hicho ni kipande kidogo tu, kwa wakazi wa maeneo haya kazi ipo maana lazima tupite hapo kila siku. Na hapo ni hatua chache tu kutoka kwa Mheshimiwa Spika29
ReplyDeleteJAMANI MTAANI MSISUBIRI SERIKALI KAMATI SHIKAMANENI NAJUWA MNALIWA PESA ZENU WASOMI MTAANI WENGI NA WABUNIFU TENGENEZENI AU KAWASHITAKI WAHUSIKA WA BARABARA MPAKA MAHAKAMANI AU MBUNGE WENU.
ReplyDeleteWabonge na wadiwani wakiacha posho za kukaa (sitting allowance) zitatosha kutengeneza na kukarabati barabara zinazitumiwa na wapiga kura wao..... tukatae posho, tupige vita posho! tudai barabara, sisi walipa kodi ndio tunazidi kuumia.
ReplyDeleteMnatoa mchango wa harusi laki mbili kwenda juu! Mnashindwa kuchanga kutengeneza barabara mbovu inayoharibu magari yenu? Sisi mtaa wetu tulichanga tukatengeneza barabara yetu. Sasa ni mkeka
ReplyDeleteHebu acheni utani mtaua magari nendeni mkaibane kamati ya barabara ya s/mtaa hii ndo kazi yao lakini pia hapo pana tatizo la maji kama vile chemichemi chini au kuna bomba limepasuka wasilianeni na DAWASCO haya tumeshawatafunia mezeni.
ReplyDeleteKijitonyama Mabatini!! haujui hata unapopita?
ReplyDeletejamani, si mnasema bongo tambarare? Sasa kwa nini msimuwajibishe mwenyekiti wa mtaa? Kaza buti hapo, mnakuwa hamjui wajibu wenu kama walipa kodi, ebo!
ReplyDelete