Waziri wa Malisili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akipeana mkono  na Balozi wa Uingereza nchini. Bi. Dianne Corner mara baada ya balozi  kukabidhi faru watatu walioletwa nchini kutoka Uingereza kwa ajili ya  Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi. (Picha na Pascal Shelutete)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 18, 2012

    Mh tafadhali shirikisha vyombo vyenye nidhamu kama JWTZ ktk ulinzi wa faru hao tumechoka na aibu ya watu kutowajibika kama kesi ya Serengeti

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 18, 2012

    Hizi sasa Zarau mnaonaje wadau? Michuzi usibanie hii sasa zarau tunategeshea mtego na sie tunanasa kwa uoga wakupenda misaada tusubiri lakuambiwa sasa wanataka nini na wao. MZ

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 18, 2012

    MADHARA YA UFISADI KWA VITENDO:

    Ahaha ahah ahaha !

    Hii ni kuthibitisha madhara makubwa kwa kuachia Ufisadi matokeo yake ni haya sasa kama hapa tukio hili tunashuhudia!.

    Kiasili sisi Tanzania ndio tulistahili kuwa na faru lakini kwa kuwaachia Mafisadi Wawindaji haramu aasa tumefikia kusaidiwa faru wa mbegu na Uingereza!

    Haya ni maajabu ya Mussa chini ya jua,,,sio ni kwa nini pasiwe na adhabu ya kifo kwa wawindaji haramu nchini?

    TUUKATAE UFISADI KWA VITENDO KTK SEKTA ZOTE ZA MAISHA HAPA TUNAONA FARU ITATUFIKA WAKATI ITAKUWA NI KWA SISI BINAADAMU TUNAWEZA KUKUTA SIKU TUMEWEKWA KATIKA MABOKSI NA TUKAUZWA NJE YA NCHI KWA AJILI YA BIASHARA HARAMU YA VIUNGO VYA BINAADAMU!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 18, 2012

    Rhino born in the UK, made rised in the UK?

    Ukistaajabu ya Musa utaona ya Fiarauni!!!

    Ama kweli lazima tukubali ya kuwa sasa nchi imeshafilisiwa mali ya asili zooooote!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 18, 2012

    Huku ni dalili ya kufilisika 'mazima' ktk maliasili nchini!

    Faru tuliokuwa nao maelfu kwa maelfu wameshatoweka!

    Siamini macho yangu, hivi leo tunasaidiwa Faru na Uingereza badala ya Misaada tuliyoizowea ya Sekta za Elimu, Afya na Miundombinu?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 18, 2012

    i hope wa sasa watalindwa vizuri. wale wa JK amebakia mmoja tu.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 18, 2012

    hahahahahahha dah hiiii kaaaaaali kweli kweli imefikia hatua hii dah!! yaani sisi tunaesifika kwa kua na utajiri wali maliasili imefikia hatua ya kusaidiwa na watu wanao adopt tu kuweka maliasili kama hivi vifaru kutusaidia dah . kweli dunia imeisha

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 18, 2012

    Hii ni aibu tupu!
    Faru wazaliwe Africa na Tanzania walikuwepo kibao leo wanaletwa kutoka Ulaya kama msaada? Sisi Tanzania kweli ni kichwa cha mwenda wazimu.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 19, 2012

    MADHARA YA KUBOBEA KWENYE OMBAOMBA NA KUTEGEMEA KUSAIDIWA KILA KITU....SASA TANZANIA INASAIDIWA FARU TOKA UK?????????????!!!!!! AIBU YA MWAKA HII.HAYA TUSUBIRI KUSAODOWA NA TANZANITE TOKA AFRICA KUSINI MANA SASA HATUNA TUNACHOWEZA BORA TU WAINGEREZA WAKAZANIE NA HUO MPANGO WAO WA MASHOGA WAJE WAOE WANAUME WA BONGO NA WAANZE NA VIONGOZI TU.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 19, 2012

    Wadau sijawahi ku comment ila Leo Nimecomment Kutokana na hili jambo,Kama ni hivyo basi nimenyoosha mikono,kweli nchi yetu hakijabaki kitu,....hata wanyama pori wanaowekwa Kwenye Zoo tunaletewa Kama msaada!!!!! Duuuu hiii Kali.......Mdau UK.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 19, 2012

    Naumwa...jamani naumwa!!! lol! Kitu gani hiki Mungu wetu! Tena bila aibu tunaweka foleni ya kupiga picha,,, kupokea faru wa msaada! lol! Mwenyezi Mungu inusuru nchi yangu na watu wake jamaani! Naona Huruma!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 19, 2012

    Nawapongeza wadau wooote mliotoa maoni hapo juu. Hata hivyo shida yangu ni kwamba mmekuwa mahodari wa kulaumu kuliko kutoa suluhisho la tatizo. Kila kukicha wabongo mnakuwa mahodari wa kulaumu, linapokuja suala la kutatua matatizo mloyaona kila mtu anakuwa na interests zake. Mngefanya hivi: kama tatizo lipo kwenye utawala mbovu, ondoeni hao watawala na muweke wengine watakaoleta system nzuri. Na kama ni technolojia inatakiwa, tumieni fedha za nchi kununua technolojia hiyo badala ya kuachia pesa kuliwa na wajanja wachache.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 19, 2012

    Sasa wadau, Wingereza si nchi ya baridi? Hao Faru wataweza kweli kuishi kwenye nchi ya joto kama Tz (hasa mkomazi)? Bora wangepelekwa hata NGORONGORO au Arusha NP, au Mbeya ambapo kuna kaubaridi kama ka ulaya.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 19, 2012

    Mimi nafikiri muda umefika tuseme basi sasa, kama hata faru ambao kwetu ni asili wakahesabika kama madeni ya nchi kwa vizazi vyetu vijavyo!

    Ingekuwa amri yangu hayo mafaru yangerudishwa asubuhi inayofuata siku waliyoletwa, khaaa! aibu gani hii?

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 19, 2012

    Kazi kwetu mbele ya Mwingereza tena!

    Baada ya huu msaada wa faru watatu (3) sasa tusubiri kusikia 'kiama' cha Mashariti ya msaada huu wa MWINGEREZA KWETU!

    SI MNAKUMBUKA MASHARITI YA MISAADA YA DONALD CAMERON NA SERIKALI YAKE YA UINGEREZA KWETU?

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 19, 2012

    Ahhh!

    Hebu mtutajie wao Uingereza wametaka nini kwetu Tanzania baada ya huo Msaada wao wa faru watatu?

    Hawa jamaa tumeshawasoma mipango yao!

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 19, 2012

    Duhhh tumeumia!

    Tumeingia mkenge tayari!

    Hivi tutaweza kuwatimizia jamaa mahitaji watakayotaka kwetu baada ya huu 'msaada' wa faru wa 3 ehhh?

    Wanaweza kutoa aina tatu za mahitaji tuchague sisi!

    1.Kontena 10 za Almasi!
    2.Mlima Kilimanjaro uwe wao!
    3.Ile sheria yao ya 'Jinsia moja'!

    Sasa wajameni No.1 na No.2 ni wazi hatutaziweza!!!

    Pana uwezekano mkubwa tukaangukia kwenye ubwete 'best looser. No.3 hapo juu

    Hivyo basi Mwingereza hatakuwa amepiga Offside trick na kufikia lengo lake lile???

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 19, 2012

    Enheee tumeshakwama!

    Kamasi zitatushuka kwa msaada wa faru wa Mwingereza!

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 19, 2012

    'Kupeana ni Kikoa'

    Ila wasi wasi wangu kulingana na ile ibara yao ya JINSIA MOJA tuliyo ipinga vikali ktk Mkutano wa Jumuiya ya Madola, Mwingereza asije akatumia Msaada wake huo na 'kutupanga mshikaki' Watanzania nchi nzima!

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 19, 2012

    Mnhhhh

    tutaweza kuchomoka katika bao hili alilotupiga David Cameron tena?

    Tukumbuke tulishampa ushirikiano Raisi JK kukataa 'mpango wao ule' nafikiri itafaa tumshauri Raisi JK kuwa tukae kibiashara zaidi na Mwingereza badala ya kimsaada!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...