Kwanza natoa pongezi kwa blog ya jamii Issa Michuzi kwa kutupa nafasi ya kujadili mambo mazito kama haya.
Jibu
Hoja nzuri.Ila ...
Siyo watanzania wote waishio nje ya nchi wamebanwa na maisha.
Wako matajiri wako wakawaida n.k sidhani kama kuna mtanzania maskini hapa ninapoishi ila kama yupo kwa nini tusimsaidie?

Watanzania wengi wanaipenda nchi yao ila kunakubaguwana kimtindo ndiyo maana wengine wanaamuwa kuacha kabisa kuzungumzia maswala ya nyumbani(Tanzania) kwa sababu inakuwa kama tunazungumzia maumivu tu kila siku.
Mimi nimeshakutana na mtu ana-miaka zaidi ya 40 Ulaya na kwa bahati nzuri mke wake anataka waje nyumbani kutembea na Mtanzania anakataa.Tatizo si kuwa wao ni maskini wanaingiza zaidi ya milioni kumi ya kitanzania kwa mwezi.
Tunapozungumzia kurudi Tanzania ? 
Wazungu wanaita (Maswala ya energy thief)Maana yake unamkuta mtu ametulia na familia yake vizurii(wanakula bata :) alafu unaanza kumkumbusha mambo ya Huzuni ni kama vile unamuibia furaha yake.


Ila kuna wengine wanakutana matatizo fulani ya kiubaguzi, haswa nchi za Ulaya. Wao wanakuja kwentu kwa raha na inabidi watu wetu waishi kwa raha ,baadhi ya wazungu wameanza kulielewa hili na mda si mrefu litakuwa si tatizo tena.Mtanzania ana haki ya kuheshimika kwa sheria za Umoja wa Mataifa iwe ameunja sheria au la cha msingingi ni yeye kujuwa haki yake.

Mtanzania hana aja ya kubaguliwa  kwa sababu Tanzania tumesaidia wakimbizi wengi tunakaribisha mtu wa kila aina lakini tunapokuwa nje ya nchi tunanyanyaswa mwanzo kwa sababu tunakadamu fulani wenyewe wanaamini kadamu cha akili :)kwa hiyo huwa Mtanzania wa kawaida inabidi wakupe  mda fulani kama miaka 4 hivi ya kufundishwa ubababiloni alafu unafanikiwa . Hii si haki, kunawatu wa Afrika magharibi na nchi nyingine wanakubalika hata kama wameingia kwa njia za mkato.

Sisi watoto wa Jakaya tumeamuwa tutakuwa tunarudi nyumbani na kuakikisha tunaitangaza nchi tunatangaza kweli ya Mtanzania ni nini (mfano tunapinga uharibifu wa mazingira na tutapigania hili mpaka vizazi vijavyo) alafu tunaadopt maendeleo mazuri ya huku  ili kuiletea nchi mafanikio zaidi.Hii imetokana na mtazamoa wa mtanzania wa sasa ni tofauti na ule wa Zamani.Watanzania wengi wameelimika pia mtazamo wa Dunia kwa sasa umebadilika Wageni wengi wataamia nchi za Afrika.

Nchi nyingi za Afrika zitafanikiwa  baada ya mika 15 ijayo.
Na uthibitisho wa baadhi ya Wazungu waliofanya safari za utalii huko ambao wanaamini nchi  ya Tanzania inaendelea kwa kasi imebakia kitu kidogo tu  kurekebisha baadhi ya sheria za kuishi kwenye Usasa ambazo ndizo tunaishi sasa.Hauwezi kujenga nyumba ya ghorofa ya cement na msingi uwe wa Udongo mbichi tena wenye mchanga kidogo the the :=)
Kuna haja ya kutoa elimu zaidi ya haki ya mtu na ni jinsi gani ataamini anaitetea haki yake kwenye njia sahihi.
 
Cha kufanya
1.Tuwatambue Watanzania wote waishio nje ya nchi na washirikishwe na kupewa heshma ya Utanzania kwa sababu wao   ndiyo mabaloozi wa nchi yao ugenini.Tukifanya hivi watanzania waishio nje wanaweza kuwadhamini acomodation wanachuo wengi kuja kusoma nje ya nchi.mafano Ethiopia wameleta wanachuo wengi mwaka jana hapa ninapoishi.Wanawenyeji wanaowadhamini chakula na elimu ni bure.

2.Kuweka sheria kali za Rushwaili angalau kuwe na adabu fulani mtu anapofikiria kupokea rushwa.
3.Kuwa na uhuru wa kuongea hili tunalifanyia kazi vizuri ,inabidi tuwapongeze watu wa blogs pamoja na Serikali ya sasa Raisi ,mzee mzima Nape baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa n.k kwa kuwekea mkazo hili(Heshma si hofu,hofu kwenye heshma  ni unafki)
4.Tuwe na lishe ya kawaida ambayo kila mtanzania anaweza kununuwa kwa siku.
Nchi za Magharibi zilianzisha vitu kama MC Dolnad ila sisi tuongeze wawekezaji wazalendo kwa kuiga mfano wa Jiko la Shoprite.
Wabunifu wabuni ni jinsi gani muuza miogo au chipsi anaweza kuwa na duka la kisasa la kuuzia bidhaa zake.
Nakumbuka tuna sehemu wanaziita za mamalishe kwa huku ulaya wametengeneza Hall lenye majiko Mengi ya kisasa na wameweka vyakula vya nchi maarufu kama vile India n.k
Wauzaji wanalipa kodi kwa mwekezaji ambaye anaweza kuwa ni mtu binafsi au serikali. Mwekezaji anapaswa kuangalia sehemu inafanyiwa kazi ni salama pamoja na mbambo mengine.

Kila mtanzania awe mlinzi wa mali za nchi azielewe vizuri sheria n.k
Tujenge utaratibu wa kuwapongeza viongozi wanaofanya vizuri.kuwafanya wawe mfano kuwatangaza kwenye lugha zote na wajisikie kuwa wao ndiyo mashujaa wetu.
Tanzania tunanguvu sana,ndiyo maana inakuwa vigumu kushirikiana.
Tunawatu kilapande ya Dunia. Tuna mtu katika kila lugha inayozungumzwa Duniani sidhani raia wa Uingereza wanawawakilishi katika lugha nyingi kama sisi watanzania.

Naomba radhi kama nitakuwa nimeandika kiswahili finyu :) nadhani mtalielewa lengo langu.
Mdau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 23, 2012

    mbona ujasema kiini chenyewe siyo kujisifia kuwa unakula bata watu wasiyo wastraabu wanakuja kukusumbua ila kinacho hitajika ni kwamba mtoa hoja alikuwa na lengo la kukumbusha ukumbuke nyumbani na sisi tupo hapa ulaya USA Tunajua yote yanayo endelea uwe unaingiza kiasi gani cha fedha uwe mpiga mabox tunajua lengo je? unampango wa kurudi nyumbani TANZANIA

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 23, 2012

    WACHENI KUJIUMIZA KICHWA DUNIA YA MUNGU BINADAMU WATAISHI KOKOTE WANAPOPEND WAO WANAOFIKIRIA PALE NI KWA MZUNGU HAPA NI KWA MWAFRIKA NA HAPO KWA MUHINDI AU MWARABU WATAJIJUWA WENYEWE WEKA MAISHA DUNIANI WACHENI KUFURU<ZULMA<UFISADI MUOMBENI MUNGU MUISHI MSHUKE CHINI YA UDONGO MSUBIRI HUKUMU NDIO KILICHOBAKI.

    WOTE WAKIRUDI TANZANIA KUTAKALIKA? WOTE WAKIRUDI WATALIANO KUTOKA MAREKANI ITALY KUTAKALIKA? MAYAHUDI WOTE WAKIONDOKA USA KWENDA KWAO KUTAKALIKA? MZ

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 23, 2012

    Mdau ,mambo yote uliyoyasema , mengi sana kati ya hayo ,yamekwisha tekelezwa,naona hujarudi miaka mingi sana. Nakuomba urudi ujionee, wengi wetu tuko nje muda kitambo sasa na Tanzania ya leo siyo kama ya Mwalimu ya miaka ya 70 na haya maendeleo ,tumeyapata kwa kasi isiyokuwa ya kawaida,mpaka hata wazungu wa huko uliko wanashangaa sana . Kwa mfano ukipita magomeni mapipa kuna restaurant inajulikana sana kwa jina la seaboys, ni pasafi sana ni dizaini ya ile uliyoisema Mcdonald- kuna sato wa Mwanza, mihogo uliyoitaja ipo, viazi vya kuchemusha vipo,wali,pilau,kuku wa kuzungushwa,kuokwa,ndizi choma ,chips na soda zakopo za aina zote, juice za baharessa-yaani hata hiyo Mcdonald naona ni cha mtoto. Braza tuko mbele kinoma , wewe lete familia yako likizo siku moja utajisikia uko peponi na kama una mke wa kizungu , basi huyo mke atasifia bongo kuliko utakavyosifia wewe. Zebedayo msema kweli.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 23, 2012

    Wadau sijui kama ninapotosha mada, lakini naamini Mdau wa Mada alikusudia kuwakumbusha watanzania walioko nje warudi nyumbani kuwekeza siyo tu kibiashara, bali uzoefu walioupata huko nje, teknologia, elimu, utaalamu na kikubwa zaidi kuleta athari chanya(impact) kwa jamii nzima ya watanzania. Sidhani kama alimaanisha maisha ya mmoja mmoja huko nje. Wewe binafsi utaleta athari(impact) gani kwa jamii ya watanzania hapa nyumbani? Kwa maneno mengine Tanzania itajengwa na nani ikiwa kila mmoja hataki ku-face matatizo tuliyo nayo? Tuyajadili kwa pamoja, tulioko nje na wenzetu wa nyumbani tuchanganye uzoefu, elimu, utaalam, mawazo kisha tuseme nayo kusudi kizazi kijacho kianzie na hatua nyingine.

    Mdau uliokuja na majadala huu ikitokea utasoma maoni yangu tafadhali usisite kunirekebisha kama nimepotosha mada.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 23, 2012

    Wadau wote Mtoa Makala aliyetoa jana na Mjibu Makala leo wapo sahihi.

    Kilichobaki ni matekelezo ya 'Makala'.

    1.Kila mwana Tanzania hata kama ana Uraia wa nchi nyingine ajihesabu kuwa ni sehemu yetu Tanzania kwa kuwa asili haikwepeki.

    Tunamthamini na tunahitaji mchango wake kwa maendeleo ya Taifa letu.

    Ni kama tunavyoona Serikali imefunguka kwa sasa na inahitaji ushirikiano huo muhimu kati ya sisi nchini na ndugu zetu ng'ambo na ndio maana imekuja na Miapngo kadhaa kama ile Diaspora.

    2.Kama leo anavyojibu ya kuwa sio wote wapo ktk hali ngumu ya maisha na kuwa wapo waliofanikiwa, hivyo tunahitaji ushirikiano na kuaminiana kwa nia njema, pia wale watakao kuwa hawaja fanikiwa huko Majuu ni vyema wakafanya uamuzi wa maana badala ya kuzidi kupoteza muda na nguvu huko wakarudi nyumbani na kufanya mambo mengine ya maana kama Mtoa Makala jana alivyo gusia humu Jamvini.

    PAMOJA TUIJENGE TANZANIA !

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 23, 2012

    Mimi naogopa sana kurudi bongo:-

    1) Kupigwa NGETA-->wizi,ujambazi
    2) Kupigwa MIZINGA-->omba2,harusi
    3) Kupigwa MISALA-->kupewa kesi
    4) Kupigwa VIBOMU-->uchawi,magonjwa
    5) Kupigwa CHAKACHUA->rushwa, No haki
    6) Kupigwa GANZI-->dala2, foleni
    7) Kupigwa ZENGWE-->Makelele,No privacy
    7) >>>>

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 23, 2012

    Wana Tanzania wote hasa Ma Diaspora:

    Nchi imeshaona neema inanukia na sasa inataka kuwajali wana Tanzania kwa ujumla.

    Imethibitika nchi ina Utajiri mkubwa kabisa wa :

    1.Gas

    2.Mafuta
    Dalili zipo baharini katikati ya Pemba na Tanga pia eneo la Mwambao wa kusini huko kwenye gas.

    3.Uranium

    4.Nickel

    5.Steel

    6.Gold

    7.Coltan

    8.Manganese

    9.Coal

    10.Diamonds (ukiacha zile za Mwadui Shinyanga maeneo mengine imeonekana pia)

    11.,,,,,Na rasilimali zingine nyingi tu.

    Hivyo kinachohitajika ni Rasilimali watu wa kutosha kama moja ya mtaji wa kuweza kuvuna mali hizi.

    HATUKATAI YA KUWA MAMBO MENGI YALIKUWA YANAENDESHWA NCHINI NDIVYO SIVYO HAPO KABLA, ISIPOKUWA NI DHAHIRI MABADILIKO MAKUBWA YANAKUJA NA HAKUTAKUWA NA MATATIZO JUU YA DIRA NA UENDESHAJI WETU WA MAMBO NCHINI.

    MMEHAKIKISHIWA YA KUWA KWA SASA KIPAUMBELE KITAKUWA NI KUWAMILIKISHA RASILIMALI HIZI KWA NJIA YA HISA NA MITAJI WANA TANZANIA WALIO NDANI NA NJE YA NCHI.

    HIVYO SERIKALI KWA BUSARA YA HALI YA JUU IMEONA KUNA UMUHIMU HUU WA KUWAITA NCHINI WANA TANZANIA UGHAIBUNI ILI TUJE KULA ASALI KWA MAZIWA KTK NCHI YETU NZURI YA AHADI TANZANIA.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 23, 2012

    asante ndugu zangu watoa mada kuhusu waishio ulaya au tanzania mi ni mtanzania niishie nje ya nchi kwa pande zote mbili za mada nahusika natakiwa kukaa mahali popote ninapojisikia na na ninajisikia kurudi home tz lakini maisha popote ni kama vile kwetu bongo kuna watu waishi ludewa wanakula bata na kuna watu wanaishi ludewa wanateseka sana hapo dar ni mfano mzuri pia kuna group 2 kuna watu wanaishi ahera hapo dar kuna watu wanaishi jehenamu hata shule taabu hospitali tabu lipi jema kuteseka ulaya au kuteseka bongo afadhali mi mwenzio hapa nina uhakika na hospi na shule mwenzangu uishie bongo je sisi wageni wote tuishio hapa ulaya si watanzania tu tena si watanzania hatupo wengi mataifa mengine wamejaa hapa kwa kupata kauli mbiu toka kwa viongozi wao kwamba kila mwananchi awe na pass aende ulaya arudi nyumbani kuendeleza nchi lakini nyinyi tanzania mbongo akiondoka tu hapo kwanza kuipata hiyo pass kasheshe na ikipita hapo airport kama hajasumbuliwa ana bahati kusema ukweli si watanzania bado washamba hatujaamka na tuna wivu wenyewe kwa wenyewe hatusaidiani kuanzia viongozi wetu waliopo katika mabalozi hawatusaidii watanzania tuishio nje wanatukandamiza wamekuwa kama vibaraka wa wazungu hivi mi mtanzania ninaporudi nchini kwangu labda nimebeba kativ kamoja tu lakini huo usumbufu ninaopata hapo airport mara ya pili huna haja ya kuja tena mi naomba anza kwanza kuwarekebisha viongozi wako wa tanzania kuhusu maswala yote ya uhamiaji tena kitu kikubwa na kibaya na cha aibu ambacho hata wazungu wenyewe wanashangaa sana eti kutoka nje ya nchi na kufika moja kwa moja airport kupata visa hicho kitendo kinatudhalilisha sana kuonyesha ni kiasi gani hatuna akili na umaskini uliopitiliza mipaka eti wawekezaji so stupid

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 23, 2012

    HABARI WADAU?MIMI HII MADA IMENIGUSA SANA UPANDE WANGU JANA NIMELIA BAADA YA KUISOMA.KWANZA KABISA MIMI MTANZANIA NIMEISHI UK KWA MIAKA 13,NIKIWA NINAFANYA KAZI KWENYE CARE HOMES.MWAKA JUZI NIKIWA KAZINI UK BORDER FORCE WALITUVAMIA KAZINI,WATU SABA TULIKAMATWA KAMA KUKU NA KUPELEKWA DETENTION WALICHUKUA VITU VYETU KAMA SIM, KADI ZA BANK.TUKAWAOMBA HATA NIKACHUKUE MIZIGO YANGU WALITUKATALIA NA KUJIBU KUNYA WAKISEMA,GO BACK IN YOUR HOME LAND.KESHO YAKE ASUBUHI NIMEPAKIWA KWENYE PIPA LA BONGO NA ULE UCHAFU WA KAZINI NIKIWA NIMEVALIA KANDAMBILI.NIMEINGIA AIRPORT HATA NAULI YA KUPANDA BASI NILIKUWA SINA.KWASASA NINAISHI KIJIJINI MAANA NYUMBA YANGU BONGO NILIKUWA SIJAIMALIZIA.NILIPOTEZA MUDA WANGU NATAFUTA KAZI HUKU BONGO HAKUNA MPAKA NIMEFIKIA HATUA NATAKA KUNJWA SUMU.JAMANI NYUMBANI NI NYUMBANI TU.VITU VYANGU VYOTE NILIACHA KWENYE NYUMBA WATU WAMECHUKUA BURE.ASANTENI WADAU.MOSHI.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 23, 2012

    Tatizo la Tanzania mambo mengi hayako wazi kama serikali ikiamua kuwa wazi kwakuwaeleza wananchi kuwa hiki ni haki yako na unahaki ya kukidai na kuwaambia viongozi usika kuwa usichezee haki za rai na ukikamatwa unachezea unafungwa basi maendeleo tutayaona .
    Pili serikali ni vizuri ikaweka mikakati ya kuzifanya ajira ambazo tunaziona sio rasmi kuwa rasmi kwa kuanzisha sera ambazo zinawekewa sheria bungeni zitasaidia kutengeneza ajira ambayo serikali iliyoko madarakani inawezakuwaambia wananchi kuwa tumetengeneza ajira kadhaa na ni very simple uitajikuwa rocket scientific. Mifano ya sera ninazo kama watu wa CCM mnataka wasilianenni na mimi niko huku UK nitawatengenezea sera zote za kuwasidia wananchi wa Tanzania kupata ajira na utajiri na mtarudi madarakani mwaka 2015. Mimi sio mwanasiasa ninachotaka ni kusidia nchi yangu kuweza kuendela na mimi mwenyewe kuendelea sio kwaita wazungu waje kutusaidia kuendelea badala ya sisi kujisaidia wenyewe. Hawa wazungu hawezi kutuondolea umaskini bali wataruzidishia kuwa maskini tukiendelea kuwategemea.Maendeleo ya kweli yataletwa na Watanzania wenyewe sio wazungu wala watu wengine wa nje.
    Wasilianeni na mimi CCM ilitujenge nchi pamoja mimi sinamda wa kupoteza na watu ambao hawako madarakani kwani hawezikuamua lolote linalowausu Watanzania zaidi ya kupiga kelele na hawana uhakika kama watashinda uchaguzi na kitu kingine hatujui dunia itakuwaje 2015 kwahiyo uwezi kusemea chochote ni kupoteza muda kushabikia kitu ambacho bado akipo kwenye mfumo. Kama nilivyosema mimi sio mwanasiasa na sina nia ya kuja kuwa mwanasiasa mimi ni mpenda maendeleo maana naona kunatatizo linaongezeka siku hadi siku la Watanzania kugeuza siasa ni simba na yanga wakati wageni kama wahindi na wazungu wanaendelea kutengeneza pesa na kuamisha raslimali sisi tuna angaika na malumbano kwenye mitandao ya kijamii badala ya kuhusika na kuleta maendeleo.
    Nawaomba CCM tuwasiliane ili tujenge Tanzania yetu.
    Mdau UK.
    Email: tanzaniauk@yahoo.co.uk

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 23, 2012

    Hi,mimi ni mwanadada mtanzania niguswa na mdau hapa juu ,unasema ulikatwa kama kuku pole sana.Nadhani ulikuwa tayari mitini, ndiyo maana haki hukupewa haki yako.mimi kesi yangu ni kama ya kwako,kwani nilifika bongo baada ya kuishi UK miaka 10 nikashindwa kabisa kuishi maisha ya bongo,jamaa zangu UK. marafiki ndugu jamaa wanisaidia nikarudi nasasa ni raia.bongo hata maiti haitarudi maana ni shida tupu.wewe usikate tamaa wasiliana na jamaa zako London wakusaidie urudi maana maisha ya ulaya ni matamu mno mono ,achana na wabongo ambao hajawahi kutoka huko jangwani bongo.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 23, 2012

    Mimi naogopa kurudi bongo kwa sababu mimi napenda ngono nzembe na bongo nitakufa kabla ya siku zangu. Huku nilipo ughaibuni nafyonza utamu kavu kavu na bado nipo hai. Sisemi kwamba huku ughaibuni hakuna ngoma, la hasha, ngoma ipo; lakini virusi vya bongo vikali sana.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 23, 2012

    ndg yangu usiongelee mambo ya ngono tunaongelea maendeleo kati waliopo ulaya na bongo jamani watanzania mwishio nyumbani tokeni kwanza hayo maisha mliyokuwa nayo si maendeleo mnadanganywa jamani kuwa na gari na nyumba nzuri si maendeleo maendeleo ni maisha kwa wote mana barabara hospital mashule we kama unakaa mbezi unamsaidia nini mtu wa mbagala na shida zake amka ndg yangu kwanza ukiona mtanzania bongo anatesa ujue mwizi tu mana mshahara hauendani na mahitaji anapata wapi extra money wote wizi umejaa maisha popote huku kuna watu wana maisha mazuri tu na haujo bongo vile vile kuna wanacho na wasionacho mi naona huyu mtu aliyeanzisha hii mada haitoshi tuifungulie ukarasa wa wazi tuchangie hoja zetu kwanza nyie mlioko bongo hamna ushirikiano nasi tukija hapo aiport mnatuumiza kwa kuomba rushwa labda mtu kambebeea mamake kasimu tu jamani maisha popote naomba kwanza uanze kuwasaidia walioko huko home si haturudi umeme hauna shida maji hayana shida hospital hamna shida shule watoto wetu hawalipi wanapata elimu nzuri we unaishi hapo dar umeme dili kwa karne hii jamani aibu jirekebisheni haya tuendelee mada nzuri sana

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 23, 2012

    asante wadau wachangia mada kwa kweli mi nadhani tuanze mada ya kukosoa serikali yetu hii ndio inatufanya sisi tuondoke home tz kwenda ughaibuni manake mafao maisha mazuri wanapewa wageni na wahindi sasa wachina lakini mwenye nchi mwenyewe mtanzania anaumizwa kuanzia ktk kodi mpaka haki zake mana mashirika yote ni ya wazungu na wahindi wanakwepa codi kila siku wanabadilisha kampuni na majina mapya hivi kweli tutafika jamani ndg zangu bora niwe mtumwa wa mzungu naweza kumpelekea chumvi na dawa mamangu huko magu amka ndg mtanzania sasa tunajiumiza wenyewe jamani haya asante mada nzuri tuchangiane mawazo

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 23, 2012

    ukiona serikali inauza mali asili kwa wazungu au waarabu ujue kuishiwa akili wenzenu bada ya miaka wazungu hawatakuja tena kama watalii mana twiga wote wapo hapa ulaya mmewauzia wenyewe manake ziki iliyopo kwa viongozi wetu ni kbwa rushwa imezidi mno ndg mtanzania amka sasa huyo ndg wa hoja anayesema kwa nini watanzania hawataki kuwekeza au kurudi huko simwelewi sababu kama nimesomea ualimu au udaktari kama leo serikali haijali maslahi ya walim wala madaktari hivi wananchi mnafumbia macho swala hili kweli tutafika huko tuendako wakati wabunge wana mishahara mikubwa hivi unategemea madaktari wafanyeje mwalimu anakaa kijijini anakufundishia mwanao hana mshahara hivi elimu itatoka wapi jamani bado mi nakataa hatuna maendeleo kabisa huku nyumbani bado angalieni mfano wa rwanda jamani wenzetu wametoka ktk vita lakin wana maendeleo makubwa mno usafi we dar ukufika unashika pua maendeleo yako wapi tujiulize na tuanze kuongea haya karibuni ktk mjadala

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 23, 2012

    Mbona hamuwakumbushii wale waliotoka mikoani wakakimbilia Dar na hawajawahi kurudi vijijini kwao kwa kisingizio cha usafiri duni au mambo ya uchawi au tu kwamba hakuna mahali pa kukaa.Nadhani msiwashupalie sana wa Ulaya wakati kuna watu wamekaa hapo Dar hata hawawazi kuendeleza vijijini kwao na wakati huohuo wengine wamekimbia vijijini kwao na maisha yanawaendea kombo hapo mjini.Napenda sana kushauriwa kukumbuka nyumbani kama mleta maada alivyotoa hoja zake za msingi.Ila msiwasahau hao waliokimbilia Dar na hawajawahi kurudi kwao na wala kutengeneza vibanda vya wazazi wao.Wengi wakifa hutia huzuni sana miili yao inapopelekwa huko kunakuwa hakuna hata pa kuiweka.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 24, 2012

    Asante kwa maada nzuri pia shukurani zimwendee anko na timu yake kwa kutuwezesha kuwepo humu.

    Ukweli upo pale pale nenda magharibi au mashariki,umefanikiwa au hujafanikiwa nyumbani ni nyumbani.Kuna kitu utakosa tu,labda kama hujazaliwa au kukulia TZ.Umaskini wa TZ huwezi kulinganisha na Umaskini wa ulaya na USA ni kweli lakini kwa sisi tunao kaa huku majuu tunajua hayo yote,presia na masitresi ya majuu sio kidogo.Mimi naamini maisha mazuri mtu unapokuwa huru na unajichanganya na ndugu na jamaa zako na kushiriki ktk shughuri za kila siku bila kuwa na roho ju juu ya kuchelewa kazi au kuwepo mahali fulani bila ya wewe kupenda sana hali hiyo.
    Tanzania itajengwa na watanzania,na sio vinginevyo.
    Mkataa kwao ni Mtumwa!

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 24, 2012

    MALIZENI KWANZA MATATIZO YA RUSHWA, UBOVU WA BARABARA,URASIMU, NJAA, MATATIZO YA MIGOMO YA MADAKTARI, WATOTO WA SHULE KUKAA CHINI, MALARIA, MAGONJWA YA MILIPUKO, UJENZI HOLELA, UCHAFU MIJINI, TATIZO LA UVAMIZI WA MAJAMBAZI MAJUMBANI..Nk. MKISHAREKEBISHA HAYO THEN TUAMBIANI HABARI YA KURUDI TANZANIA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...