.1. Kwa nini Watanzania wengi wanaoishi nje hawataki kurudi nyumbani japokuwa wamebanwa na Maisha ya huko? 
2. Je huku ni kukwama au kukomaa?
 3. Unawashauri nini wadau hawa?
Tafadhali elekeza majibu yako sehemu ya maoni. Tuanzie hapo kupata ufumbuzi wa kurekebisha mwelekeo wetu. Katika Tanzania ya sasa blogs zinaweza kufahamisha, kuelimisha na kukosoa jamii zaidi kuliko radio na tvs
Nianze na mawazo yangu mwenyewe;
 *Ninadhani maisha ya nje ni vigumu sana kuweka akiba kutokana na utaratibu uliowekwa na nchi hizo. Mfano USA, Australia, UK na nchi zote za magharibi utaratibu ni kufanya kazi na kipato kwa wageni wengi ni kutosha kununua chakula na mavazi, kulipa kodi ya nyumba, kulipa bills na kukidhi mahitaji mengine ya lazima ya maisha, hivyo hakitoshi kuweka akiba. 


*Muda unakimbia kama kishada, umri unapepea, wengi wao wanaona hakuna maendeleo yeyote kinyume na matarajio kwa hiyo watanzania wengi wananunua muda. Kurudi nyumbani bila kitu maalum cha kufanya ni kupingana na mpango mzima uliowafanya kwenda nchi hizo, kwa hiyo wanakomaa. Japo mwisho haujulikani. 


*Ushari wangu; kila kitu kinawezekana. Njia pekee ya kujikwamua kusudi kurudi nyumbani, kuondokana na woga wa maisha ni kushirikiana(makundi) kusudi kupata akiba na kila kundi kutumia akiba hiyo kuwekeza nyumbani kusudi kujiajiri wenyewe na kisha kurudi nyumbani kwa utaratibu na mpango ulionyooka.
Mengine nakuachia wewe Ankal na wadau.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 66 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 22, 2012

    Pengine watu hawarudi Tanzania kwa kuwa maisha ni popote.Inawezekana sababu ulizozitoa ni za msingi lakini kama anayeishi huko Australia,UK au America ameridhika na namna hiyo ya maisha nafikiri swali lako au mjadala wako unakuwa si wa msingi.
    Suala lingine la kujiuliza ni kwa namna gani watu tulio hapa nyumbani Tanzania tumefanikiwa na mfumo uliopo?Je,wengi wetu tuna maisha bora zaidi kuliko ya wapiga box?Tuna huduma za afya za uhakika?Tuna usafiri wa uhakika?Na mambo kadha wa kadha!
    Pengine swali lako lingekuwa la msingi kama ungetaka kujua ni kwa namna gani tunaweza kutumia watu walio nje kutengeneza ajira nchini au kuleta utaalamu katika sekta mbalimbali.Inapofika wapi mtu anaishi ni chaguo la mtu binafsi na kujadili kwa nini harudi nyumbani hata kama maisha yanamgonga huko aliko haina maana!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 22, 2012

    Kazi kweli kweli. Siyo kwasababu unaweza weka mawazo yako na ankal akayaandika, haina maana lazima uyatoe. Ni vizuri kufanya uchunguzi wa kina ukaleta hoja zenye ushahidi wa kutosha badala ya kuupotosha umma.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 22, 2012

    mi simo subiri wapiga box waingie

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousJune 22, 2012

      Wivu Tuuu bongo aturudi ngo kwenye nchi isiyonara vifo ndiyo sisememmmmm

      Delete
  4. AnonymousJune 22, 2012

    Mdau Mtoa Makala umenena:

    Wengi wa waishio nje Ughaibuni wanaishi kiubishi halafu sisi tuliopo huku nyumbani tukiwa kosoa wanakuja juu kama mwewe!

    Wazo lako ni zuri na la kufanyiwa kazi tuanze na madai ya Madiaspora:

    MADIASPORA:
    1.Madai makubwa ni kuwa uwepo wao nje ya nchi ni kutokuriDhika na hali ya maisha iliyopo huku nyumbani na hasa wakitupia lawama Mamlaka na Serikadi kwa ujumla.

    2.Tuhuma zaidi zinaangukia kwenye Uongozi na utendaji wa Mamlaka.

    3.Uhakika wa kimaisha hakuna nyumbani hivyo watu wametafuta Makaratasi na Uraia wa Ughaibuni.

    NYUMBANI TANZANIA:
    1.Mara kadhaa hapo nyuma Mamlaka na Serikali kwa ujumla imekuwa ikilaumiwa kwa madai mengi yakiwemo makubwa hayo matatu (3) hapo juu.

    2.Kwa sasa Mamlaka na Serikali imefanya mabadiliko makubwa ni vile inausikivu, inafikika kuliko ilivyokuwa kabla wakati wao Madiaspora walipokuwa wanaondoka nchini.

    3.Mamlaka na Serikali kwa ujumla imefanya mipango mingi sana tena kwa kuwaelekezea wao wa Ughaibuni ikiwemo vitu kama NHC(Mipango ya Shirika la Nyumba la Taifa) kwa ushirikiano na Benki Kuu, NSSF na TMRC(Mamlaka ya kudhamini amana na majengo)

    4.Serikali imetioa mwitikio mkubwa wa suala la Uraia wa nchi zaidi ya mkoja (DUAL CITIZENSHIP) ili kuwapa nafasi Madiaspora ktk kushiriki masuala mbali mbali nyumbani Tanzania.

    5.Kulingana na hali hiyo na jinsi Mamlaka za Ughaibnuni,USA,Australia,UK na nyinginezo zinavyowachukulia kwa kuwapa maisha ya Madeni (CREDIT LIFE CYLCLE SYSTEMS) ni wazi kuwa zimewachoka ni bora mtazame huku nyumbani ambako angalau Mamlaka imewajali imewatumia jicho na kuwapa mkono.

    Unakuta mtu anakaa muda mrefu Ughaibinu lakini hakuna alichokifanya na anafikia kuona watu aliowaacha huku nyuma wamesonga mbele yeye akiwa amepoteza.

    HIVYO WANDUGU, HUWEZI KUNYWA POMBE ILI UTAKAPOKUWA UMELEWA KUWEZA KUEPUKANA NA MATATIZO WAKATI POMBE IKIISHA MATAGTIZO YAPO PALE PALE, NA KUWA DAWA YA MATATIZO NI KUTAFUTA SULUHISHO.

    HATUKATAI KTK MAISHA HAPA NYUMBANI WAPO WALIOFANIKIWA NA WALIOKWAMA PIA, HATA HUKO UGHAIBUNI WAPO WALIOFANIKIWA NA WAPO PIA WALIOKWAMA MFANO WAPO WALIOOMBA MAKARATASI NA URAIA WAKASHINDWA KUFANIKISHA NA WAPO WALIOFANIKISHA.

    KWA HIVYO MAKA MTOA MAKALA ALIVYOSHAURI NI VEMA WATU BADALA YA KUZIDI KUPOTEZA MUDA BURE UGHAIBUNI WAKAAMUA KWA TIJA NA KUFANYA MAMBO KWA FAIDA ZAIDI KWA KUKAA MAKUNDI NA KUTUMIA NAFASI KAMA HIZO ZILIZOTOLEWA NA MAMLAKA ZETU ZA KISERIKALI VITU KAMA MIPANGO YA:

    1.NSSF, NHC NA TMRC
    2.NSSF-WESTADI
    3.DIASPORA
    4.AGOA (Mpango uliotolewa tokea mwaka 2000 kwa kupewa nafasi ya Kibiashara bila Ushuru Marekani)
    5.DUAL CITIZENSHIP(Itakapoanza)

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 22, 2012

    Mdau napenda nami kuchangia yangu, mimi nipo bongo ila nimekua nikitembea nchi nyingi kikazi, kwa kweli watanzania wengi wanaishi maisha ya kawaida tu, yaani muda mwingine nauli ya kutoka huko inakua ngumu, kuna mmoja niliwahi kumuuliza "vipi nyumbani?" akadai "nyumbani ni pale mtu anapoishi" kwa jibu lake alikua na maana huko nje anapoishi sasa ndio nyumbani kwake. nililipenda jibu hilo, lakini pia nikajiuliza kwa nini wakipata matatitizo kama misiba maiti husafirishwa kuletwa TZ kwa mazishi tena kwa kuwachangisha watu fedha nyingi na huku maiti ikifika wasindikizaji huishia kushangaa anpozikwa mwenzao kuwa miundimbinu ni mibovu, tuachane na hayo.
    Kubwa nililotaka kusema ni kuwa wasiogope maisha, na si vizuri ukirudi bila ya kuaandaa miundimbinu kama makazi na visenti kidogo kwa kipindi cha mwanzo wa maisha ya huku kwani utakua hujayazoea.kwa sasa bongo kuna opportunity za kuwekeza kwenye ardhi bado tuna ardhi kubwa tu ila kila mtu anataka mjini, lakini kama utaweza wekeza pembezoni mwa mji kama mkuranga, kisarawe n.k kwenye kilimo cha mazao ya muda mfupu kama matikiti, pilipili mboga, bamia nk unaweza toka muda si mwingi.
    Wadau mje bingo tupambane maisha pamoja kwani nyie mtatupa uzoefu wenu wa huko nasi tutaupeni wetu.
    TZ ya 90s sio ya 2010s.
    Ni hayo tu.
    mbegu

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 22, 2012

    Hongera sana , uliyeleta hoja hii, duh !!! yaani imepiga kwenye kichwa . njooni sasas tutoane nock out- maoni yangu ni kwamba , wengi wetu huku ulaya hatuna kitu ,na tunaona aibu kurudi kuanza upya , huku afadhali kuna kitu kina itwa pesa ya bure ya serikali ( wellfare, hii nayo inatulemaza kwamba ,ni bora kuishi huku ukapata dola 600 kwa mwezi hela ya serikali kuliko lile jua kali la bongo na uko kijiweni. kumbuka kwamba wengi wanarudi ,wale waliojiandaa. asante Zebedayo wa Zebedayo

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 22, 2012

    Muda Muhimu:

    1.Msipoeteze muda Ughaibuni bila sababu wakati mnaona wazi maisha yanazidi kuwa duni siku hadi siku.

    2.Dunia nzima imefilisika, akufukuzae hakwambii toka utaona mambo yanabadilika siku hadi siku.
    -Mfano hapo nyuma mlikuwa mnaishi mustarehe lakini sasa wanawabebesha madeni ya maisha.
    -Kila kukicha wanazidi kuwabana kisheria na sasa wengi mnaishi kwa kutegemea mafao ya Jamii badala ya kuvuna kipato cha kuendesha maisha kwa kufanya kazi, kitu ambacho ni hatari sana kimaisha !
    -Kwa kuishi kwa utegemezi wa Mafao ya Jamii mnakuwa mnabweteka na kuona Serikali ndio kila kutu Ughaibuni na kuwa kama Mateja.

    3.Kwanza ni vema mkishukuru ya kuwa Serikali ya Tanzania kwa sasa imewajali sana kwa mipango mingi tu kama ,

    -BOT/TMRC
    Dhamana za Majengo na Amana),mnaweza kujenga nyumba huku Tanzania wakati mkiwa nafanya kazi zenu nje na kuishi nje ya nchi.

    -NSSF-Diaspora,NSSF-Westadi,Mnafikiriwa sana kuwezeshwa kwa kutuma pesa nyumbani na kuwekeza kwa akiba Benki na mipango mingi tu, mfano ktk biashara ya muda ujao ya Hisa na Mitaji kama mnavyoona sasa neema ya gas na madini mengi tu kama Mafuta,Uranuim,Metals zinanukia hukuMfumo wa Masoko ya Dhamana na Mitaji ukiimarika zaidi ktk sambamba na kutanuka kwa eneo letu la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

    -Dual Citizenship.
    Ni muda mfupi ujao mtaweza kuwa na Uraia wa nchi mbili na kupata uwezeshwaji mkubwa wa kushiriki mambo huko mliko na huku nyumbani Tanzania.

    Ni muhimu mkafikiria nyumbani sasa ambako kuna MATUMAINI na KASI KUBWA YA MABADILIKO YA NEEMA YA ASALI KWA MAZIWA ,kulingana na Ukuaji wa Kiuchumi badala na kuwa na mawazo ya kizamani mkifikiri mambo ni yale yale ya Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea.

    MUDA SIO MREFU ITAKUWA NI FAIDA NA KUPATA UNAFUU WA KIMAISHA UKAWA RAIA WA JUMUIYA YA AFRIKA YA MASHARIKI BADALA YA KUWA RAIA WA NCHI KAMA UGIRIKI NA NYINGINEZO HIZO MLIZOKUWEPO HUKO.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 22, 2012

    kwani tanzania ndio unapata pesa ya kuweka akiba ukifanya kazi?afadhali hata huko nje wako na kazi sasa wakirudi hapa watafanyakazi zipi? mradi wanaishi na wanapata mahitaji yao ya lazima kutokana na kazi zao mimi sioni tatizo wapi wanaishi

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 22, 2012

    Asante sana mdau uliyeleta mada hii. Nimekuwa nikitafakari sana jambo hili na mawazo niliyokuwa nayo hayatofautiani sana na yako. Huku kinachotumaliza zaidi ni kodi ya nyumba. Na hii ingepungua kwa watanzania kuungana na kukaa pamoja. Ukichukua nyumba kubwa yenye vyumba vingi bei yake inapungua. Kwa hiyo kama mtakaa wengi humo hata mkashea sebule na vyumba mwisho mnajikuta mmelipa pango pesa ndogo sana. Wenzetu wahindi wanafanya hivyo na wameweza kuweka akiba na kurudi kwao wakiwa na cha kuanzia.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 22, 2012

    Asante ndugu kwa mada hii. Wakati mwingine tunashindwa kuungana kutokana na hulka mbaya za watanzania. Mtanzania utamishi naye kwa nia ya kusevu. Akitoka hapo anaangalia madhaifu yako na kuanza kuyashikia bango huko mitaani. Kila mtu ana madhaifu na mazuri yake. Mwingine unamkaribisha muishi ili asevu mwisho anaishia kukusengenya kwa watu wengine.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 22, 2012

    Wanaokaa nje ya nchi na hali zao ni duni wanaogopa aibu ya kurudi. Kuishi nje sio lazima uwe tajiri. Njooni hapa tuanze moja.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 22, 2012

    Wale waleeee....!!Wewe unatoa ushauri umeshaishi nje? Kuna sababu tofauti za kutorudi nyumbani...Sababu kubwa ni kiwango cha elimu ambacho wengi wanajaribu kukipata..na haiishii tu hapo. Wengine hata kama wanataka kurudi hawaoni sababu ya kulipia mtoto akasome "English media" kwa mamilioni wakati atasoma the same thing ulaya bure tena kwa standard ya juu. Sababu ya tatu ni kudeka kutokana na huduma za jamii za nchi zilizoendelea. Wewe ukishazoea huduma nzuri, kwamfano unanyanyua tu simu unapewa huduma zote, maji, umeme, gas, takataka, internet, TV, mfagia nyumba kama unataka bila kuunga foleni unarudi nyumbani ili iweje? Halafu kumbuka siyo wote wenye mpango wa kurudi nyumbani....na wale wenye huo mpango wameshaanza mikakati. Mimi binafsi nafahamu wadau kibao wanakwambia watafia huku na it doesn't make any difference unaishi wapi as long as you are happy. Lakini muhimu ni kuwa wengi wamezaa huku nje na wanaona tabu sana kurudisha watoto wao kwenye huduma mbovu za Afya, Elimu na mazingira machafu. Usidanganywe kamwe na viongozi wetu. Wao wakiugua wanapanda pipa wanaenda India, UK, USA kutibiwa...wewe utakwama na Muhimbili ambayo mpaka uhudumiwe (kama basi hawatakukata kichwa badala ya goti)umeshakufa. Suala la woga ni kweli lipo wala siyo siri...especially ukishakuwa exposed na maisha ya nje ya kiwango cha juu. Mnaorudi rudini mimi ndo kwanzaa nazidi kujichimbia hata Obama asijue niko wapi. Mdau-CA, USA

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 22, 2012

    Aisee wewe mtu umeona mbali mimi niko hapa Australia naona wabongo wanavotaabika ila waoga kishenzi kurudi bongo hadi wanatia huruma kweli kama ulivoshauri wakiunda makundi ni rahisi wakaanzisha biashara ikawalipa then kila mmoja akapata cha kufanya maana haya waishiyo si maisha ni kujulikana tu kuwa wako Australia lakini hali kusema kweli si shwari

    ReplyDelete
  14. Bora maskini ulaya kuliko maskini bongo.
    Erick Michael-Texas

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 22, 2012

    Urasiu wa serikalikwenye ajira ndotatizo. Kupata kazi ni mpaka umjue mtu na siyo swala ujuzi pekeekama nchi nyingine.Kwanisi unaona viongozi wa serikali wanaanza baba, mtoto hadi mjukuu. Nchi imekuwa kama family business mpaka nchi haina mvuto. Huo ni mtizamo wangu sijui wadauwengine wanasemaje ?

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 22, 2012

    Asante kwa hii mada kwanza kabisa watu wa nyumbani mnatukamua sana. Mnatuomba omba sana pesa bila kuelewa kuna ugumu wa kuzipata. Hivyo mkitupunguzia safari za Western Union angalau tutaweza kusevu. Pili ndugu zetu mlioko nyumbani hamuaminiki. Tukinunua viwanja either wizara ya ardhi inatuibia kwa kumuuzia mtu mwingine na kubadilisha makaratasi yote au ndugu badala ya kutusaidia kujenga wanazila.Unajikuta umewafanyia kazi watu wengine. Kwa biashara hii utajenga kweli? Utarudije nyumbani? Tatu tukiomba kazi turudi Bongo tunaambiwa wazee ni haki iyo?

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 22, 2012

    achana na sisi wewe, kwani wewe umeifanyia nini bongo? kwani huoni wazee wanavyong'ang'ana na madaraka hawataki kutoka halafu unasemaje? watu wanarudi wanakutana na mambo yaleyale ukijutahidi kujikwamua kihalali rushwa ina bana yaani pyuuu sirudi ng'oooo kwa barabara zipi? kwa umeme upi? kwa maji yapi? kwa huo mgomo wa madaktari au? full vibaka wanavunja hadi vioo vya magari ati kuna amani iko wapi? mtu unamiliki mali yako kwa wasiswasi utadhani umeiba kisa wezi kila kona, wee acha tu kaeni huko kwenye maziwa na asali ooops kwenye vumbi na dhiki, halafu ati mkataa kwao ni mtumwa si kweli nyie ndo watumwa manake mnakosa haki zenu za msingi nyumbani kwenu wenyewe na mkipiga kelele mnapewaje mkong'oto? he he hee i luv canada ni hayo tu!

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 22, 2012

    Nashukuru sana mdau kwa kuwasilisha hoja hii ambayo nadhani itakua na mawazo mengi na majadiliano ya hapa na pale vile vile, kwanza kabisa inaelekea mletaji wa mada hii yeye binafsi amekwisha onja maisha haya ya ughaibuni kwa namna moja au nyingine.
    point kubwa niliyoipata hapo ni namna gani watu waanzishe ushirikiano au makundi kuweza kusaidiana ili hatimae watu waweze kurudi nyumbani wakiwa tayari na mambo au vitu vya muhimu katisha maisha yao binafsi ili waweze kusaidika pindi watakaporejea jumla nyumbani, ukifwatilia sana majority ya wengi huku niwale ambao walikuja huku wakati TZ ikiwa na ukata mkubwa sana kwa waTZ hivyo wengi wao walitafuta njia mbadala ya kutafuta maisha ambayo ilikua ni kukimbilia ulaya, nadhani wewe unazungumzia Tz ya leo ambayo, si ile tena,na most likely wewe ni kizazi hiki cha www.com, na facebook, hivyo uelewa utakua mdogo, unazungumzia vikundi hebu nipe mfano wa kikundi kimoja wapo kilichoungana na kuleta mafanikio makubwa na kujipa ajira ambayo ilisababisha baadhi ya watz wakarudi nyumbani? au kuiga ili kuweza kusaidiana pindi mtu anapoaamua kurudi awe na uhakika wa maisha yake na familia yake kutokana na vikundi hivyo? kama si mwisho wa hivyo vigroup utakua mwanzo wa majungu? TZ ya leo unaweza kupata ajira kama umesoma, lakini inaangalia sana umri, na ukiangalia waajiriwa wengi sasa hivi ni vijana wadogo wadogo sana (which is good) na si late fourties
    of which ndio umri wa walio wengi huku ughaibuni, ambao wengi wao wamejipanga na maisha yao huku nje kwa kuwa wako ndani ya system vizuri tu, kama ni vibiashara vidogo vidogo huko nyumbani, basi maisha yanakwenda, kuna mahitaji muhimu sana ya binadamu yanayofanya watu hawarudi nyumbani,ambayo hapo TZ kuyapata ni ngumu mno, au yanahitaji mtu mwenye uwezo mkubwa sana, au wezi wa EPA,sasa kama ukoo wangu unasaidika na mimi kuwepo kwangu hapa ughaibuni, mimi mmoja nikirudi, ukoo mzima au familia nzima tutayamudu vipi hayo maisha yanayoendeshwa na mafisadi ambao ndio majority?? tukianzia na maswala ya afya, nani asiyetaka kulinda afya yake? rather than kupewa panadol zilizoexpire kwa magonjwa sugu? ni watz wangapi wanauhakika na maisha yao ya kesho, ukilinganisha na mtz aliyeko nchi za ulaya? (japo MUNGU ndie aliyeshika maisha yetu)na kwa nini watu wenye uwezo mkubwa hapo nyumbani wanahangaika kutakakusomesha watoto wao nje ya nchi?? Elimu imeshuka mno TZ, kando ya utitiri wa English medium,
    walio na familia huku ulaya wanahangaika waweze kukaka ili watoto wasome na waelimike, badala ya kusoma na kufuta ujinga tu.
    ni kweli kipato kwa nchi za ulaya ni kigumu sana, kwa ulipaji wa mambo mengi kutokana na system yao, lakini hata nyie mlioko TZ mmechangia sana kutunyang'anya hata hiki kidogo tunachopata kwa kuumia bado mnataka tugawane, simu za kutueleza shida kila mara ni za nini wakati tayari mnajua tuna shida huku??? mkija kutembea huku ni kuomba omba mpaka watu wanawakimbia, ninyi si mko sawa nyumbani, mnatuomba nini tena? mbona sisi tukija huko hatuwasumbui kuwaomba omba no matter mko kwenye position za namna gani.
    swala la MTZ kurudi nyumbani nila individual, kila mtu atakapo fikia muda wa kuona sasa ni wakati wa kurudi nyumbani atarudi kwa muda wake, kama hakuna lililotokea baya la kulazimishwa yeye kurudi, shida iliyoko kwangu haiko kwako, kama kuna mtz alirudi na kufanikiwa huko nyumbani basi ashukuru sana, atuache tu sisi tuliokomalia ulaya, maisha ni popote pale as long as umeridhika nayo. sio nyie ambao mtu akiamua kurudi bila mpango ndio mnakua wa kwanza kucheka kuwa du jamaa anasota sana hapa mjini na kachoka ile mbaya, hata msaada mnashindwa kumpa ili mumcheke vizuri. watz ughaibuni oyeee, VIVA ughaibuni!!!! mdau.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 22, 2012

    Nakubaliana na wewe mdau kwa kusema ushirikiano wa makundi kwa makundi kwa kuekeza nyumbani itasaidia kuturudisha nyumbani.Ila kinachonishangaza wapo watu wengi hapa UK ni kweli wameekeza nyumbani lakini kwa kushirikiana na ndugu zao,kisha baadae wakiamua kurudi nyumbani wanakaa kama mwaka au miwili kisha wanarudi huku UK,tena sio watazania tu na wakenya vile vile,ukiwauliza wanasema maisha ni magumu sana.
    Pia wapo watu wengine kutuma kwa ndugu zao vitega uchumi kama magari ya kubeba mizigo na daladala,hata kujenga,lakini mwisho wa siku hayo magari yanaharibika.Wengi wao wanalizwa na ndugu zao.Mtu anajenga nyumba miaka nenda rudi,kumbe ndugu yake anajijengea yake pembeni hiyo ni kwa waafrica wote.
    Nimechunguza sana wahindi au wapakistani wakifanya hivyo wanafanya kweli,akija kutafuta na akarudi kwao anarudi kiujumla,sasa sielewi ndugu zao huko ni waaminifu au inakuwaje?
    Pia kuna watu wengine kweli mawazo ya kurudi nyumbani hana kabisaaaa,anaona huku ulaya kafika.Sijui wanahofu ugumu wa maisha ya nyumbani au hicho kizungu kama ana watoto watakiongea na nani!!!Sijaelewa hiyo
    UKWELI NI KWAMBA,NYUMBANI NI NYUMBANI TU.MIMI HAPA SINA MIAKA MINGI,,ILA NI KWELI KODI ZA HAPA NA RENT KUBWA INAKUFANYA USTUKIE PESA YOTE UNAIACHA HAPA HAKUNA CHA AKIBA WALA NAULI YA KUKURUDISHA NYUMBANI,NA UZEE MTU UNAKUNYEMELEA,UKIJA KUSTUKA WENZIWE NYUMBANI WALISHAPIGA HATUA,WEWE NDO UTAONEKANA NDO KWANZA UNATOKA KIJIJINI KWENU KUJA KUANZA MAISHA DAR.

    AHLAM,,,LONDON

    ReplyDelete
  20. kambangwaJune 22, 2012

    Si sawa kwa upande wangu mimi kwa hayo jamaa aliyoyaleta, mimi nirudi kwenye nchi ambayo imeuzwa nitakuwa chizi, hadi bagladesh ameuziwanchi, sisi tupo bakini na tanzania yenu kwani sisi tukiwa huku inawauma mini?

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 22, 2012

    Napenda kuungana na watoa mada walioelemea kwenye neno "maisha ni popote". Mimi ushauri wangu ni kuwaacha walio ughibuni waendelee hukohuko ili kupunguza competition for resources hapa nyumbani. Kwa waliofanikiwa tungependa muwekeze nyumbani lakini suala la kuendelea kuishi huko nje ni poa kabisa. Msije kabisa bongo. Wakija hapa bongo wataongeza misongamano ya magaritu. Hata mkifa zikweni hukohuko kwani ardhi huku imeanza kupungua.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 22, 2012

    Asante uliyeleta mada hii. Mimi napenda kumpinga anayesema anakaa nje kwa sababu nyumbani hakuna huduma muhimu ikiwemo elimu bora. Kumbuka hata huko nje walitaabika mpaka kufika hapo walipo. Hakuna atakayejenga nyumbani kwako kama si wewe mwenyewe. Unaonesha unapenda vilivyotengenezwa na wenzako wakati huji njia waliyopitia. Angalia usije ukaliwa kiboga na wazungu kwani unaonesha unapenda miteremko.

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousJune 23, 2012

      Serikali yenu ni ya kuunga unga utakuja jenga nini? Acha ujinga hui nchi ilijengwa na viongozi wake na siyo raia Sao walioko nje. Kumbuka walipigana vita na ndomaana Leo wako hapa.

      Delete
  23. AnonymousJune 22, 2012

    kwanza nimegundua aliyeandika hii mada alikua deported, bahati yake hapa ulaya alisoma, sasa amepata kazi nzuri ndio anaandika hii mada, na hao wanaomsapoti wengi wao visa zilishindikana walinyimwa ku-renew, wakashindwa kuendelea kuishi huku, shukuruni sana mumepata vya kufanya, ila msidharau wenzenu muliowaacha huku, kwani nanyi si mlipitia haya haya? sasa iweje leo? haya tuchekeni tu. ila poleni na mmbu, maji kukatika, umeme kuzimika,sijui kama mulikumbuka generators mwanawane, angalieni sana hizo antibiotic nyingi zime-expire, muwe waagalifu kuwapa watoto, eeh kweli hata hizo dawa za mswaki, angalieni sana, nyingi ni cream za usoni wanachakachua,
    fungeni sana madirisha kwa ajili ya vumbi na vibaka, wakubwa wenu wakiugua waambieni tuko huku tutawapokea na kupiga nao picha, kama mtahitaji chochote tuagizieni tutawaletea msinunue vya china, pamoja na ugumu mkubwa tulionao huku, ila tutawasidieni tu maana ninyi ni wanzania wenzetu, tusichekane, haya ngoja naona ambulance hiyo hapo nje wanakimbia kuja kuniona maana nimeteguka mguu, baadae!!!

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 22, 2012

    Mdau ninakupongeza kwakufikiria kitu kama hiki nimuhimu sasa kuongelea hili sababu nchi nyingi zinapigania watu wake waliokuwa nje kurudi nyumbani kujenga nchi yao na nikweli huwa mafanikio yanakuja kulikoni mwekezaji asiekuwa na imani na hiyo nchi!ninakupa mfano wa nchi moja tu ambayo imejengwa na watu wake waliokimbilia nje ambayo ni china wachina wengi walikimbilia Amerca miaka hiyo wakawa wanafanya kazi kwa bidii na kazi nikiwa nihizo chafuchafu na walikuwa hawaruhusiwi kununua nyumba wala kiwanja Amerca lakini nchi yao iliwapa nguvu na kujenga nyumbani na kufungua makampuni na ndio na wawekezaji wengine wakarudi!
    Ndugu mdau sbb kwamba Mtanzania anashindwa kurudi nyumbani nikwamba yeye anabanwa kuliko mwekezaji na nchi yenyewe haimpi nguvu kumuwezesha na pia akituma hata peni nyumbani anabanwa sana kiushuru ili asiweze kurudia tena kutuma kitu!Nikweli malipo nimengi na hizi nchi pia zinatubana tusitowe kitu kuleta nyumbani lakini pia tukiwa na malengo tunaweza kujibana!Baadhi yetu wengi tumejenga nyumbani lakini haturuhusiwi hata kufungua Acount sasa mtu umewekeza nyumba nyumbani unashindwa kupewa kipa umbele ili ukapata nguvu nyingine?Taabu mdau kuanzia ndugu mpaka serikali wanatubana sana tusiweze kurudi nyumbani!lakini tunapenda nyumbani sana,tunapenda nchi yetu mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 22, 2012

    Mdau mada yako ni nzuri ila ina upofu mkubwa. kwa maneno mengine unasema watu waliko mijini warudi vijijini kwao ili walete maendeleo!
    kuna wadau tayari wamekutajia safari za westernunion, na zaidi kukwambia walioko Tanzania sio wote mambo yao shwari. kushindwa ni kokote na kushinda ni kokote, ila najua bajeti ya tanzania asilimia 60% ni msaada, kwa maneno mengine, hao unaoan wameendela ni mama jasho lao au wizi. na huwezi kusema kila mfanyakazi Bongo mambo yake mswano.
    Maendeleo unayaleta hata ukiwa mbali an nyumbani. Maraisi wa Uganda na Ghana waliweza kukiri kwa wana diaspora wao kuwa pesa wanayotuma nyumbani(remittances) kwa familia zao inazidi kipato cha zao la kahawa na cocoa. kwa maneno mengine, hao wapiga box wanaleta hulka hata kwako wewe. Kama ingekuwa unavyodai, basi kila mfanayakazi Mbongo mambo yangekuwa mazuri kwa mshahara wake, ana bakiza, anasomesha watoto wake bila shida, nauli ya basi sio shida nk.
    la mwisho, wapo watu kazi na kipato chao kizuri, lakini nia ya kuonyesha kama Bongo mlivyo hakuna, kwa hiyo utamuona tu hivi, lakini akiamua kurudi akajenga, mnabaki kushngaa, maana kwa Bongo aliyeshinda nja utamjua, aliyepanda basi utamjua kwa kuangalai, nk..hapa, huwezi, hakuna madoido na matanuzi, unaishai kivyako, mradi pesa iko benki au unatuma kwa ndugu ambao ndio hao wanauliza mbona haujafanya hiki au kile..kwa sababu ipi? maana utajiri Bongo ni kama Busha, utamjua mwenye nalo kwa kumuangalia tu. hapa mtu atakuwa yuko Basi lakini nyumabni kuna magari mawili ila kwa siku hiyo hakuan sababu ya kuyatumia..Bongo mpaka akupigie na honi ujue ana gari..ulimbukeni?

    ReplyDelete
  26. Bertha Lyimo( India)June 22, 2012

    dr shayo alionyesha njia na sasa yupo huko bongo hasikiki au ndiyo maisha mnayotaka tuje kukumbana nayo?
    Alipokuwa huku marekani yeye na mashaka walikuwa tegemeo na wasemaji wakuu wa huku kwa mada zao zilizokuwa zinatoa matumaini
    je na sisi tukirusi tutachakachuliwa?

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 22, 2012

    Mswali hayo mnayowauliza watu wa ughaibuni hata Baba yangu aliulizwa alipokuja Dar kutafuta Maisha na kuamua kuendeleza mji wake na si kurudi kwao, Dunia ni kijiji siku hizi na unaweza ukaamua uishi popote unavyotaka ndio maana tunao wazungu walioamua kuja kushi Tanzania

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 22, 2012

    nje watu wanaishi kisheria, kila pesa unayoipata lazima ikatwe kodi, watu wanaendelea bongo sababu hakuna udhibiti mzuri wa hela, i swear kungekuwa na udhibiti wala usingesubutu kusema hayo, watu wengi mno awalipi kodi na wanaolipa awalipi ipasavyo,pesa inapatikana kiujanja ujanja tu, mlinzi wa mlangoni bandarini unaweza kumkuta ana jumba mpaka ukashangaa, watu ni wababaishaji sana, wangapi wana majumba wameyapangisha awalipi kodi, kama unanielewa mnaona maisha ya tanzania marahisi ukiringanisha na nje kwa kuwa watu wengi mno ni wababaishaji, kodi hamlipi, hata mimi hela yangu ninayoipata huku ingikuwa naweza nikaifanyia makeke isikatwe kodi basi ningekuwa na maendeleo ajabu, huku kila unavyopata kingi ndivyo unavyokatwa nyingi. kwahiyo unatushauri turudi hili tuje fanya ubabaishaji? Zitto katoa ushauri kila mtanzania awe anajaza fomu ya kodi kila unapofika mwisho wa mwaka, sasa wewe subiri watanzania wote wawe kwenye system ndiyo na serikali hiwe inakusanya kodi tokana na unavyopata na ubabaishaji ubabaishaji huwe hakuna, kisha njoo hapo useme tanzania maisha ni rahisi. UKWEPAJI WA KODI TU NDIYO UNAWAOKOA MUONE MAISHA NDIYO MARAHISI.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 22, 2012

    Pamoja na ushauri wako lakini ndugu umeshafika Ulaya? Au labda huko Spain maana mzee Norway ni tofauti. Haitetemeki kiuchumi hiyo nchi mazee, darasa la kwanza mpaka PHD bure, huduma za afya bure, huna kazi unalipwa, kila mtu na daktari wake,ukifanya soo unatafutiwa mshauri akushauri kisaikolojia sio kukimbizwa jela kibongobongo,kazi za kumwaga ujue tu lugha,jamani Bongo nije kufanyeje?
    Wenye mpako wakwenda bongo waende,mie nabaki Norway hapa ndio nyumbani hata misahafu ilisema ondoka uende katika nchi nitakayokuonyesha nami nitakubariki...Bongo tunakuja kusalimia tu,barabara mbovu,watu wanakunya njiani,hamna maji, dhuluma,ujambazi yote ya nini hayo?

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 22, 2012

    Mimi nafikiri, tungesaidia watanzania wengi walio na matatizo ya ajira na kipato tanzania kwanza kabla ya kutaka kurudisha wa ughaibuni, kumbuka ughaibuni hata bila kazi na kipato unaishi. Vile vile aisilimia kubwa ya hayo maendeleo ni pesa chafu..wangapi wamejenga majumba au kuwa na biashara kubwa bila ya kuwa na maelezeko kamili ya mtiririko wa chanzo cha hizi pesa. Ughaibuni unapata unachokifanyia kazi na ni chako na si wizi wala ujanja.

    Kingine huwezi kushawishi mtu ambaye tayari anaishi kwa nafasi Ughaibuni aje kuishi katika moja ya nchi masikini wa kujitakia duniani ambapo akiumwa sinuses inabidi aende India kwa matibabu!

    Yohanna.

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 22, 2012

    unajua bwana wabongo wanalichonga sana...hata ungejitahidi vipi kuweka mambo yako sawa watasema tu kwani maendeleo au mpango mzima wa maisha mwaachie mwenyewe kwani wewe inakuhusu nini kuwa bongo au nje kutafuta maisha bila kufanikiwa. tatizo letu cc wabongo tunajifanya ni washauri wazuri sana kwa mambo yasiyotuhusu..ujinga na upumbavu tu..mtu akinunua gari mawazo mengi mtatoa ooh mara jenga kwanza oohh gari linaharibika..men so what ?? mind your own biznes and let me deal with mine..jak ass

    ReplyDelete
  32. AnonymousJune 22, 2012

    namalizia kwa kutoa sante kwa michuzi kutuwekea hii mada babu kubwa, nafikiri nyote mmefaidika na hayo yaliyosemwa na wachangiaji, wapo waliotoa maneno ya busara na wapo kenge ,konokono,vinyonga na vyura maana kwenye msafara wa mamba ,viroboto kama hao hawakosekani, ila pia nao lazima tuwashukuru kwa vile,bila watu kama hao ,hatutajua nani mwenye busara. Tanzania tuko karibia 50 million, ningependa kumkumbusha yule aliyesema kwamba anafanya safari za kwenda western union, eti ndicho chanzo cha kumkwamisha asijenge bongo, bul shit, mimi binafsi nimeshuhudia pesa inatumwa kutoka bongo kwenda kusomesha mtu aliyeko USA na huyo anayetuma hizo pesa ni mama tu mjasiliamali na kiduka chake cha kanga na ziko kesi nyingi za namna hiyo. Na wanaosema bongo kuna vumbi na vibaka , kumbukeni kwamba ,bongo ni tropical-hivyo tuna mida ya vumbi na mvua. kingine ni kwamba ,mtoa mada anazingatia sana maisha yasiyokuwa na pressure kama ya huko mliko-lakini kwa bahati mbaya wengi mmem quote vibaya. please re-think again,kingine , je mutakapofika hiyo miaka 65 hadi 70 ,muta-fit kwenye jamii ya HUKO ???? haya , yetu macho-kumbukeni kujiwekea akiba ya kwenda kulelewa kwenye majumba ya wazee,na watoto wenu hao wanaoongea kizungu watakuwa hawana taimu na nyie- watawaita ,the shit old man =ni kizungu lakini na wewe ndiye uliyemsomesha. Zebedayo wa Magomeni.

    ReplyDelete
  33. AnonymousJune 22, 2012

    Kuna mdau kasema hapo juu,mtoa mada ama ni deported,au alitaka kuja huku hakufanikiwa maana kila nnapokuja nyumbani Tz nikiyaangalia maisha na kulinganisha hapa nilipo nashindwa kupata picha na hoja ya mdau.
    Ukileta chochote kodi inazidi bei uliyonunua,kitu kinachowezekana ufanyiwe leo kinachukua miezi 2 au zaidi kufanyika,matabibu feki(dokta) dawa feki,foleni nnazoshindwa kusema.
    Sijui,lkn kusema kuna fursa nyumbani,zipi.....? hizo za kuangalia huyu mtoto wa nani? au unajuana na nani? au una mshiko kiasi gani (rushwa) upewe kipaumbele?.
    Kweli,mfumo hapa ni kulipa kwenda mbele,lkn nikijibana naweza ku-save dolla 800 kwa mwezi. Hapo farasi wa kazini tayari kapata chakula yake (mafuta) kwa mwezi mzima na nishalipa kila kinachohusika,na nikiwa na shida inasikilizwa ontime,popote ntapokwenda,vinginevyo niwe kwenye black list,leo ulinganishe na huko kweli mahali ambapo kupata cash card inachukua miezi 3!!!!!!????????. Ukweli hamtaki turudi maana tukijibana kuleta chochote kodi zenu mnazotutoza ni za kiama,ndugu ndio balaa,wanavyopenda kuagiza pasipo kujua wengine (kama huyu alieleta mada) wanakimbia huku halafu wanaleta kandia kama hizi pasipo kusema ukweli kuwa mziki huku uliwashinda.

    ReplyDelete
  34. AnonymousJune 22, 2012

    Niliwahi kusikia humu Jamvini katika Blogu mtu mmoja mwenyeji wa Iringa amekaa Norway miaka 17 lakini hajapata Karatasi wala Sheria!

    Bora angebaki Bongo tokea hiyo mwaka 1995 alipoondoka nchini huenda (miaka 10 baadae) zilipoanza kutolewa kwa mara ya kwanza mwaka 2005 angepata angalau Kadi ya Tanzania ya kupigia Kura!

    -----------------------------------
    TWENDE KWA MAHESABU YA KIUCHUMI:
    -----------------------------------
    Mfano tuseme angebaki Kijijini kwao Ludewa angelima nyanya na kabechi.

    Kwa Ekari 10 mfano Ekari moja inatoa gunia 3X10=30

    Mwaka mmoja pana Misimu kama 2 wastani gunia 30
    X2=gunia 60 kwa Mwaka.

    Bei ya gunia moja Tshs. 120,000/=

    SASA KWA MIAKA 17 ITAKUWA 60X17X TSH. 120,000/=TSHS. 122,400,000/=

    SASA KAMA ANAKULA FEDHA HIZO NUSU NA NUSU AKIBA ATABAKIWA NA TSH. 61,200,000/=

    SASA WANDUGU MWANA NORWAY AMEKOSA THS. MILIONI SITINI NA MOJA ZA AKIBA!

    INA MAANA ALIOWAACHA KIJIJINI AKIRUDI KUTOKA MAJUU ATAKUTA WANA MILIKI MAFUSO NA WAMEJENGA MAJUMBA WAKATI YEYE HATA EURO 100 (TSH.200,000/=) INAWEZEKANA HANA AMA KWAKE NI MGOGORO!

    RUDINI NYUMBANI KAMA MKIONA HAMNA MWELEKEO WOWOTE MAJUU MSIPOTEZE MUDA ZAIDI!!!

    ReplyDelete
  35. AnonymousJune 22, 2012

    MTOA MADA HONGERA LAKINI LAZIMA UKUMMBUKE HIVI SASA JAMII INAISHI LATIKA DEMOCRASY,KILA MTU ANA HAKI YA KUCHAGUA WHERE TO LIVE WHAT TO EAT,WHOM TO LOVE PASIPO NA MIZENGWE, MIMI BINAFSI NAISHI ULAYA TAKRIBAN MIAKA 25. NA SIO ATI SIKUMBUKI NYUMBANILAA, NAIPENDA SANA NCHI YANGU KWA KILA HALI. MAMA,BABA,DADA,MJOMBA WOTE WAKO BONGO. NA NI MIMI NDIO FAMILI INANITEGEMEA KWA ALLMOST EVRYTHING.

    KINACHOKATISHA TAMAA KWETU NI HII MAMBO YA CORRUPTION. KILA SIKU NINAJITAHIDI KULETA BIASHARA NDOGO NDOGO HUKO ILI NIWEZE SAIDIA NDUGU NA JIRANI MTAANI LAKINI HAKUNA KINACHOWEZEKANA KWANI KILA KITU NI KIGUMU KUFANYA , KWANI UTARATIBU WA UFANYAJI KAZI TANZANIA SIVYO KABISA, UNAHANGAISHWA SANA HATA KUTOA MIZIGO BANDARINI NI KAZI NA MUDA UNATUMIA MREFU SANA, MAOFISA WA BANDARI WANATAKA UWAPE PESA ILI UFANYIWE MABO YAKO HARAKA HARAKA KAMA HUNA BASI MZIGO WAKO UTAOZEA BANDARINI IKIFIKA MUDA WA KUSHINDWA KUTOA, BASI UNAPIGWA MNADA NA NI MISSION TAYARI IMEISHA PANGWA NANI ATANUNUA CONTINER LAKO, HIO NI SABABU MOJA YA KUKTUKATISHA TAMAA SISI TUNAOISHI HUKU ULAYA,KWANI TUMEZOEA MAISHA YA KUONA KILA KITU KINAKWENDA KWA UWAZI. KAMA UNA BIASHARA UNALIPA USHURU NA UNAENDELEA NA SHUGHULI YAKO BILA VIKWAZO LAKINI HUKO KWETU BADO SANA KILA MTU ANATAKA AKULE NDIO UTAMADUNI WA MAISHA YA TANZANIA,HOSPITALS HAKUNA, SHULE HAMNA, BARABARA HAKUNA, UCHAFU ULIOKISIRI, RAIA HAWANA HAKI, MAFISADI WANANYANYASA, NA HAKUNA SHERIA ,HIVYO NI VITISHO MOJAWAPO AMBAVYO VINATUFANYA TUOGOPE KURUDI NYUMBANI KWA AJILI YA KUISHI.KWANINI VIGOGO WANAWALETA WATOTO WAO KUJA KUSOMA HUKU ULAYA WASISOME TANZANIA? WOTE WAMEKAA WANASUBIRI RUSHWA ILI WAKAJENGE NYUMBA KWA HIO KAKA MTOA MADA HII NAONA HUELEWI AU UWEZO WAKO WA KUELEWA BADO FINYO SANA YOU NEED TO MOVE AND SEE OTHER SIDE OF THE WORLD HOW A HUMAN BEING SUPPOSSED TO LIVE,NI KWAMBA BADO SANA HUKO TANZANIA BADO TUNASUBIRI MIAKA MINGINE 1500 NILI TUWEZE ANGALAU KUFIKIA VIWANGO VYA BINADAMU KUKUPENDA KWAO. MALARIA IKLITOWEKA TUTAKUJA.

    MDAU OSLO, NORWAY

    ReplyDelete
  36. AnonymousJune 22, 2012

    wengi wetu hatutaki kurudi bongo sababu serikali yetu ya Tanzania inafuga mafisadi,na pia hakuna haki ya mwananchi bila ya kutoa rushwa,Umeme ni taabu,Maji ni shida,hospitali hakuna dawa,barabara ni mbaya,kwa kweli hakuna huduma inayoridhisha kwa wananchi!sasa mnataka turudi bongo kufanya nini?yaani misukosuko ni Mingi kila kukicha!Mtu badala ya kufanya kazi na kutafuta pesa inakubidi ushughulikie matatizo mengine mengi hadi kichwa kinauma!Taabu yote ya nini wakati ulaya tunapata huduma nzuri?Ndiyo maana Tanzania haiendeleo sababvu matatizo ni mengi sana.

    ReplyDelete
  37. AnonymousJune 22, 2012

    Nyie acheni utani.

    Bora nibebe box "majuu" kuliko kuuza maandazi na samaki Tabat, by the way nimeuza maandazi Mburahati miaka ya tisini.
    Mnaongelea akiba, diaspora, nssf kama vile ukitua tu airport wanakukabidhi mwelekeo.
    We una mtaji wa maembe wa laki moja, akiba inatoka wapi hapo?


    Ukweli ni huu, iwe bongo iwe kiwanja - maisha ni kujipanga, na usipojipanga, maisha yatakuchapa kisawa sawa. Njia pekee ya kutoka ukiwa kiwanja ni elimu ... Wanasema ukienda Rome, do what....?

    Mimi nimekuja kiwanja kimazabe mazabe, nimesafisha vyoo, nimepiga box, nimeuza burger - wakati huo huo naenda shule. Sasa hivi nna maisha yangu mazuri(Two modest houses, one paid in full, one has renters, multiple vehicles, healthy bank acccount), kazi yangu nzuri na naheshimika kazini na mtaani na akiba yangu inaendelea kukua. Nafanya kazi na cutting age technologies with world class colleague. I have opportunity to use my talents and education and I'm still growing professionally with a young family. Usiku napata usingizi mnono kwa sababu sijachakachua wala kumuibia mtu ... na kuna wabongo wengine wenzangu mambo yao safi kama mimi...I'm only 34.
    Unaniambia NSSF, Diaspora, NHC ... sikuelewi. tatizo la wabongo wengi wakija kiwanja wanataka kuishi kibongo bongo, ukipata senti tano, heshima hakuna unataka kufunga baa, baada ya mwezi welfare ... huku unavuna ukipandacho, ukichakarika na kujipanga - mambo yatanyooka, ukijibweteka - cha moto utakiona. Wakati bongo ni tofauti. Usipokuwa na godfather, umeliwa.

    Hii mada inawalenga wale waliopigika, na ushauri wangu kwao ni kuwa wajichanganye na kujipanga.

    ReplyDelete
  38. AnonymousJune 22, 2012

    Vitu muhimu vimeongelewa hapa. Kama tukiacha safari za kwenda western union hakika tutasave maanake watu nyie kwa kuomba na shida hamjambo. Halafu kutuambia turudi mi kama vile mtu akwambie wewe utoke Dar urudi kijijini kwenu, ambako hakuna umeme, maji wala daktari ukiugua tu kidogo basi posibility kubwa ni kifo! Ukiwa nazo kidogo vibaka na majambazi, hivi unajua huku tunalala milango wazi? Huko watu mnaamka saa kumi za usiku kuwahi foleni na kurudi nyumbani late wengine inabidi mbakie mjini mpaka foleni ipungue ndio mrudi nyumbani. Mambo ya mzee, mzee na kunyenyekea sana watu kazini hamna hapa, just fanya kazi yako. Nitarudi nikiwa almost karibia na time ya kupelekwa nursing home, kama watoto wangu watashindwa kunitunza, hiyo ndiyo my individual plan, of course nimeshajenga

    ReplyDelete
  39. AnonymousJune 22, 2012

    We ulioanzisha hii maada bola wewe tuache tunaoishi Huku ulaya na wewe Ishi na bongo yako unaweza kuwa wewe ni mtoto wa fisadi fulani unahuwakika na maisha sababu baba yako mwizi selekalini tujee huko hakuna maendeleo yoyote hakuna kazi hakuna hospital nzuli barabala nzuli hii mikobo hinatoka kwa kujuana . Tunaoishi Huku nje sio wote wenyemaisha magumu , msengeee tuu wewe kaa na bongo yako falahaaa mkubwa wee

    ReplyDelete
  40. AnonymousJune 22, 2012

    ili ni swala la msingi sana sababu nyumbani ni nyumbani hata iwe kichakani,ila kwa upande wa pili maisha ni popote na kila mtu na maisha yake,mimi nipo poland maisha ni magumu ila mungu mwenyewe anajua but natamani nirudi home ila naona aibu nitaanzia wapi??????

    ReplyDelete
  41. AnonymousJune 22, 2012

    hii mada ni kali kweli kweli leo kipele imepata mkunaji kwa ukweli tuliokuwa nje ya nchi kurudi ni kazi kubwa haijalishi unamaisha mazuri au la maana haya tunayoyasoma kuhusu nyumbani yanatukatisha tamaa sana vitu vyoote vya muhimu kupata ni shida na huku na huku kila kitu bwelele wengine tumeshasahau shida ya umeme,maji,kila kitu ikihitaji unapata ontime hakuna rushwa za kijinga hamna wizi ambao ndio ugonjwa mkubwa unawaowamaliza tz ajali za kutisha za kilaleo miundo mbinu mibovu n.k.n.k .nk kweli tunakumbuka sana nyumbani maana nyumbani ni nyumbani tu lakini ukianza kufikiria hayo matatizo niliyoorodhesha hapo unachoka kabisa mdau wa no jun22,01;27;00pm umeniacha hoii is you my day

    ReplyDelete
  42. AnonymousJune 22, 2012

    Mi nadhani inategemea mtu alipo uko ughaibuni anafanya nini. Wengine wana kazi zao nzuri na kufurahia wanayofanya. Wengine ni kupigika mtindo mmoja. Hata hivyo Tanzania yenyewe soko la ajira gumu na maisha vile vile. Maisha ni popote ili mradi mtu ufurahie unachokifanya.
    Japokuwa nipo nje ya Tanzania kikazi(Western Europe), kila mwaka naenda nyumbani tena mara mbili bila mawazo. Ninajua ninachokifanya na mipango mizuri na maisha yangu.

    ReplyDelete
  43. maisha ya ughaibun sio kwamba ni big deal kihiivyo,coz kipato unachomeek ni kdgo sana ,lkn unajisikia kdg km vile uko dunian ,mitahani unayopat midogo midogo unaichukulia kawaida kwasababu uko nch za w2,lkn ukilinganisha hapo kwetu ,unapata madhinla makubwa ,kuliko hata nch za w2 mf.mtz anakamatwa kwa kosa la udhurulaji wewe tangu lin!raia akawa mzurolaji nchi yk,pili hawo viongoz hp nchin ni janga la hiyo nchi ,utaishi vp nch ambayo wa m2 mgen anasaminiw kulik ww,na vile vile miundo mbinu ya hiyo nch haifai ht kulezea!

    ReplyDelete
  44. AnonymousJune 22, 2012

    Bongo inashangaza mbunge anapewa gari,kwa fedha ya walipa kodi wa aghaibuni,ushuru haikusanywi,halafu mnaandaa bajeti, rubbish

    ReplyDelete
  45. AnonymousJune 22, 2012

    Mtoa mada hao unaowataka warudi nyumbani, wakirudi utawapa ajira wewe? Wangapi wako hapo dar ambao hawana ajira wanaishia kijiweni na mwisho wa siku ndio hao wanatuvunjia nyumba zetu usiku. Ukumbuke sio wote walioenda ulaya walikuwa na maisha ya juu, baadhi Yao walikuwa ndio hao hao waliokuwa vijiweni wakaangaika mpaka wakapata nafasi ya kwenda nje ya nchi. Leo hii anajiingizia kipato chake, anaweza kuwasomesha watoto wake, anapata malazi, afya na kufunguka kiakili kwa kuona mengi ambayo hakuyaona Tanzania, leo umwambie wacha yote haya na urudi nyumbani.
    Akirudi anajikuta hana ajira, anabakia kurudi pale pale kijiweni, mwisho wa siku anabakia kuwavunjia watu nyumba au kuwa tapeli. Sasa hayo ni maendeleo au tumerudi atua nyuma.
    Kumbukeni watanzania hata wazungu maendeleo Yao yametokana na kutembea nje ya nchi zao na wingine hata kuishi huko . Mmesahau watu Kama kina Dr Livingston na Vasco Da Gama - wacheni watu wajiamulie wanachotaka kufanya. Usiwadanganye watu eti kuna misaada kutoka kwenye mabenki - mortgage sio Msaada ni liability. Ningekuwa wewe ningeomba watu waendelee kuishi huko huko na kumtafuta mmoja wa hao waishio huko nje na kushirikiana nae kufanya project mbali mbali ambazo zitakuingizia kipato.
    Wezentu wazungu nchi zao zimeendelea katakana na small business za watu binafsi na nyingi utakuta wanawakala zao nje ya nchi zao. Sisi tumebakia kupiga makelele "rudini, nyumbani kuna maendeleo" kunamaendeleo gani? Kuwa na magorofa mawili matatu ndio maendeleo? - nakumbuka ndugu yangu mmoja aliniambia wakati wa miaka ya nyuma, lile gorofa la sea view lilipojengwa watu walikuwa wanaenda na kupiga picha mbele ya gorofa na kuwatumia ndugu zao waliokuwa nje barua na kuwaambia warudi nyumbani ati kunamaendeleo.
    Maendeleo ni wewe mwenyewe, na jinsi utakanyokabili maisha yako, sehemu yoyote, mahali popote.

    ReplyDelete
  46. AnonymousJune 22, 2012

    Mtoa mada hii tunashukuru,ila nimeichambua mada yako kinaganaga nimegudua hii ni swala la wivi mkubwa.wewe huwezi kuwashauri watu watoke kwenye maisha mazuri wamdaujewaishi kwenye vumbi nene mhapo.mdau UK.Ulaya juuuuuuuuuuuuu.

    ReplyDelete
  47. AnonymousJune 22, 2012

    Shida nyingine Ughaibuni:

    Ili watu huko ndugu zetu kupata urahisi wa kufikia malengo ya kimaisha unakuta mwanamke anaolewa na Kibabu au mwanaume kijana anaoa Bibi Kizee !!!

    Siku moja tupo Jijini Dar pale Mtaa wa Samora ndani ya JM Mall jengo kubwa lenye Sepermarket na Pubs, Restaurants na Casinos akaja dada mmoja umri under 25 na Mumewe Babu wa Kizungu umri 70+ inaonekana wanatokea Majuu lakini walivyokaa meza ya pili,,, kwa kweli yule dada alijisikia vibaya sana kwa kuambatana na Mume mzee akawa anaona aibu kabisa kwetu !!!

    Jamani Wa ma Diaspora mnaona adhabu nyingine hii?

    Tunajua pana hizi Ndoa zetu za wazinzi kushitukizwa zinaitwa 'Ndoa za mkeka' sasa Penzi la namna hii ni 'PENZI LA MKEKA'

    Sasa kweli hapo mapenzi ya dhati yapo?

    ReplyDelete
  48. AnonymousJune 22, 2012

    Wabongo Jamani tuache unafiki, mie mime toka nyumbani Tanzania juzi, Hali ngumu Kama ni ni.yaani we unafikiria kuibiwa tu kioo Chako cha gari, I libidi niende kwa fundi kupata Hizo Wanaita ribiti sijui, halafu kila mtu Anataka kukuchomoa pesa, Sasa huko barabarani usiseme Dar unafanya jambo Moja tu la maana kwa siku magari utitiri barabara Hamna, ukiwa na gari ndio maendeleo? Yaani Watu kushindana tu Kwenda mlimani city kuonyesha Wana hela na wameshawahi Kwenda ulaya. Sasa Kama ulaya kubaya kwa nini wale tuliokuwa nao Huku majuu wanapenda kila mtu ajue wallis hi ulaya? Tusidanganyane Bwana, utalinganisha hapa nilipo Marekani na huko Dar kwetu?mie mtaniona hapa hapa na kazi nzuri nnafanya na Maisha nayafurahia, Kaeni na mafeki yenu huko wenzenu tumeridhika,watoto Wetu wanasoma shule za ukweli Nyie Hizo hela mnazompata wapeni hao English medium fake Mwisho wa siku ngoma Sawa kwa sababu Mimi nimesave kwenye elimu na wewe unmetumia pesa zako kulipa elimu ya watoto isiyo na kiwango .tuacheni Bwana Maisha is yetu? Pilipili usoila yakuwashia nini?

    ReplyDelete
  49. AnonymousJune 22, 2012

    Mdau mengi yalishasemwa na wadau wengine lakini na mimi si vibaya nikichangia. Kuna methali isemayo "Akili ni nywele kila mmoja wetu ana zake" na "Akili ya kuambiwa changanya na yako".

    Kila mtu anafikiri tofauti lakini nakupongeza mdau kukumbushana kwa kuwa fainali ya maisha inakuja. Kumbuka ukishaishi nje zaidi ya miaka 10 na hakuna msimamo wa maisha yako utambue kuna shida na ni shida kubwa sana. Moyo wangu unadunda upesi kila kukicha. Wasiwasi juu ya maisha ya baadaye. Strokes na heart attacks ni miongoni ya magonjwa yanayosababishwa na kufikiri sana na kufikiri huko kukihusisha woga. Nivyojua mimi storm ya uhamiaji inakuja hasa hapa kwa Obama, chukua muda tembelea mahakama za uhamihaji ndiyo utaelewa waafrika wanavyorudishwa nyumbani mafungu kwa wingi. Takwimu zinaonyesha idadi chache sana ya watanzania waliyo na vipande vya kuishi nchi hizi, japokuwa ni kweli kabisa baadhi yao bado maisha ni kimeo. Ni kweli mdau maisha ya aina hii mpaka lini? Watu wengi uishi kwa wasiwasi. Omba mungu usirudishwe bongo mafungu, maana wakishakufikisha kwenye selo zao na kukupiga bomba bongo utafika kipawa bila chochote, tafakuli!!!! Sijiogopeshi na siogopeshi wadau lakini huu ni ukweli wa mambo na lazima tuujadili kusudi kuelimishana na kuchukuwa maamuzi madhubuti. Bomba linawakumba waafrika wengi sana hivi sasa na idadi kubwa ni wana-Nigeria, Wakenya na wabongo.

    Mdau wa mada, pamoja na mchango wangu huu huku sichomoki mpaka mabadiliko ya utawala yakomaa. Inaonekana dalili ni nzuri. Huduma mbovu za jamii, mabarabara, mbu, nchi, mavumbi, umeme na mengineyo hayanitishi kwani hata huku walifanya kazi ya ziada kuboresha nchi zao ndiyo maana tunapenda kwao japokuwa inawezekana hawataki tuwepo kwao. Kwa kuwa wakikataa tusiwepo kwao na sisi tukiwabarasa kutoka kwetu watatuporaje hayo madini na maliasili mengine? Akili kichwani "You die you way I die mine".

    ReplyDelete
  50. AnonymousJune 22, 2012

    Shusheni ma-box migongoni mwenu Majuu,,,muwahi mrudi Tanzania mje mshike majembe mlime!

    Kwanini msirudi Kaliuwa Tabora kuja kukata mkaa?

    ReplyDelete
  51. AnonymousJune 22, 2012

    Mdau mtuondolee wezi na rushwa na viongozi wabovu turudi tujenge bongo!Mawazo ya watu wengi hapa nimazuri na nafikiri umeelewa kama wao wakirudi familia zao zitakuwa hazipati hata mlo mmoja sbb watakuwa wote kwenye dhiki kikwete na Ridhwan wanatanuwa na magari yakifahari!

    ReplyDelete
  52. AnonymousJune 22, 2012

    Babu wengi wao hawana mpango, kazi yao kulipia nyumba na magari yasiyoisha malipo kama mataahira badala ya pesa hizo kufanya mavitu ya maana nyumbani. Ukijifanya unazo sana na kumbe ni pesa za box kweli watu wa huku watakuliza, lakini ukiwambia watu wanaokufanyia shughuli zako huku bongo kuwa ukila pesa zangu kinyume na haya tunayokubaliana bora ukajitundike mwenyewe kwenye kitanzi kwa kuwa napata pesa kwa shida sana sitokubali zipotee.

    Mdau wabongo wengi nje hawana mpango kwani wajanja wote wanaramba TEKNOLOGIA kama walivyofanya Wajap(Japanese), Wachichi(Chinese) na Wakoko (South Koreans). Leta hiyo utaalamu(teknologia) tukomae na wabunge na serikali iweke bajeti yake mambo yaanze kugeuka. Wananchi waanze kilimo bora na umwagiliaji kwa kutumia utaalamu unaopatikana nyumbani.

    Kubaki nje kwa sababu ya kimombo, mabarabara na vitu vyote vizuri vya nje ni ulimbukeni na fikira duni.

    Mwisho kabisa, Ujumbe wangu kwa madaktari wetu bongo, safari hii mkigoma, mkasababisha vifo mahospitalini wananchi lazima watatafuta njia ya kuwarekebisha.

    ReplyDelete
  53. AnonymousJune 22, 2012

    Watu mnaponda tuuu... ponda tuuu... Kwani huko mliko wao walianzia wapi mpaka wakafika walipo?? Watu walirudi wakaungana na kuleta maendeleo manayoyaona (nothing comes easy) na mabadiliko hayatokei over night. Lazima watu hasahasa waliosoma kidogo wajipange na ushauri ambao wako huko bila elimu umuhimu wa kurudi nyumbani. Enough is enough tunahitaji mabadiliko na mitazomo mipya ya kimaish bongo. Watu lazima tujufunze kuiga kama wachina na kupeleka technologia nyumbani. Mimi binafsi nilikaa huko Ulaya nakupewa uraia lkn nikaamua kurudi bongo sasa natengeneza pesa balaaa... huezi amini naondoka mpaka milioni 10 kwa mwezi na ninachokifanya ni very genuine (Nafanya maintance kwenye makommputa systems, coding, auto machines) mtu asikudanganye pesa ipo hapa Bongo. Magharibi mnabanwa sana na kuzaulika sana(slaves)!!!! Mibaridi kali, ubaguzi na mengine mengi licha ya kufaidi vichache. Maisha nini kama huna raha? maisha yenyewe mafupi kaanini!! USHAURI WA BURE---> Hatakama wewe huna karatasi au unalo lkn umelostika jifunze Coding/programming language huuitaji shule wala mwalimu, unachohitaji Computer na internet pia kujijengea mazoa ya kusoma. Elewa vizuri programming language kisha ibuka zako bongo. Asikuambie mtu aiseee.... pesa ipo... siunajua ICT ndo inaanza bongo? Pesa ipo hapahapa.... ukiendea kuogopa kugongwa na pikipiki then utagongwa na subway/metro/tunnelbanna hahah.... maisha ni risk popote...... Angalieni sana kuko kuna mikansaa... umeme wao ni wa nuclear broo.. mavyakula yao ni yamakopo.... ndo maana wengi wenu hamna afya!!! Wajanja wanarudi mipumbavu inan'gan'gania.....

    ReplyDelete
  54. AnonymousJune 22, 2012

    hivi mtu anapoandika kwanza hafikirii anaandika nini maana mtoa mada amesema unapata mahitaji muhimu akimaanisha watu wa diaspora na huwezi kuweka akiba yani unachopata hakitoshi na ushauri wake anasema watu washirikiane kimakundi ili kuweka akiba sasa kama kwenye hilo kundi watu hawana uwezo wa kuweka akiba wanatumia kny mahitaji muhimu tu hiyo akiba itawekwa vp na hao wanavikundi?????
    je kitu kingine hao wanaopata tabu wanaishi kwa status gan?mwanafunzi?mpewa uraia?kuishi kinyume cha sheria?

    ReplyDelete
  55. AnonymousJune 22, 2012

    Pesa za wa-Tanzania (shilingi) zilizowekezwa nchi za nje ili kuepuka ulipaji kodi, ni lazima zirudishwe. La sivyo, wafadhili wa geni wa bajeti watagoma. Hii ni siri kubwa. Wamo mbioni kugoma. Hawaoni kwa nini wafadhili budget ya Tanzania na huku wa-Tanzania wanaiba na kuficha pesa zao nchi za nje!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  56. AnonymousJune 22, 2012

    Mdau Asante kwa mada hii.
    Mimi niko ulaya na maisha yangu si mabaya. Nadhani walengwa ni wale wanaojilipua. Watanzania wanaojifanya Wakongo na Waburundi ili wapate asylum. Wale waliofika miaka ya nyumba kabla ya misukosuko ya uchumi na kutanuka kwa ulaya mambo yao si mabaya. Kwa ufupi kama Mtanzania anakipato chake na uwezo wa kumudu maisha basi afurahie Maisha yake kama kazi. Kama mtanzania yuko detention au anajificha akiona wenzie kwa sababu anadai yeye ni mkimbizi basi afikirie kurudi nyumbani.
    Kuhusu kushirikiana na kuchangia gharama kama Rent mimi naona ni uamuzi wa mtu binafsi. Nina fahamu watanzania walioamua kuishi pamoja kubana matumizi wakaishia kuaibishana na kuripotiana polisi. Na hakuna wanachopenda polisi wa huku kama ugomvi wa nyinyi kwa nyinyi. Mimi niko radhi nilipe hela nyingi niishi kwa raha bila karaha kuliko kujitia wasiwasi ili kubana matumizi.
    Kuhusu Tanzania mimi narudigi kila mwaka kusalimia ndugu na jamaa. Mambo mengi yanazidi kuwa mabaya nilikuja mwaka jana July-August na kulikuwa hakuna umeme maeneo mengi tu ya Dar na Arusha. Maji hakuna, mafuta ya magari ilikuwa foleni, bei za kubabaisha watu wenye magari wakaanza mambo ya vidumu (hatari tupu). Majengo yanazidi kuchakaa, biashara zimechukuliwa na wageni. Hizo shule za english medium zingine utapeli mtupu shule hata choo hakuna. Yeyote aliyeko nje mwenye maisha mazuri akiamua kurudi nje iwe ni uamuzi wake. Kama hujazoea foleni benki, hospitali, Sheli, basi fikiria kwanza. Kama una watoto ni bora wapate elimu kwanza ukirudi umestaafu unakula pensheni. Rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma vinakatisha tamaa. Halafu kuvunjiana majumba, kuibiana. Matapeli wanauza nyumba na viwanja vya watu bila aibu. Huku ulaya huuziwi kanyaboya. Kama ni gari au nyumba mauziano yanafanyika kisheria hakuna mambo ya karata tatu serikalini.

    ReplyDelete
  57. AnonymousJune 23, 2012

    WEWE MDAU MTOA MADA HII HUNA AKILI TENA PUMBAFU WA MWISHO WEWE.UNATAKA TULIOKO NJE TURUDI TANZANIA UTATU AJIRI WEWE?NENDA SHULE KAPUNGUZE HUO USAHA KICWANI YOUR AN IDIOT MAN YOU FOOL.LONDON YES YES YES YES.BONGO NO NO NO MAN.

    ReplyDelete
  58. AnonymousJune 23, 2012

    better uzaliwe mbwa au paka huku ulaya kuliko binaadam huko nyumbani.upande bifsi kuna kurogana kusikokua na mpango.kuchukiana.majungu.na upande wa serekali zetu kila kitu ni rushwa unafikiri nani atarudi huko.naikiwa umepata bahati mbaya labda umefiwa au umeamua kwenda nyumbani kidogo.ktk airport zetu wewe mbongo unatolewa rushwa wageni wanapita kama kwao.JEWS UBATAN

    ReplyDelete
  59. AnonymousJune 23, 2012

    Nimetoka Tanzania wiki tatu zilizopita .... acheni kudanganya watu, bongo hali ni mbaya!!
    Watu wapo hoi halafu wana madharau ya hali ya juu.
    Kama una watoto majuu, wakuze hukuhuku.Mleta mada ni aina ya watu ambao mawazo yao ni mgando, kama umezaliwa kibondo isiwe sababu ya wewe kufia kibondo.
    Get a life dude!!

    ReplyDelete
  60. AnonymousJune 23, 2012

    wewe uliyesema watu wanajilipua ulaya huna lolote kwanza unawaonea wivu, wewe unanini?zaidi kuchakaa kubeba box?waliojiandikisha wakimbizi wanamajumba makubwa pesa kila wiki bila jasho,wewe mpaka ukabebe box,angalia ulivyo chakaa mshenzi wewe.

    ReplyDelete
  61. AnonymousJune 23, 2012

    Naomba jamani mtuache sisi tulioamua kuja ulaya kutafuta elimu na maisha.Kwanza tuache tu unafiki wewe hapo uishie Dar wakikwambia urundi kwenu Sumbawanga utarudi?au ndio unafiki hata Mungu hapendezwi nao.Mimi niko ulaya napiga box na shule naenda na G.P.A kali ya kuweza kufanya kazi kwenye kampuni za maana kwa ufupi sina wasi wasi kabisa na maisha baada ya shule.Kuhusu,kurudi bongo haiitaji kuwa mwanafilosofia kuelewa kwani watu hawataki kurudi bongo,fikiria wewe ni mzazi umemleta mtoto wako ulaya kusoma na umelimepa gharama zote mwenyewe bila msaada wa bodi ya mikopo,kisha baada ya shule utamshauri mtoto wako arundi bongo akalipwe mshahara wa bei ya chini kuliko hela alizotumia kusomea,ukweli ni kwamba hata kwenye biashara haiwezi tokea,ushauri bora utakao mpa mwanao ni kwamba mwanangu nimekupa elimu yakimataifa unaweza kufanya kazi popote Duniani pale penye kulinga na ubora wa elimu yako.Pili nikwamba hawa watu wanaopiga kelele watu warudi bongo hawajui wanachokiongea wengi wao hata ulaya hawapajui na kutokana na kutokuwa na tafsiri halisi ya maisha ya ulaya wengi hasa walioko nyumbani wanafikiria maisha ya ulaya ni magumu na wapiga box niwengi kuliko wenye kazi nzuri,hii inachangia kutowapa motisha vijana wanyumbani wenye hamu ya kupata mafanikio maishani kkujaribu bahati zao nje ya nchi.Tena mimi naona nyiyi mlioko nyumbani mshukuri sana wasomi walioko nje waendelee tu kuwa nje kwasababu na hii serikali yetu na uchumi wetu ulivyo sio imara hii inasababisha kutokuwepo kwa ajira na kama ukitaka madiaspora warundi nyumbani kushinda na wazawa ,wazawa wata poteza ajira zao pia utakakuwa unatafuta ghasia za siasa,mimi naona serikali ijiimarishe kwanza ndio hizi habari za diaspora zizungumzwe.Kwa mimi nitarudi bongo kwa lazima kama seriakli ikisema itanirudishia gharama zote nilizotumia kuishi ulaya kipindi cha masomo yangu,wakija dili kama za hivi mbona watarudisha wasomi wengi nyumbani.Sasa ninyi mnaolalamika wa nje warudi ndani huu ni muda waku ishikia bango serikali kuboresha maisha kwa kila mtanzania.

    ReplyDelete
  62. AnonymousJune 24, 2012

    Hivi nyinyi mbona mnawakomalia watu walio huku nje warudi. Mbona nyinyi hamtoki huku dar au mjini mkarudi vijijini. maana yake ni kuniambia mimi nirudi one step behind. Maisha popote guys either ughaibuni au bongo na kurudi nyumbani ni plans zangu kama mambo yako sawa huku that's fine lakini everybody should mind their own business na mpunguze mizinga na kuomba kununuliwa vitu huku mtafikiri mmewekeza hela. Watu hawaokoti hel huku na hela inaenda kwa mipango kama life zuri bongo endeleeni kufurahi huko si tutakuja kusalimia na kurudi na nyie mkiweza karibuni

    ReplyDelete
  63. na pia walioko vijijini naokufa bila kupata matibabu na maji salama msisahau kuwachukua bongo mjini na wao wakatajirika wakaingiza hayo mamilioni na wakajenga majumba makubwa maana shida haiko ulaya tuuu maana hiyo misaaada mnayopewa inatoka huku huku tulipo ulaya mnaosema kuna shida sijasikia hata siku moja tanzania imewapa msaaada usa. uk, au ulaya yoyote msaaada japo msaada wa nazi na dagaaa wa kigoma, pumbavu nyiee mlidhani mkisikia kazi ya box ndo kama box wanalobeba wamachingaa pale kariakoo huku box ni la simu sio box la tofali

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...