Turn off for: Swahili
Mwenyekiti wa chama cha madereva wa wabunge Bw Juvenille Joseph akizungumza na madereva hao leo nje ya viwanja vya bunge
Madereva wa wabunge wakiwa wameshikana mikono kuonyesha mshikamano wao katika kutetea mikataba yao

Na Francis Godwin,Dodoma
MADEREVA wanaowaendesha wabunge wawalipua wabunge hao wadai wanafanya kazi bila mikataba ya kazi huku wakilipwa posho kidogo wawafananisha wabunge na mafisadi .
Madereva hao wamesema kuwa wabunge wamekuwa mbele kutetea madereva wanaofanya kazi hiyo hapa nchini kupewa mikataba wakati kwa upande wao wabunge hao wamekuwa wakiendelea kuwafanyia ufisadi kwa kutowalipa fedha zao wala kuingia mikataba ya kisheria.
“Wabunge wetu wanaongoza kwa kuikosesha serikali mapato yake na ajira kwa vijana kupungua kutokana na baadhi yao kushindwa kutoa mikataba ya kazi wala kuwalipa mishahara ambayo serikali kupitia bunge ilipendekeza kwa ajili ya madereva wa wabunge toka mwaka 2008 .
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi mjini Dodoma leo  madereva hao walisema kuwa mbali ya wabunge hao kuendelea kuhubiri juu ya ajira kwa vijana na maslahi ya madereva ila wameshindwa kabisa kuwalipa madereva wao misharaha inayotakiwa kulipwa na badala yake fedha zinazotolewa kwa ajili ya madereva na bunge zimekuwa zikichukuliwa na wabunge hao na wao kuishia kuwalipa posho isiyowawezesha kuendesha maisha yao.
Kwani walisema kuwa sehemu kubwa ya wabunge hao wameanza kuendesha magari yao wao wenyewe baada ya kushindwana na madereva waliokuwa wakiwaendesha awali baada ya kushindwa kuwalipa mishahara na posho zilizobainishwa kisheria na ofisi ya bunge.
Hata hivyo walisema kuwa suala hilo la wabunge kushindwa kuwalipa vizuri madereva si kwa wabunge wa CCM pekee bali ni wabunge karibu wote wakiwemo wa vyama vya upinzani ambao baadhi yao kwa sasa wanajiendesha wenyewe baada ya kukimbiwa na madereva wao kwa kushindwa kuwalipa.
Pia walisema matukio ya ajali kwa wabunge yamezidi kuongezeka kutokana na wabunge hao kushindwa kufanya kazi na madeva na kuishia kuifanya kazi hiyo wao wenyewe na matokeo yake kutokana na mawazo ama kuwa na mambo mengi kichwani wamekuwa wakishindwa kuyamundu magari yao na kuishia kusababisha ajali za barabarani ambazo baadhi ya ajali hizo zimekuwa zikisababisha vifo ama ulemavu kwa wabunge hao.
“Leo ukitazama hapa bungeni Dodoma utaona idadi kubwa ya wabunge wanajiendesha wenyewe kama si mbunge kuwaendesha wenzake basi mbunge amekuwa akijiendesha mwenyewe na wapo wanaokuja na madereva hadi hapa Dodoma na baada ya hapo dereva amekuwa akipewa nauli ya kurudi jimboni na mbunge anaendelea kujiendesha mwenyewe kama njia ya kubana matumizi “
Aidha walisema kuwa miongoni mwa madereva waliokosa ajira ni pamoja na wale waliokuwa madereva wa mawaziri na manaibu mawaziri ambao hawakurejea tena baada ya Rais Jakaya Kikwete kutangaza mabadiliko ya baraza la mawaziri hivi karibuni ambapo mawaziri hao kwa sasa wamegeuka kuwa madereva wenyewe.
Makamu mwenyekiti wa chama cha madereva wa wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Adam Said alisema kuwa sababu ya wabunge wengi kukimbiwa na madereva ni kutokana na maslahi duni wanayoendelea kulipwa na kuwa hivi sasa baadhi ya wabunge baada ya kukimbiwa na madereva wamelazimika kuwatumia ndugu zao kama njia ya kukwepa kuwalipa mishahara .
Pia alisema maisha ambayo madereva hao wamekuwa wakiishi mjini Dodoma ni heri ya omba omba kutokana na wabunge hao kuwalipa kiasi cha shilingi 50,000 ama chini ya hapo na kutaka kuitumia kwa muda wa wiki moja ama mwezi mzima jambo lililopelekea madereva hao kupanga vyumba mtaani na kuishi katika chumba kimoja zaidi ya watatu kama sehemu ya kubana matumizi.
Mwenyekiti wa chama cha madereva wa wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Juvenille Joseph alithibitisha madaia ya madereva hao na kuwa tayari uongozi wake umefikisha malalamiko ya madereva hao katika ofisi ya chama cha wafanyakazi mkoa wa Dodoma pamoja na ofisi ya spika wa bunge Anne Makinda ili kushughulikia madai hayo.
Alisema kuwa kwa sasa wanakusudia kuitisha mkutano wa dharura wa madereva wote wanaowaendesha wabunge ili kuweza kuwa na msimamo wa pamoja katika kupigania haki zao na baada ya hao watawatumia barua wabunge ambao wanajiendesha wenyewe ili waweze kujiunga na chama hicho cha madereva wa wabunge .
Kwani alisema kuwa katika barua iliyotolewa na ofisi ya bunge Novemba 3 mwaka 2008 barua yenye kumbukumbu namba FA.155/206/01/70 ikiwa na kichwa yahusu posho ya ubunge Malimbikizo July –Octoba 2008 ilibainisha posho na mishahara hiyo.
Joseph alisema kuwa posho ya mafuta lita 1000 kwa lita shilingi 2500 kwa wakati huo ilikuwa ni kiasi cha shilingi milioni 2.5 kwa mwezi , Matengenezo yagari asilimia 40 ya thamani ya mafuta ambayo ilikuwa ni milioni 1 kwa mwezi , posho ya dereva siku 10 kwa shilingi 30,000(vijijini ) ilikuwa ni shilingi 300,000 na posho ya mbunge siku 10 kwa kila atakazokuwepo kijijini kwa kila siku shilingi 45,000 ilikuwa ni shilingi 450,000 huku mshahara wa dereva kwa mwezi ulikuwa ni shilingi 100,000 na kufanya jumla kwa mwezi kuwa bajeti ya shilingi milioni 5,115,000 kwa wakati huo.
Ila pamoja na sasa posho za wabunge kupanga ila bado wabunge wamekuwa wakiwalipa madereva wao kiasi cha shilingi 70,000 hadi 90,000 kwa mwezi fedha ambazo haitoshi kwa maisha ya sasa hivyo kutaka fedha za madereva kuingizwa katika akaunti zao na madereva wote wa wabunge kuwa na mikataba ya kazi badala ya kuendelea kufanya kazi kirafiki na kindugu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Che GuevaraJune 22, 2012

    Hakya Mbongo! Hii kali! eh! ama kweli ukishangaa ya SUMATRA na Mikataba ya madereva utaona ya WABUNGE na madereva wao!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 22, 2012

    Kwa nini Mbunge uendeshwe? Wabunge waendeshe wenyewe. Huu ni umwinyi wa hali ya juu. Wabunge ambao ni mawaziri inaeleweka wao waendeshwe. Mbunge kama anaona hawezi kuendeshe mwenyewe basi aaijiri dereva na makubaliano yawe kati yake na dereva na wa la siyo tatizo la serikali.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 22, 2012

    Hao ndio waundaji wa misumeno ya TZ nyuma ya pazia.waache sasa uwakate wenyewe nyuma na mbele kwereza.

    kazeni butu madereva.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 22, 2012

    Kwanini wabunge wanahitaji maderva??? Kwani wao ni vilema? Kwanini wasiendeshe wenyewe?? Niutumwa na kundekeza uzembe kuwaendesha wabunge.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 22, 2012

    Mpaka kieleweke!

    Haiwezekani wewe Dereva uendeshe Toyota VX-V8 la thamani ya Tsh. 200 Milioni, yeye Bosi wako anavuta Mamilioni halafu wewe Mshahara wako usizidi Tshs. 100,000/=

    ????

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 22, 2012

    Kweli bongo tumelala. Serikali inalipa mshahara wa mbunge na wa dereva wake? Kwani hao wabunge wasiendeshe magari yao wenyewe? Magari wapewe bure, mafuta bure, na hata mtu wa kuliendesha ni bure??? Kazi ya mbunge ni nini hasa zaidi ya kutetea mifuko yake. Hii inakasirisha sana kuona waliowachagua watoto wao wanashindwa kwenda shule wakati wabunge wenyewe kila kitu kwao ni bure.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 23, 2012

    Wachilia mbali MBUNGE TANZANIA kuendesha gari mwenyewe,tunasikia RAISI KAGAME WA RWANDA ANAENDESHA GARI MWENYEWE!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...