THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Matukio katika Msiba wa willy Edward

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts Limited, inayochapisha gazeti la Jambo Leo na jarida la Jambo Brand Tanzania, Juma Pinto (kushoto) na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Benny Kisaka (wa pili kushoto) wakiwa kwenye msiba wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa Jambo Leo, marehemu Willy Edward Ogunde ulioopo nyumbani kwa kaka wa marehemu Mburahati, Dar es Salaam leo asubuhi. Wiily amefariki ghafla leo alfajiri mjini Morogoro alikokuwa akihudhuria semina ya siku moja ya masuala ya Sensa. Kutoka kulia ni ndugu zake marehemu; Dennis Ongiri, Joseph Rabach na Julius Rabach.

Waandishi wa habari wa gazeti la Jambo Leo na Jarida la Jambo Brand Tanzania wakishiriki kwenye msiba wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, marehemu Willy Edward. Mwili wa marehemu Willy unasafirishwa mchana huu kutoka Morogoro kwenda kuhifadhiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam. Taratibu za mazishi zinaendelea kuratibiwa kwa ushirikiano wa ndungu na viongozi wa Jambo Concepts, lakini kwa mujibu wa Kaka wa marehemu Rabach ni maaishi yatafanyika nyumbani kwao marehemu, mjini Mugumu Wilaya ya Serengeti, mkoani Mara. Siku ya mazishi itatangazwa baadaye.


Mjane wa marehemu Willy Edward, Rehema, akiwa kwenye majonzi

Akina mama waombolezaji wakiwa kwenye msiba

Mpiga picha wa TBC, Mary Hondo, akimfariji Rehema. 

Mtoto wa mwisho wa marehemu, Willy Edward, Caren akiwa katika msiba

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts Limited, inayochapisha gazeti la Jambo Leo na jarida la Jambo Brand Tanzania, Juma Pinto akihojiwa na Grace Kingarame wa TBC katika msiba huo. 
(PICHA ZOTE NA  KAMANDA WA MATUKIO)


Kuna Maoni 2 mpaka sasa.

  1. Anonymous Anasema:

    Eee Mwenyezi Mungu ninakuoma umpe nguvu Dada Rehema katika kipindi hiki kigumu. Amina

  2. HK Anasema:

    "INNA LILLAHI WAINNA ILAYHI RAJIUN" Poleni sana ndugu jamaa na marafiki wa marehem, pole sana mjane na watoto wa marehem wote, Mwenyeez Mungu awape nguvu na kuwajaaliya subira, uvumilivu na faraja, khasa katika wakati huu mgumu wa maombolezo. Maskini huyo mwanawe wa mwisho, pengine hata hajuwi kilichotokea wala kinachoendelea hapo. Pole sana "cute" Mola akulinde, akukuze kwa salama na amani, akujaaliye kila lililo jema na akunusurishe na mabaya yote - AMEN.