Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts Limited, inayochapisha gazeti la Jambo Leo na jarida la Jambo Brand Tanzania, Juma Pinto (kushoto) na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Benny Kisaka (wa pili kushoto) wakiwa kwenye msiba wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa Jambo Leo, marehemu Willy Edward Ogunde ulioopo nyumbani kwa kaka wa marehemu Mburahati, Dar es Salaam leo asubuhi. Wiily amefariki ghafla leo alfajiri mjini Morogoro alikokuwa akihudhuria semina ya siku moja ya masuala ya Sensa. Kutoka kulia ni ndugu zake marehemu; Dennis Ongiri, Joseph Rabach na Julius Rabach.

Waandishi wa habari wa gazeti la Jambo Leo na Jarida la Jambo Brand Tanzania wakishiriki kwenye msiba wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, marehemu Willy Edward. Mwili wa marehemu Willy unasafirishwa mchana huu kutoka Morogoro kwenda kuhifadhiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam. Taratibu za mazishi zinaendelea kuratibiwa kwa ushirikiano wa ndungu na viongozi wa Jambo Concepts, lakini kwa mujibu wa Kaka wa marehemu Rabach ni maaishi yatafanyika nyumbani kwao marehemu, mjini Mugumu Wilaya ya Serengeti, mkoani Mara. Siku ya mazishi itatangazwa baadaye.


Mjane wa marehemu Willy Edward, Rehema, akiwa kwenye majonzi

Akina mama waombolezaji wakiwa kwenye msiba

Mpiga picha wa TBC, Mary Hondo, akimfariji Rehema. 

Mtoto wa mwisho wa marehemu, Willy Edward, Caren akiwa katika msiba

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts Limited, inayochapisha gazeti la Jambo Leo na jarida la Jambo Brand Tanzania, Juma Pinto akihojiwa na Grace Kingarame wa TBC katika msiba huo. 
(PICHA ZOTE NA  KAMANDA WA MATUKIO)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 17, 2012

    Eee Mwenyezi Mungu ninakuoma umpe nguvu Dada Rehema katika kipindi hiki kigumu. Amina

    ReplyDelete
  2. "INNA LILLAHI WAINNA ILAYHI RAJIUN" Poleni sana ndugu jamaa na marafiki wa marehem, pole sana mjane na watoto wa marehem wote, Mwenyeez Mungu awape nguvu na kuwajaaliya subira, uvumilivu na faraja, khasa katika wakati huu mgumu wa maombolezo. Maskini huyo mwanawe wa mwisho, pengine hata hajuwi kilichotokea wala kinachoendelea hapo. Pole sana "cute" Mola akulinde, akukuze kwa salama na amani, akujaaliye kila lililo jema na akunusurishe na mabaya yote - AMEN.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...