Mcheza Sinema Deidre Lorenz (shoto) akiwa na 
Rais wa IBF-USBA Afrika Masharini na  Kati
na Ghuba ya Uajemi,Onesmo Ngowi.
Mcheza sinema toka Nchini Marekani Deidre Lorenz (BOFYA HAPA UMJUE) amewasili mjini Moshi tayari kushiriki kwenye mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon zitakazofanyika juni 24. Lorenz amewasili leo na ndege ya Ethiopian Airlines ambao ndio wafadhali wa mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon zinazofanyika jumapili ya mwisho ya mwezi wa sita kila mwaka.

Ujio wa Lorenz ambaye amecheza sinema nyingi zikiwamo Santorini Bule, Perfect Strangers, The Big Fight umeleta msisimko mkubwa katika mji huu mkuu wa Kilimanjaro. Ujio wake umefuatia matayarisho ya muda mrefu ambayo yanaendana na hadhi yake.

Akizungumza na waandishi wa habari waliofika kumshuhudia mcheza sinema huyu, Lorenz alisema kuwa ameisikia kuwa mlima wa Kilimanjaro uko Kenya kwa kwa muda mrefu na ana furaha kubwa sana ya kufika ili kushughudia kuwa mlima huu maarufu duniani uko Tanzania.

 “Nimekuwa nautangaza sana ujio wangu kwenye blog na tovuti yangu, wapenzi wangu pamoja na watu wengi wanangojea kurudi kwangu nikawaambie niliyoyashughudia” alisema Deidre Lorenz ambaye ameshawahi kuteuliwa zaidi ya mara tatu kwa tuzo za Oscar. Lorenz alisema kuwa kwa miaka mingi alifikiri kuwa mlima Kiliamnjaro uko Kenya kwa jinsi nchi hiyo jiraniminavyoutangaza nchini Marekani.

“Sasa nimeona mwenyewe kwa macho yangu kuwa kweli mlima (Kilimanjaro) huu maarufu duniani uko Tanzania na sio Kenya” alisema Deidre Lorenz ambaye anaishi kwenye jiji la New York City linalofahamika kama jiji la pesa (International Financial Capital) la kimataifa. Lorenz ameshukia katika hoteli ya Bristol Cottages iliyopo karibu na benki ya Standard Chattered mkabala na bustani ya Manispaa ya Uhuru Park.

Mji wa Moshi na viunga vyake vinarindima kwa ujio wa watalii wengi kutoka Marekani ambao wamekuja kushiriki kwenye mbio hizi zilizojijengea umaarufu mkubwa kwa kuitangaza Tanzania nchini Marekani. Mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon zilianzishwa na Marie Frances mwaka 1991 baada ya kuombwa na balozi wa zamania wa Tanzania nchini Misri.

Mbio hizi zimejijengea umaarufu mkubwa na zimeshawahi kupata tuzo nyingi baadhi zikiwa zimetolewa na Wonders of the World Magazine lenye wasomaji zaidi ya milioni 5 likiwa limezipa nafasi ya 2 kama mbio zenye hadhi ya kukimbiwa duniani wakati jarida la Forbes la Marekani lenye wasomaji wengi duniani limeipa nafasi ya kwanza. Ndio maana Manispaa ya Moshi itampa barabara na kuiita “Marie Frances Boulevard”mwaka 2009.

Mbio hizi hukimbiwa na watalii wa Warekani wanaokuja Tanzania kupanda mlima Kilimanjaro na kutembelea mbuga za wanyama. Mt. Kilimanjaro Marathon zinajulikana kama 7 continental races zikiwa zinakimbiwa katika mabara 7 ya dunia.

Ratiba ya Deidre Lorenz inaonyesha kuwa kesho ijumaa atakitemnbelea kituo cha watoto yatima cha Upendo kinachoendeshwa na watawa wa Precious Blood. Lorenz atakaa na watoto hao na kuwasomea hadithi mbalimbali za watoto zilizoandikwa na Waltz Disney mwandishi maarufu wa karne ya ishirini wa Marekani.

Siku ya jumamosi atatembelea hospitali ya KCMC ambapo atakutana na manesi ili kuwapa shavu kwa kazi yao nzuri wanayoifanyia jamii. Jioni ya jumamosi atahudhuria Pasta Party ambapo atapata nafasi ya kukutana na wakimbiaji wengine na kuchagua namba ya kukimbia kesho yake siku ya jumapili tarehe 24 juni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 22, 2012

    Naona Bwana Mkubwa kambana huyo binti mpaka anasimama pembezoni mwa pavement. Cultural difference, wenzetu wana kitu kinaitwa personal space kwa kawaida ni urefu wa handshake, zaidi ya hapo unamfanya mwenzio kuwa uncomfortable:-) kama mkiwa wengi personal space haifanyikazi lakini mkiwa wawili hiyo ni lazima hata mkiwa ndani ya elevator hakikisha unaacha hiyo personal space:-)

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 22, 2012

    Bora tu aje ajionee maana inasikitisha wizara ya utalii imetulia haitangazi ipasavyo vivutio vya Tanzania. Nilisikitika siku moja nilienda Australia nikakutana na kijana mmoja akauliza vitu gani vya kitalii vipo TZ nikasema kuna Mt.Kilimanjaro akasema no that is in Kenya daah niliishiwa pozi nikamfafanulia akashangaa sana. Viongozi jitahidini jamani nchi yetu ina vingi vya kujivunia vitangazeni siku hizi utandawazi mkubwa ni rahisi sana

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 22, 2012

    TANZANIA IMEZUBAA TANGU ENZI HIZO WANAKUBALI TU HATA KUJITETEA KUPINGA TMATANGAZO YA KENYA KUWA MLIMA KILIMANJARO UKO KENYA MPAKA LEO SIJUI WATANZANIA TULIROGWA ILI TUKAE KIMYA WENZETU WANAUTUMIA KWA KUJINUFAISHA NA SISI WATANZANIA TUNAKUFA NA NJAA DOLLERS ZOTE ZINAANZIA KUTEREMKA KENYA HALAFU SISI NDIO TUNAPEWA VISENTI . INA MAANA KENYA WALITUZIDI AKILI MPAKA LEO?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 22, 2012

    Hiyo hadithi ya mlima kilimanjaro uko kenya naona imeshapitwa na wakati sasa. Mwambie mtu atafute kwenye google. Nashangaa sana kwa miaka hii kudhania landmark ya nchi yoyote iko nchi nyingine ni uvivu wa kufikiria.
    Nawakilisha.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 22, 2012

    sidhani kama ni maarufu, mnakuza tu mambo

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 22, 2012

    Weka na za yule bwana asiye na miguu aliyepanda mlima kilimanjaro hadi kileleni.

    http://www.ctv.ca/CTVNews/CanadaAM/20120619/spencer-west-reflects-on-kilimanjaro-summit-experience-120619/

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 22, 2012

    Yaani wizara ya utalii inashindwa kujitangaza sawawa maliasili zetu kweli hata hiyo inawashinda au mawazo yenu nikuchukua chako mapema? Jinga you kabisa

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 22, 2012

    Huyu si maarufu wala nini, hata yeye mwenyewe anashangaa mnavyomkweza.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 22, 2012

    Hahaha! Hata huyo dada mcheza sinema hajui kuangakia Google map hadi asafiri kote huko kwenda Kilimanjaro TZ halafu arudi kwao kuwahakikishia wenzake! Msilete utani hapa.

    Hata ingalikuwa miaka ya arubaini na saba basi ukisoma ramani utaelewa tu. Ibaki kuwa njaa za kenya tu na ubwege wa TZ.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 22, 2012

    Mhe.Ngowi akitekenya tekenya anaweza ubeba mzigo huo !

    ...distance gani tena?

    Si mnajua tena?,,,kuku hawa wa kisasa maharage ya Mbeya maji mara moja!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...