Michu,
 February nilitembelea Morogoro vijijini nikakuta shule ya kata inayoitwa Mdokonyole Primary School ina watoto karibu 200 na madarasa mawili tuu. Darasa moja lilikuwa limekamilika na moja watoto wanakaa chini kwenye magogo sakafuni.Wengine wanasome nje chini ya miti.  

Nilivyorudi Dar nikaamua nifanye kile ninachoweza kama Mtanzania mwenye uchungu na hali ile, nikafungua ukurasa Facebook nikawaomba watu wanisaidie kuweza kuweka sakafu na plaster , mimi nikaanza na mchango wa dollar 100. 

Wengi waliniunga mkono,ndani na nje ya nchini ( wengine diaspora) pole pole tukachangisha Tsh 4,239,000! leo hii watoto wanasoma kwenye darasa lenye sakafu ya simenti, plaster ukutani na kwenye madawati ! 

Hivi sasa tunatengeneza mlango na blackboards za ndani na kwa wale wanao soma nje,

Bado tunahitaji kukamilisha madirisha, watoto wanahitaji vitabu , waalimu vitabu vya muongozo, viatu, mabegi ya shule na kikubwa zaidi kujenga madarasa 5 na ofisi ya waalimu na vyoo. Pale tunapoweza kusaidia tunachangia na pamoja tunaweza, huu ni mfano mdogo tuu lakini umeleta mabadiliko makubwa na hamasa . 

Tembelea kurasa ya Action Tanzania kwenye Facebook ...
Get involved and make a difference - because you can!

Mdau SS

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 11, 2012

    Mkubwa na kushukuru na na kusifu kwa kufanya kitu ambacho wengi wetu hatutaki kufanya au tunajifanya kana kwamba hatuoni. cha msingi tu mkuu, jaribu kufanya dizaini ya madarasa yenye gharama nafuu. Hii picha hapa inaonyesha darasa hili limegharimu zaidi pasipo sababu, kwanza ,umetumia tofari za choma ambazo zinatumika nyingi na simenti nyingi sana inatumika kwa ujenzi huu. Kumbuka kwamba mfuko mmoja wa simenti unaweza kukupa tofari 35 imara sana na zikijengwa na fundi mzuri ,basi hata plasta siyo lazima. kingine ninachokiona kwenye picha ni madirisha yako ni makubwa mno na yako juu sana ,pia kuta zako ni ndefu mno pasipo sababu, je hao watoto watarefuka zaidi ya futi 5 au 6 ??? kwa kuupunguza urefu wa kuta zako ,utaokoa tofari,simenti,bati,na muda. Obeja baba. wako Zebedayo ,mna Badugu. Jamani tuchangieni mada kama hizi. Cha ajabu ,punde kukionekana -Ukristo na uislam -mama yangu weee,paka na panya-yaani umechokoza nyuki. Hebu elimikeni.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 11, 2012

    Napenda nimpongeze saaaana mdau aliyeona kero na mapungufu ya serikali na akaweza kuhukua hatua binafsi na kufanikisha kiasi hicho. hongera sana na naomba tuendelee, sisi tumetoka kuhangia millioni 50 kwa ajili ya mambo yanayowagusa wasiojiweza. ILA Mdau aliyetangulia 05:01:00 napenda nimfahamishe kuwa madarasa ni muhimu sana yawe makubwa ya kutosha na ceiling height kuwa ndefu ili room size iwe kubwa. pia madirisha yanahitajika kuwa makubwa hata zaidi na yawe chini. wanafunzi wanahitaji hewa ya Oxygen yakutosha kuweza ubongo kufanya kazi. kwa hiyo huo ni upungufu wa ufahamu wa mdau. ila sina uhakika na research yake kuwa kujengea matofali ya cement nirahisi kuliko ya kuchoma. Naamini kuwa kama ni kijijini wanachimba udongo na kuchoma wenyewe. ILA amenishtua na kusikitisha sana alipoingiza udini??? katika swala muhimu kama hili.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 11, 2012

    DUH !!!! yale yale . Huo ubongo unaohitaji oxygen yote hiyo,basi utakuwa umelala kama maziwa mtindi, kingine ,hata mimi nashangazwa sana na hao watu wanaokimbilia kuitoa maoni ya Udini,ndiyo maana nikalikataa jambo hilo-sasa wewe umeshitushwa na nini ??? au hukunisoma vizuri na kunielewa point yangu-hata wewe ulipoliona neno dini tu-hapo hapo ukashambulia ,ndo wale wale !!!! kingine , tembea uone mengi ,mimi nimekupa dizaini za madarasa za nchi nyingine -wenzetu wanavyojenga na oxygen imo madarasani na wanafunzi wanafaulu hadi kunyakua PHD,kipimo mtu mzima ukisimama ukinyosha mkono unagusa kwenye ceiling. Kingine tofari za choma zinazofyatuliwa huko vijijini, wengi huwa hawazingatii udongo gani,maadam ni mwekundu basi twende kazini,matokeo yake ni hafifu sana na baadaye zinahitaji simenti nyingi sana ya kujengea na muda mwingi . Nafikiri nimekusaidia .Asante,nipo bado jaribu tena.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...