Kama ilivyo kawaida kwa wataalamu wa masuala ya habari na kijamii wa mtandao wa MO BLOG unaotisha kwa sasa, Mhariri Mkuu wa Mtandao huo Lemmy Hipolite na Meneja Mipango Zainul Mzige ‘hamad’ uso kwa uso na mtangazaji maarufu wa Radio na Televisheni hapa nchini Millard Ayo.

MO BLOG: Kitu kingine ambacho MO BLOG ingependa kufahamu ni kuondoka kwako ITV, fununu zinasema kuwa ulikuwa ni mtiti, ni ya kweli haya?

MILLARD AYO: Ningependa watu wakifahamu ni kuwa mimi sina ugomvi na ITV wala sikuondoka kwa ugomvi.Kwanza kufanya kwangu kazi ITV naamini Mungu alikuwa anaona na alipanga ndio maana hata hivi sasa kuna uwezekano kuwa nafasi nyingine nilizo nazo maishani kwangu nisingezipata, pengine hata ‘Clouds’ wasingeniona na wasingenifuata.ITV ndio ilimtambulisha Millard Ayo.

ITV niliondoka vizuri ndio maana nitawaheshimu na nitazidi kuwatangaza vizuri popote nitakapokwenda.Kwa sasa hapa ‘Clouds Radio’ nafanya show yangu ya ‘Amplifaya’ ambayo ina sehemu inayohusisha Blogs, Facebook na Twitter. Katika kipengele hicho nasoma sana habari zao wanazo zi’tweet’ na nasema nimezitoa ITV. Kusoma mahojiano yote Bofya Hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 18, 2012

    "BOFYA HAPA" hapabofyeki hapo yaani hamna link hapo.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 18, 2012

    Sasa Milard Ayo sawa,

    Kama unatuhakikishia kuwa umeondoka vizuri sehemu yako ya kazi ya zamani,unasema pia utawatangaza vizuri kokote hizo ni DALILI NZURI KUWA huna kinyongo na mtu wala nia mbaya dhidi ya yeyote!, ila hizo TWEET kutoka sehemu yako ya awali ya kazi ndio vipi tena?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 18, 2012

    Millard ukumbuke Msemo wa Kiswahili ya kuwa 'mtumikie kafiri upete mradi wako'!

    Bepari anapopata ng'ombe wa kukamua maziwa ng'ombe akichomoka hivi Mchungaji wa ng'ombe au mwenywe Bwenyenye kama awali ataweza kulala usingizi?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 18, 2012

    Millard Ayo umesahau waliokutangulia jinsi walivyoondoka ktk Shirika hilo hilo?

    1.Kundi la Ze Comedy ?
    2.Jerry Muro ?
    3.Na Wanahabari kibao ?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 18, 2012

    Milard Ayo,

    Shirika la Kichagga hilo,ulimuuliza mama Razia Khan akueleze?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 19, 2012

    Jamani punguzeni choko choko. Hana haja ya kukashifu sehemu iliyomfanya kufika hapo alipo ni sehemu ya maisha. Millard anaweza hitaji information muhimu sana kwa future plan yake kutoka management ya ITV,ivi akianza kuongea ovyo itamsaidia nini!!!!! naamini kila shirika lina mapungufu yake na kila mtu anaustarabu wake. Cha msingi ni kusonga mbele na kuchukua mazuri unayojifunza, mabaya unawaachia wahusika. direct Advise always appreciated. millard kuwa strong na choko choko,usiongee,nothing will change from your life. Goodlucky on your way forward.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 19, 2012

    Big up bro.. una God Fearing the most I like from you. Shut your mouth and step forward.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...