Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam, Dkt Paul Msemwa akielezea Mafanikio ya Maradi wa ICT unao fadhiliwa na SPIDER uliopo Makumbusho.
Mratibu wa Miradi inayo fadhiliwa na SPIDER nchini Bw Theophilus Mlaki akifafanua jambo katika mkutano na viongozi wa Miradi hiyo.
Wajumbe wa Mkutano na Viongozi wa Miradi iliyo fadhiliwa na SPIDER nchini wakifuatilia maelezo ya Dkt Paul Msemwa.

Na Sixmund J. Begashe wa Makumbusho Tanzania

Miradi iliyo fadhiliwa na Program ya Kiswidish ya ICT katika nchi zinazo endelea (SPIDER) inayoratibiwa na idara ya komputa ya Nchini Sweden, imepata mafanikio makubwa kutokana na usimamizi mzuri wa viongozi wa miradi hiyo, hayo yameelezwa na Mratibu wa Miradi inayo fadhiliwa na SPIDER nchini Bw Theophilus Mlaki alipo kuwa akiwapongeza Viongozi wa miradi hiyo iliyopo hapa nchini katika mkutano wa viongozi hao uliofanyika katika ukumbi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.

Bwana Mlaki ameyataja mafanikio hayo kuwa ni pamoja na madaktari wengi wa wilayani Rufiji kuanzia ngazi ya kata hadi wilaya kupewa elimu ya namna ya kutumia simu za kiganjani kutuma ujumbe kwa akinamama wajawazito kuwakumbushia tarehe zao za kuudhuria tiba na hata kutoa taarifa kwa ngazi zinazo husika pale tatizo linapo shindikana na hatua za haraka kuchukuliwa ili kupunguza vifo vya akinamama hao na watoto, pia ameutaja mradi wa Jua Art Foundation kuwa umefanikiwa kwa kuwaelimisha wananchi wa mikoa mbali mbali nchini juu ya tatizo larushwa na namna ya kuepukana nalo, JAF imeweza kurekodi picha ya video ambayo baadae itaoneshwa katika vituo vywa runinga ili kuwawezesha watanzania wasio pata chanjo hiyo waweze kuipata.

Bwana Mlakini ameongeza yakuwa kwa kupitia mradi wa ICT ulio chini ya Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni umeonesha mafanikio kwa kuwawezesha watoto wakitanzania wanao tembelea makumbusho hiyo kujifunza namna ya kupiga picha , kuziweka katika computer( kuhifadhi kumbu kumbu za matukio mbali mbali), kuwawezesha vijana na watoto wenye mahitaji maalum na wenye vipaji kurekodi muziki na kutengeneza video za muziki ili mahitaji yao yaweze kusikilizwa na walio wengi, pia ameutaja mradi wanne unaoendeshwa na Tume ya Haki za binadamu, kuwa umeshatengeneza software itakayo wawezesha watanzania walio wengi kutuma ujumbe wa simu ya mkononi kuelezea malalamiko yao mbele ya tume na malalamiko hayo kupokelewa kwa mfumo wa computer ambapo uongozi watume utayashughulikia kwa haraka zaidi.

Akiishukuru SPIDER, Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dkt Paul Msemwa amesema kuwa mradi huu utaendelea kuwanufaisha watanzania walio wengi na kutoa wito kwa vijana, watoto na watu wazi, kujitokeza kuitembelea makumbusho na nyumba ya Utamaduni ili kujinufaisha na na mradi huu.

Huu ni mkutano wa Tatu wa Viongozi wa Miradi iliyo fadhiliwa na SPIDER kufanyika ambapo mkutano wa kwanza ulifanyika mwaka 2011. Program hiyo ya SPIDER ya nchini Sweden imesha ifadhili zaidi ya SEK 2,000,000 sawa na Tsh milioni 480 kutekeleza miradi inayohusu ICT na Maendeleo nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 04, 2012

    Hingera sana SPIDER - Sweden kwa kuyajali maisha ya watanzania. Mungu azidi kuwabariki.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...