THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

mkaazi wa bagamoyo adai kuota matiti kwa kutumia arv'sMkaazi wa kijiji cha Magomeni Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani,  Khamisi Tanga (46), ameota  matiti katika hali isiyo ya kawaida ikidaiwa imesababishwa na kutumia dawa za kupunguza  makali ya Ukimwi   ARV’S.
     Akizungumza na waandishi wa habari waliokwenda Wilayani humo kufanya utafiti kuhusu utekelezaji wa sheria ya Ukimwi na Chama cha Waandishi wa habari za Ukimwi (AJAT),Khamisi (Pichani) alisema alipatwa na mkasa huo miaka mitatu iliyopita.
    Akisimulia namna alivyoanza kuugua alisema awali aliona matiti yake yakiongezeka ukubwa kila kukicha lakini hakujua kama lingeweza kuja kuwa tatizo kubwa kama lilivyo sasa.
    Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya ilimbidi kwenda kliniki anayohudhuriaga kupata dawa na kuwaeleza manesi ambapo walimjibu kuwa imesababishwa na dawa anazotumia na hivyo kulazimika kukatizwa dozi hiyo na kupewa aina nyingine.
    Hata hivyo Khamisi alisema kwamba pamoja na kubadilishiwa dozi hajaona kama kuna mabadiliko yoyote aliyoyapata na kuongeza kwamba hivi karibuni alipewa dawa nyingine ambazo kati ya hizo kuna zile ambazo zilimsabishia matiti na tayari ameanza kupatwa na maumivu aliyokuwa akisikiaga awali wakati matiti yalivyokuwa yanaanza kuota.
     Kwa mujibu wa Khamisi ameshahangaika kupata matibabu hadi Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili lakini hadi leo hajapatiwa tiba stahili ya kumaliza tatizo hilo.
    “Jamani Watanzania naomba wanisaidie kwa njia yoyote ile ili niondekane na hali hii kwani inanidhoofisha sana na kunikosesha raha hasa mbele ya wanaume wenzangu.
"Kwani hapa navyoongea na nyie waandishi nilipimwa hadi kansa na matiti ndio kama hivyo mnavyoyaona yanaendelea kukua na huniuma sana hasa wakati ninapolala,”alisema kaka huyo.
Pia alitumia fursa hiyo kumuomba Rais Jakaya Kikwete kumsaidia ili arudi katika hali yake ya uanaume kwa kuwa maisha kwa sasa kwake yamezidi kuwa magumu kwa kuwa hawezi kufanya kazi yoyote kutokana na hali hiyo.
Mtaalam wa magonjwa, Dk. Dina Komakoma,akielezea kuhusu sababu za kutokewa kwa hali hiyo kwa wagonjwa wenye maambukizi ya VVU ni jambo la kawaida japo hutofautiana.
Dk. Komakoma alisema wengine hujikuta wakinenepa au wakikonda sana na hili la Khamis sio mtu wa kwanza kupatwa na hali hiyo na kuongeza kwamba inapotokea mgonjwa akapata hali tofauti kama hiyo anapaswa kusitishiwa dawa


Kuna Maoni 11 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  Pole sana kaka Khamis, inasikitisha sana.

  Ugonjwa huu tutapona kweli? Manake usipoleta wewe utaletewa na mwenzio mwenye tamaa zake.

 2. Anonymous Anasema:

  huyu mtu apelekwe India , huko hakuna kinachoshindikana -wahindi kwa matibabu ni wachawi !!!! sasa , duh !! jamani nauliza -kweli hizi dawa zinaotesha maziwa ??? je ikiwa mwanamke mwenye virusi akizitumia , naye ataota maziwa -labda sehemu nyingine ?? maana tayari maziwa anayo, au hapa daktari Komakoma ,imekaa kaa je ?? Kingine , jamani wanaume tuwaheshimu wanawake zetu-siyo kushika shika maziwa kwa nguvu-kumbe yanauma, na pia ,kumbe si rahisi kuwa mwanamke, lakini tunavyowanyanyasa !!!! .Jamani TUKOME. Zebedayo-kweli inauma.

 3. Anonymous Anasema:

  "anayohudhuriaga". mhhhhhhhhhh!!!!

 4. Anonymous Anasema:

  Nashauri TFDA waangalia element zinazotengeneza ARV na wafananishe za homoni za kike zinazojihusisha na matiti.Hii itasaidia kufahamu ukweli wa hizi dawa kwa kuwa watengenezaji si Mungu ambaye amekamilika katika uumbaji wake.Na kama TFDa hawatakuwa na uwezo wa kutambua hilo jambo mapema wawapatie kazi hii taasisi zetu za elimu ya juu,wanafunzi wanaofanya kozi za uzamili au uzamivu inaweza kuwa ni tasinifu ya kwao.Taasisi za kuzitumia ni kama MUHAS, NM-AIST, n.k. Pole kaka na hilo na endelea kuwa mvumilivu kwani Muumba analipa kwa kila anayevulimilia apatapo na msiba/shida

 5. Anonymous Anasema:

  ewe mungu muweza muumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake....tunakuomba sisi waja wako tujaalie mema ya huko peponi na tufanyie wepesi katika kumalizia hii dunia

  kwani dalili zote za mwisho wa dunia zilizoandikwa kwenye kitabu cha dini zinaonekana na zimekamilika

  kilichobaki tu ni kurudi kwa nabii issa au yetu ili kila mmoja abebe mzigo wake.

  mungu atakupa salama ameen.

 6. Anonymous Anasema:

  Michuzi mbona kichwa cha habari sio sahihi? itakuwaje anadai ilhali ushahidi huo hapo kafunua na pia wataalamu wamethibitisha kuwa amefikwa na hayo kwa kutumia dawa alizokuwa akitumia? Hapo utasemaje kuwa anadai?

 7. Gangai Anasema:

  Hii inawezekana kuwa jamma alipewa dawa za"hormons"za kukuuza matiti kwa wale wanaume wanaofanyishiwa operation ya kubadilika kutoka mwaume kuwa mwanamke! Ingekuwa Ulaya angedai fidia.
  David O. Gang'ai

 8. Anonymous Anasema:

  Pole ndugu yetu!

  Mola atakusitiri na mtihani huu!

 9. Anonymous Anasema:

  jamani hichi ni kitu cha kawaida huku ulaya haswa watu kibao wanashikwa na matatizo haya hii inaitwa GYNECOMASTIA

 10. Anonymous Anasema:

  ''jamani hichi ni kitu cha kawaida huku ulaya haswa watu kibao wanashikwa na matatizo haya hii inaitwa GYNECOMASTIA

  Mon Jun 18, 06:01:00 PM 2012''

  Asante kwa darasa fupi!!
  Inakuwa ngumu kidogo kuingia akilini!

  Eh! huku virusi huku 'kifua' jamani!

 11. Anonymous Anasema:

  Pole sana kaka kwa hayo. Ila GYNECOMASTIA husababishwa na hormone za kike ambazo ARVs esp HAART zinazi-induce angalia links hizi zinaweza kukusaidia jinsi ya kufanya kupunguza hormone hizi za kike mwilini lakini pia tafuta dawa ingine.

  1: http://www.livestrong.com/article/187828-how-to-reduce-male-breasts-without-surgery/

  2: http://www.mayoclinic.com/health/gynecomastia/ds00850/dsection=causes

  3: http://www.thebody.com/cgi-bin/bbs/showflat.php?C=&Board=gaymen&Number=42305

  Pia google na utapata lots information kuhusu haya matatizo na jinsi ya kuyatatua.

  Akhsante:

  Mama H