WANANCHI katika Halmashauri ya Wilaya ya Siha wameshauriwa kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ili kuepuka gharama za papo kwa papo ambazo si rahisi kuzimudu.

Rai hiyo imetolewa na Meneja Ofisi ya Kanda NHIF Moshi, Chris Mapunda wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Siha Kusini wakati wa zoezi la Uhamasishaji kwa wananchi kujiunga na CHF wilayani humo.

“Mfuko wa Afya ya Jamii ni utaratibu wenye unafuu wa uchangiaji kabla ya kuugua na unamwezesha mwananchi wa kawaida kumudu gharama za matibabu pale anapougua nah ii inamsaidia mwanchi kumupunguzia gharama za matibabu,” alisema Mapunda.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Afya ya Mfuko huo katika Wilaya ya Siha Bw. Amini Lengati Munuo aliwasihi wananchi hao kuona umuhimu wa kujiunga na Mfuko huo ili wawe na uhakika wa matibabu wakati wowote.

“Halmashauri ya Wilaya ya Siha imepandisha gharama za papo kwa papo kitu ambacho kitakuwa kigumu kwa mwananchi wa kawaida kuweza kutoa fedha kila anapofika kupata huduma na kwa maana hii ni vyema mkajiunga na Mfuko huu ambao uchangiaji wake ni wa mara moja,” alisema.

Aidha alisema kuwa dhamira ya Serikali kuanzisha Mfuko huo ni nzuri na inayolenga kupunguza gharama za matibabu na hasa kwa wananchi wenye vipato vya msimu ambao hawana uwezo wa kulipia gharama za papo kwa papo kila wanapougua. Halmashauri ya Wilaya ya Siha imepanga kiwango cha mchango wa CHF kwa mwaka kuwa ni Shs 10,000 kwa Kaya ambayo ni baba, mama, na watoto wane chini ya umri wa miaka 18.

“Zoezi la uhamasishaji kwa wananchi kujiunga na mpango huu katika Wilaya ya Halmashauri ya Siha ni endelevu hivyo wananchi jitokezeni kwa wingi kujiandikisha katika Vituo vya Afya na Zahanati zilizopo karibu na maeneo mnayoishi ‘’ aliongeza Bw. Pita Kasaka ambaye ni mratibu wa Mfuko huo wa Wilaya.

Akitoa shukrani, Mganga Mkuu wa Halmashuri ya Wilaya ya Siha Dr Best Magoma ameushukuru Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Ofisi ya Kanda na Makao Makuu kwa kushiriki kikamilifu katika Uhamasishaji kwa kutumia gari la matangazo la Mfuko huo. “Kwakweli tunawashukuru sana wenzetu wa NHIF kwa ushiriki wao, tunaamini ujumbe umewafikia wananchi, maana kwa muda mfupi tumeanza kuona mwamko wa wananchi wa kujitokeza na kuanza kujiandikisha” Amesema Dr Best Magoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...