Na Masoud Masasi, Dodoma 
SERIKALI imefanya mabadiliko katika halmashauri hapa nchini kwa kuwateua wakurugenzi wapya 14 huku ikiwavua madaraka wengine nane ambao walionekana kushindwa kuwajibika ipasavyo katika halmashauri zao na kufanya ubadhirifu wa fedha za halmashauri zao. 

Pia katika mabadiliko hayo wakurugenzi kumi na moja wamepewa onyo kali huku wengine 22 wakihamishwa vituo vya kazi ambapo wakurugenzi watatu wakipumzishwa kufanya kazi katika halmashauri hizo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ubadhilifu wa fedha . 

Akitangaza mabadiliko hayo mbele ya waandishi wa habari jana mjini Dodoma Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi)Hawa Ghasia alisema mabadiliko hayo yanatokana na 
kuboresha nidhamu na utendaji wa kazi kwa wakurugenzi hao. 

‘’Wakurugenzi 14 wameteuliwa ili kuziba nafasi zilizoachwa wazi huku
 wakurugenzi nane wakivuliwa madaraka hayo na Waziri Mkuu wengine watatu wakipumzishwa kabisa ambapo wakurugenzi 22 wakihamishwa katika vituo vyao na kupelekwa sehemu nyingine” 

“Mabadiliko haya ni kuboresha utendaji wa kazi katika halmashauri zetu
 pamoja na kuongeza nidhamu na uwajibikaji wa kazi kwa wakurugenzi ambao walikuwa si waadilifu katika kutelekeza majukumu yao”alisema 
Ghasia. 

Waziri huyo aliwataja wakurugenzi wapya walioteuliwa kuwa ni Jenifer
 Omollo ambaye anakuwa mkurugenzi wa Mji wa Kibaha,Fidelica MyovelaMkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Musoma na Khadija Maulid Makuwani ameteuliwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora. 

Aliwataja wengine kuwa ni Ibrahim Matovu ameteuliwa kuwa mkurugenzi
 halmashauri ya Muheza,Idd Mshili halmashauri ya Mtwara,Julius Madiga Mkurugenzi Halmashauri ya Manispaa yaMorogoro na Kiyungi Mohamedi Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Shinyanga. 

Wengini ni Lucas Mweri ameteuliwa Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya
 Nanyumbu,Miriam Mmbaga halmashauri ya Kigoma,Mwamvua Mrindoko Mkurugenzi mtendaji Nachingwea,Pendo Malembeja Halmashauri ya Kwimba huku Pudenciana akiteuliwa mkurugenzi wa Ulanga.



Ruben Mfume Halmashauri ya Ruangwa na Tatu Selemani amekuwa mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Kibaha ambapo waziri Ghasia alisema uteuzi huo ulifanyika april 24 mwaka huu. 

Waziri huyo alisema wakurugenzi waliovuliwa madaraka kutokana na
 makosa mbalimbali katika Halmashauri zao kuwa ni Consolata Kamuhabwa(Karagwe),Ephraim Kalimalwendo(Kilosa),Elly Jesse 
Mlaki(Babati),Eustach Temu(Muheza),Jacob Kayange(Ngorongoro),Hamida Kikwega. (Chato),Majuto Mbuguyu(Tanga) na Raphael Mbunda halmashauri ya Manispaa ya Arusha. 

Waziri Ghasia aliwataja wakurugenzi ambao wamepewa onyo kali kuwa ni
 Judetatheus Mboya(Newala),Lameck Masembejo(Masasi),Abdallah Njovu(Tandahimba),Jane Mutagurwa(Shinyanga),Silvia Siriwa(Sumbawanga),Kelvin Makonda(Bukombe),Alfred Luanda(Ulanga),Fanuel Senge(Tabora),Maurice Sapanjo(Chunya),na Beatrice Msomisi halmashauri ya Wilaya ya Bahi. 

Pia waziri huyo alibainisha kuwa katika mabadiliko hayo wakurugenzi
 watatu ambao ni Xavier Tiweselekwa wa halmashauri ya Wilaya ya Misungwi,Erica Mussica kutoka halmashauri ya Sengerema na Theonas 
Nyamhanga wamepumzishwa kufanya kazi katika halmashauri hizo. 

“Maamuzi haya yalifanyika katika kipindi cha mwaka 2011/12 na hawa waliopewa onyo walitendeka makosa yao katika halmashauri zao hivyo pia wakurugenzi 22 wamehamishwa katika vituo vyao vya kazi na kupangiwa sehemu nyingine ili waweze kuimarisha utendaji kazi wao”alisema. 

Alisema tayari wakurugenzi wanne waliotuhumiwa katika ubadhilifu mbalimbali katika halmashauri zao wameshafikishwa mahakamani huku wengine wakiendelea kufanyiwa uchunguzi ambapo amesema wakibainika watapelekwa mahakamani pia. 

Alisema wale ambao walionekana hawakuhusika katika ubadhilifu katika
 vituo vyao vya kazi walipangiwa kazi nyingine huku wale walionekana utendaji wao sio mzuri walipumzishwa kabisa. 

Waziri huyo pia aliwataka wakurugenzi wapya walioteuliwa na wale wa zamani kuhakikisha wanafanya kazi kwa uhadilifu ili kuweza kuendelea kuboresha utendaji wa kazi katika mamlaka za serikali za mitaa nchini. 

Hata hivyo alisema hataweza kumchukulia hatua yoyote mkurugenzi kwa kusikia taarifa za mitaani na kuwataka wale wenye malalamiko kupeleka ushahidi kwake ambapo atafanya uchunguzi kabla ya mhusika kuchukuliwa hatua za kisheria. 

‘’Tukisema tuanze kuchukuwa hatua kwa kusikia taarifa za mitaani basi
 tutajikuta tukifukuza wakurugenzi wote kinachotakiwa ni kuwa na ushahidi uletwe na utafanyiwa kazi na hatua zitachukuliwa kwa Yule 
atakayebainika”alisema waziri Ghasia. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 22, 2012

    mimi kama mwananchi naona hao walioonekana wana dosari wapelekwe mahakamani kwa makosa waliofanya sio kuwaachisha kazi wakati wameshakuwa mabilionea... huko sio kuwafukuza kazi, bali nikuwasaidia kwani sasa wana uhuru wakula mali walliochuma kimakosa bila wasiwasi wowote.
    mdau

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 22, 2012

    Angalau sasa tunaona utekelezaji mzuri kwa mbaaali. Wezi wasionewe aibu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 22, 2012

    Hongera mama kwa kuwaondoa mafisadi

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 22, 2012

    Mbona hayo mabadiliko makubwa hayaonekani una waipigia kampeni ccm?

    Kuhamishwa kituo nayo ni hatua ya nidhamu, mbona analipwa gharama za uhamisho na kadhalika?

    Kwa hoyo ukiwa vua ukurugenzi ndo kusema kazi umemaliza au? Mahakamani hawafikishwi au kwa vile vila hela waliyolalmba ilikuwa ya familia yao?

    TUMECHOKA NA LONGO LONGO ZA KIUTENDAJI TANZANIA.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 22, 2012

    HIVI JAMANI MIMI NAULIZA HIVI MKOA NA WILAYA NA MIJI YA KIGOMA NDIO IMESAHAULIKA KABISA KATIKA TANZANJA HII? KILA KUKICHA IRINGA,MBEYA,SINGIDA,LUSHOTO,BABATI,MWANZA,ARUSHA,MOROGORO,LINDI,MTWARA,SONGEA,KILWA,BAGAMOYO. HIVI KIGOMA SIO TANZANIA KABISA? BASI WAPENI NA HAO UHURU WAO WAJITEGEMME WENYEWE WAWE NA NCHI YAO KATIKA TANZANIA ,MAANA NAONA HAKUNA LOLOTE LINALOFANYIKA KIMAENDELEO ZAIDI YA KUSAHAULIWA KAMA KIPOFU KITUO CHA BASI. HATA RUKWA CHIVI SASA KUNA MAENDELEO ANGALAU INASIKIKA KATIKA MEDIA ZA HABARI ZA TANZANIA,AU KAMA KIONGOZI AKIWA KATIKA POWER BASI ANATETEA KWANZA KWAO? HUO NI UBAGUZI NA NI KINYUME CHA HAKI ZA BINADAMU,HAIWEZEKANI NCHI YA TANZANIA NI PAMOJA NA KIGOMA LAKINI MKOA UMESAHAULIKA KAMA BABU ALIEFARIKI MWAKA 1958.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 22, 2012

    Jamani mbona mnemsahau Mkurugenzi wa jiji la mwanza amejenga hoteli ya kifahari Kwenye fukwe ya ziwa maeneo ya nyegezi, yaani pale ofisi za jiji la mwanza wamekuwa miungu watu, mmulike Mkurugenzi huyu wa jiji la mwanza, ufisadi na uonevu uko wazi kabisa

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 23, 2012

    poa yote mema

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...