THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Timu ya Mchezo wa Cricket ya Totteridge ya Uingereza yatoa msaada wa Vifaa vya michezo kwa Tanzania

Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha Tanzania, London nchini Uingereza, Bwana Yusuf Kashangwa (tatu kushoto), akipokea msaada wa Vifaa vya mchezo wa Cricket kwa Tanzania kutoka kwa Mwenyekiti wa Timu ya Cricket ya Totteridge Millhill, Bwana Stewart Wenham (kwanza kushoto). Msaada huo wa Vifaa vilikabidhiwa kwa Mkurugenzi, Bwana Kashangwa, ni moja ya ushirikiano mzuri uliopo baina ya Timu ya Tanzania ya mchezo wa Cricket, Shirikisho la mchezo huo hapa Uingereza na Timu ya Cricket ya Watford. Wengine pichani ni maafisa wa Kituo cha Biashara cha Tanzania, London.Timu ya Cricket ya Watford ikiongozwa na Bwana Gulfraza Riaz, imekuwa ushirikiano wa karibu na Timu yetu ya Taifa ya mchezo wa Cricket, Tanzania, vile vile timu hiyo imekuwa mstari wa mbele kuitangaza Tanzania katika mchezo huo hapa nchini Uingereza, pamoja na kuandaa michezo ya majaribio kwa Tanzania kila mara.
Bwana Gulfraz, akisalimiana na Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha Tanzania, London, Bwana Yusuf Kashangwa kabla ya makabidhiano ya msaada wa Vifaa vya mchezo kwa Timu ya Cricket ya Tanzania.