Taswira za vipindi vya luninga nchini Tanzania haitokuwa kama ile ambayo wengi wetu tumeizoea. Kuna kitu kipya na cha aina yake.Ni Talk Show inayokwenda kwa jina The Mboni Show ambayo mwenyeji au host wake ni mwanadada Mboni Masimba.
The Mboni Show, kitakuwa kinarushwa kila siku ya Alhamisi,Saa 3 Kamili Usiku Mpaka Saa 4 na kisha marudio yake yatakuwa yanafanyika Saa 7 Mchana na Saa 10 jioni siku ya Jumamosi. Kwa maana hiyo ni kipindi ambacho,bila shaka, kitakufanya usibanduke hapo utakapokuwa ukikitazamia kwa muda wa takribani saa  1. Yote hayo ni kupitia kituo cha televisheni cha EATV(East Africa Television).
Lakini Mboni Masimba ni nani? Kipindi chake kitahusu nini na kitakuwa na tofauti gani kutoka katika vipindi vingine kadhaa vilivyoko katika stesheni mbalimbali za luninga? Ili kupata majibu kwa maswali hayo na mengine,nilimtafuta Mboni Mashimba. 

Fuatilia mahojiano hayo katika Blog yetu 
dada ya BongoCelebrity




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 11, 2012

    kile kipindi alichojitahidi kuwapatanisha wale wadada wawili sikukipenda maana inaonekana wazi kabisa alimlazimisha yule dada mwenye mume kumsamehe mwenzie. halafu pia yule mwanaume alitakiwa awe pale ili aelewe kuwa maneno aliyoambiwa kuhusu mkewe yalikuwa ya uongo. kiatakuwa kipindi kizuri sana ila ajitahidi kutafuta ushauri kabla hajarusha kipindi chake hewani

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 11, 2012

    Mbona ni ileile ya Janet talk show, mambo ya copy & paste tuuu, wa TZ kwa kuiga bwana..?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...