Ndugu Wananchi,
          Kama ilivyo ada naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehma, kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kumaliza nusu ya kwanza ya mwaka 2012 salama. 
Kwa kutumia utaratibu wetu wa kuzungumza nanyi kila mwisho wa mwezi, leo napenda kuzungumzia mambo mawili. 
Jambo la kwanza ni suala la usafirishaji haramu wa binadamu nchini na la pili ni la mgomo wa madaktari.  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 01, 2012

    Bravo raisi wetu umesema na wananchi tumekuelewa

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 01, 2012

    DUuu tumeelewa kweli kuskiza upande mmmoja tu so vizuri sasa tumejua ukweli Mzima

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 01, 2012

    Nimemuelewa rais, lakini suala la Ulimboka kupigwa na kunyanyaswa kwa jinsi ambavyo lipo inaonekana serikali imeshiriki,...nikisema serikali nina maana ya jeshi la polisi, ulinzi au zaidi usalama wa taifa, mara nyingi rais anakuwa hapewi taarifa usalama wa taifa unavyofanya mambo yake. Circumstancial evidence inaonyesha kwa vyovyote vile serikali imehusika, Rais anasema ukweli ila kuna watu wengi chini yake wenye kuweza kufanya matatizo hayo.
    Lingine, rais yupo sahihi tunaelewa matatizo ya nchi maskini, lakini sikubaliani kabisa na serikali kutotomia pesa nyingi kuimarisha hospitali zetu,....kwanini hao viongozi wanatibiwa nje? Rais angefanya hiyo kuwa ajenda yake muhimu...sahau kila kitu lakini hospitali za hapa nchini ziwe na uwezo wa kufanya matibabu yote hata mkiagiza madaktari nje ni sawa lakini kila kitu kifanyike hapa kwenye hospitali zetu...hakuna sababu za kupeleka wagonjwa India, S. Africa au Kenya, ni aibu mhe. rais wetu.
    Angalieni pia maslahi ya madaktari na angalau yalingane na wabunge au na kada nyingine zinazolipwa sana, jamani madaktari wana kazi ngumu sana. Michuzi naomba usibanie maoni yangu

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 01, 2012

    Kweli serikali ihakikishe ishughulikie taasisi zake, zisitoe hela kwenye taasisi binafsi.Taasisi binafsi wamejiita binafsi yani PRIVATE, kwa nini serikali ishughulike na hizo taasisi binafsi badala ya za Watanzania wote???

    Hafu lingine ni kweli madaktari ni muhimu. Lakini,kada zingine hazimaanishi siyo muhimu sana. Mfano,kama ulinzi wa nchi ukiwa dhaifu manake usalama wa nchi ni dhaifu manake hakuna atayekuwa na amani,kwa hiyo serikali inatakiwa iangalie kwamba wanajeshi,polisi,wanausalama, magereza na wengineo wanakuwa katika mazingira mazuri kuanzia vifaa,mishahara.n.k.

    Mfano mwingine, ukitaka kuwa na vifaa vizuri vya hospitali, unahitaji wahandisi wataobuni hizo mashine na hawa si madaktari. Bila ya kuwa na vifaa vizuri vya hospitali utabibu ni mgumu. Hawa hawa wahandisi wanahitaji kuboresha vifaa vyetu vya ulinzi kuanzia antimissiles, fighter jets, armor vehicles, navy ships, drones, n.k. Muhimu sana kwa usalama wa nchi. Na hawa wahandisi nao wanahitaji mazingira mazuri ya kufanya kazi kuanzia mishahara, n.k.

    Waalimu kuanzia shule ya msingi hadi maprofesa wa vyuo vikuuu.Hawa ndiyo wanawaandaa wafanyakazi wote wa nchi hii. Kuanzia Raisi mpaka mwalimu wa chekechea, na hao madaktari. Kwa hiyo hawa nao wanahitaji mazingira mazuri kuanzia mshahara, n.k.

    Na kada zinginezo.

    Kwa hiyo kwa ujumla kada zote zinategemeana hakuna iliyojuu ya nyingine. Kada moja ikilega lega nchi itayumba. Kwa hiyo cha msingi kila mmoja atungulize utu/uzalendo hafu mambo mengine yatatatulika taratibu Muumba akipenda. Kama na siye tuliokuwa kwenye kada zingine tukigoma madaktari itakula kwao pia. Mfano moto nyumbani kwake umetokea yuko gorofa ya juu hawezi kushuka chini wala kwenda juu, mtu wa zima moto atamwambia amegoma, sijapata maslahi. Askari naye atasema nimegoma hakuna maslahi, n.k.

    Raisi kaelezea vizuri jinsi maslahi ya wafanyakazi yanavyoboreshwa. Na maisha ya wafanyakazi wengi yamekuwa mazuri.Tembelea sehemu nyingi wafanyakazi wengi aidha wanamagari ya kutembelea au wanampango wa kununua baada ya siku kadhaa. Miaka kumi iliyopita haikuwa hivyo.

    TUWE WAZALENDO TUTENDE HAKI KWA KILA RAIA/BINADAMU KULINGANA NA SHERIA INAVYORUHUSU. TANZANIA NI YA WATANZANIA WOTE,IKIHARIBIKA INAKULA KWETU WOTE. JUKUMU LA KUILINDA NA KUIENDELEZA NI LA KILA MTANZANIA KULINGANA NA NAFASI YAKO. KAMA UKO NECTA SAHIHISHA NA TOA ALAMA KWA USAWA KULINGANA NA ALIVYOPATA KWA KILA RAI, MAHAKAMANI TOA HUKUMU KULINGANA NA SHERIA INAVYOSEMA USIMWANGALIE MTU AU MFUKO, UKIWA DEREVA WA TAKSI MTOZE MTU KWA UHALISIA WA UMBALI USIANGALIE SURA,UKIWA TRAFIKI TUNZA USALAMA USIANGALIE MKONO WA DEREVA WA DALA DALA KAMA AMEUFUMBA AU LA KUKUPANDISHIA KITU FULANI, N.K.

    NAWAKILISHA BWANA ADMINISTRATOR

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 01, 2012

    Think outside the box.
    Serikali inamtesa Ulimboka kwa kujua inajichafua wakati huu upinzani ukiwa mgumu.
    Wat if watu wa upinzani wamemtesa jamaa kwa kujiita polisi na usalama wa Taifa?
    Wat if kikundi cha watu kimefanya kuichafua serikali ya JK?
    Ni mawazo tu binafsi

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 01, 2012

    madai ya haki za madocta kweli ni muhimu ila kuchukua sheria mikononi mwao sio haki yao, nani kawapa haki ya kuweka maisha ya walalahoi rehani?
    wamechanga hela 40,000$ sasa kama kweli hao madocta wanajali hali za wagonjwa wangemuweka rehani ulimboka wanunue ct scan mashine kuokoa maisha ya mamilioni ya watanzania, baba kikwete leo umeongea pamoja

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 02, 2012

    Mheshimiwa Raisi tunakushukuru kwa hotuba na ufafanuzi uliotuoa. Jambo ambalo naweza kusema ni kwamba ni kweli wooote tunahitaji maisha mazuri ila kiukweli kazi ya madaktari ni ngumu sana. Ni wangapi hapa ukiona damu mwili wote unakusisimuka? fikiria vidonda vilivyooza, fikiria maiti na magonjwa mengine mazito yote haya daktari anayavumilia na hatihati ya kuambukizwa magonjwa pia. Mimi ni mwalimu nakubali ndio tunawandaa watu wote katika fani mbalimbali nasema udaktari wafikiriwe zaidi na zaidi.
    Mh. Rais jambo unalotakiwa kutafakari ni hali ya mambo yanavokwenda na ni kwanini wananchi wanahic serikali ina hela nyingi ila inazitumia kwa wachache. Angalia posho ya sh.10,000 kwa daktari au laki moja na linganisha na ya mbunge halafu uchambue kati ya hao nani ana kazi ngumu?
    Pili kumekuwa na mambo mengi ya ufisadi kwanini hyo mianya isifungwe ili hizo pesa ziweze kusaidia madaktari na wengineo? Haya tumesikia kuwa kuna watu wana hela uswisi za kuendesha wizara kwa miaka mitano kwanini zisirudishwe watu wakaboreshewa maisha hata kwa mikopo ya riba nafuu? Ukimtamkia mtanzania mshahara wa laki tisa anastuka utadhani ni mkubwa lakini tuangalie kwamba mtu ana watoto labda watatu wako sekondari ada ni laki nne kila mwezi hyo tayari ni 1.2m ambayo imeshavuka mshahara nyongeza anapata wapi? akishalipa ada mtoto anahitaji pocket money kila mwezi tufanye kima cha chini 50 elf mara watoto watatu ni 150*12=? haya tuje kodi ya nyumba wenye nyumba wanataka umlipe kwa mwaka akikuhurumia ni miezi 6 tuseme unaishi nyumba ya laki 2 mara 12ni 2.4. Nauli ya daladala ama mafuta ya gari, chakula nyumbani n.k hivi vyote ni basic needs huyu mtu tena hana starehe unafikiri ataacha kuomba rushwa? atakuwa na mood ya kufanya kazi kwa moyo wote? tunajua ni wito ila hali ya maisha ni ngumu mno ni vizuri kukaa na wabunge na mawaziri mkajipunguzia posho kidogo ili tugawane keki sawa, then uhakikishe kuwa fedha zote chafu zinarudishwa kwa serikali naamini migogoro mingi itapungua. Nakutakia mafanikio mema katika kulitumikia taifa.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 02, 2012

    mdau wa 0922PM 2012

    Kuna "rare professions" bila maneno meeengi, madaktari wanastahili kulipwa zaidi. Dunia nzima mshahara wa Daktari SIO sawa na wa polisi, bwana jela, zimamoto au usalama.

    Mazingira ya kazi, kiwango cha elimu, vyote hivi vina apply na ndio maana hata kimataifa kiwango chao kipo juu cha malipo.

    Fuatilia ujue rubani mzoefu analipwa kiasi gani, na zimamoto analipwa kiasi gani. Pamoja na kuwa rubani anamtegemea zimamoto kwa uokozi haina maana walipwe sawa. Hii toffauti ni duniani kote kutokana na mazingira ya kazi zenyewe.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 02, 2012

    madaktari hao hawatufai tena, wameshakuwa wanasiasa na maafa walio ya sababisha hata wapewe 10mil, haita saidia kitu kwa maana watu wamepoteza wapenzi wao , wazazi wao watoto wao jirani na hata ndugu kisa mgomo, mi naomba potelea mbali na liwalo na liwe kama ufa watu wamesha kufa tena kwa maelfu hivyo hakuna cha kupoteza FUKUZA WOTE tangaza ajira upya, hao waliofukuzwa wakagombee ubunge maana ndicho wanachokitarajia

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 02, 2012

    Yaani kwa kweli madaktari wanalipwa hela ndogo sana. ila kwa kiwango cha Bongo ni kubwa. I get 4 times than Bongo Dr. and I'm not a doctor and the same time people are telling us from Ughaibuni come back home huko ughaibuni matatizo tu. I will come for vista and if there is a opportunity to invest I will do it! Poleni Wagonjwa na poleni Madaktari.. wezetu mpo huko jitooleni na mnaokoa maisha mengi ya watu katika mazingira magumu.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 02, 2012

    Ok Heko JK umesema sahihi. Mi nauliza What if ni jamaa tu wanamdai Dr mambo yao binafsi!! Wamemtokea< Hakuwa amewalipa hadi deadine walizoset!?

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 02, 2012

    Wewe anonimas unaesema unalipwa pesa nyingi ughaibuni lakini pia husemi kuwa pesa hiyo inakatwa kodi kubwa, unalipa kodi ya nyumba kubwa kuliko TZ na unalipa bills kibao, mwisho wa siku huna hata hiyo pesa ya kuinvest, unless ukope. Tena maisha ya ughaibuni jamani unaweza jikuta mwisho wa mwezi una 0 balance kwenye akaunti yako au umeoverdraft. Acheni kudanganya watu Bongo mwisho wa siku tukiweka matangazo ya kuomba michango ya mazishi humu watagoma kutuchangia! Vile vile maombi yataongezeka wakati huku nako mabills kibao!!

    Mdau ughaibuni

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 02, 2012

    We wa ughaibuni unachekesha kweli,opportunity za kuinvest huzioni au unataka uje ugongewe mlangoni? Na ni ngumu kuziona kama hata pa kutumia "a" na "an" huwezi kutofautisha! Ovyoo!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 02, 2012

    TUMUOMBEE DR APATE NAFUU NA KUPONA. SERIKALI IFANYE KZI KWELI KUWEZA KUWAPATA WAHUSIKA WA TUKIO HILI. KWA KIPINDI HIKU KUANZA KUMLAUMU FULANI AU SERIKALI. KWANZA WAPATIKANE WALIOFANYA KITENDO HICHO CHA KINYAMA KAZI NI MHE NCHIMBI NA IDARA ZOTE ZINAZOHISIKA WAFANYE KAZI NA KUTOA JIBU HARAKA. HALI INATISHA SANA KWA USALAMA WA NCHI YETU. HUU NI MTIHANI WA 1 MHE NCHIMBI

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 02, 2012

    Hongere muheshimiwa Rais, ukweli umedhihirika wazi, madokta kiukweli warudi kazini mliyowakubalia na kuwafanyia ni mengi,. Jamani, turidhike, sisi tunalipa kodi mkapewa mishahara n.k lakini sisi ndio mnatugomea tufe, kikubwa asiyetaka kweli aache tu kwa roho safi,. Kila mtu ana umuhimu katika eneo lake, WAZENI UTU KWANZA, wakati mkifikiria mengine badae,. RAI: madaktari, rudini kazini. tuangalieni sisi watanzania, angalieni vipato vya wafanyakazi wengine, compare mtapata majibu,. tumewavumilia now hapana,.. rudini kazi or acheni kazi tu wengine wakae,. ahsante

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...