Ingawa alikuwa mfanyabiashara maarufgu na tajiri sana, Bw. Sewa Haji Paroo (pichani) inahadithiwa alikuwa mcha Mungu na alijulikana kwa kusaidia wasio na uwezo na wagonjwa, ambapo alisaidia Wahindi, Waarabu na Waswahili bili kuchagua wala kubagua.

Mwaka 1892, alijitolea jengo la ghorofa tatu mjini Bagamoyo na kulifanya kuwa shule ya kwanza yenye wanafunzi mchanganyiko ambalo lipo hadi hii leo, na baadaaye akaanzisha hospitali, nyumba ya kuishi wapagazi na kambi ya wakoma.

Jijini Dar es salaam, alijitolea fedha kwa ajili ya ujenzi wa hospitali kubwa kwa wakati huo iliyoitwa Sewa Haji, ambayo baada wakoloni wa Kiingereza walipokuja waliibadilisha jina na kuitwa  Princess Margaret Hospital ambapo  mwaka 1961 ikaitwa  Muhimbili (BOFYA HAPA). Kwa heshima yake  hadi leo kuna  wodi wa Sewa Haji katika hospitali hiyo ya Taifa.

Sewa Haji Paroo  alifariki dunia mnamo mwezi wa  February mwaka 1897 akiwa na umri wa miaka  46.  
Katika rambirambi zake kwa kifo chake, Gavana wa Tanganyika wakati huo alisema: “Wema wake haiyumkini ulipunguza mateso ya maelfu ya watu, na alitoa mchango muhimu  katika  sehemu ya historia iliyosahaulika katika maendeleo ya Afrika Mashariki”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 01, 2012

    yaani angaishi miaka 90 sijui angefanya mangapi...kuna watu wanajali jamii kwa ujumla...

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 01, 2012

    mbonawapo wengi sana kina sewa haji lakini tatizo ni uwarabu ndio maana hawawezi kusfiwa kwani katika nchiyetu muarabu hafai kusifiwa,

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 01, 2012

    jina libadilishwe liandikwe dkt ulimboka ameahidi atatumia milioni 63 za matibabu yake nje ya nchi kuwatibu wagonjwa wote wa wodi ya sewa haji

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 01, 2012

    siyo tu nchi yetu jamani, hata uharabuni au uhindini mwafrika asifiwi, ndo hali halisi ni sera ya nchi, ipo hadi marekani hiyo

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 01, 2012

    Naamini kuwa kwa kila mgonjwa anayetibiwa Muhimbili, basi Marehemu Sewa Haji anapata thawabu. Mwenyezi Mungu (SWT) amlaze mahali pema peponi. Kwa taarifa ya mdau wa pili, Marehemu Sewa Haji alikuwa ni mhindi Mwislamu wa Bagamoyo. Picha yake ilyokuwa imetundikwa pale Sewa Haji Ward iliibiwa/iliondolewa 1988 most probably na mijitu iliyoona kuwa Mwislamu hastahili sifa. Kuna Waarabu wengi Watanzania wanafanya mema kwa siri, hasa Ndugu Bakhressa (Mwarabu Mswahili) kwa kusaidia zahanati, vituo vya yatima na kuwalipia mamia ya watoto ada za shule kwa kujua kuwa malipo yao yako kwa Muumba wetu kama tulivyoamrishwa na dini yetu.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 01, 2012

    there we go again na ile karata ya dini, kazi kweli kweli.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 01, 2012

    sasa ndugu zangu, swala zima la kuwa mwasisi wa muhimbili na dini vinauhusiano gani maana mwenzenu mmeniacha nyuma kidogo

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 01, 2012

    Namshukuru MWENYEZIMUNGU, Naomba amlipe huyu bwaba na alieleta maelezo haya na wote waliyoyapokea kwa wema. Ameen,

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 01, 2012

    Mdau wa nne hili sio kweli. BONGO UBAGUZI UPO.America unasifiwa despite asili yako ni wapi..Mfano kuna watu wengi wamekuja states kutoka nchi mbalimbali wao wanawaita wamerekani baada ya kupata uraia. Wao wanacho angalia wewe utawanufaisha nini nchi yao, hata utoke wapi? Ndio maana wanaendelea hawajali asili yako, ukizaliwa nchi unayo haki ya kugombea urais. Uwe hapa 100 generations , 1 generations wote mko sawa under eyes of the law practically, sio bongo ni theoretically. Kwenye law ya nchi ipo, lakini watu wanao enforce the law hawafuati.

    Mifano ni mingi sana, mfano wahindi( gavana wa Louisiana , waarabu(wapo former senator from Michigan, representaive fr california, na wengi sana ukitaka uliza then nitakupa list yao.Tatizo la sisi tanzania, na baadhi ya nchi za third world ni kwamba tuna changanya chuki binafsi na siasa. Mfano, bongo wahindi, waarab au wasomali au watu wenye asili ya kutoka sehemu mbali mbali ambao you can identify by looking at their ethnicity not by birth. Kuna baadhi ya watu wanaamini sio raia kamili. Lakini cha ajabu akiwa ni mwafrika mwenye asili ya kibantu( ambaye asili yake kutoka nchi nyingine yoyote anaonekana ni mtanzania sana), ambaye huenda hajazaliwa.
    Mifano iko alfu, mfano salim ahmed salim aliwahi kuwa waziri mkuu. Amewakilisha tz miaka mingi sana. Alipokuja kugombea urais, eti ni mwarabu. Wahindi wengi ni wabunge, kwa sababu ya uwezo wa kifedha. Mfano mmoja, jamaa mmarekani ambaye ana asili ya kisomali, alikuja tz five years ago as investor, he is multi millionaire. Amekuja tz, nilikutana na mfanyakazi wake on the African investors meeting huku usa. Akasema huyo bwana alikuja usa mdogo, akapata uraia, ana makampuni mengi ikiwemo supply ya gas za majumbani. Kifupi, alikua anakamatwa kila siku bongo eti ni mkimbizi kutoka Somalia. Na askari wa barabarani sababu ya kuonekana ni msomali. POLISI WENGI BONGO, WANACHAFUA JINA LA NCHI KWA KUCHUKUA SHERIA MKONONI BILA YA KUJUA WALIFANYALO. MFANO HUYO BWANA AMERUDI AMERICA, CHANGE HIS MIND TO INVEST THERE.KWA UKWELI BONGO UBAGUZI UPOO.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 01, 2012

    bongo ubaguzi kwa kwenda mbele mtake msitake tena mwarabu anachukiwa zaidi na ukiangalia mwarabu ndio anaeishi karibu zaidi na sisi waswahili au watu weusi

    mzungu na mhindi haishi karibu na mtu mweusi au mswahili lakini wanapata sifa na kupendwa zaidi kuliko mwarabu amabe ni mtu anaeishi mchanganyiko na mweusi

    warabu ndio ndugu zetu mtake msitake warabu hawatubagui na wala hawajitengi katika maisha tunajichanganya nao kila kona

    tuachane na ubaguzi warabu ndio wenzetu wazungu wanaangalia mafanikio yao lakini tunawaweka mbele sana

    mzungu katupandikizia chuki na warabu duniani huku africa mzungu katuchonganisha na warabu kwa kusema waliuza watumwa je ni nani alikuwa mteja au mnunuzi?

    warabu wa hapa tanzania wanatujengea na kuitusaidia sana na asilimia kubwa ya watanzania tunapata ajira kwa warabu kwenye viwanda maduka malori mabasi nk yanayomilikiwa na warabu

    mungu ibariki tanzania mungu wabariki warabu wazidishe imani na mapenzi na nchi yetu.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 02, 2012

    What is going on in Tanzania? Kila mara nikisoma comments hata kama title ni kitu kingine kabisa mtu atatumbukiza udini na ukabila twaenda wapi jamani ? Inasikitisha sana. Naomba tubadilike, mimi ni mweusi nimekuwa na waarabu tumecheza na kusoma shule pamoja tunakula pamoja bila matatizo. Hebu hii sumu ya udini na ukabila tuipatie maziwa iishe nguvu. Tusijiwashie moto wenyewe jamani. Hakuna kitu kikubwa cha kuleta maendeleo kama amani na upendo vikitoweka hivi basi tumekwisha. Kama mtu ana roho mbaya ama tabia mbaya ni yeye tusihusishe kabila wala dini yake. MUNGU TUSAIDIE KATIKA HILI

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 02, 2012

    Kwa uelewa wangu mie mdogo hospitali ya Muhimbili au Princess Magret ilijengwa miaka ya 1950! sasa mtu aliyekufa 1897 ameijenga vp? au ndo ile ku-glorify kila kitu na dini! Ngoja Sheif Ponda ataishikia bango hii karibuni

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 02, 2012

    Tanzania ubagunzi ni Kama kawa mnachukiana ninyi kwa ninyi sembuse wageni Tanzania tumebarikiwa na Mungu kuwa raslimali nyingi hata kuliko USA lakini tunashidwa kuitumia raslimali hiyo kwa sababu tu ya chuki binafsi.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 02, 2012

    yaani tulivyopata uhuru nasi pia tukaungana na dhuluma ya hati miliki.

    kwa uadilifu, tulitakiwa tuendelee kuiita sewa haji hivyohivyo au tunaogopa nini?

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 02, 2012

    Tanzania ubaguzi upo kwa sana, udini upo kwa sana, kuanzia mitaani mpaka maofisini, thats why hatuendelei, mtu badala ya kuangalia fulani kafanya nini kwa faida ya wote, unakuta mtu anaangalia ni nani kafanya regardless hicho kitu kina faida kwa jamii.. mijitu ina roho mbayaaa!!!! ukabila, udini ndo umetujaa

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 02, 2012

    Mwaka 1997, mwalimu Nyerere alisema katika mkutano wa waandishi wa habari Kilimanjaro Hotel kitu kama "Ukimkuna Mtanzania, chini ya ngozi yake utamkuta mkabila". Licha ya juhudi zilizofanywa katika kipindi cha miaka 50 tangu uhuru, bado kuna Watanzania wengi ambao ni wabaguzi wa kikabila, dini na rangi. Huu ni ukweli. Ukitaka utibiwe lazima ujue kwanza una ugonjwa. Kitu cha kusikitisha ni kuwa Tanzania ilikuwa mstari wa mbele katika harakati za kutokomeza ubaguzi wa rangi Afrika Kusini, Msumbiji, Rhodesia/Zimbabwe, Namibia na Angola. Lakini sasa joka lenye sumu hatari ya ubaguzi linatamba waziwazi bila kujifunika. Ukweli ni kuwa tukipanda mbegu ya miiba ya ubaguzi, tutavuna matapishi ya sumu ya chuki na vurugu. Namalizia kwa kumnukuu hayati Kambarage tena "Dhambi ya ubaguzi haiishi, ukimbagua mtu wa rangi nyingine, kesho utambagua Mtanzania menzako". Naongeza kuwa hii SI nadharia ya Mwalimu Nyerere bali ni ukweli wa elimujamii, yaani sociology. Mwanafalsafa na msaikolojia Pierre Lacan anasema "Ubaguzi ni mfumo wa mawazo (state of mind). Wabaguzi LAZIMA wawe na 'lengo/target' ya kubagua". Kwa hivyo basi, hiyo nurosi (neurosis) ya kibaguzi itakuwa inahamahama mpaka mbaguzi apate 'lengo mhanga'. Leo mbague Patel kesho utambagua Tarimo, Masawe na Makame. Ijapokuwa sosholojia si sayansi ya kihesabu, bado ina kanuni zake zinazoambatana na saikolojia/elimunafsi. To be forewrned is to be forearmed, for verily, a word to the wise is enough!

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 02, 2012

    Siku zote nikidhani Sewa Haji was a Zaramo kumbe Mhindi Mwislamu! Kwa kweli ametufaa waTanzania na ana haki ya kuenziwa siku zote. Nadhani hata hiyo wodi moja haitoshi,hospitali nzima ingepewa jina lake au basi hata barabara moja jijini. Tumechoshwa na majina ya wanasiasa walafi kila siku kwenye barabara zetu.

    Kuhusu ubaguzi wajameni tuwe waangalifu,wakati mwengine tunaweza kujibagua kabla hatujabaguliwa...

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 02, 2012

    Kwani huu mji wa Dar es salaam kajenga nani? walulizeni wakuja jamani. Ujinga kitu kibaya sana. Kusoma si kuelewa. Wako waliosoma na madigrii lakini hawajaelimika. Bado Tz watu hawajastaarabika kabisa. Huyu aliyejenga sewa Haji ndio katika wastaarabu. Yeye wala hajataka kusifia namna hii. Alikuwa anataka atajwe kwa wema na watakaotumia sehemu. Enzi hizo Sewa Haji ilikuwa Hospitali kubwa sana. Acheni ujinga someni na mfahamu historia na kuchallange uongo uliotungwa na wakoloni na ambao unaendelea mpaka leo.

    ReplyDelete
  19. Kwann jina libadilishwe?acheni unafiki hapo historia ndo ilipokuwa inafutwa ya shekh sewa haji paroo,hosptal haikuwa tatzo,tatzo n kwa nn huyu muislam afanye mazur namna hii ndipo chuki ikadhihirika hadi leo hii tunayaona,hapakuwa na sababu ya kubadili jina mwenye hoja namkarbsha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...