Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpokea makamu wa Rais wa Afrika ya Kusini, Kgalema Motlanthe, aliyewasili nchini leo kwa ajili ya ziara ya siku mbili, ambapo atakuwa na mazungumzo na Makamu wa Rais Dkt. Bilal na kesho atatembelea Mazimbu mkoani Mororgoro.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na kuzunguma jambo na makamu wa Rais wa Afrika ya Kusini, Kgalema Motlanthe, aliyewasili nchini leo kwa ajili ya ziara ya siku mbili, ambapo atakuwa na mazungumzo na Makamu wa Rais Dkt. Bilal na kesho atatembelea Mazimbu mkoani Mororgoro.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na makamu wa Rais wa Afrika ya Kusini, Kgalema Motlanthe, baada ya kuwasili nchini leo kwa ajili ya ziara ya siku mbili, ambapo atakuwa na mazungumzo na Makamu wa Rais Dkt. Bilal na kesho atatembelea Mazimbu mkoani Mororgoro. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.
Hawa Wasouth hawana mpango kabisa,
ReplyDeleteAngalieni umuhimu wetu wanauona wakiwa na mahitaji na matatizo tu.
Wamerutapeli kwenye Shirika lao la ndege wakavunja mkataba na sisi na kukomba faida yote wakarusha madege yote kuelekea kwao.
Ona sasa kunatazamiwa Uchaguzi AU kule Addis Ababa mwezi huu wanae Mgombea wao wanataka tuwaunge mkono.
Hakuna lingine analofuata huyo Makamu wao wa Raisi!
unajua mara nyingi sisi wananchi tunaambiwaga tu kwamba kiongozi kutoka nchi fulani amekuja kwa ziara ya siku kadhaa, ila hatuambiwi haswa ni nini wanachizungumzwa.
ReplyDelete