Meya wa Manispaa ya Moshi Mjini, Jafari Michael (kushoto) akipiga mpira wa pool kuashilia ufunguzi rasmi wa mashindano ya Safari Pool Taifa ngazi ya Mkoa katika klabu ya Makanyaga Mkoani Kilimanjaro.
Meya wa Manispaa ya Moshi Mjini, Jafari Michael (kulia) akimkabidhi t-shirt na pesa nahodha wa timu ya Makanyaga wakati wa ufunguzi rasmi wa mashindano ya Safari Pool ngazi ya Mkoa wa Kilimanjaro.

Na Mwandishi Wetu.

KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Safari Lager leo imekabidhi vifaa vya michezo katika mikoa mitano inayoshiriki mashindano ya Safari Pool Taifa ambayo yanatarajiwa kuanza leo katika mikoa hiyo

Vifaa hivyo ni t-shirt pamoja pesa za nauli kwa kila timu na pesa za zawadi kwa timu zitakazoshinda katika fainali za mikoa hiyo ambazo wamekabidhiwa manahodha wa kila klabu shiriki.

Mikoa iliyokabidhiwa vifaa na pesa hizo ni Shinyanga,Kilimanjaro,Manyara,Tabora na Kagera.

Makabidhiano hayo yalifanywa na wageni rasmi mbalimbali kila Mkoa ambapo Tabora alikuwa Ofisa utamaduni wa Wilaya, Mark Katunzi,Shinyanga alikuwa Ofisa Utamaduni wa Wilaya, Asha Mbwana, Kagera alikuwa, Ibrahim Mabruk, Manyara alikuwa, Ofisa Elimu ya Watu Wazima, Fausta Akoro na Kilimanjaro alikuwa Jafari Michael ambao kwa ujumla waliwataka wachezaji wa Pool kuuheshimu mchezo na kuwa na nidhamu katika kipindi chote cha mashindano na watambue kuwa kwenye mashindano lazima apatikane mshindi wa kwenda kushiriki Taifa kuuwakilisha Mkoa.

Aidha waliishukuru Kampuni ya Bia Tanzania kwa kufadhili mashindano hayo kwani yanawafanya vijana faidike na kiasi cha fedha wanachoshindania licha ya burudani waipatayo ambayo inawaepusha na mambo mengi yasiyo na faida mtaani



Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza kesho na kumalizika Julai 8 mwaka huu ambapo timu itakayoibuka bingwa kwa upande wa Mkoa itajinyakulia kitita cha sh. 700,000 huku mchezaji mmoja mmoja akiondoka na sh. 350,000 kwa upande wa wanaume na wanawake wa kwanza atazawadiwa sh. 250,000 taslimu.

mshindi wa pili kwa upande wa timu, atazawadiwa sh. 350,000, mshindi wa tatu, 200,000, wa nne sh. 100,000 na kifuta machozi cha sh. 50,000 kitatolewa kwa timu zitakazoshiriki.

Halikadhalika kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja kwa upande wa wanaume mshindi wa pili atapata sh. 200,000, wa tatu sh. 150,000 na wa nne sh. 100,000 ambapo wanaume kwa wanawake wanne kati ya wanane watakaopoteza mchezo katika awamu ya pili watazawadiwa sh. 50,000, na wakataopoteza katika awamu ya kwanza wanane kati ya 16 wataambulia sh. 20,000.

Aidha kwa upande wa wanawake kwa mchezaji mmoja mmoja mshindi wa pili atazawadiwa sh. 150,000, wa tatu sh. 100,000 na wa nne ataambulia sh. 50,000.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...