Diwani wa kata ya Machame Mashariki,Rajabu Nkyaa akitoa maelezo kwa mkuu wa wilaya ya Hai Novatus Makunga kuhusu kivuko cha Mande ambacho kimezolewa na mafuriko ya mvua katika mto weruweru Mwezi Januari mwaka jana
Kivuko cha sasa cha gogo la mti
Mwenyekiti wa kijiji cha Nkuusinde,Hamilton Swai akimwongoza mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga
Mwenyekiti wa kijiji cha Nkuusinde,Hamiliton Swai,akimwongoza mkuu wa wilaya ya Hai bwana Novatus Makunga kukagua Kivuko cha waenda kwa miguu cha Mande ambacho kimezolewa na mafuriko ya mto Weruwer,nyuma ni diwani wa kata ya Machame mashariki Bw. Rajabu Nkyaai.
Wananchi wa vijiji vitano katika kata ya Machame Mashariki wilayani Hai kwa zaidi ya mwaka sasa wanalazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma mbalimbali kwa kuogopa kutumia kivuko cha gogo la mti katika eneo la Mande katika Mto Weruweru.
Uoga huo unatokana na kufariki dunia kwa mama na binti yake walioteleza na kusombwa na maji katika mto Weruweru
wananchi wa vijiji vya nkuundoo na nkuusinde vilivyoko machame mashariki wamemueleza mkuu wa wilaya ya hai bw novatus makunga kwamba eneo hilo la mande lilikuwa na kivuko ambacho kilisombwa na maji kufuatia mafuriko ya mto weruweru mapema mwaka jana
Hamiliton swai,mkazi wa kijiji cha Nkuusinde ameeleza kuwa baada ya kuteleza na kusombwa kwa mama huyo akijaribu kumuokoa binti wananchi wa vijiji hivyo wanalazimika kuzunguka kupitia daraja lililopo karibu na nyumba ya Mengi
Akifafanua kuhusu kifo cha huyo mama,Swai alisema kuwa baada ya kuteleza kwa binti yake naye alijaribu kumfuata kwa lengo la kumuoko ndipo waliosombwa na maji na baadaye miili yao kukutwa wakiwa wameshafariki dunia.
Anasema kuwa walikuwa wanatoka kukoboa mahindi katika mashinne zilizoko upande wa pili wa mto huo mkubwa.
Diwani wa kata ya Machame Mashariki,Rajabu Nkyaa alisema kuwa huduma ambazo zipo kila upandew haziwezi kuepukika na wananchi na hivyo kusababisha maingiliona ya mara kwa mara
Alisema kuwa kivuko cha mande ni muhimu kutokana na kutumiwa na jamii za pande hizo wakiwemo wanafunzi,waumini wa dini na wagonjwa
Alitaja huduma za kijamii ambazo wananchi wanalazimika kuzifuata kwa kila upande wa mto huo kuwa ni pamoja na kanisa la Lyamungo Umburi na kituo cha afya cha Umburi pamoja na shule za sekondari Lyasiska,Lyamungo na Nkuu
Huduma nyingine ni zahanati ya Nkweshoo pamoja na mashine ya kukoboa nafaka na kukamua mafuta ya alizeti zilizoko katika chama cha ushirika cha machame nkuu nkuu
Akizungumza mara baada ya kukagua eneo hilo mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga ameeleza kutokana na umuhimu wa kivuko hicho cha mande kwa jamii tayari gharama za kukirejesha kiasi cha shilingi milioni 62.1 zimewekwa katika bajeti ya usafirishaji wa serikali la mitaa(LGTP)
Makunga alisema kuwa kutokana na kivuko hicho kutegemewa na idadi kubwa ya wananchi,serikali inalichukulia kwa uzito mkubwa tatizo hilo la kivuko cha awali kusombwa na maji ya mafuriko katika mto Weruweru
Picha Namba 1:Diwani wa kata ya Machame Mashariki,Rajabu Nkyaa akitoa maelezo kwa mkuu wa wilaya ya hai Novatus Makunga kuhusu kivuko cha Mande ambacho kimezolewa na mafuriko ya mvua katika mto weruweru Mwezi Januari mwaka jana
Picha Namba 1:Diwani wa kata ya Machame Mashariki,Rajabu Nkyaa akitoa maelezo kwa mkuu wa wilaya ya hai Novatus Makunga kuhusu kivuko cha Mande ambacho kimezolewa na mafuriko ya mvua katika mto weruweru Mwezi Januari mwaka jana
Poleni sana wafiwa.
ReplyDeleteKwa wanakijiji sasa ndio muone je kura zenu zinazaa matunda au ndio wizi wa viongozi.
Mbao zipo nyingi huko Moshi, mkipatiwa nguzo mbili na mkaziunga vizuri kwa mbao itatosha kuliko kusubiri serikali ifanye hii kazi. Unaweza kushangaa kampeni za mwaka 2015 bado hamjapata kivuko
SO sad
wachaga mjenge kwenu. Acheni michango ya harusi mjini huku.
ReplyDeleteHii ni aibu wa wamachame tajiri sana hawa huku mjini!! Ila n hiyo dress code ya mkuu!! Duh
ReplyDelete